Mshiriki
 wa mafunzo ya Airtel Fursa mkoani Iringa Bi Fatuma Mkini (kushoto ) 
akipokea cheti cha ushiriki wa mafonzo hayo kutoka kwa afisa mahusiano 
na matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki mara baada ya mafunzo ya Airtel 
Fursa kumalizika mkoani Iringa kwa vijana zaidi ya 200 kushiriki.
 Vijana
 washiriki wa mafunzo ya siku moja ya Airtel Fursa mkoani Iringa 
wakimsikiliza afisa mahusiano na matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki 
(kulia) wakati wa ufungizi wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika Ukumbi 
wa Highland mjini Iringa jana.
Wawakilishi
 wa vijana zaidi ya 200 mkoani Iringa walioshiriki kupata mafunzo ya 
ujasiriamali kupitia mradi wa Airtel fursa wakiwa katika picha ya pamoja
 na afisa mahusiano na matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki na wafanyakazi
 wengine wa Airtel mkoa wa Iringa mara baada ya kukabidhiwa  vyeti kwa 
niaba ya wenzao.
 (picha na mpiga picha wetu)
BAADA 
ya kukata tamaa ya maisha kwa muda mrefu baadhi ya vijana mkoani Iringa 
wameeleza kufurahishwa na kampuni ya simu ya Airtel Tanzania kwa 
kuwapatia mafunzo ya jinsi ya kuanzisha na kuendesha biashara zao kwa 
faida kupitia mpango wa Airtel FURSA
Wakizungumza
 na mara baada ya mafunzo ya siku moja ya Airtel FURSA yaliyofanyika 
katika ukumbi wa Highlands mjini Iringa kwa kuwashirikisha vijana zaidi 
ya 200,washiriki hao walisema kuwa mafunzo hayo ni ukomb0zi mkubwa kwao 
kwani baadhi yao walikuwa wakilazimika kushinda vijiweni kutokana na 
kukosa fursa ya mafunzo kama hayo .
Washiriki
 wa mafunzo hayo Bi Husna Sanga na Bw Okelo Kasim wakizungumza kwa niaba
 ya wenzao walisema kuwa mbali ya kuwa wa hatua ya kampuni hiyo ya simu 
ya Airtel kutoa mafunzo hayo si tu kunawasaidia kupata elimu kuendesha 
biashara na miradi mingine ya kiuchumi bali ni sehemu ya ukombozi kwao 
na familia zinazowazunguka .
Alisema
 Bi Sanga kuwa sehemu kubwa ya vijana hasa mabinti walikuwa wakirubunika
 na kujiingiza katika biashara zisizofaa kama za uuzaji wa miili yao 
kutokana na kutokuwa na elimu ya uanzishaji wa biashara ndogo ndogo 
ambao zingewakomboa kiuchumi hivyo kupitia mpango huo wa Airtel FURSA ni
 wazi kilio chao kimepata majibu.
"Wapo 
baadhi ya mabinti wenzetu ambao wanalazimika kufanya biashara ya kuuza 
miili yao ili kupata kipato na mwisho wa siku wanapoteza maisha kwa 
ugonjwa wa UKIMWI , ila kwa sisi ambao tumepata elimu hii kupitia Airtel
 FURSA tunaweza kuwa mfano kwa wengine ambao wanafikiri kazi ni kuuza 
miili yao pekee"
Huku 
Bw Kasim mbali ya kupongeza kampuni ya simu ya Airtel Tanzani kwa 
kuwakumbuka vijana bado alisema kuwa kama njia ya wao kupongeza kampuni 
hiyo ya simu kwa vijana wote waliopata mafunzo hayo kwenda kuonyesha 
mfano kwa wenzao kwa kufanya kazi ya kubuni miradi na kuendesha shughuli
 zao kifanisi zaidi.
Kwa 
upande wake afisa mahusiano na matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki kuwa 
Kutokana na mradi huo wa Airtel FURSA vijana wengi watanufaika zaidi na 
wanafaidika na mradi huo ni wale wenye miaka kati ya 18-24
Alisema
 kuwa mradi huo umelenga kuwafikia vijana kote nchini na hadi sasa zaidi
 ya mikoa tisa wamefikiwa na mradi huo wa Airtel FURSA .
Bi 
Kaniki alitaja mikoa ambayo tayari imefikiwa na mradi huo Mbeya, Arusha,
 Dodoma, Mtwara, Mwanza, Mtwara, Dar es Salaam , morogoro, Tanga, Tabora
 na Iringa kuwa hadi sasa zaidi ya vijana 1700 wamefikiwa.
Alisema
 kuna njia mbili za kuwawezesha vijana njia ya kwanza kupatiwa Mafunzo 
ya ujasiriamali na njia ya pili kupatiwa vitendea Kazi .
Hivyo 
aliwataka vijana wote nchini ambao watasikia taarifa ya kuwepo kwa 
Airtel Fursa katika Mkoa wao basi kuweza kuchangamkia Fursa hiyo ambao 
hutolewa bure.
Alisema
 ili kijana aweze kufaidika au kushiriki kwenye Airtel FURSA atatakiwa 
kutuma ujumbe mfupi kwenda kwa namba 15626 na kuweka maelezo yafuatayo:-
 Jina, Umri, aina ya biashara na eneo. Pia wanaweza kutuma maombi yao 
kwa kupitia barua pepe airtelfursa@tz.airtel.com ambapo watatakiwa 
kutuma jina kamili, umri, na aina ya biashara.
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment