Pages

Ads 468x60px

Monday, January 4, 2016

WAZIRI WA AFYA UMMY MWALIMU AKAGUA KAMBI YA KIPINDUPINDU YA NYANKUMBU MKOANI GEITA


Wananchi wa Mkoa wa Geita wameaswa kufuata kanuni za usafi wa mazingira ili kudhibiti maumbukizi ya ugonjwa wa kipindupindu,Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu mara baada ya kutembelea kambi ya kipindupindu iliyopo kwenye kituo cha afya cha Nyankumbu,mkoani hapamli1
Waziri Ummy akivaa vifaa maalum vya kujikinga na kipindupindu kabla ya kuingia kwenye kambi hiyo,kulia ni Mganga mfawidhi wa Kituo hicho Josephat Msafiri.(Picha Zote na Catherine Sungura WAMJW-GEITA)
mli2 
  Waziri Ummy akivua vifaa hivyo mara baada ya kutoka kuwasalimia wagonjwa wa kipindupindu waliolazwa kwenye kambi hiyo,wagonjwa waliopo hadi leo mchana ni wagonjwa wanne mli3 
  Waziri huyo akiongea na mmoja wa wagonjwa wa kipindupindu waliolazwa kwenye kambi hiyo mli4 
  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwasalimia wagonjwa wa kipindupindu(hawapo pichani)kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita Dkt.Joseph Kisala mli5 
  Baadhi ya wagonjwa wa kipindupindu waliolazwa kwenye kambi ya kituo cha afya cha Nyankumbu

Mengine kutoka Hospitali ya Muhimbili kuhusu mashine za CT Scan..


Agizo la Rais Magufuli la kupatikana kwa mashine mpya ya CT Scan katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili limeonekana kuzaa matunda baada ya Serikali kununua mashine mpya ambayo imegharimu dola za Kimarekani milioni 1.7.
Kutokana na mashine ya awali kuhabikika kila wakati Serikali imegharamia mashine mpya ambayo imeelezwa kuwa na uwezo mkubwa wa kufanya kazi tofauti na nyingine zilizowahi kutumiwa na hospitali hiyo.
Neema Mwangoko ambaye ni afisa Uhusiano wa hospitali hiyo amesema mashine hiyo mpya ina siku tatu tangu ifungwe na tayari imehudumia wagonjwa 26 mpaka sasa na bado ipo kwenye majaribio.
Naibu waziri wa afya Dk.Hamis Kigwangala ambaye alifanya ziara katika hospitali hiyo amepongeza hatua hiyo na kutaka watendaji waboreshe huduma zinazotolewa na hospitali hiyo kwa wateja wake.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATEMBELEA NFRA NA UJENZI WA OFISI YA MKURUGENZI PERAMIHO


 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mahindi yaliyohifadhiwa nje ya majengo ya maghala ya  Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA mjini Songea  akiwa katika ziara ya siku tatu mkoani Ruvuma Januari 4, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri  Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mahindi yaliyohifadhiwa nje ya majengo ya maghala ya  Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA mjini Songea  akiwa katika ziara ya siku tatu mkoani Ruvuma Januari 4, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri  Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mahindi yaliyohifadhiwa nje ya majengo ya maghala ya  Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA mjini Songea  akiwa katika ziara ya siku tatu mkoani Ruvuma Januari 4, 2016.  
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Jego la Halmashauri ya Wilaya ya Peramiho akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Januari 4, 2015.  
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Maposele wilayani  Peramiho baada ya kukagua ujenzi wa  jingo la Ofisi ya Mkurugenzi wa wilaya hiyo akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma  Januari 4, 2016. (PIcha na Ofisi a Waziri Mkuu
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungungua tawi la Benki ya Posta la Songea akiwa katika ziara ya mkoa wa  Ruvuma Januari 4, 2016. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Uratibu, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama .
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akitazama kadi ya akaunti yake ya Benki ya Posta Tanzania aliyokabidhiwa  baada ya kuifungua alipokuwa akifungua tawi la Benki hiyo la Songea Januari 4, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassi Majaliwa akiagana na watuMishi wa Benki ya Posta, Tawi la Songea baada ya kufungua tawi lao Januari 4, 2016. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Rukwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
(Picha na Ofisi ya Waziri  Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akivalishwa vazi la jadi la  Wangoni baada ya kuwasili kwenye   kwenye kijiji cha Maposele  na kukagua ujenzi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Peramiho Januari 4, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikabidhiwa  ngao silaha  na mzee Daniel Gama  baada ya kuwasili kwenye kijiji cha Maposele  na kukagua ujenzi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Peramiho Januari 4, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikabidhiwa silaha za jadi na mzee Daniel Gama  baada ya kuwasili kwenye kijiji cha Maposele  na kukagua ujenzi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Peramiho Januari 4, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama ngoma ya mila ya kabila la Wangoni wakati alipowasili    kwenye kijiji cha Maposele  na kukagua ujenzi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Peramiho Januari 4, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAKAMU WA RAIS MHE SAMIA AWASILI MKOANI GEITA KUANZA ZIARA LEO


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa Geita Mhe. Fatma Mwassa alipowasili Uwanja wa Ndege wa GGM Geita leo Januari 04,2016 kwa ajili ya kuanza ziara ya siku mbili  ya kukagua  na kuzindua miradi ya maendeleo Mkoani humo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na akina mama wa UWT Geita alipowasili Uwanja wa ndege wa GGM Geita Leo Januari 04, 2016 kwa ajili ya kuanza ziara ya siku mbili ya kukagua na kuzindua mirdeleo Mkoani humo
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na baadhi ya wawekezaji wa Mgodi wa GGM Mkoani  Geita alipowasili Uwanja wa ndege wa GGM Geita Leo Januari 04, 2016 kwa ajili ya kuanza ziara ya siku mbili ya kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo Mkoani

Matatu kutoka Ikulu kwa Rais Magufuli leo January 4…



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli leo amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wanne Ikulu, Dar es salaam.
Taarifa kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa alisema Rais Magufuli alikuwa na na mazungumzo na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Juma Assad kuhusu kupunguza gharama za matumizi ya kuendesha serikali na kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
CAG
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Prof. Mussa Juma Assad akizungumza na Rais Magufuli.
Prof. Assad ameagizwa pia na Rais Magufuli kuhakikisha Tanzania inaongeza ukusanyaji wa mapato kutoka 14% ya pato la Taifa.
Rais Magufuli pia amekutana na Mkurugenzi wa Mashitaka Tanzania, (DPP) Biswalo Eutropius Mganga ambaye amesema mazungumzo yao yalihusiana na mikakati ya namna ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka inavyopaswa kufanya kazi ili kuendana na kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano isemayo “Hapa Kazi Tu”.
DPP
Rais Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi wa mashtaka Bw. Biswalo Eutropius Mganga
Kiongozi Mwingine aliyekutana na Rais Magufuli ni Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuber Ally ambaye amempongeza Rais Magufuli kwa kazi nzuri.
SHEH2
Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zuber Ally akizungumza na Rais leo Ikulu
 
Blogger Templates