
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Waziri Mkuu wa India Narendra Modi katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi kabla ya kuondoka katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili nchini.

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi akishukuru kabla ya kuondoka baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili nchini.

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi akipungia mkono vikundi vya utamaduni vilivyokuwa vikitoa buradani katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili nchini.

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi akiwa na watoto wa Kitanzania wenye asili ya kihindi kabla ya kuondoka Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi akiwa na watoto wa Kitanzania wenye asili ya kihindi kabla ya kuondoka Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wafanyakazi wa kitengo cha mizigo katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa JINIA jijini Dar es Salaam mara baada ya kumsindikiza mgeni wake Waziri Mkuu wa India Narendra Modi. PICHA NA IKULU
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni
wake Waziri Mkuu wa India Narendra Modi katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Na.
Immaculate Makilika- MAELEZO
Serikali
ya India na Tanzania zimesaini mikataba ya miradi ya maendeleo katika sekta za
maji, kilimo, viwanda, teknolojia ya habari na mawasiliano na afya katika
kuimarisha mahusiano ya nchi hizo mbili ili kusaidia wananchi wake.
Mikataba
hiyo imesainiwa leo, wakati Waziri Mkuu wa India Mhe. Narendra Modi alipokua akifanya
mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mikataba
wa kwanza uliosainiwa inahusisha mradi wa kusambaza maji katika mikoa ya Pwani
na Dar es Salaam.
Aidha,
mkataba wa pili unahusisha mradi wa kusambaza maji Zanzibar ambao unatarajiwa
kugharimu dola za kimarekani milioni 92 ambapo
mradi huo unatarajiwa kufikia miji 17 nchini na mkataba mwingine utahusisha mafunzo
ya ufundi yatakayosaidia kuzalisha wataalamu mbalimbali.
“Lengo
letu ni kusaidiana na kuimarisha
mahusianao yetu katika kukuza uchumi na kutengeneza fursa mpya za ajira kwa
wananchi wetu” alisema Waziri Modi.
Waziri
Modi aliongeza kuwa Serikali ya India itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania
katika masuala mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuongeza wigo wa
biashara na hatimaye kukuza uchumi wa nchi hizo.
Kwa
upande wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli alisema
Serikali India imekua na ushirikiano mzuri na Tanzania hasa katika masuala ya
maendeleo ambapo imeweza kuwekeza nchini kiasi shilingi za Kimarekani dola
bilioni 2.4 na kuzalisha ajira 54,176.
Baadhi
ya misaada iliyotolewa na Serikali ya India ni pamoja na mashine ya vipimo vya ugonjwa wa kansa katika
hospitali ya Bugando, itakayosaidia wakazi wa kanda ya ziwa na nchi nzima kwa
ujumla pamoja na kuongeza na kuimarisha ushirikiano kati ya Shirika la viwanda
vidogo vigodo la India kushirikiana na Tanzania katika kukuza viwanda vidogo na
vya kati nchini.
Katika
masuala ya teknolojia ya habari na mawasiliano, Serikali hiyo imeahidi kuleta
wataalamu wao nchini Tanzania kwa lengo la kutengeneza program mbalimbali ili
kuisaidia Tanzania katika masuala ya ulinzi wa mitandao pamoja na kutengeneza
namna bora za ukusanyaji wa mapato ya nchi.
Katika
masuala ya viwanda, Serikali ya India imeahidi kuanzisha viwanda vya
kutengeneza dawa za binadamu zitakazotibu magonjwa mbalimbali ikiwemo malaria, figo na
kisukari, ikiwa ni pamoja na kutengeneza vifaa tiba vitakavyotumika katika
hospitali mbalimbali nchini kwa lengo la kupunguza gharama ya kununua vifaa
hivyo nje ya nchi.
Aidha,
Rais Magufuli alisema kuwa nchi ya India ina uhitaji mkubwa wa mazao ya kilimo
hasa jamii ya kunde hivyo akawataka wakulima kutumia fursa hiyo kuzalisha mazao
hayo kwa wingi.
“India
inauhitaji wa tani 200 za mazao jamii ya kunde, wakulima mnatakiwa kuzalisha mazao
hayo kwa wingi kwa vile tayari kuna soko la uhakika, na tutahakikisha madalali
hawatakuwepo ili mkulima asikandamizwe” alisema Rais Magufuli.
Katika
sekta ya uwekezaji nchini, India ni nchi ya tatu kwa uwekezaji Tanzania ikifuatiwa
na Uingereza pamoja na China.
0 comments:
Post a Comment