Mwenyekiti
 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe 
(kushoto), akizungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama ya Kisutu 
Dar es Salaam leo.
Askari wa FFU wakiimarisha ulinzi mahakamani hapo.
Wafuasi wa Chadema wakionesha alama ya vidole viwili wanayoitumia.
| Viongozi wa Chadema wakitoka katika mahakama hiyo baada ya kusikiliza kesi hiyo. | 
Vijana waliokamatwa wakiwa katika mahakama hiyo.
Na Dotto Mwaibale
WATU 
wanane akiwemo Raia mmoja wa Korea na raia mmoja wa Kenya wamepandishwa 
kizimbani kwa kusambaza taarifa za matokeo ya urais katika Mtandao wa 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi yakiwa na kichwa 'M4C election result 
management system' bila kuthibitishwa kwa lengo la kupotosha umma. 
Sanjari
 na hilo, Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), amewasilisha mahakamani 
hati ya kuzuia dhamana ya washtakiwa kwa kile alichadai kuwa ni kwa 
sababu ya usalama na kwa maslahi ya Taifa.
Washtakiwa
 hao ni Mashinda Mtei (49) mkazi wa Tengeru Arusha, Julius Mwita (40) 
mwanasiasa na ni mkazi wa Magomeni, Frederick Fussi (25) IT, mkazi wa 
Mbezi, Julius Matei (45) raia wa Kenya, Meshack Mlawa (25) mchungaji na 
ni mkazi wa Keko, Anisa Rulanyan (41) Mhandisi, mkazi wa Kawe, Jose Nimi
 (51) mkazi wa Uingereza na Kim Hyunwook (42) raia wa Korea.
Wakili
 wa Serikali Mkuu Edwin Kakolaki alidai jana mbele ya Hakimu Mkazi 
Respicius Mwaijage wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam 
kuwa washtakiwa wanashtakiwa kwa mashtaka matatu.
Ilidaiwa
 kuwa katika shtaka la kwanza linawakabili washtakiwa wote, ambapo 
inadawa kati ya Oktoba 25 na 26 mwaka huu, wakiwa katika vituo tofauti 
tofauti ndani ya jiji la Dar es Salaam walitoa taarifa za uongo kwenye 
mitandao wakati wakijua hazijadhibitishwa.
Kakolaki
 alidai washtakiwa hao walisambaza taarifa hizo kwenye mtandao huo na 
katika mitandao mingine ya kijamii ambayo ni  Facebook na Twitter 
kutangaza matokeo ya urais ya mwaka huku kwa lengo la kuposha umma huku 
wakijua hayajadhibitishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Katika
 shtaka la pili linamkabili Matei, Nimi na Hyunwook, ambapo wanashtakiwa
 kuwa Oktoba 26 mwaka huu wakiwa katika hoteli ya King iliyopo Kinondoni
 , Dar es Salaam wakiwa na hati za kusafirilia zenye namba A1532119, 
930879 na M 27687807 walijiingiza katika ajira ya kukusanya na kusambaza
 matokeo ya urais ya uchaguzi wa mwaka huu ya Chama cha Demokrasia na 
Maendeleo (Chadema ) bila kibali.
Pia, 
alidai katika shtaka la tatu lina mkabili Matei peke yake ambaye akiwa 
raia wa Kenya mwenye hati ya kusafirilia namba A1532119 akiwa ndani ya 
jiji  la Dar es Salaam alijihusisha na biashara katika Saccos ya Wanama 
bila kibali.
Baada 
ya washtakiwa hao kusomewa mashtaka hayo, walikana kuhusika na tuhuma 
hizo, ambapo Kakolaki alidai upelelezi bado haujakamilika na pia alidai 
DPP amewasilisha hati ya kuzuia dhamana kwa sababu ya usalama na maslahi
 ya Serikali.
Wakili
 wa washtakiwa hao Peter Kibatala, alidai kuwa mashtaka yanayowakabili 
wateja wake yanadhaminika, kwa hiyo aliiomba mahakama iwapatie dhamana.
Pia, 
alidai hati hiyo ya DPP haiko mahakamani hapo kihali na kuiomba Mahakama
 itupilie mbali hati hiyo kwa sababu haina mashiko kisheria.
Kibatala
 alidai kuwa hati ya mashtaka iko tofauti na hati ya DPP kutokana na 
kifungu kilichokuwepo kuwa si sahihi, kwa hiyo kama ni hivyo hati hizo 
zote hazifai, kutokana na mapungufu hayo.
Baada 
ya Kibatala kudai hivyo, wakili Kakolaki alidai kuwa hati ya DPP ipo 
kihalali mahakamani na anayuetakiwa kuthibitisha hilo na mahakama kwa 
hiyo waiyachie mahakama.
Alidai
 kuhusu kifungu kilichotumika ni sahihi, akaiomba mahakama itupilie 
mbali hoja za Kibatala na washtakiwa wanyimwe dhamana kwa mujibu wa 
sheria, baada ya DPP kuwasilisha hati hiyo.
Hakimu Mwaijage alisema uamuzi wa hoja hizo atazitoa Oktoba 30 mwaka huu na washtakiwa aliamuru warudishwe rumande.
Nje ya mahakama
Washtakiwa
 hao waliondoka katika eneo hilo la mahakama wakiwa chini ya ulinzi 
mkali wa Jeshi la Polisi ambapo wakiwa ndani ya magari ya polisi 
walikuwa wakionesha alama za vidole viwili.
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment