Pages

Ads 468x60px

Monday, November 30, 2015

VETA YAKUTANA NA WADAU WA UMEME,VIWANDA NA MAGARI KUJADILI UTEKELEZAJI WA MAFUNZO




Washiriki wa warsha hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na mwakilishi wa mgeni rasmi ambaye ni mshauri wa mradi huo Bw. Ahmed Athumani.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Soko la Ajira ,Mipango na Maendeleo wa VETA, Ahmed Athuman akizungumza katika warsha ya wadau wadau wa viwanda,umeme na magari kujadili utekelezaji wa mradi wa mafunzo yanayotolewa kwa ushirikiano kati VETA na wadau hao iliyofanyika katika ukumbi wa Giraffee Hoteli jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wadau wakifatilia maada mbalimbali katika kujadili utekelezaji wa mradi wa mafunzo yanayotolewa kwa ushirikiano kati VETA na wadau hao iliyofanyika katika ukumbi wa Giraffee Hoteli jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii
MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA)imekutana na wadau wa viwanda,umeme na magari kujadili utekelezaji wa mradi wa mafunzo yanayotolewa kwa ushirikiano kati yake na viwanda.

Akizungumza na wadau wa mamlaka hiyo wakati akifungua warsha hiyo Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Soko la Ajira ,Mipango na Maendeleo wa VETA, Ahmed Athuman alisema moja ya sababu zinazokwamisha ajira kwa vijana nchini ni ukosefu wa mafunzo ya vitendo kwa vijana wanaohitimu katika taasisi mbalilmbali unaosababishwa na kutokukwepo kwa ushirikiano thabiti kati ya Taasisi za Mafunzo na Viwanda.

Amesema kuwa VETA inatoa mafunzo yatakayomuwezesha muhitimu kuajiriwa au kujiajiri kutokana na mafunzo ya vitendo yanayotolewa kutokana na mahitaji yaliyopo nchini 


Ahmed amesema kuwa ushirikiano wa wadau utaleta matokeo chanya kwa vijana kuweza kufanya kazi kutokana mafunzo walioyapata katika taasisi za mafunzo ya ufundi Stadi.

Bilioni 4 za sherehe za uhuru kupanua barabara ya Mwenge-Moroco yenye urefu wa kilomita 4.3


index 
Sehemu  ambako utaanzia upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco jijini Dar es salaam yenye urefu wa kilometa 4.3 kwa kuongeza njia mbili za barabara za lami kufuatia agizo la Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli la kutumia fedha shilingi bilioni  nne zilizopaswa kutumika kugharamia Shamrashamra za siku ya Uhuru Desemba 9, 2015 kutumika kufanya upanuzi wa barabara hiyo.PICHA NA IKULU.

…………………………………………………………………………………

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameamuru fedha zilizopaswa kutumika kugharamia shamra shamra za siku ya Uhuru ambazo zingefanyika tarehe 09 Desemba 2015, kutumika kufanya upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco jijini Dar es Salaam yenye urefu wa kilometa 4.3 kwa kuongeza njia mbili za barabara za lami.
  Tayari fedha hizo kiasi cha shilingi bilioni nne zimepelekwa kwa wakala wa barabara hapa nchini TANROADS kwa ajili ya utekelezaji wa agizo hilo, linalopaswa kuanza mara moja.

Akizungumza na Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi PATRICK MFUGALE Ikulu Jijini Dar es Salaam, Dkt. Magufuli ametaka ujenzi wa barabara hiyo uanze haraka ili kukabiliana na adha ya msongamano wa magari katika barabara hiyo Kujengwa kwa njia hizo kutaifanya barabara ya Morroco hadi Mwenge kuwa na njia tano.  Wakati huo huo, Rais John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba Ikulu Jijini Dar es salaam.

Katika Mazungumzo hayo Prof. Lipumba amempongeza Dkt. Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia kwa kutoa hotuba nzuri ya uzinduzi wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyokonga nyoyo za Watanzania.
  Kwa Upande wake Rais Magufuli amempongeza Prof. Lipumba kwa msimamo wake thabiti wa kupinga ufisadi na amemtakia heri katika shughuli zake.

Gerson Msigwa.
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU. Dar es Salaam.

30 Novemba,2015

Ufisadi wa $600m hati fungani za Serikali: Tusikubali ya Rada, hatua zichukuliwe

Taasisi ya Serious Fraud Office ya Uingereza ( SFO ) inafanya mazungumzo na Benki ya Standard Group ya Afrika ya Kusini Lakini iliyoorodheshwa katika soko la hisa ya Uingereza ( London Stock Exchange ) ili kumalizana kuhusu tuhuma za rushwa katika ununuzi wa hati fungani za Serikali ya Tanzania yenye thamani ya dola za kimarekani milioni Mia Sita ( $ 600m ). Mazungumzo hayo yanafanywa mbele ya Jaji katika mji wa London.
Ndugu wanahabari, ni jambo la kawaida kwa serikali yoyote duniani kuuza hati fungani. Mnamo mwaka 2011/2012 Serikali kupitia Wizara ya Fedha iliuza hati fungani ( Bonds ) zenye thamani ya dola za kimarekani 600 milioni ($600 million), dhamana hizo za serikali zilinunuliwa na benki ya kigeni  (Stanbic) ambayo ni mali ya Standard Group ya Afrika ya Kusini, yenye makao makuu yake huko London, Uingereza.
Hata hivyo, sehemu ya fedha hizo haikuingia kwenye akaunti za Serikali ya Tanzania na pia gharama za Bond hiyo zilipaishwa kupitia wakala wa kati kati ( middle men ) na hivyo kupelekea rushwa ya takribani $60 milioni kutolewa Kwa maafisa waliothibitisha biashara hiyo.
Ndugu wanahabari, taasisi za kiuchuanguzi za nchini Uingereza, hasa ile ya kushughulikia makosa ya rushwa (Serious Fraud Office-SFO) tayari imeshafanya uchunguzi wake wa awali kwa kuhusisha pande zote zinazohusika, na wamegundua kuwepo kwa rushwa kubwa katika mchakato huo, jambo ambalo liliwafanya washauri uongozi wa benki hiyo hapa nchini kuondolewa na kurejeshwa nchini Uingereza kwa hatua zaidi. Hata hivyo SFO na Standard Group wanataka kulimaliza jambo hili Kwa mtindo wa walivyomaliza suala la radar.
Ndugu wanahabari, Chama changu cha ACT-Wazalendo, kinazitaka mamlaka za kiuchunguzi hapa nchini, kuwachukulia hatua ikiwa ni pamoja na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wale wote waliohusika na upotevu wa $600 milioni, ambazo kwa pesa ya Tanzania ni zaidi ya shilingi 1.2 trilioni.  Hicho ni kiwango kikubwa sana cha fedha, ikilinganishwa na makusanyo ya Mamlaka ya Maapato Tanzania (TRA). Tunaitaka Benki Kuu ya Tanzania, FIU Tanzania na PCCB kuweka hadharani taarifa ya chunguzi zao na kueleza ni kwanini hawajachukua hatua mpaka sasa.
Ndugu wanahabari, chama cha ACT-Wazalendo, kinaunga mkono jitihada za Rais wetu Dr John Pombe Joseph Magufuli, za kutumbua majipu, hivyo tungependa kuona Mheshimiwa Rais akichukua hatua kwenye jambo hili ambalo lina maslahi mapana ya nchi yetu, hasa ikizingatiwa na uzoefu tulionao katika masakata kama hayo yanayohusisha nchi za kigeni, mfano mmojawapo ni sakata la rada, ambalo vyombo vyetu vya uchunguzi vilisema hakukuwa na rushwa, na baadaye serikali ya Uingereza ilithibitisha pasina shaka kwamba kulikuwa na rushwa, na baadaye serikali yetu ilirudishiwa sehemu ya fedha zilizozidi kwenye manunuzi ya rada ( chenji ya rada ).
Chama cha ACT Wazalendo kinasubiri taarifa ya makubaliano ( settlement ) Kati ya SFO na Benki ya Standard Group ( Benki mama ya Stanbic ) ili kushauri zaidi hatua za kuchukua. Ikumbukwe kuwa Benki ya Stanbic ndio ilihusika na kashfa ya Tegeta Escrow na mpaka sasa haijachukuliwa hatua zozote kama ilivyoagizwa na Bunge. Benki hiyo imewaficha waliochota fedha za escrow mpaka Leo.
( imesainiwa )
Masasi, 30 Novemba 2015
Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto, Mb
ACT-WAZALENDO

UCHUNGUZI WA SAKATA LA WATUHUMIWA WA WIZI WA MAKONTENA 329 KUCHUKULIWA HATUA

 Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai  Bw.Diwani Athumani (CP) akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo katika picha leo jijini Dar es Salaam kuhusu uchunguzi wa sakata la watuhumiwa wa wizi wa makontena 329.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Bw.Diwani Athumani (CP) alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu uchunguzi wa watuhumiwa wa wizi wa makontena kwa Mamlaka ya Bandari na Mamlaka ya Mapato Tanzania.

Na Nyakongo Manyama-Maelezo
Tarehe : 30/11/2015.

Kufuatia agizo laWaziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa la kuwataka watuhumiwa wa wizi wa makontena 329 katika bandari ya Dar es salaam kuchukuliwa hatua na Jeshi la Polisi, tayari Jeshi hilo limewashikilia watuhumiwa kumi na mbili wanaohusika na wizi huo. Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (CP) Diwani Athumani amesema kuwa, uchunguzi unaofanywa na wataalamu waliobobea katika makosa ya uhalifu wa kifedha umeweza kuwabaini watu kumi na mbili ambao wamehusika na wizi huo.

“Kati ya watuhumiwa hao kumi na mbili, watano wanashikiliwa na Jeshi la Polisi na saba bado wapo katika upepelezi na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani,” alisema Kamanda Athumani.Wanaoshikiliwa kutokana na tuhuma mbalimbali ni Kamishna wa Idara ya Forodha na Ushuru TRA Bw. Tiagi Masamaki, Meneja Kitengo cha Huduma za Ushuru na Bi. Habib Mponezia, Msimamizi Mkuu wa Kitengo cha Ushuru wa Forodha.

Watuhumiwa wengine ni pamoja na Bi. Eliaichi Mrema, Msimamizi Kitengo cha Mawasiliano ya Kompyuta Bw. Haroun Mpande na Mchambuzi Mwandamizi wa Masuala ya Biashara Bw. Hamis Omary.Aidha Kamanda Athumani amewaomba wananchi wenye taarifa za ubadhilifu wa mali za Umma kuendelea kulisaidia Jeshi la Polisi katika kutekeleza majukumu yake.

JOHNNIE WALKER YAZINDUA KAMPENI MPYA YA “FURAHA ITAKUFIKISHA MBALI”



 Meneja Chapa (Pombe kali) wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL),Shomari Shija (wa kwanza kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya Johnnie Walker iliyopewa jina la “Furaha itakufikisha mbali” yenye lengo la kuhamasisha watu kuwa na utamaduni wa kupenda na kufurahia kile wanachokifanya katika kujiletea maendeleo binafsi. (katikati) ni Mkuu wa masoko bidhaa za pombe kali za Diageo-Serengeti Breweries Limited (SBL), Stanley Samtu na kulia ni Dj maarufu kutoka Ireland Frank Jez. “Johnnie Walker” ni chapa maarufu ya pombe kali inayosambazwa na Kampuni ya bia ya Serengeti hapa nchini.
 Mkuu wa masoko bidhaa za pombe kali za Diageo-Serengeti Breweries Limited(SBL), Stanley Samtu (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya Johnnie Walker iliyopewa jina la “Furaha itakufikisha mbali” yenye lengo la kuhamasisha watu kuwa na utamaduni wa kupenda na kufurahia kile wanachokifanya katika kujiletea maendeleo binafsi. (Kushoto) ni Meneja Chapa (pombe kali) wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Shomari Shija na (kulia) ni Dj maarufu kutoka Ireland Frank Jez. “Johnnie Walker” ni chapa maarufu ya pombe kali inayosambazwa na Kampuni ya bia ya Serengeti hapa nchini.
 Mkuu wa masoko bidhaa za pombe kali za Diageo-Serengeti Breweries Limited(SBL),Stanley Samtu (katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya Johnnie Walker iliyopewa jina la “Furaha itakufikisha mbali” yenye lengo la kuhamasisha watu kuwa na utamaduni wa kupenda na kufurahia kile wanachokifanya katika kujiletea maendeleo binafsi. (Kushoto) ni Meneja Chapa (pombe kali) wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Shomari Shija na (kulia) ni Dj maarufu kutoka Ireland Frank Jez. “Johnnie Walker” ni chapa maarufu ya pombe kali inayosambazwa na Kampuni ya bia ya Serengeti hapa nchini.
Mkuu wa masoko bidhaa za pombe kali za Diageo-Serengeti Breweries Limited (SBL), Stanley Samtu (kushoto), Meneja Chapa (pombe kali) wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Shomari Shija (kulia) na Dj maarufu kutoka Ireland Frank Jez (katikati) wakionyesha bidhaa mbalimbali za Johnnie Walker wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya Johnnie Walker iliyopewa jina la “Furaha itakufikisha mbali” yenye lengo la kuhamasisha watu kuwa na utamaduni wa kupenda na kufurahia kile wanachokifanya katika kujiletea maendeleo binafsi. “Johnnie Walker” ni chapa maarufu ya pombe kali inayosambazwa na Kampuni ya bia ya Serengeti hapa nchini.

CHAPA maarufu ya pombe kali inayosambazwa na Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries “Johnnie Walker” imezindua kampeni mpya iliyopewa jina la “Furaha itakufikisha mbali” siku ya leo katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam ikiwa na lengo la kuwahamasisha watu kuwa na furaha katika kila wanachokifanya kwa vile furaha huleta maendeleo na sio kinyume chake kama wengi wanavyodhani.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye uzinduzi wa Kampeni hiyo katika hoteli ya Serena, Mkuu wa kitengo cha Masoko pombe kali wa Kampuni ya bia ya Serngeti (SBL) Stanley Samtu alisema “Kama chapa, Johnnie Walker imesimama daima kwenye upande wa maendeleo. Imekuwa hivyo kwa miaka takribani 200 tangu mwanzilishi Johnnie Walker alipoanza ufundi wake.

 Uzoefu umetufundisha kwamba maendeleo hayatakiwi kuwa safari ya kupanda tu na isiyo na kikomo bali tunaweza kupiga hatua na kufurahia katika malengo tunayoweza kuyafikia kila kukicha. Hiyo ndio maana halisi ya kampeni hii ya Furaha itakufikisha mbali zaidi”.

Kufurahia kile unachokifanya ni sehemu kubwa na muhimu ya kufanikiwa na kuwa na maendeleo. Katika juhudi za kufikisha ujumbe kwa wahusika, Johnnie Walker inategemea kuwamulikia baadhi ya nyota katika fani mbalimbali waliojizolea umaarufu kutokana na mafanikio walioyafikia. Hawa ni pamoja na Sheria Ngowi wa tasnia ya mitindo, Dj Frank Jez kutoka Ireland na Dj Peter Mo. Vijana hawa wote wamebobea katika kile wanachokifanya na wamekuwa mfano wa kuigwa nchini. 

Wamekuwa sehemu ya dunia ya watu ambao wanaaamini kuwa chanya siku zote katika kazi ni moja kati ya vitu viliyowasaidia kufika mbele zaidi katika fani zao.

Viongozi wa Ofisi ya Rais- Utumishi wala kiapo cha Uadilifu

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw.HAB Mkwizu (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji wa Maadili wa Ofisi ya Rais-Utumishi Bw.Mathew Kirama fomu maalum ya kuweka Ahadi ya Uadilifu kwa Watumishi wa Umma mapema leo ofisini kwake.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Tixon Nzunda (kushoto) akielekeza namna ya kutoa Ahadi ya Uadilifu kwa watumishi wa Umma zoezi lililofanyika mapema leo Ofisi ya Rais-Utumishi jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw.HAB Mkwizu akitia saini fomu ya Ahadi ya Uadilifu kwa watumishi wa Umma ya Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Tixon Nzunda (kulia) ofisini kwake mapema leo.
 Wakuu wa Idara na Vitengo wa Ofisi ya Rais-Utumishi wakila kiapo cha  Uadilifu kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw.HAB Mkwizu (kushoto) mapema leo.

