Pages

Ads 468x60px

Tuesday, October 27, 2015

WALIOSAMBAZA MATOKEO YA URAIS KINYUME CHA SHERIA WAPANDISHWA KIZIMBANI MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR ES SALAAM



Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe (katikati), akizungumza na mmoja kati ya vijana nane waliofikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam leo, kwa tuhuma za kusambaza matokeo ya kura za mgombea nafasi ya urais wa chama hicho katika mitandao ya kijamii kinyume na utaratibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Imedaiwa vijana zaidi ya 190 walikamatwa kwa kosa hilo.
 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama ya Kisutu Dar es Salaam leo.
Askari wa FFU wakiimarisha ulinzi mahakamani hapo.
Wafuasi wa Chadema wakionesha alama ya vidole viwili wanayoitumia.

Viongozi wa Chadema wakitoka katika mahakama hiyo baada ya kusikiliza kesi hiyo. 
Vijana waliokamatwa wakiwa katika mahakama hiyo.



Na Dotto Mwaibale
WATU wanane akiwemo Raia mmoja wa Korea na raia mmoja wa Kenya wamepandishwa kizimbani kwa kusambaza taarifa za matokeo ya urais katika Mtandao wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi yakiwa na kichwa 'M4C election result management system' bila kuthibitishwa kwa lengo la kupotosha umma. 

Sanjari na hilo, Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), amewasilisha mahakamani hati ya kuzuia dhamana ya washtakiwa kwa kile alichadai kuwa ni kwa sababu ya usalama na kwa maslahi ya Taifa.

Washtakiwa hao ni Mashinda Mtei (49) mkazi wa Tengeru Arusha, Julius Mwita (40) mwanasiasa na ni mkazi wa Magomeni, Frederick Fussi (25) IT, mkazi wa Mbezi, Julius Matei (45) raia wa Kenya, Meshack Mlawa (25) mchungaji na ni mkazi wa Keko, Anisa Rulanyan (41) Mhandisi, mkazi wa Kawe, Jose Nimi (51) mkazi wa Uingereza na Kim Hyunwook (42) raia wa Korea.

Wakili wa Serikali Mkuu Edwin Kakolaki alidai jana mbele ya Hakimu Mkazi Respicius Mwaijage wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kuwa washtakiwa wanashtakiwa kwa mashtaka matatu.

Ilidaiwa kuwa katika shtaka la kwanza linawakabili washtakiwa wote, ambapo inadawa kati ya Oktoba 25 na 26 mwaka huu, wakiwa katika vituo tofauti tofauti ndani ya jiji la Dar es Salaam walitoa taarifa za uongo kwenye mitandao wakati wakijua hazijadhibitishwa.

Kakolaki alidai washtakiwa hao walisambaza taarifa hizo kwenye mtandao huo na katika mitandao mingine ya kijamii ambayo ni  Facebook na Twitter kutangaza matokeo ya urais ya mwaka huku kwa lengo la kuposha umma huku wakijua hayajadhibitishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Katika shtaka la pili linamkabili Matei, Nimi na Hyunwook, ambapo wanashtakiwa kuwa Oktoba 26 mwaka huu wakiwa katika hoteli ya King iliyopo Kinondoni , Dar es Salaam wakiwa na hati za kusafirilia zenye namba A1532119, 930879 na M 27687807 walijiingiza katika ajira ya kukusanya na kusambaza matokeo ya urais ya uchaguzi wa mwaka huu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema ) bila kibali.

Pia, alidai katika shtaka la tatu lina mkabili Matei peke yake ambaye akiwa raia wa Kenya mwenye hati ya kusafirilia namba A1532119 akiwa ndani ya jiji  la Dar es Salaam alijihusisha na biashara katika Saccos ya Wanama bila kibali.

Baada ya washtakiwa hao kusomewa mashtaka hayo, walikana kuhusika na tuhuma hizo, ambapo Kakolaki alidai upelelezi bado haujakamilika na pia alidai DPP amewasilisha hati ya kuzuia dhamana kwa sababu ya usalama na maslahi ya Serikali.

Wakili wa washtakiwa hao Peter Kibatala, alidai kuwa mashtaka yanayowakabili wateja wake yanadhaminika, kwa hiyo aliiomba mahakama iwapatie dhamana.

Pia, alidai hati hiyo ya DPP haiko mahakamani hapo kihali na kuiomba Mahakama itupilie mbali hati hiyo kwa sababu haina mashiko kisheria.

Kibatala alidai kuwa hati ya mashtaka iko tofauti na hati ya DPP kutokana na kifungu kilichokuwepo kuwa si sahihi, kwa hiyo kama ni hivyo hati hizo zote hazifai, kutokana na mapungufu hayo.

Baada ya Kibatala kudai hivyo, wakili Kakolaki alidai kuwa hati ya DPP ipo kihalali mahakamani na anayuetakiwa kuthibitisha hilo na mahakama kwa hiyo waiyachie mahakama.

Alidai kuhusu kifungu kilichotumika ni sahihi, akaiomba mahakama itupilie mbali hoja za Kibatala na washtakiwa wanyimwe dhamana kwa mujibu wa sheria, baada ya DPP kuwasilisha hati hiyo.

Hakimu Mwaijage alisema uamuzi wa hoja hizo atazitoa Oktoba 30 mwaka huu na washtakiwa aliamuru warudishwe rumande.

Nje ya mahakama
Washtakiwa hao waliondoka katika eneo hilo la mahakama wakiwa chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi ambapo wakiwa ndani ya magari ya polisi walikuwa wakionesha alama za vidole viwili.

Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salim Mwalimu, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sauti, Profesa Mwasiga Baregu na viongozi wengine wa Chadema walijitokeza mahakamani hapo kufuatilia shauri hilo.

TWIGA KUCHEZA NA MALAWI NOVEMBA 7




Timu ya Taifa Tanzania ya Wanawake ya Mpira wa Miguu (Twiga Stars) inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Taifa ya Wanawake ya Malawi Novemba 7, 2015 jijini Dar es salaam.
Mchezo huo wa kirafiki ni sehmu ya kujipima kwa Twiga Stars inayonolewa na kocha Rogasian Kaijage, ambayo ilishiriki Fainali za Michezo ya Afrika (All Africa Games) mwezi Agosti – Septemba nchini Congo – Brazzavile.
Awali Twiga Stars ilikua icheze mchezo huo nchini Malawi Oktoba 24, kabla ya chama cha soka nchini humo (FAM) kuahirisha mchezo huo, na sasa mchezo huo utacheza nchini Tanzania Novemba 07, 2015.

Baba Levo na Udiwani Kigoma, Idris kufungiwa Instagram.. Kingwendu kashinda ubunge



Kwenye list ya mastaa ambao wamejitosa kwenye Siasa 2015, Baba Levo nae yumo… Baba Levo ameshukuru sana kwa ushindi wake huku akisema kwamba japo kashinda na anakuwa Diwani Kigoma mjini kwa miaka mitano lakini muziki hatouacha na atajitahidi pia kusaidia vijana wenye vipaji Kigoma ili waweze kutambulika kwa sanaa wanazofanya.
Baba Levo
Baba Levo
Kingwendu nae aliingia kwenye Siasa japo Kura hazikutosha hivyo kashindwa kuibuka na ushindi, amesema kushindwa kwake kunafanya ajipange upya kwa ajili Siasa kwenye msimu mwingine wa Uchaguzi 2020 Tanzania.
kingwendu
Mchekeshaji Kingwendu.
Account ya Instagram ya staa wa Big Brother, Idris Sultan haiko hewani… kama ulishtuka kutokumuona upande huo basi taarifa ikufikie kwamba Wamiliki wa Mtandao wa Instagram wameifungia account yake kwa muda kwa sababu alikiuka kanuni za Mtandao huo.
Idris
Idris Sultan.
Idris amesema alifungiwa baada ya kupost kipande cha video kutoka kwenye movie ambacho yeye hakujua kwamba hiyo movie imefungiwa… Idris amesema yuko kwenye mipango ya kujadiliana na Wamiliki wa Mtandao huo ili wamfungulie.

VODACOM KUMKABIDHI KIIZA KITITA CHAKE



Mshambuliaji wa Simba, Hamis Kiiza.

NA MWANDISHI WETU
MSHAMBULIAJI wa Simba, Hamis Kiiza, anatarajiwa kukabidhiwa zawadi yake ya Sh milioni 1/-ya Mchezaji Bora wa Mwezi na wadhamini wakuu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, baada ya kuibuka kidedea Septemba.


