Mgombea wa urais
kupitia tiketi ya chama cha CHADEMA Edward LOwassa amesema kuwa
hatokubali matokeo ya uchaguzi wa urais yanayoendelea kutolewa na tume
ya uchaguzi nchini Tanzania NEC.
Amesema kuwa ana ushahidi wa kutosha kwamba kuna udanganyifu uliofanyika.Amesema kuwa kura za chama hicho zimepunguzwa katika vituo vingi vya kupigia kura.
Wanadai kwamba kura zilizohesabiwa katika maeneo tofauti haziambatani na matokeo yaliotolewa.
Lowassa ameongezea kwamba maeneo yote ambayo walipata ushindi yamecheleweshwa huku kukamatwa kwa maajenti wa chama hicho akidai kuwa ni ishara za kutaka kuiba kura.
0 comments:
Post a Comment