Pages

Ads 468x60px

Friday, December 11, 2015

Mawaziri wa Rais MAGUFULI walivyojadiliwa na UVCCM leo, kuna msisitizo wa haya mawili..


Jana Rais wa Tanzania John Magufuli alitangaza Baraza jipya la Mawaziri, likiwa na jumla ya Wizara 18 pamoja na Mawaziri 19.
Wadau wengi nchini wametoa maoni yao kuhusu uteuzi huo wakiwemo Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM.
Katika maoni yao UVCCM kupitia kwa Katibu wa Idara ya Uhamasishaji Egla Obed wamempongeza Rais kwa uteuzi mahiri na makini wa Baraza hilo ambalo ni dogo lakini limekamilika katika kuhakikisha linagusa kila sekta na kuhakikisha linapunguza na kubana matumizi yasiyo ya lazima.
Kuhusu uteuzi wa Mawaziri wengi vijana, UVCCM amesema haya >>> “Tumeridhishwa na uteuzi huu ambao umesheheni mawaziri na Manaibu wenye uwezo na weledi mkubwa sana, hatuna mashaka kwamba watafanya kazi kwa kasi na uzalendo, tumefarijika zaidi kwa kuwa lina vijana wengi ambao ni nguvu kazi ya Taifa, tunaiona dhamira ya dhati ya Rais kuhakikisha Tanzania inapata mabadiliko ya haraka” >>> Egla Obed.
Na kuhusu  ishu kazi na kasi ya Rais Magufuli je? Majibu yao ni haya >>Serikali itimize wajibu wake wa kuhakikisha inawawezesha wananchi kiuchumi na Mawaziri wana kazi kubwa ya kuhakikisha wanaendeleza mapambano ya kubana matumizi yasiyo ya lazima ili fedha zielekezwe kwenye kuboresha huduma za kijamii, Watanzania hatatuwaelewa Mawaziri wetu kama hawatofuata maagizo ya Chama yaliyoanza kutekelezwa kwa kasi na Rais” >>> Egla Obed.

WASANII WA KIKE WAASWA KUFANYA KAZI KWA BIDII


Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Leah Kihimbi akitoa hotuba katika Warsha ya siku mbili kuhusu wasanii wanawake kupinga ukatili wa kijinsia, mafunzo hayo yamefanyika ili kuhitimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia na kusheherekea siku ya msanii Tanzania iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Rais wa Shirikisho la Sanaa za Maonyesho Tanzania Agnes Lukanga akitoa mada katika warsha ya siku mbili kuhusu wasanii wanawake kupinga ukatili wa kijinsia, mafunzo hayo yamefanyika ili kuhitimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia na kusheherekea siku ya msanii Tanzania iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.

WATUHUMIWA 40 WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA UKWEPAJI KODI.

JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linawashikilia watuhumiwa 40 ambao wanahojiwa kwa tuhuma za kula njama na kuikosesha serikali mapato. Uchunguzi unafanywa kwa pamoja na maafisa wa Jeshi la Polisi na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kwa lengo la kubaini jinsi ambavyo makontena 329 na mengine 2489 yalivyotolewa bandarini kinyume cha taratibu.

Kati ya hao, watuhumiwa 26 ni watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)na watumishi 03 kutoka Bandari kavu (ICD) YA AZAM wanatuhumiwa kuhusika na upotevu wa makontena 329. Aidha, watuhumiwa 11 ambao ni watumishi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)  kwa kuhusika na upotevu wa makontena 2489.

Uchunguzi unaoendelea pia unahusisha kupitia kumbukumbu mbalimbali na kadhia za forodha ili kubaini mtindo uliotumika na kuwabaini wote waliohusika katika mchakato huo. Makontena 329 yaligundulika kukosekana kwenye ICD ya AZAM kuanzia mwezi Julai hadi Novemba 2015, wakati  makontena  2489 yaligundulika kutolewa Bandarini kuanzia Mwezi Machi mpaka Septemba, Mwaka 2014   kinyume cha taratibu kwa lengo la kukwepa kodi na ushuru. 

Uchunguzi bado unaendelea ili kuwabaini wote wanaohusika na hatimaye majalada ya kesi yatapelekwa kwa mwanasheria wa serikali ili watuhumiwa watakaobainika kuhusika na makosa mbalimbali wafikishwe mahakamani.
Kamanda wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na watuhumiwa 40 washikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum kwa tuhuma za ukwepaji kulipa kodi pamoja na mtu mmoja ambaye anatafutwa na Jeshi la Polisi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya REGIONAL CARGO SERVICES LTD,ABDULKADIR S/O KASSIM ABDI, Miaka 38, Mkazi wa Temeke Mikoroshini.
Kamanda wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova akionyesha picha ya Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya REGIONAL CARGO SERVICES LTD,ABDULKADIR S/O KASSIM ABDI, Miaka 38, Mkazi wa Temeke Mikoroshini ambaye anatuhumiwa kwa kutoa makontena 329 kwenye bandari kavu ya AZAM (AZAM ICD) bila kulipia kodi anayetafutwa na jeshi hilo pia ni mmoja wa wakurugenzi wa kampuni za “JAS EXPRESS FREIGHT LTD” na “XL CLEARING AND FOWARDING Co. LTD” ambazo zote zilitumika kutoa makontena hayo. Ameonyesha picha ya mtuhumiwa huyo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Meneja wa Huduma na elimu kwa mlipa kodi kutoka wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Diana Masalla akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Kukusanya jumla ya shilingi 10,075,979,462.08 kutoka kwa makampuni 22 ambayo yalihusika na uondoshwaji wa makontena bandarini kinyume cha sheria na taratibu za forodha hadi kufikia tarehe 10 Desemba 2015. 

Pia kati ya hao makampuni 06 amesema kuwa yamelipa kodi yote iliyokadiriwa pamoja na adhabu, ambapo makampuni 16 yamelipa sehemu ya kodi iliyokadiriwa pamoja na adhabu. 

Aidha, makampuni 26 hayajalipa kodi kiasi cha shilingi 4,789,924,609.69 pamoja na kwamba zoezi la ukadiriaji limefanyika. 

hata hivyo amesema kuwa leo ni siku ya mwisho iliyotolewa na Mheshimiwa Rais kwa wafanyabiashara waliokwepakulipa kodi ya makontena,

Amewasisitiza wananchi wote watoe taarifa kuhusu vitendo vya ukwepaji kodi kutumia namba 0784210209. Pia taarifa za mwenendo wa wafanyakazi wa TRA Wasio waadilifu zitolewe kupitia simu namba 0689 122515 na ujumbe mfupi 0689 122516.
Baadhi ya Waandishi wa habari waliohudhulia katika mkutano na Kamanda wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova wakimsikiliza leo jijini Dar es Salaam.

AIRTEL YAENDELEA KUFUNGUA FURSA KWA VIJANA HAPA NCHINI

Katika kupambana na wimbi la kupunguza umaskini hapa nchini, kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania kupitia mpango wake wa “Airtel FURSA Tunakuwezesha” unaendelea kutoa mafunzo ya biashara ya ujasiriamali kwa vijana wenye lengo la kuwawezesha na kuwainua vijana hapa nchini .

Mafunzo hayo ya biashara ambayo yamekuwa yakiendeshwa hapa nchini katika mikoa mbali mbali , wiki ijayo yatafanyika Dar Live  Mbagala Kuu karibu na Big Bon  siku ya Jumanne tarehe 15 ili kuwawezesha vijana kuweza kukabiliana na wimbi hili gumu la kuendesha biashara na kuweza kukidhi mahitaji yao ya kila siku na kuweza kuinua uchumi wa nchi hii.

Akizungumzia kuhusu mafunzo hayo ambayo yamekuwa yakiendelea hapa nchini, Meneja huduma kwa jamii  wa Airtel , bi Hwa Bayumi, alisema “mafunzo haya yanalengo la kuwasaidia vijana wenye umri kati ya miaka 18- 24 ambao wanakiu ya kujikwamua na umasikini. Vile vile “Airtel FURSA Tunakuwezesha” Airtel inawawezesha vijana kwa kuwapatia elimu ya biashara na nyenzo za kuimarisha biashara zao.

Hivyo basi tunapenda kuwakaribisha vijana wote waishio jijini Dar Es Salaam kuweza kuhudhuria mafunzo haya ambayo yatatolewa bure kabisa bila gharama yoyote. Ili kijana aweze kushiriki  anatakiwa kufika pale Dar Live siku ya jumanne tarehe 15 kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi jioni.

Vile vile ili kijana kushiriki au kufaidika na mpango wa Airtel Fursa atatakiwa kutuma ujumbe mfupi kwenda kwa namba 15626 na kuweka maelezo yafuatayo:- Jina, Umri, aina ya biashara na eneo. 

Pia wanaweza kutuma maombi yao kwa kupitia barua pepe airtelfursa@tz.airtel.com ambapo watatakiwa kutuma jina kamili, umri, na aina ya biashara. Maelezo kuhusu program ya Airtel FURSA pia yanapatikana kwenye tovuti ya Airtel www.airteltanzania.com> aliongeza, Bayumi.

MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA MABALOZI WA NORWAY NA MALAWI

 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Hanne-Marie Kaarstad, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Dec 11, 2015 kwa mazungumzo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Mhe. Hawa Ndilowe, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, jana Dec 10, 2015 kwa mazungumzo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan, akiagana na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Hanne-Marie Kaarstad, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Mhe Makamu, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Dec 11, 2015.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Mhe. Hawa Ndilowe baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam,jana Dec 10, 2015. Picha na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Hanne-Marie Kaarstad (kulia kwake) na Mkurugenzi  wa Idara ya Ulaya na Marekani, Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine (kulia) na Msaidizi wa Balozi (kushoto) mara baada ya mazungumzo ao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo Desemba 11, 2015.
MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA MABALOZI WA NORWAY NA MALAWI
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jana amekutana na Balozi wa Malawi nchini Tanzania na kufanya naye mazungumzo yaliyolenga kukuza uhusiano wa nchi hizi mbili, sambamba na kuongeza tija ya maendeleo huku wakifahamishana nia ya kuwa na miradi ya pamoja itakayolenga kuongeza uhusiano wa pamoja na kupunguza changamoto zinazozikabili nchi hizi.
Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Makamu wa Rais leo Desemba 11, 2015 amekutana na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mheshimiwa Hanne-Marie Kaarstad ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo walizungumzia kuhusu uongezaji wa mahusiani na ushirikiano hasa katika suala la mazingira. Balozi Kaarstad ni mpya nchini Tanzania na ujio wake ameelezea kuwa unalenga katika kuongeza tija kwa nchi hizi mbili na kwamba Norway itabakia kuwa rafiki wa karibu wa Tanzania.
Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
Ikulu, Dar es Salaam

JIJI LA MBEYA LAPATA MEYA MPYA DAVID MWASILINDI (CHADEMA) DIWANI KATA YA NZOVWE



Meya Mteule wa jiji la Mbeya Diwani wa Kata ya Nzovwe(CHADEMA) Ndugu David Mwasilindi ambaye aliibuka kidedea kwa kupata kura 34 dhidi ya Mpinzani wake wa CCM aliyepata kura 14 katika uchaguzi uliofanyika Desemba 10 katika ukumbi wa Mkapa jijini humo.
Katibu Tawala Wilaya ya Mbeya Ndugu Quip Mbeyela ambaye ndiye aliyekuwa Mwenyekiti katika Kikao cha Baraza la Madiwani ambacho kiliketi kufanya uchaguzi wa kumpata Meya wa jiji hilo pamoja na Naibu Meya katika Halmashauri ya jiji la Mbeya .

Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya jiji la Mbeya Dkt Samuel Lazaro akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani ambalo liliketi kwa ajili ya kumchagua Meya pamoja na Naibu Meya katika Ukumbi wa Mkapa jijini humo.

Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Jiji la Mbeya Dkt Samuel Lazaro akiteta jambo na Meya Mteule wa jiji la Mbeya Mh.David Mwasilindi katika kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya jiji hilo.

