Pages

Ads 468x60px

Saturday, December 5, 2015

NEWS ALERT: WATUMISHI NANE WA TRA WAPANDISHWA KIZIMBANI LEO


Mshitakiwa namba moja katika kesi ya kuhujumu uchumi, Tiagi Masamaki (katikati) na washitakiwa wenzake wakitoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam leo mchana baada ya kusomewa mashitaka yao.

MAOFISA wanane wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), akiwemo Kamishna wa Forodha wa mamlaka hiyo Tiagi Masamaki (56) wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kutoa makontena 329 bandarini bila ya kulipiwa kodi na kuisababishia Serikali hasara ya sh. bilioni 12.7 za kitanzania.

Ukimuondoa Masamaki maofisa wengine waliopandishwa kortini ni Habibu Mponezya (45) Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja,Bulton Mponezya (51) 

Wakili wa Serikali Mwandamizi Christopher Msigwa akisaidiana na Peter Vitalis ameadi leo mchana mbele ya Hakimu Mkazi Huruma Shahidi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kuwa watuhumiwa hao wanatuhumiwa kwa makosa mawili.

Alidai makosa mawili ya uhujumu uchumi ni kula njama ya kuidanganya Serikali na kuisababishia Serikali hasara. Kesi hiyo ni namba 35/2015 ya uhujumu uchumi. 

Ilidaiwa katika shtaka la kwanza katika tarehe tofauti kati ya Juni 1 na Novemba 17 mwaka huu, sehemu isiyojulikana ndani ya Jiji la Dar es Salaam kwa pamoja walikula njama ya kuidanganya Serikali kuwa sh. bilioni 12.7 zimetolewa kwa kutoa makontena 329 katika Bandari Kavu ya Azam, baada ya kodi zote kutolewa.

Katika shtaka la pili, washtakiwa wanatuhumiwa katika ya Juni Mosi na Novemba 17 mwaka huu ndani ya Jiji la Dar es Salaam walishindwa kutimiza majukumu yao kwa namna inavyotakiwa na kusababisha Serikali kupata hasara ya sh. bilioni 12.7.

Baada ya washtakiwa hao kusomewa makosa yao, Hakimu Shahidi aliwaeleza kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, kwa hiyo hawatakiwi kujibu chochote kama kweli au si kweli.
Aliongeza kuwa Mahakama Kuu ndiyo inamamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, kwa hiyo kama wanataka dhamana wapeleke maombi ya dhamana katika mahakama hiyo.
"Kama mnataka dhamana pelekeni maombi Mahakama Kuu kwa sababu mahakama hii hawezi kutoa dhamana," alisema Hakimu Shahidi 
Hata hivyo, upande wa utetezi ulidai kuwa kesi hiyo ifikishwa mahakamani hapo bila kibali na pia waliomba mshtakiwa namba nne Mrema anamtoto mchanga kwa hiyo wanaiomba mahakama imfikirie.
Wakili Msigwa alidai upelelezi bado unaendelea, wanaomba tarehe nyingine ya kutajwa. Kesi hiyo itatajwa Desemba 17 mwaka huu kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika
Watuhumiwa hao wakisindikizwa na maofisa wa polisi kuingia chumba cha Mahabusu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Hapa Masamaki na wenzake wakiingia ndani ya gari kuelekea gereza la Segerea.

WAFANYAKAZI 35 WASIMAMISHWA KAZI TRA,KAMPUNI 43 ZABAINIKA KUKWEPA KODI.


Kaimu Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dk. Philip Mpango akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika mkutano na 
Kaimu Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dk. Philip                                               Mpango jijini Dar es Salam leo.

Na ChalilaKibuda,Globu ya Jamii
BAADA ya Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa kufanya ziara ya kushitukiza katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kubaini upotevu wa Makontena 329, mapya yaibuka kwa Makampuni 43 kuhusika kukwepa kodi ya Sh.Bilioni 12.6 katika Bandari Kavu inayomilikiwa na Said Salim Bakh ressa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dk. Philip Mpango amesema kuwa kampuni hizo 43 zilipitishiwa Kontena katika Bandari Kavu ya Said Salim Bakhressa na kutaka ndani ya siku sita kuanzia leo kampuni zote ziwe zimeshalipia kodi kutokana na idadi ya kontena.

Dk. Mpango amesema katika kampuni ambazo zilizokwepa kodi ambazo zilipitisha Kontena 329 wameshalipa zaidi ya Sh. Bilioni Tano(5) ambapo wanatakiwa kulipa kodi iliyobaki kuweza kumaliza kodi ya Sh.Bilioni 12.6 kwa kipindi alichoweka Rais Dk .John Pombe Magufuli. 

Amesema kuwa hatilafu za kupotea kwa makontena hayo, kazi hiyo walishakuwa wameanza kwa bahati mbaya Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa Majaliwa aliwawahi wakati alipofanya ziara katika mamlaka hiyo.

Kampuni zilizokwepa Kodi ya mapato kwa makontena 329 ni Lotai Steel Tanzania LTD yenye makontena 100,Tuff Tyres Centre Company kontena 58 Binslum Tyres Company LTD, Kontena 33, Tifo Global Mart (Tanzania) Company Limited Kontena 30,IPS Roofing Campany Ltd Kontena 20,Rashywheel Tyre Center Com.Ltd Kontena 12, Kiungani Trading Company Ltd 10 Homing International Limited Kontena 9, Red East Building Kontena Saba,Tybat Trading Co Ltd, Kontena Tano,Zing Ent Ltd,Kotena Nne,Juma Kassem Abdul, Kontena Tatu, Salum Continental Co.Kontena Mbili, Zuleha Abbas Ali Kotena Mbili na Snow Leopard Building Kontena mbili na waliobaki walikuwa na kontena moja moja.

Hata hivyo TRA imewasimamisha kazi watu 35 wakiwemo 27 waliokamatwa katika geti namba tano ambao hadi sasa wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano na uchunguzi .


Aidha amewataka wafanyakazi kuwasilisha mali zao ili kuweza kuangalia uwezo wake katika utumishi kama zinaendana na umiliki huo.

Serikali yaahidi kuendelea kuweka mazingara bora na wezeshi katika Tasnia ya Filamu


 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Mwamini Juma Malemi (katikati) akizungumza na wasanii pamoja na wadau wa filamu (hawapo pichani) wakati wa kufungua kikao cha wadau wa Filamu kujadili namna ya kuimarisha na kuboresha miundombinu katika tasnia ya filamu leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fisoo na kulia ni Rais wa Shirikisho la Filamu Nchini Bw. Simon Mwakifwamba
 Wasanii na wadau wa filamu wakisikiliza kwa makini mada zilizokua zikiendelea wakati wa kikao cha wadau wa Filamu kujadili namna ya kuimarisha na kuboresha miundombinu katika tasnia ya filamu leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Mwamini Juma Malemi (katikati waliokaa) katika picha ya pamoja na wasanii na wadau wa filamu nchini leo jijini Dar es Salaam baada ya kufungua  kikao cha wadau wa Filamu kujadili namna ya kuimarisha na kuboresha miundombinu katika tasnia ya filamu. Wapili kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fisoo na wapili kushoto ni Rais wa Shirikisho la Filamu Nchini Bw. Simon Mwakifwamba.

 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Mwamini Juma Malemi (kushoto) akiwasili kuelekea kufungua kikao cha wadau wa Filamu kujadili namna ya kuimarisha na kuboresha miundombinu katika tasnia ya filamu leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fisoo na kulia ni Rais wa Shirikisho la Filamu Nchini Bw. Simon Mwakifwamba.

MAGEREZA KUHAMASISHA UTALII WA NDANI KATIKA MIAKA 54 YA UHURU WA TANGANYIKA


KAZ1 
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza John Minja akiwasilia katiki viwanja vya Magereza Mkoa wa Kilimanjaro kwa ajili ya hafla ya kukabishi bendera kwa watumishi 39 wa Jehi hilo wanaotarajia kuadhimisha miaka 54 ya Uhuru wa Tanganyika kwa kupanda Mlima Kilimanjaro.
KAZ2 
Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja akikabidhi bendera ya Magereza kwa kiongozi wa Msafara Kamishna Msaidizi wa Magereza Alexander Mmasy leo tarehe 04/12/2015 wakiwa wanajiandaa kupanda Mlima tarehe 06/12/2015 ili ifikapo tarehe 09 siku ya Uhuru wa Tanganyika wawe kileleni
KAZ3 
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza John Minja akitoa nasaha kwa wapanda mlima wa Jeshi la Magereza (Hawapo pichani)
KAZ4 
Baadhi ya wadau wa Magereza Utalii Klabu walio tayari kupanda Mlima Kilimanjaro wakisikiliza kwa makini nasaha za Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja katika hafla ya kukabidhiwa bendera ya Jeshi hilo kuipeleka katika Kilele cha Mlima huo.

KAZ5 
Baadhi ya wadau wa Magereza Utalii Klabu walio tayari kupanda Mlima Kilimanjaro wakiimba nyimbo za hamasa baada ya kupokea bendera kutoka kwa Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja katika hafla ya kukabidhiwa bendera ya Jeshi hilo kuipeleka katika Kilele cha Mlima huo.
KAZ6 
Wapanda Mlima Kilimanjaro wa Jeshi la Magereza wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Jeshi la Magereza John Minja (Katikati),wa tatu kulia ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Arusha SACP Hamis Nkubasi, na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kilimanjaro SACP Venant Kayombo, wa tatu kushoto ni Mnadhimu Mkuu wa Magereza Mkoa
KAZ10 
Wadau wa Magereza Utalii Klabu wakiwa katika mazoezi mbalimbali ya kukimbia na kutembea katika viunga vya mji wa Moshi ikiwa ni maandalizi ya kuelekea katika kilele cha Mlima Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 54 ya Uhuru wa Tanganyika sambamba na kuamasisha utalii wa ndani.
KAZ12 
Picha zote na Mrakibu Msaidizi wa Magereza Deodatus Kazinja na Koplo Mfaume Abdalah wa Jeshi la Magereza
……………………………………………………………………………………………..
Na Deodatus Kazinja Katika kuadhimisha miaka 54 ya uhuru wa Tanganyika tarehe 9 Desemba watumishi wapatao 39 Jeshi la Magereza wakiwa katika uwiano wa wanaume 30 na wanawake 9 wataadhimisha siku hiyo kwa kupanda mlima Kilimanjaro na kutembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro.
  Washiriki hawa wanatoka katika vituo vya Makao Makuu ya Magereza, Chuo cha Taaluma ya urekebishaji Ukonga Dar es salaam, Kikosi Maalum cha Kutuliza Gasia Magereza (KMKGM), Pwani, Dar es salaam, Iringa, Mbeya, Mara, Tabora, Tanga, Kilimanjaro na Arusha ambao kwa gharama zao wameamua kuadhimisha miaka 54 ya uhuru wa Tanganyika kwa kufanya utalii wa ndani.
  Akiongea na waandishi wa habari Kamishna Jenerali wa Magereza nchini John Casmir Minja katika hafula fupi ya kuwakabidhi bendera watumishi hao katika viwanja vya Magereza Mkoa wa Kilimanjaro amesema amefurahishwa mno na uamuzi wa askari hao kwa vile unalitangaza Jeshi la Magereza nje ya mipaka yake.Kamishna Minja alisema pia mbali na kulitangaza Jeshi la Magereza unawaweka timamu watumishi hao katika kufanya kazi zao vizuri ikiwa ni kuunga kauli mbiu ya serikali ya Awamu ya Tano ya Hapa Kazi tu.
  Aidha Kamishna huyo alitumia fursa hiyo kuishukuru serikali kwa namna ambavyo imekuwa ikijitolea kulisaidia Jeshi la Magereza ambapo alitoa taarifa kuwa tayari mikataba ya kununuliwa magari yapatayo 905 na ujenzi wa nyumba za watumishi zipatazo 9500 imesainiwa na magari yataanza kuingia mapema Januari 2016.
  Kwa upande wake mwenyekiti wa Magereza Utalii Klabu ambaye pia ni Mhasibu Mkuu wa Jeshi la Magereza Ndugu Estomih Hamis mbali na kumshuruku Kamishna Minja akwa namna ambavyo amejitolea katika kufanikisha uanzishwaji wa Klabu hiyo kuelezea dhima nzima ya utalii huo.
  “ Tumeamua kuadhimisha miaka 54 ya uhuru wa Tanganyika kwa mfumo huu kwa sababu kadhaa. Mosi , ni kuunga mkono jitihada za serikali za muda mrefu za kuhamasisha utalii wa ndani ambacho ni chanzo kimojawapo cha kuongeza mapato ya ndani ya serikali” “Pili, ni kuleta mwamko kwa watumishi wa umma na watanzania kwa ujumla katika kutembelea vivutio vya utalii vya ndani kuliko ilivyo sasa ambapo sehemu kubwa ya watalii ni wageni kutoka nje ya Tanzania”
  Aidha, ndugu Hamis aliongeza kuwa zoezi la upandaji mlima Kilimanjaro ni zuri kwa kuimarisha afya za watumishi hivyo kujiepusha na magonjwa kama vile kisukari, shinikizo la damu na utimamu wa mwili na hasa kwa askari wanaotakiwa kuwa hivyo muda wote. Tukio la watumishi wa Magereza kupanda mlima Kilimanjaro litakuwa ni la pili kwa mwaka huu ambapo mara ya mwisho walipanda mlima tarehe 6 March, 2015 wakiwa ni jumla ya watumishi 20 ambapo 16 walifanikiwa kufika kileleni na wanne kurudia njiani kwa sababu mbalimbali.
  Zoezi la upandaji mlima lililopita lilifanyika kwa mafanikio makubwa kiasi cha kuibua hoja y wa unndwaji wa chombo cha pamoja kinachoweza kuratibu shughuli za utalii ndani ya Jeshi la Magereza kwa kuwaunganisha watumishi wote.
  Hoja hiyo ilifanikiwa kwa kuundwa kwa Klabu ya Utalii ya Magereza, klabu ambayo iko katika hatua za mwisho za usajili. Tayari Klabu hiyo inao viongozi wakiongozwa na Mwenyikiti ndugu Hamis, katibu wake akiwa ni Mkaguzi wa Magereza Dominick Mshana na Mweka Hazina ni Mrakibu Msaidizi wa Magereza Erasto Kipingu. Nani analipa gharama za utalii huo?
  Akijibu swali hilo katibu wa Klabu hiyo Mkaguzi Mshana alisema kwa hivi sasa watumishi hao wanapanda kwa gharama zao wenyewe kutoka katika mishahara yao ambapo karibu kila mshiriki amechanga wastani wa shilingi 300,000.Mshana amesema ni matumaini yake kuwa katika siku za mbeleni kama watapatikana wadhamini gharama hizo zinaweza kupungua sana kutoka mifukoni mwa washiri. 
  Aidha amesema gharama za kupanda mlima na kutembelea vivutio vingine kwa ujumla ni kubwa kwa mtu mmoja mmoja lakini kunakuwa na unafuu mkubwa watu wakipanda kama kikundi.

