Meza Kuu , Kutoka Kushoto ni Ndugu Maumba Mgaya, Mwenyekiti wa Jumuiya, Bi Magreth Mjindo na Ndugu Andrew Katibu.
Mnano
 tarehe 7/11/2015, Jumuiya ya watanzania waishio nchini Thailand 
ilikutana na kujadiliana mambo mbalimbali ya jinsi gani wanaweza 
kusaidiana katika mambo mbalimbali, TIT ilianzishwa mnano mwezi wa nne 
mwaka, 2015 na inahusisha watanzania mbalimbali, 
wanafunzi,wafanyabishara na wafanyakazi waishio na kufanya nchini 
Thailand. Mkutano mkuu wa Jumuiya ulifanyika katika Hoteli ya Amari 
Boulevard Mjini Bangkok na kuhudhuriwa na wanajumiya mbalimbali.
Pamoja
 na kujadiliana mambo mbalimbali kulifanyika uchaguzi wa viongozi ambapo
 wafuatao walichaguliwa kuwa viongozi wa jumuiya kwa kipindi cha 
mwaka mmoja:
Mwenyekiti:                                                   Bwana Maumba Mgaya
M/Kiti:                                                            Bw. Alois Ngonyani
Katibu:                                                            Bw.Andrew Wajama
Katibu Msaidizi:                                             Bw. Emmanuel Mushi
Mhazini:                                                          Bw. Adolf Kigombola
Mhazini Msaidizi:                                           Bi.Tumaini Kalindile
Afisa Mawasiliano:                                         Bw. Emmanuel Nyamageni
Afisa Mawasiliano Msaidizi:                          Bw. Jordan Hossea.
Pamoja
 na uchaguzi kulifanyika sherehe fupi ya kumpongeza Bi Magreth Dionis 
Mjindo ambaye amemaliza Shahada ya uzamili ya maendeleo ya jamii na 
anarejea nyumbani kulitumikia Taifa.
Jumuiya
 inapenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wadhamini wao Ndugu Florean 
Rwehumbiza, Dada Lucy Kileo pamoja na Ndugu Kivea Mbwana (Homeboy) kwa 
kusimamia uchaguzi na kufanikisha kufanyika kwa mkutano huu muhimu. 
Shukrani za pekee ziende kwa Kampuni ya Broadhurst Pacific, kwa 
kusimamia, kudhamini  na kufanikisha tukio hili muhimu.
Mhazini wa Jumuiya Ndugu Adolph Kigombola akisoma taarifa ya fedha.
Tunapenda
 kuwapongeza na kuwashukuru viongozi waasisi wa jumuiya waliomaliza muda
 wao ambao ni ndugu Saidi Husein Kitenge Mwenyekiti wa kwanza wa jumuiya
 na makamu wake Ndugu Masui Vicent Munda na ndugu Antidius Muchunguzi 
bila kuwasahau maafisa mawasiliano wetu akiwemo ndugu Felix Mwema na Bi 
Diana Richard.Mungu awabariki kwa kuitumikia vema TIT.
Aidha
 Jumuiya inawakaribisha watanzania mbalimbali walioko nchini Thailand au
 wanaotarajia kuja nchini Thailand kushirikiana na jumuiya yetu.
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment