Pages

Ads 468x60px

Saturday, October 31, 2015

LEMBELI AELEZA HATMA YAKE BAADA YA KUUKOSA UBUNGE, AJIBU TETESI JUU YAKE IKIWEMO YA KUUZA REDIO YAKE


Aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Kahama Mjini, James Lembeli ameelezea kinachoendelea katika maisha yake ya kisiasa hasa baada ya kushindwa katika uchaguzi wa mwaka huu akiwa ndani ya chama chake kipya cha Chadema.

Akiongea katika taarifa rasmi kwa wananchi wa jimbo hilo, Lembeli amesema kuwa hivi sasa atajikita zaidi katika shughuli za chama chake pamoja na shughuli alizokuwa akizifanya kabla ya kuwa mbunge wa jimbo hilo.

Alisema kuwa ataendelea kufanya kazi zake na mashirika ya kimataifa kama mjumbe wa Bodi mbalimbali. Pia, ataendelea kufanya kazi ya kusimamia radio yake (Kahama FM) ambayo amedai kuwa taarifa zilizosambazwa kuwa ameiuza kulipa deni la mkopo aliopewa kuendesha kampeni sio za kweli.

Pia, Lembeli amewashukuru wananchi waliojitokeza kumuunga mkono na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika masuala ya maendeleo na ataendeelea kushirikiana nao kukamilisha miradi mbalimbali aliyokuwa ameanza kuitekeleza kwa juhudi zake binafsi.

Kadhalika, Lembeli amekanusha taarifa zilizokuwa zimesambazwa kuwa alikamatwa na jeshi la polisi mara tu baada ya Jumanne Kishimba wa CCM kutangazwa kuwa mshindi.

Kuhusu afya yake, alisema kuwa yeye ni mzima tofauti na habari zinazoendelea kuenea kuwa ni mgonjwa hasa baada ya kupata ajali ya gari na matokeo kutangazwa.

TAARIFA YA ZADIA KUHUSU KUFUTWA KWA MATOKEO YA UCHAGUZI ZANZIBAR.



Logo ya Zadia
Jumuiya ya Wazanzibari Waishio Nchini Marekani (ZADIA), imekuwa ikifuatilia kwa karibu na makini zaidi zoezi zima la Uchaguzi Mkuu visiwani Zanzibar na Tanzania kwa ujumla. Kwa kiasi kikubwa mchakato wa uchaguzi ulifanyika kwa njia za amani na utulivu.
 Hata hivyo ZADIA imeshtushwa mno na tamko la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Mh. Jecha Salim Jecha la kutangaza kuufuta Uchaguzi Mkuu Zanzibar na matokeo yake.
Ama kwa hakika kitendo hicho hakikuwa cha busara na kinapelekea kurudisha nyuma maendeleao ya demokrasia Zanzibar, na vilevile hakiashirii mustakbali mwema kwa nchi yetu tuipendayo. 
Wazanzibari wameelezea maoni na matakwa yao kwenye visanduku vya kupigia kura, na maoni na matakwa yao hayo yanapaswa kusikilizwa na kuheshimiwa.
Kwa hivyo, ZADIA inatoa wito kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar, kumalizia mchakato mzima wa kuhesabu kura kwa majimbo yaliyobakia na kutoa matokeo ya mwisho ya Uchaguzi na kumtangaza mshindi ili kuiepusha Zanzibar yetu tuipendayo kuingia katika hali ya mtafaruku na mifarakano isiyokuwa na tija bali kuleta hasara.
ZADIA pia inaungana na jumuiya zote za kimataifa ambazo zimetoa msimamo wao juu ya uchaguzi wa Zanzibar, hasa ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, ambao ni kiungo madhubuti kati ya Wazanzibari walioko Zanzibar na wenzao wanaoishi nchini Marekani.
Aidha, tunapenda kumkumbusha Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Dakta Ali Mohammed Shein kuwa Wazanzibari walimpa amana kubwa ya kuwaongoza, na kwa hivyo ni wajibu wake kuienzi amana hiyo kwa kuchukuwa hatua za kiungwana za kuitoa Zanzibar kwenye mgando huu wa kisiasa. Hali hii iliyopo sasa inaleta wasiwasi miongoni mwa raia na imekua ikiathiri maisha yao ya kila siku, na ikiachwa kuendelea huenda ikaathiri pia mustakbali maisha yao kwa jumla.
ZADIA pia inamtolea wito Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kutumia mamlaka yake aliyonayo kuhakikisha Zanzibar inatoka kwenye mkwamo huu wa kisiasa na kwamba anaondoka madarakani akiiacha Zanzibar ikiwa katika hali ya amani na utulivu. Kwa kufanya hivyo atauthibitishia ulimwengu kuwa kweli Tanzania ni kisima cha amani.
Na mwisho tunawaomba Wazanzibari, wapenzi wa Zanzibar, na Watanzania wote kwa ujumla popote pale walipo, wajitahidi kufanya mawasiliano na Jumuiya nyengine za Kimataifa ili ziingilie kati suala hili kabla nchi yetu haijaingia kwenye mtafaruku mkubwa wa kisiasa na kijamii na hata kupelekea kuhatarisha amani ya nchi yetu.
Mungu Ibariki, Zanzibar.

RAIS DK.JAKAYA KIKWETE AZINDUA KAMPUNI YA SOKO LA BIDHAA KUSAIDIA WAKULIMA NCHINI

02
Rais Dk.Jakaya Kikiwete akizundua kampuni ya Soko la Bidhaa  katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Serena jijini Dar es Salaam.
05 
Rais Dk.Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti na Bodi ya Kampuni ya Soko la Bidhaa wakati wa uzinduzi wa kampuni hiyo leo jijini Dar es Salaam.
01
Rais Dk.Jakaya Kikwete akizungumza wakati uzinduzi wa Kampuni ya Soko la Bidhaa iliyofanyika katikza ukumbi wa Serena jijini Dar es Salaam Oktoba 30, 2015.
03
Waziri wa Fedha na Uchumi,Saada Mkuya akizungumza na wakati uzinduzi wa kampuni ya Soko la bidhaa  jijini Dar es Salaam.
04
Sehemu wataalam mbalimbali wakiwa wamekekti katika uzinduzi wa Kampuni ya Soko la Bidhaa  jijini Dar es Salaam.



Rais Dk.Jakaya Kikwete amesema kuanza kwa kampuni ya soko la bidhaa kutasaidia wakulima kupata soko la uhakika na kukuza uchumi pamoja na kupata bima katika kilimo.
  Hayo ameyasema leo wakati uzinduzi wa Kampuni ya soko la bidhaa jijini Dar es Salaam,Dk.Kikwete amesema wakulima wamekuwa wakilima lakini masoko yao hayana uhakika na kilimo hakina tija.
  Amesema kuwa mfumo utasaidia wakulima kupata bei ya uhakika wa kuuza mazao yao na wanunuzi kufahamu bei ya soko la bidhaa wanayoihitaji. Dk.Kikwete ameitaka watu wanaofanya kazi kuwa waaminifu katika kuweza kuwafanya wakulima wanufaike na soko hilo kwa kuwaletea maendeleo ya kuendeleza na kuachana na kutafuta masoko ambayo mwisho wa siku wanauza kwa hasara.
  Aidha amesema soko la bidhaa litawaondolea wakulima ukopwaji ambao umekuwa ukiwakatisha tamaa na kushindwa kuendeleza kilimo chenye tija. Amesema wakulima wamekuwa wakifanya kazi zao za kilimo wakiwa na changamoto kubwa ya kukosa soko la uhakika na kufanya mazao kununuliwa na watu wachache kwa bei ya chini.
  Dk.Kikwete amesema wakulima wakiwa wana soko la uhakika kutafanya waweze kuingia katika bima kutokana na kilimo kuonyesha mwanga katika sekta hiyo.Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Soko la Bidhaa (TMX),Nasama Masinda amesema kuwa soko hilo wataanzia mazao ya Ufuta,Korosho pamoja na mpunga .
  Amesema wamejipanga katika kuhakikisha wanaweka uwazi wa soko katika bidhaa hizo kwa wanunuzi na wauzaji kuwa na bei inayoendana na soko.

MAGUFULI AWASHUKURU WAPIGA KURA


 Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wapenzi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi waliojitokeza kwa wingi kwenye hafla fupi ya kumpongeza Dk. John Pombe Magufuli kwa ushindi alioupata katika uchaguzi wa uliofanyika oktoba 25 mwaka 2015. 
 Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete (kulia)akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahma Kinana(katikati) pamoja na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda wakati wa sherehe ndogo ya kushukuru wapiga kura walioipa CCM ushindi.
 Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli akiwashukuru wananchi wote waliompigia kura kwenye uchaguzi wa Rais uliofanyika tarehe 25, oktoba ambapo aliibuka mshindi katika uchaguzi huo.
 Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli akiwashukuru wananchi wote
waliompigia kura kwenye uchaguzi wa Rais uliofanyika tarehe 25, oktoba
ambapo aliibuka mshindi katika uchaguzi huo.
 Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo kwa  wananchi waliojitokeza kumpongeza nje ya Makao Makuu ya CCM Ofisi Ndogo Lumumba.
Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli akionyesha cheti alichokabidhiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi mara baada ya kushinda kiti cha Urais kwenye uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba mwaka 2015.
 Mama Samia Suluhu aliyekuwa Mgombea Mwenza akionyesha cheti chake cha Umakamu wa Rais kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliokuja kumpongeza.
 Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli akimtambulisha mke wake Janeth Magufuli mbele ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliokuja kumpongeza.
 Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Rais mteule wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza kwenye hafla hiyo ya kumpongeza Dk. John Pombe Magufuli nje ya Ofisi Ndogo CCM Lumumba.
 Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli akiwaaga wakazi wa jiji la Dar es Salaam mara baada ya kumalizika hafla ya kuwasalimu na kuwashukuru kwa kumpigia kura zilizompa ushindi wa kiti cha Urais.
Wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwa wingi kumpongeza Dk. John Pombe Magufuli nje ya ofisi ndogo CCM Lumumba.

KIWIA AKANUSHA KUZIMIA BAADA YA MATOKEO KUTANGAZWA. ASEMA ANATARAJIA KUFUNGUA KESI MAHAKAMANI KWANI BADO HAJASAINI MATOKEO.


Highness Kiwia akionyesha moja ya karatasi yenye makosa
Aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza na Mgombea wa nafasi hiyo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema chini ya mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi Ukawa Highness Kiwia, anatarajia kufungua kesia ya kupinga matokeo ya uchaguzi jimboni humo kwa madai kwamba haukuwa wa huru na haki kutokana na kugubikwa na changamoto mbalimbali.

Kiwia ambae ameshindwa kutetea jimbo hilo baada kuchukuliwa na Angelina Mabula kutoka Chama cha Mapinduzi CCM, aliyasema hayo jana wakati akizungumza na wanahabari kuhusiana na Uchaguzi huo.

Alieleza kuwa katika vituo mbalimbali jimboni humo kulikuwa na makosa mengi ambayo ni pamoja na uwepo wa vituo hewa, idadi ya wapiga kura kutofautiana na idadi ya waliojiandikisha katika daftari la kupigia kura pamoja na majina ya wapiga kura kukutwa katika majimbo tofauti na yale waliyojiandikishia.

Katika hatua nyingine Kiwia alikanusha taarifa kuwa alimtuma mwakilishi kwa ajili ya kusaini fomu ya matokeo kwa niaba yake na kwamba siku ya kutangaza matokeo alishindwa kupokea matokeo hayo na hivyo kuzilai.

Kwa upande wake Tungaraza Njugu ambae ni Kiongozi wa Kanda ya Ziwa Victoria Chadema, alisema kuwa zoezi la uchaguzi mwaka huu linapaswa kulaaniwa kwa kuwa halikuendeshwa kidemokrasia kutokana na kukiuka taratibu mbalimbali za uchaguzi.

Katika Matokeo ya Kiti cha Ubunge Jimboni Ilemela, Mgombea wa CCM Angelina Mabula aliibuka mshindi baada ya kupata kura 85,424 na kufuatiwa na mgombea wa Chadema Highness Kiwia aliepata kura 61,679 ambapo kwa upande wa Madiwani CCM ilishinda Kata 16 huku Kata Tatu zikichukuliwa na upinzani.
Aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza na Mgombea wa nafasi hiyo kupitia Chadema
Aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza na Mgombea wa nafasi hiyo kupitia Chadema akiongea na wanahabari
 
Blogger Templates