December 14 ni siku ambayo Ligi Kuu ya Uingereza iliendelea tena ambapo moja kati ya mechi zilizochezwa ni ile ya Leicester City dhidi ya Chelsea. Mchezo huo uliyochezwa kwenye uwanja wa King Power ulimalizika kwa Chelsea kufungwa goli 2-1, matokeo yaliyoifanya Chelsea kufikisha jumla ya mechi 9 ilizofungwa katika mechi 16 walizocheza msimu huu.
Matokeo hayo yamemfanya Kocha Jose Mourinho
kuwa na wasiwasi na wachezaji wake kuwa wanamsaliti tofauti na jinsi
wanavyojipanga kwenye mazoezi lakini mwisho wa siku wanakuja kupoteza
pointi tatu. Mourinho aliongea huku akifoka wakati akifanya mahojiano na vyombo vya habari.
“Inachosha
sana kutizama kazi ambayo tumefanya ikisalitiwa, wakati mwingine nahisi
kama vile nilijitahidi kuimarisha uwezo wa wachezaji wetu msimu
uliopita na sasa inaonekana wameshindwa kustahimili ushindani katika
kiwango hicho. Hatuwezi maliza katika nafasi 4 za kwanza ila
tukijitahidi huenda tukacheza katika ligi ya Europa. Naona haya bila
shaka”>>>> Mourinho
0 comments:
Post a Comment