Pages

Ads 468x60px

Saturday, November 14, 2015

WATU 150 WAUAWA KATIKA MASHAMBULIO HUKO PARIS


Ufaransa imetangaza hali ya hatari na kufunga mipaka yake baada ya watu zaidi ya 120 kuuawa kwenye mashambulio kadha mjini Paris.
Watu 120 wameuawa katika ukumbi wa sanaa wa Bataclan, katikati mwa mji wa Paris.

Watu wenye silaha walishika mateka watu waliokuwa kwenye ukumbi huo kabla yao kuzidiwa nguvu na maafisa wa polisi.
Watu wengine waliuawa kwenye mlipuko uliotokea karibu na uwanja wa michezo wa taifa wa Stade de France ambako mechi ya kirafiki kati ya Ufaransa na Ujerumani ilikuwa ikiendelea.
Wasimamizi wa mji wa Paris wamewataka raia kusalia manyumbani na wanajeshi 1,500 wametumwa kushika doria Paris.
Shambulio mbaya zaidi linaonekana kuwa hilo la Bataclan, ambako ripoti zinasema watu waliokuwa wamehudhuria tamasha ukumbini walipigwa risasi na kuuawa baada ya kushikwa mateka.

Akiongea baada ya kufika katika ukumbi huo baadaye, Rais wa Ufaransa Francois Hollande ameapa kuwa wahusika watakabiliwa "bila huruma".Mashambulio mengine yalitokea karibu na mighahawa ya Le Petit Cambodge na Le Carillon katika mtaa nambari 10 ambako mwandishi wa BBC anasema aliona watu 10 wakiwa wamelala chini, wakiwa wamejeruhiwa vibaya na wengine kufariki
Mtu aliyeshuhudia ameambia gazeti la Liberation kwamba naye alisikia risasi zaidi ya 100 zikifyatuliwa katika mghahawa wa La Belle Equipe katika mtaa nambari 11.
Milio ya risasi pia ilisikika katika kituo cha kibiashara cha Les Halles.

Rais wa Marekani Barack Obama amelitaja shambulio hilo kuwa "jaribio lisilokubalika la kuhangaisha raia wasio na hatia" na kuahidi kusaidia Ufaransa kukabiliana na waliohusika.
"Hili si shambulio tu dhidi ya raia wa Ufaransa. Ni shambulio dhidi ya binadamu wote na maadili yetu ya pamoja," amesema.
"Tutafanya kila tuwezalo kuwasaidia watu wa Ufaransa na mataifa kote duniani kuhakikisha magaidi hawa wanakabiliwa.”

Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron amesema ameshtushwa sana na shambulio hilo na kuahidi kufanya "lolote tunaloweza kufanya kusaidia."

JUMUIYA YA WATANZANIA WAISHIO THAILAND WAMCHAGUA BW. MAUMBA MGAYA KUWA MWENYEKITI WA TIT

Meza Kuu , Kutoka Kushoto ni Ndugu Maumba Mgaya, Mwenyekiti wa Jumuiya, Bi Magreth Mjindo na Ndugu Andrew Katibu
Meza Kuu , Kutoka Kushoto ni Ndugu Maumba Mgaya, Mwenyekiti wa Jumuiya, Bi Magreth Mjindo na Ndugu Andrew Katibu.
Mnano tarehe 7/11/2015, Jumuiya ya watanzania waishio nchini Thailand ilikutana na kujadiliana mambo mbalimbali ya jinsi gani wanaweza kusaidiana katika mambo mbalimbali, TIT ilianzishwa mnano mwezi wa nne mwaka, 2015 na inahusisha watanzania mbalimbali, wanafunzi,wafanyabishara na wafanyakazi waishio na kufanya nchini Thailand. Mkutano mkuu wa Jumuiya ulifanyika katika Hoteli ya Amari Boulevard Mjini Bangkok na kuhudhuriwa na wanajumiya mbalimbali.
Pamoja na kujadiliana mambo mbalimbali kulifanyika uchaguzi wa viongozi ambapo wafuatao walichaguliwa kuwa viongozi wa jumuiya kwa kipindi cha 
mwaka mmoja:
Mwenyekiti: Bwana Maumba Mgaya
M/Kiti: Bw. Alois Ngonyani
Katibu: Bw.Andrew Wajama
Katibu Msaidizi: Bw. Emmanuel Mushi
Mhazini: Bw. Adolf Kigombola
Mhazini Msaidizi: Bi.Tumaini Kalindile
Afisa Mawasiliano: Bw. Emmanuel Nyamageni
Afisa Mawasiliano Msaidizi: Bw. Jordan Hossea.
Pamoja na uchaguzi kulifanyika sherehe fupi ya kumpongeza Bi Magreth Dionis Mjindo ambaye amemaliza Shahada ya uzamili ya maendeleo ya jamii na anarejea nyumbani kulitumikia Taifa.
Jumuiya inapenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wadhamini wao Ndugu Florean Rwehumbiza, Dada Lucy Kileo pamoja na Ndugu Kivea Mbwana (Homeboy) kwa kusimamia uchaguzi na kufanikisha kufanyika kwa mkutano huu muhimu. Shukrani za pekee ziende kwa Kampuni ya Broadhurst Pacific, kwa kusimamia, kudhamini na kufanikisha tukio hili muhimu.
Mhazini wa Jumuiya Ndugu Adolph Kigombola akisoma taarifa ya fedha
Mhazini wa Jumuiya Ndugu Adolph Kigombola akisoma taarifa ya fedha.
Tunapenda kuwapongeza na kuwashukuru viongozi waasisi wa jumuiya waliomaliza muda wao ambao ni ndugu Saidi Husein Kitenge Mwenyekiti wa kwanza wa jumuiya na makamu wake Ndugu Masui Vicent Munda na ndugu Antidius Muchunguzi bila kuwasahau maafisa mawasiliano wetu akiwemo ndugu Felix Mwema na Bi Diana Richard.Mungu awabariki kwa kuitumikia vema TIT.
Aidha Jumuiya inawakaribisha watanzania mbalimbali walioko nchini Thailand au wanaotarajia kuja nchini Thailand kushirikiana na jumuiya yetu.

KAMPUNI YA NIKO INSURANCE LIMITED YABADILI JINA NA KUWA SANLAM GENERAL INSURENCE


 Afisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam General Insuarence Ndugu Manasseh Kawaloka  Akitoa Hotuba yake Kwenye halfa ya Kampuni ya NIKO Insuarence Limited Ilipobadili Jina na kuwa Sanlam General Insuarence.
Kampuni ya Bima Niko limited Imebadili jina na kuwa Sanlam General Insuarence Limited.

Mabadiliko hayo yanalenga Kupanua Wigo Na kuimarisha uwepo wake Nchini Tanzania na Afrika Mashariki  kwa Jumla.Sanlam General Insuarence Itaendelea Kutoa Huduma Mbalimbali za BimaKwa Wateja Binafsi na Mashirika Nchini Tanzania.Huduma za Sanlam General Insuarence  ni Pamoja na za Biashara na Binafsi kama vile Magari,Moto Na Nyinginezo.
   Sanlam General Insuarence  Yenye Makao Makuu yake Nchini Afrika KusiniInamiliki 46%ya Hisa za Niko.Kupitia Kampuni yake Tanzu ya Masoko yanayokua yaani Sanlam Emerging Markerts..
Picha  ya Viongozo wa Kampuni ya Sanlan Pamoja na NIKO Insuarence wakiwa wameshikana mikono Mara baada ya Uzinduzi wa Sanlam General Insuarence.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam General Insuarence Ndugu Manasseh Kawaloka Alisema Kuwa Sanlam Group ni Kampuni yenye Heshima Kubwa,Hivyo Mabadiliko ya NIKO Insuarence Kuwa Sanlam General Insuarence  Utaleta Ufanisi wa Hali ya Juu Pamoja Utendaji wa Kibiashara Kwa Kampuni Hiyo.Akieleza zaidi alisema Watanzania  sasa watapata nafasi zaidi ya Kupata Aina mbalimbali za Bidhaa za Bima Zenye ubunifu kufidia Majanga Binafsinna ya Kibiashara .
Kampuni ya Iliyobadili Jina Sanlam General Insuarence  Inatoa Huduma Mbalimbali za Bima Katika Wigo Mpana Kwa Wateja  Binafsi Pamoja na Mashirika  Nchini Tanzania .Huduma Zitolewazo na Kampuni ya Bima ya Sanlam General Insuarence  Zinalenga Biashara na Watu Binafsi Kama Magari ,Moto ,Uhandisi pamoja na Bima Maalum.Kabla ya Kubadili Jina Kampuni ya NIKO Insuarence Imekuwa Ikitoa Huduma Nchini Tangu Mwaka 2005.
Ndugu Josep Mungai Mkurugenzi Mtendaji wa Sanlam General Insuarence Akitoa Hotuba yake wakati wa Uzinduzi huo.
Mabadiliko ya NIKO Insuarence Limited kuwa Sanlam General Insuarence  Yanafuatia Mabadiliko ya Kampuni ya African Life Assuarence ya Tanzania na Kuwa Sanlam Life Insuarence.Sanlam General Insuarence  Inatoa utaalamu na Uzoefu wa Hali ya Juu kwa Wateja wake Pamoja na Wadua wengine wanaofanya kazi na Kampuni hiyo.

ZOEZI LA USAJILI WA WABUNGE LAANZA LEO MJINI DODOMA.

Maafisa wa Bunge wakipokea nyaraka toka kwa wabunge wateule katika zoezi lililoanza leo Mjini Dodoma.
Wabunge wateule wakipiga picha kwa ajili ya vitambulisho vitakavyotumika kwa ajili ya matumizi ya Bunge Leo Mjini Dodoma
Mbunge wa Jimbo la Mwanga Mkoani Kilimanjaro Mh. Jumanne Maghembe akikabidhi nyaraka zake wakati wa zoezi la usajili linaloendelea leo Mjini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Sengerema Willium Ngeleja akisajili kwa Afisa wa bunge
Maafisa wa benki wakiwapa maelezo wabunge wakati wa zoezi la usajili linaloendelea Mjini Dodoma
Maafisa wa Bunge wakimkabidhi nyaraka Moja ya Mbunge wakati wa Zoezi la Usajili leo Mjini Dodoma

Wakazi wa jijini Dar es Salaam wafurika Ufukwe wa Coco Beach kujionea Samaki mkubwa aina ya Nyangumi


Wakazi wa jijini Dar es Salaam wakijipatia kitoweo na mafuta ya samaki mkubwa jamii ya nyangumi aliyeonekana Novemba 13 katika ufukwe wa Bahari ya Hindi eneo la Coco Beach jijini Dar es Salaam. Wakazi hao waliofika katika eneo hilo huku wakiwa na vyombo vya kubebea mafuta ya samaki huyo. Mashuhuda hao walisema kuwa mafuta yake ni dawa ya watoto, hata hivyo wataalam wa afya hawakuweza kupatikana kuelezea usalama wa nyama ya samaki huo pamoja na mafuta yake.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Oysterbay Zefrin Lubuva alizitaka mamlaka zinazohusika na afya kufika na kuthibitisha usalama wa kitoweo hicho kwa afya za wakazi hao.  (Picha na Francis Dande)

 Wakazi wa jijini Dar es Salaam wakijipatia kitoweo na mafuta ya Samaki mkubwa jamii ya Nyangumi aliyeonekana Novemba 13 katika ufukwe wa Bahari ya Hindi eneo la Coco Beach jijini Dar es Salaam.
Wakazi wa jijini Dar es Salaam wakijipatia kitoweo na mafuta ya Samaki mkubwa jamii ya Nyangumi aliyeonekana Novemba 13 katika ufukwe wa Bahari ya Hindi eneo la Coco Beach jijini Dar es Salaam.

Mambo yameanza Dodoma, ratiba ya Bunge ni hii + picha ZA Wabunge waliofika..



Kama umetembelea mitandao ya kijamii utakuwa umeona pilikapilika za kinachoendelea Dodoma sasahivi, baada ya Uchaguzi Mkuu kuisha wale wote waliopita kwenye nafasi ya Ubunge wanasubiri shughuli ya kuapishwa halafu Vikao vya Bunge vinaanza.
Nimeipata Ratiba ya kitakachoendelea Dodoma kwa jumla ya siku saba mfululizo, yani kuanzia jana November 13  mpaka November 20 2015… Ratiba yenyewe hii hapa.
Bunge
Bunge II Bunge III
MAGHEMBE
Mbunge Mteule wa Jimbo Mwanga K’njaro, Prof. Jumanne Maghembe akiwasilisha nyaraka zake wakati wa kusajiliwa Bungeni Dodoma.
NGELEJA
Mbunge Mteule wa Sengerema, William Ngeleja nae kwenye foleni ya usajili katika Viwanja vya Bunge Dodoma.
Prof JAY
Joseph Haule a.k.a Professor Jay alipost hii picha kwenye ukurasa wake wa Instagram jana, halafu akaandika >>> ‘Hi everybody, MJENGONI DAY ONE!!!
WABUNGE
Wabunge wengine pia wakiendelea na utaratibu wa kusajiliwa Dodoma.

Maduka ya dawa jirani na hospitali yanafungwa!! kingine kilichonifikia kutoka Wizara ya afya ni hiki


Jana katibu mkuu wa Wizara ya afya Dk.Donan Mmbando alizungumzia kuhusu mikakati ya kutaka kufunga maduka ya dawa yaliyo karibu na hospitali za Serikali kwa madai ya malalamiko ya wizi wa dawa hizo kutoka hospitali.
Leo Msemaji wa Wizara hiyo Nsachris Mwamwaja amezungumzia moja ya mikakati ya Wizara hiyo ni pamoja na kuhakikisha kunakuwepo na maduka ya dawa ndani ya hospitali ambayo yatakuwa ya Serikali chini ya Bohari kuu ya dawa MSD.
“Hospitali ya Muhimbili ina maduka ya dawa ndani, tumepanga kuhakikisha kila hospitali ya Serikali inakuwa na duka ndani, na tutahakikisha dawa zote zitakuwepo, lengo ni kuondoa malalamiko ya watu kuwa yale maduka ndio chanzo cha kukosekana kwa dawa mahospitalini”...Nsachris Mwamwaja
“Ni kweli haya maduka yapo sehemu ambazo wauguzi ndio hutoa maelezo wagonjwa wakanunue hizo dawa katika maduka hayo, wagonjwa wanaotumia huduma za mifuko ya jamii pia watakuwa wakitumia maduka ya hospitali za Seeikali, nia yetu ni wagonjwa wapate dawa bila usumbufu wowote”..
Kingine kilichosikika kutoka ndani ya Wizara hiyo ni utapeli ambao umekuwa ukifanywa kwa waajiri ambapo kumejitokeza wimbi la matapeli na kuwapangia watu maeneo ya kwenda kufanya kazi kitu ambacho si kweli kwa kuwa Wizara hiyo haijatoa majina ya ajira na haijawapangia watu vituo vya afya.
“Kuna taratibu za kukufanya uingizwe kwenye mfumo wa kulipwa na Wizara, ni ngumu kuingia kirahisi huo ni udanyangifu unaofanywa na baadhi ya watu ambao si waaminifu katika baadhi ya ofisi..pia wizara haitoa barua wala kuajiri bali inatoa majina na kupeleka kwa waajiri husika”…
 
Blogger Templates