Pages

Ads 468x60px

Friday, October 30, 2015

DK. JOHN POMBE MAGUFULI AKABIDHIWA CHETI CHA USHINDI WA URAIS WA TANZANIA AWAMU YA TANO JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva (kulia), akimkabidhi cheti cha Urais Rais Mteule wa Tanzania Dk.John Magufuli katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam leo. Kushoto ni Makamu wa Rais Mteule, Samia Hassan Suluhu.
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva (kulia), akimkabidhi cheti cha Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu katika hafla hiyo.
 Rais Mteule wa Tanzania, Dk. John Magufuli (kulia), akiwapungia mkono wananchi wakati wa hafla hiyo ya kukabidhiwa cheti cha urais. Kutoka  kushoto ni mgombea urais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira na mgombea nafasi hiyo kupitia Chama cha ADC, Chief Lutalosa Yemba.
 Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi (kushoto), akimpongeza Rais Mteule wa Tanzania Dk. John Magufuli baada ya kuchaguliwa kuwa rais.
 Makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakishangilia wakati Rais Mteule wa Tanzania Dk.John Magufuli alipokuwa akitoka Ukumbi wa Diamond Jubilee kukabidhiwa cheti cha urais.
 Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye hafla hiyo.
  Rais Mteule wa Tanzania, Dk.Magufuli akimuonesha Rais Jakaya Kikwete cheti cha ushindi.
 Rais Mteule wa Tanzania, Dk.Makufuli akiwa katika picha ya pamoja na wagombea urais wenzake wa vyama vingine.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimpongeza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva kwa kusimamia vizuri uchaguzi mkuu wa 2015.
Rais Jakaya Kikwete na Rais Mteule Dk.John Pombe Magufuli wakiwa katika picha ya pamoja na wake zao kwenye hafla hiyo.

Magufuli akabidhiwa Hati ya Ushindi Nafasi ya Urais

Rais mteule wa Tanzania John Pombe Magufuli akionesha cheti chake cha ushindi alichokabidhiwa muda huu katika ukumbi wa Diamond Jubilee



Na Anitha Jonas na Beatrice Lyimo- MAELEZO.
 
Watanzania wametakiwa kukubaliana na matokeo ya  Uchaguzi Mkuu  wa mwaka 2015, yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) kwa kuwa  ni ya haki na hakuna aliyeibiwa kura.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Waangalizi wa Uchaguzi kutoka nchi za Jumuiya ya Madola nchini na ambaye Rais Mstaafu wa Nigeria, Goodlucky Jonathan kwenye halfa ya kumkabidhi hati Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) iliyofanyika  leo kwenye ukumbi wa Diamond  Jubilee  jijini Dar es salaam.

“Uchaguzi ulikuwa wa haki na amani na hakuna yeyote aliyeibiwa haki yake kwani matokeo hayo yamedhibitishwa kuwa ya uhuru na haki kwa kufuata misingi ya sheria na taratibu zilizopo” alisema  Rais Mstaafu Jonathan.

Kwa upande wa mgombea urais kupitia chama cha ACT wazalendo Bibi. Anna Mghwira amesema kuwa chama chake kimemkubali matokeo ya uchaguzi uliompitisha Dkt. John Magufuli.

Vilevile ameongeza kuwa wagombea wote walizungumza kuhusu mabadiliko hivyo ana imani na mshindi wa nafasi hii atalisimamia ipasavyo.

“Watanzania wanahitaji mabadiliko hasa katika Katiba Mpya itakayotokana na maoni ya Watanzania, kuimarisha umoja wa kimataifa, kuinua uchumi wa nchi, kusimamia shughuli za Serikali pamoja na kuboresha usawa wa kijinsia kati ya mwanamke na mwanamume,” aliongeza Bibi Mghwira.

Mbali na hayo mgombea huyo wa urais kupitia chama cha ACT wazalendo amemkabidhi Rais Mteule Ilani ya chama hicho kama muongozo kwa yale yaliyopungua katika Ilani ya cha chake.

Aidha Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) Jaji Mstaafu Damian Lubuva amewapongeza wananchi kwa kuwa na mwamko mkubwa wa kupiga kura na kuliendesha zoezi hilo kwa amani.

Pia Jaji Mstaafu Lubuva alimkabidhi hati ya ushindi mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi.

KIKWETE AMPONGEZA DK MAGUFULI KWA KUCHAGULIWA RAIS WA AWAMU YA TANO WA TANZANIA



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza kwa furaha mshindi wa kinyang'anyiro cha Urais kwa tiketi ya CCM na Rais Mteule Dkt John Pombe Joseph Magufuli mara baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva kutangaza kutangaza rasmi matokeo ya uchaguzi mkuu Ikulu jijini Dar es salaam ambako walifuatilia kwa pamoja matangazo hayo ya moja kwa moja kupitia vituo vya televisheni jioni hii Oktoba 29, 2015

Rais Kikwete akimsomea Magufuli sms za pongezi kutoka kila pembe ya dunia.

Mkono wa Pongezi kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete.

Dk John Pombe Magufuli akipokea simu moja wapo za pongezi kutoka kwa Mgombea wa ACT Wazalendo, Anna Mgwira.

Mazungumzo na vicheko vya furaha vikiendelea
 
Blogger Templates