Benki ya ADB yatoa mkopo wa bilioni 750 kwa Tanzania kwa ajili miradi miwili ya maendeleo





LI1Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile kushoto akisaini mkataba kutoka Benki ya Maendeleo Afrika kwa ajili ya Mradi wa Ujenzi ,kulia ni mwakilishi wa benki hyo Dkt. Tonia Kandiero akitia saini wakati wa makabidhiano hayo leo jijini Dar es salaam.
LI2 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile kushoto akikabidhiana hati ya makubaliano ya msaada wa fedha kwa ajili ya mradi wa ujenzi na mwakilishi wa benki hyo Dkt. Tonia Kandiero wakati wa makabidhiano hayo leo jijini Dar es salaam.
LI3 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile kushoto akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa makabidhiano ya fedha kwa ajili ya mradi wa ujenzi kulia akiwa na mwakilishi wa benki hyo Dkt. Tonia Kandiero wakati wa makabidhiano hayo leo jijini Dar es salaam.
LI4 
Mtendaji Mkuu wa wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale akiongea na waandishi wa habari baada ya makabidhiano ya fedha kwa ajili ya mradi wa ujenzi uliofanyika leo jijini Dar es salaam.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AMWAKILISHA RAIS MAGUFULI KWENYE MKUTANO WA TANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA NA CHINA, JIJINI JOHANNESBURG LEO.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Rais wa China, Xi Jinping, wakati wa Mkutano Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China (China-Africa Forum) uliofanyika leo Dec 4, 2015 jijini Johannesburg. Mhe. Samia amemwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (mwenye kitambaa cheupe) akiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China (China-Africa Forum) uliofanyika leo Dec 4, 2015 jijini Johannesburg. Mhe. Samia amemwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (mwenye kitambaa cheupe katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wakuu wa Nchi za Afrika baada ya ufunguzi wa Mkutano huo Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China (China-Africa Forum) uliofanyika leo Dec 4, 2015 jijini Johannesburg. Mhe. Samia amemwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan (kulia) akiwa katika mazungumzo na Rais wa Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi, walipokutana kwenye ufunguzi wa Mkutano huo Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China (China-Africa Forum) uliofanyika leo Dec 4, 2015 jijini Johannesburg. Mhe. Samia amemwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Shulu Hassan, akisalimiana Mwambata wa Kijeshi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini (Defence advisor) Brig. Gen Ibrahim A. Kimario, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Olver Tambo jijini Johanesburg jana Desemba 3, 2015 kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini, Radhia Msuya.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Shulu Hassan, akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini, Radhia Msuya, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Olver Tambo jijini Johannesburg jana Desemba 3, 2015 kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China.

