Kijiji cha Magozi chenye wakulima
zaidi ya 1000 wanaolima mpunga kwa kutumia kilimo cha umwagiliaji ambao
unasababisha bwawa la mtera kukosa maji kutoka mto Ruaha kwa sababu za
kilimo cha umwagiliaji. Pamoja na wakulima Hawa pia wapo wakulima wa
Mbalali mkoa wa Mbeya ambao wote kutokana na shughuli hizo za kilimo
husababisha ufuaji umeme kukwama katika bwawa la Mtera na Kidatu
mkoani Morogoro.
Waziri wa Nishati na Madini
Profesa Sospeter Mwijarubi Muhongo kushoto anayezungumza na Richard
Kasesela Mkuu wa wilaya ya Iringa alitembelea bonde hilo na kukagua
shughuli za kilimo zinazoendelea katika bonde hilo na kusababisha
upotevu wa maji katika mto Ruaha ambao unapeleka maji katika mabwawa ya
kufua umeme Mtera, Mkuu wa wilaya ya Iringa ameitisha mkutano wa wadau
wote siku ya jumatatu tarehe 21 mwezi huu . ili kufanya majadiliano na
kupanga mkakati wa Kuokoa bwawa la mtera.
Waziri wa Nishati na Madini
Profesa Sospeter Mwijarubi Muhongo akikagua eneo hilo na Mkuu wa Wilaya
ya Iringa Mh. Richard Kasesela leo.
Waziri wa Nishati na Madini
Profesa Sospeter Mwijarubi Muhongo akizungumza na baadhi ya wakulima hao
wakati alipokagua bonde hilo kulia anayemsikiliza ni Mkuu wa wilaya ya
Iringa Mh. Richard Kasesela.
Waziri wa Nishati na Madini
Profesa Sospeter Mwijarubi Muhongo akizungumza na mkuu wa wilaya ya
Iringa Mh. Richard Kasesela wakati alipotembelea bonde la Usangu lenye
shughuli za kilimo cha Umwagiliaji.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh.
Richard Kasesela akimwelezea jambo waziri wa Nishati na Madini wakati
alipokagua bonde la Usangu katika kijiji cha Magozi chenye wakulima wa
mpunga zaidi ya 1000.
0 comments:
Post a Comment