RAIS DKT. MAGUFULI, WAZIRI MKUU MAJALIWA, WAMTEMBELEA MAKAMU WA RAIS, MHE. SAMIA OFISINI KWAKE IKULU DAR.

sa1 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, (kushoto) akizungumza na Makamu wake, Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, wakati Rais na Waziri Mkuu walipomtembelea Makamu Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Nov 30, 2015 kwa mazungumzo. Picha na OMR
sa2 sa3 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli (kushoto) akiagana na  Makamu wake, Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa (kulia) baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Nov 30, 2015. Wa pili (kulia) ni Naibu Katibu wa Makamu wa Rais,

RC KILIMANJARO AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA



MKUU wa Mkoa Kilimanjaro, Amos Makalla, amefanya ziara ya kushtukiza katika masoko manne ya Manispaa ya Moshi pamoja na dampo za kukusanyia uchafu, ili kujionea hali ya usafi na utendaji kazi katika mkoa huo. Katika ziara hiyo, RC Makalla alitumia muda huo kuwaagiza watendaji wake, hususan katika mchakato mzima wa kuifanya Moshi iwe kwenye usafi.
Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, RC Amos Makalla mwenye miwani, akikagua soko lililopo kwenye Manispaa ya Moshi, mkoani humo, baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kujionea hali ya usafi katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

Akizungumzia ziara yake hiyo, Makalla alitoa siku tatu kwa watendaji wa Manispaa ya Moshi kuhakikisha kwamba lundo la takataka katika soko la Kwasadala linaondoshwa haraka iwezekanavyo. Alisema hawezi kukubali kuona Manispaa hiyo inashuka kiwango chake cha kuifanya Moshi inaendelea kuheshimika katika suala zima la usafi.
Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, RC Amos Makalla aliyesimama mlangoni, akiendelea na ziara yake ya kushtukiza kwenye Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro kujionea hali ya usafi katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

“Pamoja na kuagiza kuondoshwa kwa uchafu huo, pia nataka kuona Mkoa wetu wote unakuwa kwenye hali ya usafi, magari ya usafi yazoe taka kwa wakati, uongozi wa masoko uthamini usafi bila kusahau uongozi wa Hospitali ya Hai unakamilisha haraka ukarabati wa vyoo,” alisema Makalla. Kwa mujibu wa RC Makalla, kitendo cha kuiweka Moshi katika mazingira ya uchafu si tu inaondosha kwa kasi ile heshima yake, bali pia itazalisha ugonjwa wa mripuko, ukiwamo ule wa Kipindupindu unaosikika kuweka katika kambi katika baadhi ya wilaya nchini Tanzania.

CCM YAKANUSHA TAARIFA ZA MITANDAONI KWAMBA IMEKUBALI KUMKABIDHI MAALIM SEIF IKULU

Chama cha Mapinduzi CCM kimekanusha Taarifa iliyozagaa katika Mitandao ya Kijamii kwamba Chama hicho kimeridhia aliyekuwa Mgombea wa Urais wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akabidhie nchi kuiongoza kwa miaka mitano. 

Akikanusha Taarifa hiyo mbele ya Waandishi wa Habari Afisini kwake Kisiwandui Naibu Katibu Mkuu wa CCM Vuai Ali Vuai amesema taarifa hiyo ni uzushi uliotungwa ili kuwatia taharuki WanaCCM na Wananchi kwa Ujumla. 

Amesema toka kusambaa kwa Taarifa hiyo Jana amekuwa akipigiwa simu na Watu mbalimbali wa ndani na nje ya nchi kujua ukweli wa Taarifa hiyo hasa ikizingatiwa kuwa ilidaiwa kusainiwa na Naibu huyo. “Huu ni Uzushi Mkubwa na kwamba unafaa kupuuzwa maana hauna lengo jingine zaidi ya kuwagawa WanaCCM” Alismema Vuai. 