 Baadhi ya washiriki katika Mkutano huo kutoka nchi mbalimbali za Afrika waliohudhuria ufunguzi wa mkutano huo leo jijini Johannesburg.

Mkutano wa 10 wa uhamaji kutoka mfumo wa Analogia kwenda Digitali kwa nchi za SADC wahitimishwa jijini Dar es salaam.

 Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji wa Serikali Bw. Assah Mwambene akifunga Mkutano wa 10 wa  uhamaji kutoka mfumo wa Analogia kwenda Digitali kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kwa niaba ya Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo jana. Tanzania imepata heshima ya kuwa mwenyeji wa mkutano huo baada  ya  kuonekana kufanya vizuri katika uhamaji wa matumizi ya mfumo wa analogia kwenda digitali kwa wakati.
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji wa Serikali Bw. Assah Mwambene (katikati) akiwaonesha jambo kupitia Kitumi chake cha Mkononi (IPAD) Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Ally Simba (kulia) na Naibu Mkurugenzi wa Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) Bw. Fredrick Ntobi (kushoto) kabla ya kufungwa kwa Mkutano wa 10 wa uhamaji kutoka mfumo wa Analogia kwenda Digitali kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) jijini Dar es salaam.
 Washiriki wa Mkutano wa 10 wa uhamaji kutoka mfumo wa Analogia kwenda Digitali kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa mkutano huo jijini Dar es salaam.
Mada mbalimbali zikiwasilishwa kwa washiriki wakati wa  Mkutano wa 10 wa uhamaji kutoka mfumo wa Analogia kwenda Digitali kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) jijini Dar es salaam.

KITUO CHA RADIO CHA HITS FM RADIO CHATIWA MOTO NA WATU WASIO JUULIKANA USIKU WA JUZI



HI1 
Vifaa  vyote vya kutangazia katika Studio ya Hits FM Radio vilivyoteketea kwa moto usiku wa juzi  katika studio hiyo mara baaada ya kuvamiwa na watu wasipjuulikana  huko Migombani Mjini Zanzibar
HI2 Waandishi wa habari wakisikiliza kwa makini maelezo yanayotolewa na Mkuu wa kituo cha  Hits FM Mohammed Abdallah hayupo pichani mara baada ya kuunguzwa kituo cha  Radio hiyo.
HI02Mwandishi  wa habari akimuhoji Mkuu wa Utawala wa Afisi kuu ya CCM FM Salum Khatibu Reja alipofika katika kituo cha Radio ya Hits FM na kujionea hali ya kituo hicho.
HI3 
Waandishi wa habari wakisikiliza kwa makini maelezo yanayotolewa na Mkuu wa kituo cha  Hits FM Mohammed Abdallah hayupo pichani mara baada ya kuunguzwa kituo cha  Radio hiyo.
HI4 
Mwenyeki ti wa MCT Suleiman Seif katikati akifafanuwa  jambo  kwa waandishi wa habari kuhusiana  na kutiwa moto  Hits FM Radio  usiku wa juzi iliyopo Migombani Mjini Zanzibar. 

MRATIBU UN ARIDHISHWA NA MATUMIZI YA UFADHILI TABORA



IMG_5494
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiendelea na ukaguzi wa Bwawa hilo.
IMG_5496Muonekano wa mradi wa ujenzi wa Bwawa la Charco la Nguvumoja.
IMG_5520 
Wananchi wakiendelea kuchimba bwawa hilo.
IMG_5447 
Ofisa Kilimo na Ushirika wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Samaluku Joseas (kushoto) akisoma taarifa ya maendeleo ya miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa katika mkoa wa Tabora. Pichani wa pili kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Afisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan (wa tatu kushoto) wakipitia taarifa hiyo kwa pamoja kabla ya kuelekea kukagua miradi hiyo.


IMG_5482Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa tatu kushoto) aliyeambatana na Afisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan (wa pili kushoto) walipowasili kukagua mradi wa ujenzi wa Bwawa la Charco la Nguvumoja kwa mtindo wa utoaji wa chakula kutoka Shirika la Chakula Duniani (WFP) kwa kazi inayofanywa na mradi wa misitu ya Miyombo. Kushoto ni Ofisa Tawala msaidizi anayeshughulikia Uchumi na Tija wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Dkt. Phillips Mtiba pamoja na Ofisa Kilimo na Ushirika wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Samaluku Joseas (wa pili kulia).
IMG_5486
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiendelea kupata maelezo ya mradi huo.

IMG_5532Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nguvumoja watakaonufaika na mradi wa bwawa hilo.
IMG_5538#HapaKaziTu; ndio maneno aliyokuwa akiyasema Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez wakati akichimbia sehemu ya bwawa hilo alipofanya ziara ya kukagua mradi huo wa Bwawa la Charco la Nguvumoja.
IMG_5540Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akichimba udongo na sururu huku Afisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah Hassan akijaza udongo unaochimbwa kwenye ndoo.
IMG_5553#HapaKaziTu; Wanakijiji pamoja na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez wakishangilia kwa pamoja huku wakiunga kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ya #HapaKaziTu sambamba na mabango 17 ya malengo ya maendeleo endelevu (Sustainable Development Goals-SDGs) walioyowafikia wanakijiji wa Nguvumoja.
 
 
MRATIBU Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Mipango ya Maendeleo la Umoja huo Bw.Alvaro Rodriguez, amesema kwamba umoja huo utaendelea kufadhili miradi ya maendeleo katika mkoa wa Tabora yenye lengo la kuboresha maisha ya wananchi.
Hayo alisema jana baada ya kuzuru miradi inayofadhiliwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa mkoani Tabora.

Miradi hiyo ni ya ujenzi wa bwawa la nguvumoja kwamtindo wa utoaji wa chakula kwa kazi inayofanywa na mradi wa misitu ya miyombo.
Katika ziara hiyo ambayo alikuwa na Ofisa kutoka Kitengo cha ushirikiano wa kimataifa wizara ya mambo ya nchi za nje, Bi. Maulidah Hassan Mratibu huyo aliridhishwa na mafanikio ya miradi hiyo ambayo imelenga kupiga vita umaskini na kutunza mazingira.

Ziara ya Mratibu huyo mkoani Tabora ni moja ya ziara yake ndefu ya kutembelea miradi inayofadhiliwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa katika mikoa ya Singida, Tabora na Kigoma.

Alipotoka Singida jana asubuhi alifika katika moja ya Wilaya kame nchini, Wilaya ya Igunga na kuona mradi unaofadhiliwa na Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) wa ukarabati wa bwawa la Charco.

Bwawa hilo ambalo litahudumia watu takribani 6,100 kutoka vijiji vya Nguvumoja, Ndembezi na Iborogelo lilijengwa awali na miradi ya TASAF lakini wakati wa mvua za Elnino tuta lake lilivurugika vibaya.

Akizungumzia bwawa hilokaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Igunga ambaye pia ni Ofisa Kilimo na Ushirika wa Wilaya ya Igunga, Samaluku Joseas, akizungumza alisema kwenye bwawa hilo kwamba Umoja wa Mataifa kupitia WFP wanawezesha ukarabati wa bwawa hilo kwa kutoa chakula kwa wachimbaji.

Aidha imeelezwa kuwa tuta hilo likikamilika litakuwa na uwezo wa kuhudumia kaya 1,200 na Ng’ombe elfu moja na kuweza kuhifadhi maji kwa mwaka mzima.Imeelezwa kuwa wajenzi wanapewa debe moja la Mahindi kwa kina cha mita moja na urefu wa mita nne na upana wa mita tatu na nusu lita ya mafuta ya kula na Njegere kilo tatu.Kumalizika kwa bwawa hilo kutasaidia kupunguza umbali wa wananchi katika kutafuta maji.

Awali wananchi walilazimika kusafiri kilomita 30 kupata maji katika bwawa la Manzugi kuchota maji na kunywesha mifugo.Aidha imeelezwa kuwa baadae wanyama watatengewa eneo la kunywa maji.
Aidha alitembelea kikundi cha ufugaji nyuki, utunzaji wa mazingira pamoja na usindikaji wa matunda pori cha Membo , wilayani Uyui.

Kikundi hicho kilichopo wilayani Uyui kimeanzishwa Mei 8,2007 na Katibu wa kikundi Nasibu Baraka alisema kikundi hicho chenye wanachama 30 kimefanyakazi kubwa ya kupiga vita umaskini.Alisema ili kukabiliana na adui njaa na umaskini kikundi hicho kwa ufadhili wa UNDP kimewezesha kujiajiri wenyewe, Kusindika matunda ya asili kwa ajili ya jamu na divai,kilimo cha bustani, kilimo cha chakula na biashara, ujenzi wa majikobanifu,usagaji wa unga na kupika keki za Muhogo mbichi kwa Karanga na Asali.

Akisoma risala kwa Mratibu wa UN Tanzania alisema kwamba wamekuwa na mafanikio makubwa kutokana na ruzuku mbalimbali za UNDP ikiwamo mafunzo.

Aidha amesema kwamba kwa sasa wanatumia sola badala ya mafuta ya taa huku mradi wa Miyombo ukiendelea kuleta neema.Aidha ametaka umoja huo kuwasaidia kuwa na mshine za kisasa cha kusindika matunda na chakula.

Viongozi hao walifika katika mradi huo kuangalia mafanikio ya mradi huo unaotekelezwa chini ya mpango wa miaka mitano wa Msaada wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa,(UNDAP).Aidha mradi huo umelenga kupunguza umaskini kutunza mazingira kwa njia ya uragibishi na na kufunza wananchi kuhusu suala la ufugaji nyuki na utunzaji wa mazingira.

Naye Ofisa utawala msaidizi wa mkoa anayeshughulikia Uchumi na Tija Dk. Phillips Mtiba akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa Tabora, Ludovick Mwananzila ambaye hakuwepo kutokana na majukumu mengine kwenye mikutano na wananchi kuhusu miradi ya TASAF, alisema baada ya kumaliza kukagua miradi kwamba wameridhika na miradi inayofadhiliwa na UN katika mkoa huo.

Alisema pamoja na kwamba walitembelea miradi michache lakini ni dhahiri mkoa wa Tabora umefurahishwa na misaada iliyotolewa ambayo inatia moyo na kusaidia harakati za serikali za kukomboa wananchi wake kutoka katika lindi la umaskini na ukosefu wa huduma muhimu kama za maji na hifadhi ya mazingira.

Pamoja na kushukuru kwa misaada hiyo kwa wanatabora na maendeleo yao, alitaka UN isiwachoke kusaidia vipaumbele vya mkoa huo ambavyo ni kujitokeza kwa chakula na hifadhi ya misitu.“ Nashukuru sana kwa msaada tunaoendelea kupata kutoka UN kwa ajili ya maendeleo ya wana Tabora na Tabora kwa ujumla na niseme tu kwamba kama wana Tabora kuna vitu ambavyo tunaweza kufanya na mengine hatuwezi kuyafanya na hapo ndipo sasa tunapoweza kuona umuhimu wa nafasi ya wafadhili na wadau mbalimbali katika shughuli za maendeleo.” Alisema Dk. Phillips.

Alisema ingawa walikuwa na muda mfupi na kutembelea miradi michache , alitamani waje kurudi kuona miradi mingi zaidi ili watambue kwamba miradi hiyo inabadilisha wana Tabora na hawachezei fedha za ufadhili.


Alisema suala la uhakika wa chakula kwa wananchi ni muhimu kwao kutokana na ukweli kuwa wananchi wakiwa na chakula hata fedha zao zitakaa mfukoni na kufanya kazi nyingine za maendeleo. Alisema kutokana na hali hiyo wataendelea kuomba kusaidiwa katika eneo hilo.

Aidha alitaka mkoa wa Tabora kuendelea kusaidiwa kutunza misitu ya Miyombo kwa ajili ya manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho kwa kuwa misitu ni kivuta mvua na maji ndio pembejeo namba moja katika uzalishaji wa chakula.

Alishukuru UNDP kwa kusaidia kuhifadhi misitu hiyo ili kuwapo na uvunaji endelevu kwa kusaidia jamii kuitunza na kuismamia rasilimali hiyo na kuitumia katika fursa za kiuchumi kama ufugaji nyuki.
Leo Mratibu huyo ataendelea na ziara yake katika mkoa wa Kigoma.

IMG_5583
 
Blogger Templates