Kiiza alichaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Septemba baada ya kufanya vema katika mwezi wa kwanza wa ligi hiyo, akiisaidia timu yake ya Simba kushinda mechi tatu mfululizo, huku Mganda huyo akifunga mabao matano, ikiwamo ‘hat-trick’ katika pambano dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu, Kiiza atakabidhiwa kitita chake hicho na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Ian Ferrao, wakati wa mchezo wa Simba dhidi ya Majimaji Oktoba 31, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Alisema kuwa kampuni yao itaendelea kutoa zawadi kwa wachezaji wanaofanya vizuri kila mwezi, ikiwa ni sehemu ya mikakati na mchango wao katika kuinua kiwango cha michezo, hususan soka nchini na kubadilisha maisha ya wachezaji wanaoshiriki Ligi Kuu.
“Katika kuendeleza mikakati yetu ya kuinua soka hapa nchini pamoja na kuboresha maisha kwa wachezaji wanaoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Vodacom Tanzania, itamjaza kiasi cha Sh milioni moja mshambuliaji wa Simba, Hamis Kiiza kutokana na kuchaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa ligi hiyo kwa Septemba msimu huu,” alisema Nkurlu.
Juu ya tuzo hiyo, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, ameishukuru na kuipongeza Vodacom Tanzania ubunifu huo wa kuwazawadia wachezaji wanaofanya vizuri kwani kitendo hicho huchangia kuendeleza vipaji na kuwahamasisha wachezaji kufanya vizuri zaidi na kuzisaidia timu zao.

“TFF tunaamini zawadi kama hizi zinazotolewa kwa Mchezaji Bora wa Mwezi, zinaweza kuwa chachu kwa wachezaji wa klabu za Ligi Kuu kujituma zaidi kwa faida yao, klabu zao na soka la Tanzania kwa ujumla,” alisema.

WILFRED LWAKATARE WA CHADEMA AIBUKA KIDEDEA UBUNGE BUKOBA MJINI.


Hatimaye Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa chama cha demokrasia na maendeleo -Chadema Bw. Wilfred Muganyizi Lwakatare ameibuka kidedea leo hii kuwa Mbunge wa Bukoba Mjini akiibuka kidedea dhidi ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini kwa tiketi ya CCM, Khamis Kagasheki. Matokeo hayo yametanga usiku huu punde na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Bukoba mjini Bw. Aron T. Kagurumjuli. Kura za Udiwani Chadema/ Ukawa imeshinda Kata zifuatazo: Kahororo, Kagondo, Kibeta, Kitendaguro, Nshambya, Hamugebe, Kashai, Bakoba na Bilele. CCM imepata Kata ya Rwamishenye, Buhembe, Miembeni, Nyanga na Ijunganyondo. Picha na Faustine Ruta, Bukoba
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Bukoba mjini Bw. Aron T. Kagurumjuli akitoa matokeo usiku huu wa saa 2:30 na kumtangaza Lwakatare kwamba ndie mshindi na Nafasi hiyo ya Ubunge Bukoba Mjini.
Bw. Aron T. Kagurumjuli (Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Bukoba mjini) akiendelea na zoezi la kutangaza matokeo usiku huu.
Mshindi wa nafasi ya Ubunge wa Bukoba Mjini Bw. Wilfred Muganyizi Lwakatare kupitia Chama cha CHADEMA akifurahia baada ya kuibuka kidedea katika kinyang'anyiro hicho baada ya kumwangusha mgembea mwenza aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo la Bukoba Mjini kwa tiketi ya CCM, Khamis Sued Kagasheki usiku huu.
Picha na Faustine Ruta, Bukoba
LICHA ya kuonekana kana kwamba hapakuwa na dalili zozote za fujo wakati wa zoezi la upigaji kura za Ubunge na udiwani, hali ilibadilika leo jumatatu asubuhi baada ya wafuasi wa chama cha Chadema kutaka matokeo mapema baada ya kupata matokeo hayo usiku wa kuamkia leo hii kuwa Chadema imeshinda katika Kata 9 kati ya 14 wafuasi hao waliandamana katika maeneo ya mji wa Bukoba wakitaka majibu yatolewe mapema. Kitu ambacho hakikufanyika na Jioni hii kuleta kasheshe na ghasia. Hali hiyo ilisababisha polisi wa kutuliza ghasia kuingilia kati na kuwatawanya vijana hao ambao mpaka usiku huu walikuwa wamepandwa na jazba katika eneo la ofisi za Halmashauri ya Bukoba. Vurugu zikiwemo kurushiana mawe zilitokea. Ndipo polisi walitumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi waliokusanyika katika Ofisi za Halmashauri na kuanza kurusha mawe wakishinikiza kutangazwa kwa matokeo ya ubunge. Hali hiyo ilitulia baada ya Viongozi wa Chadema kuwatuliza na ndipo Matokeo yakatangazwa.
Taarifa zinasema kuwa kulikuwa na mchuano mkali kati ya wagombea hao wawili ambao ni Wilfred Lwakatare wa chama cha Chadema na aliyekuwa Mbunge wa Bukoba Mjini kupitia chama cha CCM Khamis Sued Kagasheki. Kitu kilichopelekea kurudiwa kuhesabiwa kwa kura zote na kupata uhakika wa kutosha.
Kura zilizokubalika ni 54,211 sawa na asilimia 98.54, kura zilizoharibika ni 805 sawa asilimia 1.46, Matokeo ni kama ifuatavyo TLP kura 81 sawa na asilimia 0.2, ACT kura 453, Khamis Sued Kagasheki wa CCM amepata kura 25,565 sawa na asilimia 47.2, Wilfred Muganyizi Lwakatare wa Chadema amepata kura 28,112 sawa na asilimia 51.9Wafuasi wa Chadema walionekana wakiwa wamekusanyika katika Ofisi za Halmashauri Bukoba wakidai kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa huo wa Wabunge. Vingozi wa Chama cha Chadema wakiteta jambo, kushoto) ni Bw. Chief Kalumuna Mshindi wa Udiwani Kata ya Kahororo aliyeshinda kiti hicho katika Uchaguzi huu wa 2015. (Kulia) ni Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema wilaya ya Bukoba Victor Sherejei. Bw. Wilfred Lwakatare kupitia Chama cha CHADEMA akiteta jambo na Diwani wa Kata ya Kahororo kupitia Chama cha Chadema katika Ofisi za Halmashauri ya Bukoba mjini huku wakisubiri matokeo ya Ubunge Bukoba Mjini. Bw. Wilfred Lwakatare kupitia Chama cha CHADEMA Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema wilaya ya Bukoba Victor Sherejei (kulia) mbele akiteta na Chief Kalumuna Diwani wa kata kahororo wakibadilisha mawazo wakati wakisubiri matokeo usiku huu.Waandishi wa habari na Makada wa Chama cha Chadema wakiwa katika Ofisi za Halmashauri ya Bukoba Kidedea...Chif Kalumuna(kulia) wa Kata ya Kahororo akiwa amembeba mshindi bw. Wilfred Lwakatare Wafuasi wa Chadema walionekana wakiwa wamekusanyika kutaka kuvamia Ofisi za Halmashauri ya Bukoba kudai kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa wabunge na Polisi walikuwa tayari kuwakabili vilivyo na kuzuia umati huo mkubwa. Wafuasi wa Chadema wakitaka Matokeo yatolewa baada ya kuchukuwa muda tangu asubuhi mpaka jioni hii. Taswira jioni hii maeneo ya karibu na Ofisi za Halmashauri. Hapa ikabidi kiongozi wa Chadema aliyeshinda katika Kata ya  Kashai kupitia chama hicho awatulize kwamba matokeo yanaenda kutolewa jioni hii. Wafuasi wa Chadema wakitaka Matokeo Wafuasi wa Chadema wakitaka Matokeo ya Kiongozi wao.

Sentensi saba za Mchekeshaji Kingwendu baada ya kushindwa Ubunge Kisarawe

Muigizaji Kingwendu ni miongoni mwa mastaa ambao wamechukua headline za kugombea Ubunge kwenye Uchaguzi Mkuu 2015 kama Afande Sele, Professor Jay, Muigizaji Frank na wengineo.
Stori iliyonifikia ni kwamba muigizaji huyo hakufanikiwa kupata Ubunge kupitia tiketi ya CUF katika  jimbo la Kisarawe mkoa wa Pwani.
Akiongea na ripota wa millardayo.com alisema…’Matokeo ya mwanzo yalikuwa yanaonesha kwamba mimi naongoza, lakini mwishoni katika hesabu ikaonekana amenishinda‘- KINGWENDU
‘Matokeo yanaonesha Suleimani Jako wa CCM ameshinda, nimejaribu na nimethubutu kwa mara ya kwanza..! najua nimekosea wapi na ntajipanga upya na ntaenda kusomea siasa zaidi’– KINGWENDU
‘Hakuna mtu aliyenishawishi kugombea ubunge, bali ni mimi mwenyewe niliamua baada ya kuona pia baadhi ya wasanii wenzangu wanagombania‘-KINGWENDU
 
Blogger Templates