Amesema kilichopo nikwamba CCM inajiandaa kwa ajili ya uchaguzi wa Marejeo kama ambavyo Tume ya Uchaguzi ilitangaza kuufuta Uchaguzi na hivyo kurudiwa upya. Aidha Vuai amesema kuwa tayari wamewasiliana na Wanasheria wao pamoja na wataalamu mbalimbali ili kuwabaini waliohusika kusambaza Taarifa hizo na kuwapeleka katika Vyombo vya Sheria. 

“Tumeshafanya mawasiliano na Wataalam wetu na tukiwabaini Sheria ya Makosa ya mtandao itachukua nafasi yake” Alisema Vuai. 

Katika taarifa hiyo iliyosambaa na kudai kusainiwa na Vuai Ali Vuai ilisema kuwa Chama cha mapinduzi kimeridhia na kukubali kumpa nchi Maalim Seif Sharif kupitia chama chake cha Cuf kuwa ndio rais wa uchaguzi ulopita,na yeye ndio atakayeongoza serikali ya umoja wa kitaifa. 

Taarifa hiyo ilieleza kuwa CCM imekubali kushirikiana na maalim Seif katika kuongoza nchi chini ya serikali ya umoja wa kitaifa na kukubali kutoa makamo wa kwanza wa rais na nusu ya mawaziri. 
Vuai amerejea kauli yake kuwa mazungumzo yanayofanywa na Viongozi wa Kitaifa kwa kushirikiana na Viongozi Rais Wastaafu wa Zanzibar hayawezi kubatilisha maamuzi ya Tume ya kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliopita.

RAIS MAGUFULI AONANA NA MABALOZI WA CHINA NA KOREA

ba7 
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana  na aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba  Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba. Profesa Lipumba amempongeza Rais kwa kuchaguliwa kwake kwa kishindo na pia ameipongeza hotuba ya Rais Magufuli aliyoitoa wakati wa kufungua Bunge la 11 mjini Dodoma 30, 2015
ba9 
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akifanya mazungumzo na aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba  Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba. Profesa Lipumba amempondeza Rais kwa kuchaguliwa kwake kwa kishindo na pia ameipongeza hotuba ya Rais Magufuli aliyoitoa wakati wa kufungua Bunge la 11 mjini Dodoma 30, 2015
ba10 
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiagana na aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba  Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba. Profesa Lipumba amempondeza Rais kwa kuchaguliwa kwake kwa kishindo na pia ameipongeza hotuba ya Rais Magufuli aliyoitoa wakati wa kufungua Bunge la 11 mjini Dodoma 30, 2015. 
ba1 
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana  na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30, 2015
ba2 
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30, 2015
ba4 
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana  na Balozi wa Korea ya Kusini  hapa nchini Mhe. Chung IL Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30, 2015. Balozi huyo pia alitumia nafasi hiyo kumuaga Rais kwa kuwa muda wake wa kufanya kazi nchini umemalizika.
ba6 
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na Balozi wa Korea ya Kusini  hapa nchini Mhe. Chung IL Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30, 2015. Balozi huyo pia alitumia nafasi hiyo kumuaga Rais kwa kuwa muda wake wa kufanya kazi nchini umemalizika.

VIJANA WA IRINGA WAWEZESHWA NA AIRTEL FURSA

 Mshiriki wa mafunzo ya Airtel Fursa mkoani Iringa Bi Fatuma Mkini (kushoto ) akipokea cheti cha ushiriki wa mafonzo hayo kutoka kwa afisa mahusiano na matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki mara baada ya mafunzo ya Airtel Fursa kumalizika mkoani Iringa kwa vijana zaidi ya 200 kushiriki.
 Vijana washiriki wa mafunzo ya siku moja ya Airtel Fursa mkoani Iringa wakimsikiliza afisa mahusiano na matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki (kulia) wakati wa ufungizi wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Highland mjini Iringa jana.
Wawakilishi wa vijana zaidi ya 200 mkoani Iringa walioshiriki kupata mafunzo ya ujasiriamali kupitia mradi wa Airtel fursa wakiwa katika picha ya pamoja na afisa mahusiano na matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki na wafanyakazi wengine wa Airtel mkoa wa Iringa mara baada ya kukabidhiwa  vyeti kwa niaba ya wenzao.
 (picha na mpiga picha wetu)