Wajumbe wa baraza la Madiwani Halmashauri ya jiji la Mbeya wakifuatilia kwa umakini majadiliano katika mkutano huo.


Baadhi ya watumishi wa jiji la Mbeya wakiteta jambo katika mkutano huo wa baraza la Madiwani la Halmashauri ya jiji la Mbeya ambalo liliketi na kumchagua Meya na Naibu wa jiji hilo ambaye ni David Mwasilindi (CDM) baada ya kupata kura 34 dhidi ya mpinzani wake wa CCM aliyepata kura 14.

Diwani akizungumza katika baraza hilo.

Madiwani wakiimba wimbo wa taifa baada ya kukamiliza zoezi la uchaguzi katika baraza hilo la Madiwani halmashauri ya jiji la Mbeya .



Baadhi ya wananchi na wafuasi wa vyama mbalimbali jijini mbeya wakifuatilia kwa umakini uchaguzi wa kumpata Meya wa jiji la Mbeya na Naibu Meya wakiwa nje ya ukumbi wa Mkapa jijini humo .



Tukifuatilia Mkutano .


Na EmanuelMadafa,Mbeya
Hatimaye Halmashauri ya jiji la Mbeya limepata Meya wake mara baada
ya kufanyika kwa uchaguzi wa kugombea
nafasi ya Meya na Naibu Meya watakaoongoza halmashauri ya jiji la Mbeya katika
kipindi cha miaka mitano ijayo.

Meya huyo mpya wa jiji la mbeya ametokana na Chama cha Chadema Mch
David Ponela Mwashilindi kutoka kata ya Nzovwe pamoja na Naibu wake Mch David Nelson Ngogo kutoka kata
ya Nsalaga ambao wote wametokana na chama hicho.

Katika uchaguzi huo uliofanyika Desemba 10 kwenye ukumbi wa Mkapa na kusimamiwa na Katibu
tawala wa wilaya ya Mbeya Quip Mbeyela,alimtangaza mshindi wa Umeya kuwa ni
Mwashilindi aliyepata kura 34 akimshinda mgombea wa nafasi hiyo kutoka
CCM,Kefas Mwasote Changani aliyeambulia kura 14.

Kwa upande wa nafasi ya Naibu Mbeya mshindi wa kura nyingi
aliyetangazwa ni Mch Ngogo(Chadema) aliyeipata kura 34 dhidi ya mgombea wa CCM
katika kinyang’anyiro hicho,Modest Pantaleo Shiyo aliyeambulia kura 14 na hivyo
kukifanya chama cha Chadema kuongoza halmashauri ya jiji hilo.

Mara baada ya kutangaza matokeo hayo yaliyowashirikisha madiwani
wa Chadema 34 dhidi ya wale wa CCM 14,msimamizi wa uchaguzi huo,Mbeyela alisema
kuwa vyama vyote vilivyoshiriki kwenye mchakato huo sasa umekwisha na
wanachotakiwa kukifanya madiwani wote ni kuchapa kazi kwa nguvu ili kusukuma
kwa kasi maendeleo ya jiji hilo.

Akizugumza mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa nafasi ya
Naibu Meya,Ngogo alisema kuwa atahakikisha kuwa anaheshimu haki na uhuru wa
kila diwani katika kushauri na kutoa maoni bila kujali itikadi ya vyama vyao
kwa kuwa kazi kubwa iliyo mbele yao ni kuwatumikia wananchi wote.

Mstahiki Meya wa jiji hilo kutoka Chadema,Mwashilindi akiwashukuru
madiwani wote kwa kura nyingi alizopigiwa,alisema kuwa atahakikisha kuwa
anashirikiana na madiwani wote na kuhakikisha kuwa kata zote za jiji hilo
zinapiga hatua kubwa na huo ndio mtazamo wake.

Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji hilo,Dk Samwel
Lazaro alisema kuwa atahakikisha watendaji wa halmashauri hiyo wanatoa
ushirikiano wa kutosha kwa madiwani wote pale wanapohitaji ufafanuzi wa
kitaalamu ili kila jambo wanalotaka kulifahamu wapate kwa wakati.
 
Blogger Templates