Pages

Ads 468x60px

Tuesday, November 17, 2015

SERIKALI YAIPONGEZA JUHUDI ZINAZOFANYWA NA TAASISI YA

DSC_1839
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Saidi Meck Sadiki akizungumza mbele ya wanahabari, madaktari na baadhi ya akina mama waliokuwa na watoto waliozaliwa kabla ya wakati maarufu kama Njiti (Hawapo pichani). Kushoto ni DoriS Mollel ambaye ni Mwanzilishi na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation (DMF) na wengine ni maafisa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Muhimbili wakishuhudia tukio hilo maalum la taasisi ya DMF ilipotoa vifaa hivyo katika kitengo cha Jengo la Watoto.
DSC_1865
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Meck Sadik akipata maelezo juu ya vifaa hivyo vilivyotolewa na Taasisi ya DMF.
DSC_1870
Msimamizi wa wodi ya akina mama wanaopatiwa huduma ya Kangaroo dhidi ya watoto wao ambao walizaliwa njiti, akimpatia maelezo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alipotembelea wodi hiyo leo.
DSC_1924
Picha ya juu na chini Mkuu wa Mkoa wa Dar e Salaam akiwafariji baadi ya wakinamama waliojifungua watoto kabla ya wakati maarufu njiti wakati alipotembelea wodi hiyo ya watoto mapema leo.
DSC_1929
DSC_1939
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akimpatia zawadi ambayo ni jozi ya soksi kwa ajili ya kusaidia watoto njiti kwa mmoja wa wamama waliokuwa katika wodi hiyo ya watoto njiti.

MWANAMITINDO WA KIMATAIFA MIRIAM ODEMBA KUWA JAJI MAALUM


Maandalizi ya fainali ya shindano la Miss Universe Tanzania 2015 bado yanaendelea Mwanamitindo wa Kimataifa Miriam Odemba atakuwa jaji maalum katika kinyang’anyiro hiki cha kumpata mrembo wa Miss Universe Tanzania 2015. 
Majaji wengine watakaoshiriki katika kumtafuta mnyange wa mwaka huu ni Sheria Ngowi, Maria Sarungi Tsehai, Mariam Ndaba na Priyal wa sia couture.

Zoezi la usaili limeshakamilika na hatimaye kupata warembo watakaojiunga na kambi ya Miss Universe kesho siku ya jumatano kabla ya fainali tarehe 20 mwezi huu.

Warembo waliobahatika kuingia kambini ni 14 tu, majina na mikoa waliyotoka kwenye mabano Mariam Isack (Dar es salaam), Lilian Luth(Dar es salaam), Stacey Sulul(Dar es salaam),Willice Donard(Dar es salaam), Lorraine Marriot(Dar es salaam), Dalena David(Dar es salaam), Mercy Zephania(Dar es salaam), Dinnah Kaijage(Dar es salaam), Melody Typhone(Dar es salaam), Joselyn Mirashi(Arusha), Nancy Matta(Mbeya), Christina Shimba(Iringa), Belinda (Mwanza).

 Mwaka huu Miss Universe imefanya usaili katika mikoa sita tofauti ikiwamo Tanga, Iringa, Mbeya, Arusha, Mwanza na Dar es salaam.

DK. TULIA NJIA NYEUPE UNAIBU SPIKA


 Dk. Tulia Ackson amepita bila kupingwa baada ya kuchaguliwa na wabunge wa CCM kugombea nafasi ya Unaibu Spika katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Mmoja wa wagombea wa nafasi ya Unaibu spika Bahati Abeid akizungumza mbele ya wabunge wa CCM.
 Mhe. Mariam Kisangi akizungumza mbele ya wabunge wa CCM kwenye ukumbi wa NEC mjini Dodoma ambapo yeye pamoja na Bahati Abeid walijitoa na kumpa nafasi Dk.Tulia Ackson kupita bila kupingwa
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiongea wakati wa kuendesha zoezi la kumpata Naibu Spika  kwenye ukumbi wa NEC, CCM Makao Makuu mjini Dodoma.

