Makamu
 wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, 
akisalimiana na Rais wa China, Xi Jinping, wakati wa Mkutano Mkuu wa 
Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China (China-Africa Forum) 
uliofanyika leo Dec 4, 2015 jijini Johannesburg. Mhe. Samia 
amemwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo.
Makamu
 wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan 
(mwenye kitambaa cheupe) akiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Tano wa Wakuu wa 
Nchi za Afrika na China (China-Africa Forum) uliofanyika leo Dec 4, 2015
 jijini Johannesburg. Mhe. Samia amemwakilisha Rais Dkt. John Pombe 
Magufuli katika mkutano huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia 
Suluhu Hassan (mwenye kitambaa cheupe katikati) akiwa katika picha ya 
pamoja na baadhi ya Viongozi wakuu wa Nchi za Afrika baada ya ufunguzi 
wa Mkutano huo Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China 
(China-Africa Forum) uliofanyika leo Dec 4, 2015 jijini Johannesburg. 
Mhe. Samia amemwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano 
huo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia 
Suluhu Hassan (kulia) akiwa katika mazungumzo na Rais wa Msumbiji, Mhe. 
Filipe Jacinto Nyusi, walipokutana kwenye ufunguzi wa Mkutano huo Mkuu 
wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China (China-Africa Forum) 
uliofanyika leo Dec 4, 2015 jijini Johannesburg. Mhe. Samia 
amemwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Shulu 
Hassan, akisalimiana Mwambata wa Kijeshi wa Tanzania nchini Afrika ya 
Kusini (Defence advisor) Brig. Gen Ibrahim A. Kimario, wakati 
alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Olver Tambo jijini Johanesburg 
jana Desemba 3, 2015 kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Tano wa 
Wakuu wa Nchi za Afrika na China. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini 
Afrika ya Kusini, Radhia Msuya.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia 
Shulu Hassan, akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya 
Kusini, Radhia Msuya, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Olver
 Tambo jijini Johannesburg jana Desemba 3, 2015 kwa ajili ya kuhudhuria 
Mkutano Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China.

 
 
 
 
 
 







 
 
0 comments:
Post a Comment