BAADA ya kukata tamaa ya maisha kwa muda mrefu baadhi ya vijana mkoani Iringa wameeleza kufurahishwa na kampuni ya simu ya Airtel Tanzania kwa kuwapatia mafunzo ya jinsi ya kuanzisha na kuendesha biashara zao kwa faida kupitia mpango wa Airtel FURSA

Wakizungumza na mara baada ya mafunzo ya siku moja ya Airtel FURSA yaliyofanyika katika ukumbi wa Highlands mjini Iringa kwa kuwashirikisha vijana zaidi ya 200,washiriki hao walisema kuwa mafunzo hayo ni ukomb0zi mkubwa kwao kwani baadhi yao walikuwa wakilazimika kushinda vijiweni kutokana na kukosa fursa ya mafunzo kama hayo .

Washiriki wa mafunzo hayo Bi Husna Sanga na Bw Okelo Kasim wakizungumza kwa niaba ya wenzao walisema kuwa mbali ya kuwa wa hatua ya kampuni hiyo ya simu ya Airtel kutoa mafunzo hayo si tu kunawasaidia kupata elimu kuendesha biashara na miradi mingine ya kiuchumi bali ni sehemu ya ukombozi kwao na familia zinazowazunguka .

Alisema Bi Sanga kuwa sehemu kubwa ya vijana hasa mabinti walikuwa wakirubunika na kujiingiza katika biashara zisizofaa kama za uuzaji wa miili yao kutokana na kutokuwa na elimu ya uanzishaji wa biashara ndogo ndogo ambao zingewakomboa kiuchumi hivyo kupitia mpango huo wa Airtel FURSA ni wazi kilio chao kimepata majibu.

"Wapo baadhi ya mabinti wenzetu ambao wanalazimika kufanya biashara ya kuuza miili yao ili kupata kipato na mwisho wa siku wanapoteza maisha kwa ugonjwa wa UKIMWI , ila kwa sisi ambao tumepata elimu hii kupitia Airtel FURSA tunaweza kuwa mfano kwa wengine ambao wanafikiri kazi ni kuuza miili yao pekee"

Huku Bw Kasim mbali ya kupongeza kampuni ya simu ya Airtel Tanzani kwa kuwakumbuka vijana bado alisema kuwa kama njia ya wao kupongeza kampuni hiyo ya simu kwa vijana wote waliopata mafunzo hayo kwenda kuonyesha mfano kwa wenzao kwa kufanya kazi ya kubuni miradi na kuendesha shughuli zao kifanisi zaidi.

Kwa upande wake afisa mahusiano na matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki kuwa Kutokana na mradi huo wa Airtel FURSA vijana wengi watanufaika zaidi na wanafaidika na mradi huo ni wale wenye miaka kati ya 18-24

Alisema kuwa mradi huo umelenga kuwafikia vijana kote nchini na hadi sasa zaidi ya mikoa tisa wamefikiwa na mradi huo wa Airtel FURSA .

Bi Kaniki alitaja mikoa ambayo tayari imefikiwa na mradi huo Mbeya, Arusha, Dodoma, Mtwara, Mwanza, Mtwara, Dar es Salaam , morogoro, Tanga, Tabora na Iringa kuwa hadi sasa zaidi ya vijana 1700 wamefikiwa.

Alisema kuna njia mbili za kuwawezesha vijana njia ya kwanza kupatiwa Mafunzo ya ujasiriamali na njia ya pili kupatiwa vitendea Kazi .

Hivyo aliwataka vijana wote nchini ambao watasikia taarifa ya kuwepo kwa Airtel Fursa katika Mkoa wao basi kuweza kuchangamkia Fursa hiyo ambao hutolewa bure.

Alisema ili kijana aweze kufaidika au kushiriki kwenye Airtel FURSA atatakiwa kutuma ujumbe mfupi kwenda kwa namba 15626 na kuweka maelezo yafuatayo:- Jina, Umri, aina ya biashara na eneo. Pia wanaweza kutuma maombi yao kwa kupitia barua pepe airtelfursa@tz.airtel.com ambapo watatakiwa kutuma jina kamili, umri, na aina ya biashara.

 
Blogger Templates