RAIS MAGUFULI ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO KATIKA UBALOZI WA UFARANSA NCHINI


po1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Ufaransa nchini kufuatia vifo vya Watu zaidi 130 vilivyotokana na mashambulizi ya kigaidi.
po2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Malika Berak kufuatia vifo vya Watu zaidi 130 vilivyotokana na mashambulizi ya kigaidi.
po3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Ufaransa nchini Malika Berak Tanzania mara baada ya kusaini Kitabu cha Maombolezo na kutoa salamu za pole kwa Rais wa Ufaransa Mheshimiwa Francois Hollande kufuatia vifo vifo vya Watu zaidi 130 vilivyotokana na mashambulizi ya kigaidi.
po4
. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wa pili akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Ufaransa (kushoto) pamoja na Maofisa mbalimbali wa Ubalozi huo mara baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo.
po5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Malika Berak mara baada ya kusaini kitabu cha Maombolezo Ubalozini hapo.
………………………………………………………………………………..
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli amesaini kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es salaam kufuatia vifo vya watu zaidi 130 vilivyotokea November 15, 2015 kutokana na mashambulizi ya ugaidi mjini Paris, Ufaransa.
  Pamoja na kutia saini kitabu cha maombolezo, Mheshimiwa Dr. Magufuli ametoa salamu za pole kwa Rais wa Ufaransa Mheshimiwa Francois Hollande na kumuombea uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu Dokta Magufuli ambaye amepokelewa na Balozi wa Ufaransa hapa Nchini Bibi Malika Berak amesema Tanzania imeguswa na vifo hivyo na inaungana na Ufaransa katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
  Aidha Rais Magufuli amewaombea majeruhi wote wa tukio hilo wapone haraka ili waweze kuungan a na familia zao na kuendelea na shughuli zao za kila siku Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli amewasili Mjini Dodoma jioni hii kwa shughuli mbalimbali za kikazi.
  Mheshimiwa Magufuli amesafiri kwa gari kutoka Dar es salaam hadi Dodoma na taarifa ya shughuli atakazozifanya mtaarifiwa baadaye.
Imetolewa na; Gerson Msigwa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, IKULU November 17, 2015

KOBE 201 WALIOKUWA WAKISAFIRSHWA NJE YA NCHI WAKAMATWA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA J.K NYERERE


Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru akikagua mabegi matano yenye Kobe 201 yaliyokamatwa usiku wa kuamkia leo na askari wanyamapori kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama katika uwanja wa Kimataifa wa J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam.  

Watuhumiwa hao wa usafirishaji wa wanyamapori wametajwa kuwa ni David Mungi mkazi wa Muheza Mkoani Tanga na Mohammed Suleiman (43) mkazi wa Zanzibar ambao katika tukio hilo walishafanikiwa kupita kwenye mitambo ya ukaguzi lakini mbwa maalum (sniffer dogs) wakasaidia kugundua uhalifu huo. Kwa pamoja watuhumiwa hao walikamatwa na tiketi za kusafiria kuelekea nchini Malaysia. 
Kobe wapatao 201 waliokamatwa na askari wanyamapori kwa ushirikiano na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kutumia mbwa maalum (sniffer dogs).   
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Dorina Makaya kulia na Mmoja wa Askari wanyamapori wakiangalia kobe 103 waliotelekezwa eneo la Tabata hivi karibuni baada wahalifu waliohusika kuhofia kukamatwa na vyombo vya dola. 
(Picha na Hamza Temba - Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Maliasili na Utalii)

Jaji mkuu wa Tanzania akutana na watendaji wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi


 
Jaji mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman (wa tatu kutoka kulia) katika picha ya pamoja na watendaji kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi walipomtembelea ofisini kwake hivi karibuni, Kulia kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Alphayo Kidata akifuatiwa na Subira Sinda Msajili wa Hati. Nyuma ya Katibu Mkuu ni David Mushendwa Kamishna wa ardhi Msaidizi Sheria, Blasia Kibano (Wa kwanza kulia) aliyekuwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Sheria pamoja na Juma Lughela.

SERIKALI KUBORESHA HUDUMA YA MAJI KWA WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM.


Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Maji, Athumani Sharif akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mikakati ya Serikali kutatua tatizo la upatikanaji wa maji jijini Dar es Salaam mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa. (Picha na Fatma Salum.)

Na. Georgina Misama - Maelezo
SERIKALI  inatarajia kuzalisha maji lita milioni 270 kwa siku baada ya kukamilika kwa mradi wa upanuzi wa Chanzo cha Maji cha Ruvu Chini na upanuzi wa mtambo wa kusafishia maji.

Mradi huo  unaotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Kimarekani la Millenium Challenge Co-operation umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 66.24 na unatarajiwa kukamilika wakati wowote baada ya kukamilika kwa kazi ya kulaza bomba linalosafirisha maji toka Ruvu chini kuja Jijini Dar es Salaam.

Akiongea na waandishi wa habari, leo Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Maji, Bw. Shariff Athumani amesema kwamba mradi wa upanuzi wa mtambo wa ujenzi wa bomba la Ruvu Chini utapunguza kero ya maji kwa wakazi wote wanaotumia maji kutoka Ruvu Chini.

Akiyataja maeneo yatakayofaidika na kukamilika kwa mradi huo ni pamoja na Bagamoyo na vitongoji vyake, Bunju, Mabwepande, Boko, Tegeta Kunduchi na Mbezi Beach. Maeneo mengine ni pamoja na Mbezi Juu, Salasala, Kawe, Makongo, Chuo Kikuu, Mikocheni, Msasani, Masaki, Mwananyamala, Kinondoni, Magomeni, Sinza, Manzese, Ubungo, Mabibo, Kigogo, Buguruni, Ilala, Kurasini, Bandarini na maeneo yote ya katikati ya jiji la Dar es Salaam.

NEC YATANGAZA VITI VYA MADIWANI WATEULE1393

              Mkurugenzi wa Uchaguzi wa  NEC Bw. Kailima Ramadhani                           akizugumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya  viti maalumu vya Udiwani ambavyo Madiwani wake wameteuliwa na Tume hiyo  ni viti 1393, kutoka katika Vyama vya CCM,CHADEMA,NSSR-MAGEUZI pamoja na CUF.Mkutano huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam ,Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Huduma za Sheria wa NEC Emmanuel Kawishe.

Waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Uchaguzi wa  NEC Bw. Kailima Ramadhani
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii)

TUME ya Taifa ya Uchaguzi( NEC) imesema hadi sasa viti maalumu vya Udiwani ambavyo Madiwani wake wameteuliwa na Tume hiyo  ni viti 1393, kutoka katika Vyama vya CCM, CHADEMA, NSSR- MAGEUZI  pamoja na CUF.

Hayo yamesemwa leo Jijijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka NEC Bw. Kailima Ramadhani wakati akitoa  taarifa kwa Umma kuhusu uteuzi wa madiwani wanawake wa Viti Maalumu.

Aidha Bw.Ramadhani amesema kuwa idadi ya Viti maalumu Vya Udiwani ni  1,408 nakwamba kutokana na majimbo nane na kata thelathini na Nne ambapo  Uchaguzi haujakamilika kwa Sababu mbalimbali, hatua hiyo itasababisha kubakia viti 15 ambavyo vitagawanywa mara baada ya Uchaguzi kukamilika ili kufikia idadi ya viti 1,408 kutoka viti 1393 vinavyo tambulika kwa sasa.

Aidha amefafanua kuwa kutokana na Viti hivyo  Maalumu Vya Udiwani Vilivyoteuliwa  na NEC, Chama Cha Mapinduzi CCM kimepata viti 1,022,Chama Cha Demokrasia na Mawendeleo CHADEMA 280,Chama Cha Wananchi CUF-79, ACT WAZALENDO viti 6 pamoja na NSSR  MAGEUZI viti 6.

Amesema kuwa tume imeamua kutoa taarifa ya uteuzi wa  viti maalumu Vya Udiwani Nchi nzima ya Madiwani waliyoteuliwa na Tume  kutokana na Kanuni za Kudumu za Mikutano ya Halmashauri, Mabaraza ya Madiwani yanatakiwa kuitishwa siku thelathini tangu tarehe ya Uchaguzi ifanyike.

Katika hatua Nyingine Mkurugenzi huyo wa Uchaguzi  NEC amesema kuwa  mwisho wa Uchaguzi katika Majimbo na Kata ambazo hazikufanya Uchaguzi ni Desemba 20 mwaka huu, ambapo katika jimbo la Uranga Mashariki pamoja na Lushoto uchaguzi utafanyika Novemba 22 mwaka huu,nakuwaomba  Wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili kuchagua kiongozi wanaomtaka.

SIKU YA WATOTO NJITI


 Mwanzilishi wa Mfuko wa Doris Mollel, Doris Mollel akizungumza katika kilele cha maazimisho ya siku ya watoto waliozaliwa kabla ya siku (njiti) katika mkutano ambao umefanyika leo kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH). Kulia ni mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick akizungumza kwenye maadhimisho hayo leo.
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja, Aminiel Aligaesha akifuatilia mkutano huo leo pamoja na wauguzi waandamizi wa hospitali hiyo.

JAMVI LA VIJANA LA UMATI MWEZI HUU LIMEKUWA CHACHU YA KUHAMASISHA VIJANA KATIKA MASUALA YA AFYA YA UZAZI


 Vijana wa YAM ( Youth Action Movement) ambao ni waandaaji wa tamasha hili linalofanyika kila mwezi wakionesha igizo lao lililobeba ujumbe unaosema ni jukumu la wazazi kuwaelimisha vijana juu ya afya ya uzazi na ujinsia ili kuwakinga na maambukizi ya VVU mimba katika umri mdogo na ngono katika umri mdogo.
Mwenyekiti wa UMATI dar es salaam Mr.Harith Shomvi ambae alikuwa mgeni rasmi  katika tamasha hilo akihutubia wananchi na kuwasisitiza wapate huduma za uzazi wa mpango na upimaji ambazo zilikuwa zikitolewa bure katika tamasha hilo. Tamasha hilo lilikuwa na kauli mbiu isemayo "JE kutoa  elimu  juu ya afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana ni jukumu la nani?

VODACOM YAJIZATITI KUBADILISHA MAISHA YA WATANZANIA KUPITIA TEKNOLOJIA


 Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari alipokuwa akitangaza mikakati ya kampuni hiyo kuipeleka Tanzania katika ulimwengu wa teknolojia na itakavyotumia kubadilisha maisha ya watanzania na kuwa bora zaidi.Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya waandishi wa habari na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania, wakiwa katika mkutano wa waandishi wa habari na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Ian Ferrao (hayupo pichani)alipokuwa akitangaza mikakati ya kampuni hiyo kuipeleka Tanzania katika ulimwengu wa teknolojia na itakavyotumia kubadilisha maisha ya watanzania na kuwa bora zaidi.Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.

JOB NDUGAI NDIYE SPIKA MPYA WA BUNGE LA 11 LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Hatimaye Job Yustino Ndugai CCM amechaguliwa kuwa Spika wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuchaguliwa kwa kura 254 sawa na asilimia 70% ya kura zilizopigwa akifuatiwa na mgombea wa CHADEMA Goodluck Ole Medeye ambaye amepata kura 109.

Hata hivyo wagombea hao ambao walikuwa 7 kati ya 8 wameweza kutoa shukrani na pongezi kwa Ndugai wakisema anastahili na ndio maana akachaguliwa na kumtaka aongoze vyema bunge hilo.

 Job Ndugai ameibuka mshindi wa kiti cha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupata kura 254 sawa na asilimia 70 ya kura zote ambapo jumla ya kura zilizopigwa ni 365

Matokeo ya kura za Spika.

A: Job Ndugai (CCM)- 254
B: Goodluck Ole Medeye (CHADEMA) - 109
C: Hashimu Rungwe (CHAUMA)- 0
D: Peter Sarungi (AFP) -0
E: Dkt Godfrey Malisa (CCK)- 0
F: Richard Lymo (T.L.P) -0
G: Robert Kisinini (DP) -0
Kura zilizoharibika ni 2
 
Blogger Templates