Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji wa Serikali Bw. Assah
Mwambene akifunga Mkutano wa 10 wa uhamaji kutoka mfumo wa Analogia
kwenda Digitali kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini
mwa Afrika (SADC) kwa niaba ya Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni
na Michezo jana. Tanzania imepata heshima ya kuwa mwenyeji wa mkutano huo
baada ya kuonekana kufanya vizuri katika uhamaji wa matumizi ya
mfumo wa analogia kwenda digitali kwa wakati.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji wa Serikali Bw. Assah Mwambene
(katikati) akiwaonesha jambo kupitia Kitumi chake cha Mkononi (IPAD) Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Ally Simba (kulia) na Naibu
Mkurugenzi wa Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) Bw. Fredrick
Ntobi (kushoto) kabla ya kufungwa kwa Mkutano wa 10 wa uhamaji kutoka
mfumo wa Analogia kwenda Digitali kwa nchi za Jumuiya ya
Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) jijini Dar es salaam.
Washiriki wa Mkutano wa 10 wa uhamaji kutoka mfumo wa
Analogia kwenda Digitali kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi
za Kusini mwa Afrika (SADC) wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa mkutano
huo jijini Dar es salaam.
Mada
mbalimbali zikiwasilishwa kwa washiriki wakati wa Mkutano wa 10 wa
uhamaji kutoka mfumo wa Analogia kwenda Digitali kwa nchi za Jumuiya
ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) jijini Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment