Pages

Ads 468x60px

Friday, December 18, 2015

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA KATIKA MITAMBO YA GESI YA TEGETA JIJINI DAR.




Ni majira ya saa 10 na dakika 10 Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Mhongo ndipo alipofika katika mitambo ya kuzalisha umeme wa gesi ya Tegeta jijini Dar es Salaam kinachomilikiwa na Tanesco bila ya kutoa taarifa na kukuta wafanyakazi pamoja na wahandisi wa kituo hicho cha umeme wakiendelea na kazi katika mitambo hiyo. 

Na kukagua mitambo hiyo leo  na kubaini kuwa umeme uniti moja inatengenezwa kwa gharama ya shilingi 90 na kuuzwa kwa wananchi kwa shilingi 180 ikiwa ni kiwango kikubwa kwa mwananchi wa kawaida.

Pia Mhongo amesisitiza kuwa umeme unatakiwa kushuka bei ili kila mwananchi anufaike na umeme hapa nchini.
Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Mhongo akipokea vifaa vya kuzuia kusikia sauti kuingia masikioni mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Mitambo ya Gesi ya Tegeta jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Mhongo akizungumza na Meneja wa Mitambo ya gesi ya Tegeta jijini Dar es Salaam, Mohamed Kisiwa mara baada waziri wa Nishati na Madini kutembelea mitambo ya umeme wa gesi wa Tegeta jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Mhongo akipewa maelekezo na Meneja wa Mitambo ya gesi ya Tegeta, Mohamed Kisiwa mara baada ya waziri huyo kutembelea mtambo huo bila kutoa taarifa na kuhoji baadhi ya matengenezo katika mtambo huo.
Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Mhongo akitembezwa na Meneja wa Mitambo ya gesi ya Tegeta Mohamed Kisiwa mara baada ya kutembelea mitambo ya Tegeta jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya Mitambo ya Gesi iliyotembelewa na Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Mhongo leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Mhongo akipewa maelekezo na Meneja wa Mitambo ya gesi ya Tegeta, Mohamed Kisiwa jijini Dar es Salaam leo.

MAJALIWA AKUTANA NA SHEIKH MKUU


liw1
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubakar Zuberi, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Desemba 18, 2015.
liw2
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubakar Zuberi, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Desemba 18, 2015. Kulia ni  Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhad Musa. (PIcha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Serikali yasaini makubaliano ya ujenzi wa Barabara Arusha.



uj1
Mkurugenzi wa barabara Wizara ya Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Ven Ndiyakumana kushoto akisaini mkataba wa awali kuhusu mkopo wa fedha wa riba nafuu utakaosaidia ujenzi wa Barabara ya Arusha hadi Holili kulia ni Naibu Mkurugenzi wa Idara ya ushirikiano Afrika kutoka Japan (JICA) Bw. Hideyuki Manioka wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo Jijini Dar es salaam.
uj2
Mkurugenzi wa barabara Wizara ya Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Ven Ndiyakumana kushoto akikabidhiana mkataba wa awali kuhusu mkopo wa fedha wa riba nafuu utakaosaidia ujenzi wa Barabara ya Arusha hadi Holili na Naibu Mkurugenzi wa Idara ya ushirikiano Afrika kutoka Japan (JICA) Bw. Hideyuki Manioka wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo Jijini Dar es salaam.PICHA ZOTE NA ALLY DAUD-MAELEZO
…………………………………………..
Na Raymond Mushumbusi Maelezo
Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano leo imesaini mkataba wa makubaliano ya awali ya ujenzi wa barabara kutoka Arusha mpaka Holili.
 
Makubaliano hayo yamesainiwa na Mkurugenzi wa Barabara kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Ven Ndyamukama kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Naibu Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano (JICA) Bw Hideyuki Manioka  kwa niaba ya Serikali ya Japan.
 
Mhandisi Ven Ndyamukama amesema kuwa Tanzania imesaini mkataba huu wa awali ambao baada ya majadiliano ya awali kati ya Tanzania na Japan, serikali ya Japan itatoa mkopo wa riba nafuu kwa serikali ya Tanzania ili kuwezesha kuanza kwa utekelezaji wa mradi huu mapema marchi mwakani.
 
“Wamekuja kufanya utafiti na kufatilia taarifa tulizo nazo kuhusu mradi huu na kupeleka taarifa serikali ya Japan na tunategemea June mwakani kusaini hati ya kupata mkopo ambao utawezesha ujenzi wa barabara hii ” Alisema Mhandisi Ndyamukama.Pia ameongeza kuwa baada ya mkopo huo kutolewa wao kwa upande wao wamejipanga katika kufanya mradi huo ukamilike kwa wakati ikiwemo upatikanaji wa wakandarasi kwa ajili ya mradi huo.
Aidha Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano (JICA) Bw Hideyuki Manioka  amesema kuwa wataendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo.
 
Mradi huu wa barabara toka Arusha mpaka Holili  yenye urefu wa kilometa105 umefadhiliwa na Serikali ya Japan kupitia Wakala wa mambo ya Ujenzi(JICA) na unatarajiwa kuanza mapema mwakani,hii ikiwa ni juhudi za Serikali katika kuboresha miundombinu hasa ya barabara kwa kuzifanya barabara nyingi nchini kuwa katika kiwango cha lami.

WAZIRI KITWANGA ALA KIAPO CHA KUWA MWENYEKITI WA TUME YA UTUMISHI YA JESHI LA POLISI NA MAGEREZA 75

75
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akila kiapo cha kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza mbele ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza. Katikati ni Msajili wa Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta.
76
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akisaini hati ya kiapo mara baada ya kuapishwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza mbele ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza.
77
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) akimpongeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga mara baada ya kumuapisha kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza, katika tukio lililofanyika katika Mahakama hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza.

HARAKATI ENDELEVU ZA KIKUNDI CHA “BUKOBA MPYA PROJECT” ZOEZI LA KUTOKOMEZA MAZALIA YA MBU KATA ZA MANISPAA BUKOBA

HARAKATI ENDELEVU ZA KIKUNDI CHA “BUKOBA MPYA PROJECT”

ZOEZI LA KUTOKOMEZA MAZALIA YA MBU KATA ZA MANISPAA YA MJI BUKOBA

Ndugu Wadau,

“Bukoba Mpya Project” ni zao la harakati endelevu chini ya Bukoba Wadau Media katika kuchangia kuhamasisha Wanabukoba wa ndani na nje ya Tanzania kushiriki katika kuinua hali ya mji na maisha ya wakazi wa Bukoba.  Wanachama wa harakati hizi ni waamini wa itikadi ya UMOJA na MAENDELEO. Mpaka sasa jumla ya wanachama wasioupungua 50 kutoka ndani na nje ya Bukoba na Tanzania kwa ujumla wanashiriki harakati hizi.

Wakiongozwa na imani kwamba “maendeleo yanaletwa na mimi”, Wana Bukoba Mpya wamepanga kuanza jitihada ya kupambana na Malaria kwa kutokomeza mazalia ya mbu kwenye maeneo yote ya Manispaa ya Bukoba. Jitihada hii itatekelezwa kwa zoezi la kupulizia dawa za kuua mazalia ya mbu kwenye Kata zote 14 za Manispaa ya Bukoba. Zoezi litaanzia na Kata za Greenbelt  (Kahororo,Buhembe, Kitendaguro ,Ijuganyundo,Nyanga,Kibeta na Nshambya) mara tu baada ya siku kuu kuisha kisha litaendelea kwenye kata zingine zote kadri ratiba itakavyotolewa.

Kila mmoja anayeguswa na athari za mbu na anavutiwa na jitihada hii anaalikwa kushiriki kwa njia moja au nyingine. Unaweza kufanya hivyo kwa:

·         Kuthibitisha kushiriki moja kwa moja kwenye zoezi tarehe na mahali litakapofanyika·         Kwa kuhamasisha ndugu na jamaa zako wafike kushiriki (hii ni kwa walio mbali na nje ya Tanzania)
·         Kwa kuchangia pesa, madawa na vifaa vya zoezi (orodha ya vifaa na utaratibu utapatiwa)

Viongozi, Watendaji na Wananchi kwa ujumla waombwa kutoa ushirikiano na kushiriki kwa kadri wanavyoweza pale zoezi hili litakapofanyika katika maeneo yao.

Kwa mawasiliano na maelezo zaidi juu ya jinsi ya kushiriki wasiliana nasi kwa njia zifuatazo:
Mob: 0784 505045 / 0768 397241 /0713 883020 /0754 505043.

Imetolewa na:
Kitengo cha Uhamasishaji Jamii
Bukoba Wadau Media.

UJUMBE WA SHIRIKA LA NYUMBA UGANDA WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO NHC TANZANIA


Ujumbe wa Shirika la Nyumba la Taifa la Uganda (NHCC) ukiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo, Parity Twinomujuni (aliyeketi mbele ya logo ya NHC) ukijadiliana masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya nyumba nchini na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa la Tanzania, Nehemia Kyando Mchechu. Ujumbe huo umekuwapo katika ziara ya siku mbili ya mafunzo nchini kujifunza namna utendaji wa Shirika la Tanzania unavyofanyika ili waweze kupata njia za kuweza kuboresha Shirika zaidi Shirika la NHCC Uganda.
Ujumbe wa Shirika la Nyumba la Taifa la Uganda (NHCC) ukiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu Parity Twinomujuni (aliyeketi mbele ya logo ya NHC) ukijadiliana masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya nyumba nchini na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa la Tanzania, Nehemia Kyando Mchechu. Ujumbe huo umekuwapo katika ziara ya siku mbili ya mafunzo nchini kujifunza namna utendaji wa Shirika la Tanzania unavyofanyika ili waweze kupata njia za kuweza kuboresha Shirika zaidi Shirika la NHCC Uganda.
Mojawapo ya nyumba za NHC Mwongozo zilizotembelewa na Ujumbe wa Shirika la Nyumba la Taifa la Uganda (NHCC) ukiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu Parity Twinomujuni. Ujumbe huo umekuwapo katika ziara ya siku mbili ya mafunzo nchini kujifunza namna utendaji wa Shirika la Tanzania unavyofanyika ili waweze kupata njia za kuweza kuboresha Shirika zaidi Shirika la NHCC Uganda.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Nyumba la Taifa la Uganda (NHCC) Balozi Agnes Kadama Kalibbala na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa la Uganda (NHCC) Parity Twinomujuni wakifuatilia mawasilisho yaliyokuwa ya kifanywa na Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa la Tanzania jana.

Waziri Ummy akabidhiwa ofisi na mtangulizi wake Dkt.Seif


sei3
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Ummy Mwalimu akipokea taarifa ya makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa Waziri wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Usatawi wa Jamaii ya Serikali ya Awamu ya Nne Dkt. Seif Rashid wakati wa kukabidhiwa rasmi ofisi leo jijini Dar es salaam.
sei1
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Ummy Mwalimu akimsikiliza aliyekuwa Waziri wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Usatawi wa Jamaii ya Serikali ya Awamu ya Nne Dkt. Seif Rashid wakati wa kukabidhiwa rasmi ofisi leo jijini Dar es salaam.
sei2
Aliyekuwa Waziri wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Usatawi wa Jamaii ya Serikali ya Awamu ya Nne Dkt. Seif Rashid (kushoto) akisalimiana na Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Dkt. Hamisi Kigwangala (kulia) leo jijini Dar es salaam.
………………………………………
NA Eleuteri Mangi-MAELEZO
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Ummy Mwalimu amekabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Waziri wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Usatawi wa Jamaii ya Serikali ya Awamu ya Nne Dkt. Seif Rashid leo jijini Dar es salaam.Akipokea ofisi hiyo, Waziri Ummy alimshukuru Dkt. Seif kwa jitihada kubwa waliyofanya ya kupambana na magonjwa kwa wananchi na kufanikisha Tanzania kuwa miongoni mwa nchi duniani ambayo imetatua tatizo la ugonjwa wa polio na kuwa “polio free”..
Aidha, Waziri Ummy amemhakikishia Dkt Seif kuendelea kushirikiana naye pale msaada wake utakapohitajika kwa kuwa anauzoefu katika masuala ya afya ili kuwahudumia Watanzania na kupambana na adui wa taifa ambaye ni magonjwa.Akikabidhi ofisi, Dkt Seif aliwapongeza Waziri Ummy Mwalimu na Naibu wake Dkt. Hamisi Kigwangalla kwa kupewa nyadhifa hizo na kuahidi kuwapa ushirikiano wake paleutakapohitajika.
Dhana ya “Hapa Kazi Tu” imechukua mkondo wake ambapo hadi sasa Mwaziri na Manaibu waziri wanatekeleza dhana hiyo kwa vitendo na siyo kukaa ofisini, kwa kwa juhudi hizo viongozi kwa kushirikiana na wananchi, Tanzania itafanikiwa kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025 ikiwa na watu wenye afya bora inayowaruhusu kufanyakazi kwa juhudi na maarifa ili kuwa maendeleo yenye tija kwa Wtanzania.

Philips launches new range of patient monitors in Tanzania

Efficia 1Royal Philips (NYSE: PHG AEX: PHIA) has announced the launch of its Efficia CM Series patient monitors in Tanzania – these cost effective products are designed to provide clinicians with access to high-quality of care, even in resource-limited facilities. These solutions highlight Philips’ commitment to enhance access and enable quality care across the health continuum – from healthy living and prevention, to diagnosis, treatment, recovery and home care, including in remote areas.
“As we innovate to improve health care, monetary constraints should not be a reason for limiting access to the best care available for improving a patient’s health,” said Roelof Assies, General Manager, Philips East Africa. “The Efficia suite is designed to bring trusted and effective Philips technology and performance at an affordable price to the health care facilities where resource limitations have prevented this access before.”
Making quality care affordable.
  Effective patient monitoring can help improve diagnosis and provide earlier intervention, which is not only critical for improving patient outcomes, but can also help hospitals improve operational efficiencies.
The Efficia CM Series patient monitors provide the same core physiological measurements and algorithms that are present in other Philips patient monitors, but are designed to be more cost-effective and scalable to the needs of budget-constrained health care facilities.The series, including Efficia CM100, Efficia CM120 and Efficia CM150, are solidly built and reliable, able to handle heavy workloads and electrostatic interference, and can be customized for a variety of patient types, acuity levels and clinical settings, and include an intuitive user-interface to ease the burden on busy clinician workflow.
The Efficia CM patient monitors can be connected to Efficia CMS200 central monitoring system, which provides centralized monitoring and real-time access to patient physiological data and displays waveforms, parameters and alarms for up to 32 patients.Efficia DFM100 – Providing therapeutic care where it is needed mostefficia 2
To deliver quality care, clinicians need to make quick, informed decisions when responding to an emergency and caring for a patient across the entire course of treatment. The Efficia DFM100 defibrillator/monitor is designed to be easy to use for both basic and advanced life support care providers to meet the demands of patient care in pre-hospital and hospital environments effectively and consistently. The Efficia DFM100 provides functionalities needed to enhance patient care, regardless of where they are located. It is also scalable to ensure affordability across all care settings.
“Clinicians are constantly under pressure to meet clinical demands on a tight budget,” said Dr. Juma A. Mfinanga, Head of Emergency Department at Muhimbili National Hospital. “The Efficia solutions work with the clinicians and the hospital; they are affordable and intuitive, allowing limited staff to focus on care first.”

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashantu Kijachi afanya ziara PSPF

may1
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dk. Ashantu Kijachi  akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw. Adamu Mayingu wakati alipokuwa akimpa maelezo baada ya Naibu Waziri huyo kufanya ziara katika shirika hilo leo jijini Dar es Salaama habari alipofanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za 
may2
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw. Adamu Mayingu (hayupo pichani) akizungumza na na waandishi wa habari (hawapo pichani) alipotembelewa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango  Mhe. Dk. Ashantu Kijachi (hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam.
may3
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw. Adamu Mayingu (hayupo pichani) akizungumza na na waandishi wa habari alipotembelewa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango  Mhe. Dk. Ashantu Kijachi

NEWS ALERT: BASI LA KAMPUNI YA NEW FORCE LAPATA AJALI MBAYA MKOANI IRINGA


 NEWS UPDATES.:Jumla ya watu. 12 wamepoteza Maisha na 22 wamejeruhiwa leo baada ya basi la New Force kupata ajali Eneo la Mahenge Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa barabara kuu ya Iringa- Dar es salaam..
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa,Peter Kakamba amethibitisha watu 12 kupoteza maisha katika ajali hiyo. Wanane ni wanae na wanne ni wanawake. Abiria 28 wamejeruhiwa wakiwemo madereva wa basi la lori na hali zao siyo nzuri.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa nane alasiri ambapo basi la kampuni ya Newforce aina ya Youtong lenye namba za usajili T483CTF likitoka Tunduma kwenda Dar limegongana na lori aina ya Scania lenye namba T616DEF katika kijiji cha Mahenge,wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa katika barabara kuu ya Dar - Mbeya.

Majeruhi wamelazwa hospitali ya wilaya ya Ilula.kilomita 45 kutoka Iringa mjini.
 
=======  ========   ========
 
WATU kadhaa wanadaiwa kupoteza maisha huku wengine wengi wakijeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria mali ya Kampuni ya NEW FORCE ONE lenye namba za usajili T483 CTF kupinduka mapema mchana wa leo katika eneo la Mahenge Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa barabara kuu ya Iringa- Morogoro, jitihada za kusafirisha majeruhi zinaendelea. 
Chanzo cha ajali hiyo, inaelezwa kuwa ni Lori la mizigo lililokuwa likitokea upande wa Morogoro, kupasuka tairi ya mbele na kupoteza muelekeo uliopelekea kuligonga basi hilo na kupinduka. Globu ya Jamii inafanya jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa kwa taarifa zaidi. tutaendelea kuwaletea taarifa kadri tutakavyozipata. 
Sehemu ya Basi hiyo baada ya kupata ajali.

MAPEMA ASUBUHI YA LEO DKT. KINGWANGALLA ATUMBUA MAJIPU YA WATUMISHI WACHELEWAJI WA WIZARA YA AFYA


IMG_9118
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla akiwaamrisha askari wa getini wizarani hapo kuweka kufuli na kutoruhusu mtumishi yoyote wa ofisi hiyo kuingia ndani ya ofisi za wizara ilipotimu saa 1:32 asubuhi mapema leo.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
IMG_9122
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla akisimamia zoezi la ufungwaji wa geti hilo, Kulia ni askari wa SUMA JKT akiweka kufuli katika lango kuu la kuingia katika ofisi za Wizara ya Afya.
IMG_9123
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla akiwauliza askari wa getini kuhusu daftari la mahudhurio ya watumishi wa wizara baada ya kufungwa geti hilo, na kupewa maelezo kuwa watumishi huonyesha vitambulisho pekee na husaini katika vitengo vyao.
IMG_9139
Mmoja wa wafanyakazi wa Wizara ya Afya akiwasili ofisini huku muda wa kuingia kazini ukiwa umepitiliza. Kushoto ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla akizungumza na mmoja watumishi wa wizara hiyo na kuagiza kuletewa vitabu vya mahudhurio kwa vitengo vyote vilivyopo wizarani hapo.
IMG_9149
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu katika Wizara ya Afya, Michael John akitoa maelezo kuhusu mahudhurio ya watumishi kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla.
IMG_9155
Magari ya watumishi wa Wizara ya Afya yakiendelea kuwasili ofisini bila ya kutambua kuwa Mheshimiwa Naibu Waziri, Dkt. Kigwangalla ametoa agizo la kuizuia watumishi wachelewaji.
IMG_9156
Askari wa getini wakimpa maelezo mmoja wa watumishi wa wizara hiyo kuwa Mh. Naibu Waziri ameagiza watumishi wote waliochelewa kuzuiliwa kuingia ndani.
IMG_9164
Mmoja wa wasaidi wa idara ya rasilimali watu akimkabidhi vitabu vya mahudhurio Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla.
IMG_9172
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla akipitia mahudhurio ya watumishi wa wizara kwa siku zilizopita.
IMG_9181
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla akipitisha mstari wa kufunga mahudhurio kwa watumishi ambao wameripiti kabla ya saa 1:30 asubuhi ya leo.
IMG_9198
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla akiendelea na zoezi hilo la kupitisha mstari kwa kila idara za wizara hiyo.
IMG_9231
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla akizungumza na waandishi wa habari kuhusu juu ukaguzi huo katika ofisi za wizara yake ya afya ili kuboresha utendaji wa wizara hiyo na vituo vyote vya sekta ya afya nchini kote.
Na Rabi Hume, Modewjiblog Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla amefanya ukaguzi wa kushtukiza katika ofisi za wizara hiyo kwa kusimama getini kuzuia wafanya kazi wote wa wizara ambao walikuwa wamefika ofisini baada ya saa 1:30 asubuhi muda ambao ndiyo mwisho wa wafanyakazi kuingia ofisini. 
Awali Dkt. Kingwangalla alifika ofisini saa 1:05 asubuhi huku akiingia ofisini kwa kutembea mwenyewe bila kutumia usafiri wa gari na kwenda moja kwa moja ofisini kwake ambapo alitoka ilipofika saa 1:32 na kwenda kusimama getini na kisha kuwaamrisha askari wa geti la kuingia katika wizara hiyo kulifunga geti hilo na wasiruhusu mtu yeyote kuingia ndani. “Fungeni geti na kila atakayefika msimruhusu kuingia ndani ninataka kuona wote ambao wanakuja wamechelewa,” alisikika Dkt. Kingwangalla akiwambia askari wa getini. 
 Baada ya kutoa amri hiyo alimtaka Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa wizara hiyo, Michael John kumpa vitabu vya kusaini kwa vitengo vyote ili aweke mstari wa kuonyesha kuwa muda wa kuingia ofisini umekwisha na akafanya hivyo kwa kuweka mstari kwenye vitabu vya mahudhurio kuwa muda wa kusaini kuingia umeisha. 
Baada ya kukamilisha zoezi hilo Naibu Waziri alizungumza na wanahabari kuwa ameamua kufanya zoezi hilo katika ofisi za wizara kwa kutaka kuona ni jinsi gani watumishi wa ofisi hiyo wamekuwa na mwitikio wa kufanya kazi kwa kasi anayoitaka rais, Dkt. John Pombe Magufuli. Alisema watumishi hao wameajiriwa na serikali ili kufanya kazi lakini wamekuwa wakichelewa kuingia ofisini na yeye kama Naibu Waziri ana wajibu wa kuwasimamia watumishi hao ili wafanye kazi ambayo serikali imewaagiza kufanya. 
“Nina wiki moja tangu nimeingia hapa ofisini kuna mambo ambayo nimeyaona hayapo vizuri na sasa naanza na hili ili tujue kuwa ni kina nani huwa wanachelewa na zoezi hili litakuwa ni endelevu, kama mimi sitasimamia watumishi wa serikali basi sitakuwa na kazi wizarani tunataka watumishi ambao wanakuwa wanafanya kazi kwa kujitoa kwa ajili ya maslahi ya taifa,” alisema Dkt. Kingwangalla. 
 Aidha Naibu Waziri huyo alimtaka Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kuhakikisha watumishi wote waliochelewa kufika ofisini wanaandika barua ya kutoa maelezo kwanini wanachelewa kufika ofisini na baada ya hapo Mkurugenzi na yeye atoe maelezo kwanini muda wa kutoka watumishi wanakuwa hawasaini kuwa wametoka. 
 Pia alishauri uongozi wa wizara ufanye mabadiliko ya mfumo wa watumishi kuingia ofisini kwa kutumia mifumo ya kisasa ya kadi au kidole “Biometric” ili kuwa na taarifa katika mifumo ya mawasiliano kujua wanaochelewa ofisini na wanaowahi kutoka na baada ya hapo uongozi utajadili adhabu za kuwapa watumishi wote ambao wamekuwa wakichelewa kufika na kuwahi kutoka ofisini.

UN TANZANIA YAZINDUA RIPOTI YA TEKNOLOJIA NA UBUNIFU 2015, NCHI ZA AFRIKA HALI SI NZURI



IMG_8928
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akizundua rasmi ripoti ya mwaka 2015 inayohusu Teknolojia na Ubunifu, ambayo imetolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la linaloshughulikia Biashara na Maendeleo (UNCTAD). Kulia ni Naibu Mkurugenzi wa Utawala, Mipango na Fedha wa Chu cha Diplomasia, Bw. Bernard Achiula na kushoto ni Dkt. Bitrina Diyamett kutoea Taasisi ya Utafiti wa Sera ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (STIPRO).
IMG_8936
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez, Dkt. Bitrina Diyamett na Bw. Bernard Achiula kwa pamoja wakionyesha ripoti hiyo kwa wageni waalikwa na wanahabari.
IMG_8864
Naibu Mkurugenzi wa Utawala, Mipango na Fedha wa Chu cha Diplomasia, Bw. Bernard Achiula akitoa neno la ukaribisho kwa wageni waalikwa kabla ya kumkaribisha Mratibu Mkazi wa UN nchini, Bw. Alvaro Rodriguez (hayupo pichani).
IMG_8872
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti ya mwaka 2015 inayohusu Teknolojia na Ubunifu, ambayo imetolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la linaloshughulikia Biashara na Maendeleo (UNCTAD).  
IMG_8832
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (katikati) akiongozana na Naibu Mkurugenzi wa Utawala, Mipango na Fedha wa Chu cha Diplomasia, Bw. Bernard Achiula (suti nyeusi) mara baada ya kuwasili wakielekea kwenye ukumbi wa mikutano wa Mozambique uliopo katika Chuo cha Diplomasia jijini Dar es Salaam
 
Blogger Templates