Rais
wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania, Mh. Dkt John Pombe Joseph Magufuli
amemsimamisha kazi kuanzia leo tarehe 27 Nov. 2015, Kamishna Mkuu wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ndugu Rished Bade kufuatia ziara ya
kushtukiza ya Waziri Mkuu, Mh. Majaliwa Kasimu Majaliwa mapema leo
asubuhi Bandarini jijini Dar es salaam.
Hatua
hiyo imekuja baada kubaini kupitishwa kwa makontena zaidi ya 300 na
kusababishia hasara Serikali ya zaidi ya shilingi bilioni 80.
Rais
Magufuli pia amemteua Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Philip
Mpango kukaimu nafasi hiyo mpaka hapo uchuguzi utakapo kamilika.
Taarifa
hiyo iliyosomwa na Katibu Mkuu Kingozi, Balozi Ombeni Sefue Ikulu
jijini Dar es salaam, imewataka maofisa wote wa TRA kutosafiri nje ya
nchi mpaka pale uchunguzi dhidi yao utakapo kamilika.
0 comments:
Post a Comment