November 6 2015 tayari ninazo zote zilizozinasa kwenye Uchambuzi wa Magazeti Redioni, hizi hapa kwenye nukuu yake pamoja na audio nilizorekodi.
Rais Dk. Magufuli amesema yeye ndiye Rais, akiri uchaguzi ulikuwa mgumu na amejifunza mengi… Changamoto za uongozi wa Dk. Magufuli zatajwa.
Rais JPM ameanza kazi kwa kumteua George Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu Tanzania, Mawaziri Wakuu wa zamani, Edward Lowassa na Frederick Sumaye hawakuhudhuria sherehe za kuapishwa Dk. Magufuli, wapingana na matokeo ya Urais.
Mawaziri na Manaibu waliomaliza muda wao
warudisha ‘MASHANGINGI’ Ikulu ili yatolewe namba na kufanyiwa matumizi
mengine… Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad bado hajarudisha magari ya Serikali japo alisema hadi Novemba 2 2015 Z’bar itakuwa haina Serikali.
JK atoa msamaha kwa wafungwa 4,100 muda mfupi kabla ya kukabidhi madaraka kwa Rais JPM… Majambazi yateka magari Tabora na kupora watu huku wakiimba ‘hapa kazi tu’!!
Aliyekuwa Askari Polisi Oysterbay amehukumiwa kifungo cha miaka 30 kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha…