Mkurugenzi
wa Kampuni ya Bricoleur Holdings ya nchini Japan, Bi. Yu Shiran
(katikati) akiongea na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu
kushirikiana kufanya kazi za sanaa na Kikundi cha Sanaa cha Tingatinga,
leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO). Kulia ni Mwenyekiti wa
Kikundi cha Sanaa (Tingatinga), Bwana Zachi Chimwanda na kushoto ni
Mkurugenzi pia wa Kampuni ya Bricoleur Holdings ya nchini Japan, Bwana
Shoji Tsuchiya.
Katibu
Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bwana Godfrey Mngereza
(kushoto) akifafanua jambo wakati wa utiaji saini wa Mkataba wa
makubaliano kati ya Kikundi cha Sanaa cha Tingatinga na Kampuni ya
Kampuni ya Bricoleur Holdings ya nchini Japan. Katikati ni Wakurugenzi
wa Kampuni ya Bricoleur Holdings ya nchini Japan Bwana Shoji Tsuchiya
pamoja na Bi. Yu Shiran.
Na
Tupokigwe Marco na Mwanahamisi Matasi
Chama cha Sanaa
cha uchoraji picha maarufu kama Tinga Tinga kimetiliana saini Mkataba wa
Makubaliano wa miaka mitano wa kufanya kazi kwa pamoja na Kampuni ya
Bricoleur Holdings Co. Ltd ya nchini Japan utakaokiwezesha chama hicho
kunufaika kwa kuuza kazi zake Kimataifa.
Akiongea leo
wakati wa utiaji saini wa Mkataba huo, Mwenyekiti wa Chama cha Sanaa cha Tinga
Tinga, Bwana Zachi Chimwanda ameeleza kuwa, utiaji saini wa Mkataba huo utakua
chachu ya maendeleo katika kuwakomboa wasanii wachoraji katika kipato chao na
kuboresha hali zao za kimaisha kwakuwa kazi zao sasa zitakuwa zikiuzwa ndani na
nje ya nchi.
Kwa upande wake
Katibu Mtendaji wa Baraza la Wasanii la Taifa (BASATA), Bwana Godfrey Mngereza
alieleza kuwa Mkataba waliosaini kati ya Tinga Tinga na watu wa Bricoleur
Holdings Co. Ltd utaimarisha kazi za Wasanii katika fani ya uchoraji ikiwemo
kuongeza vipato vyao.
''Sanaa ni kazi
lakini pia ni biashara, imefika wakati kwa wasanii kufaidika na jasho lao,
kampuni hii watakua wakitafuta masoko kule Japan ili kazi hizi za wachoraji
toka Tanzania ziweze kununuliwa hali ambayo itawaongezea kipato'', alisema
Mngereza.
Aliongeza kuwa
Mkataba uliosainiwa kati ya pande zote mbili umepitia taratibu zote za kiserikali
na Taasisi zinazohusika na mambo ya sanaa na maslahi ya msanii na msanii yule
aliyehusika katika kuchora picha fulani atanufaika na mkataba huo.
''Kwa msanii
atakehusika binafsi na uchoraji picha mkataba utamwezesha kujua atanufaika vipi
na kwa muda gani'', aliongeza Mngereza.Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Kampuni ya Bricoleur Holdings Co. Ltd, Bi. Yu Shiran ameeleza
kuwa mpango huo wa Mkataba kati yao na Tingatinga una lengo la kukitangaza
Chama hicho cha wachoraji wa Tanzania Kimataifa.
‘’Kwa kutumia taarifa
za kidijiti za Tingatinga tutaweza kushirikiana na watengenezaji mbalimbali wa
bidhaa, na ili kulithibitisha hili, sisi na Tingatinga tumekuwa katika mjadala
wa takriban mwaka mzima sasa’’, alisema Bi. Shiran.
Tinga Tinga Arts
Group lilianzishwa nchini Tanzanja na Edward Saidi Tingatinga ambaye alifariki
mwaka 1972 ambapo kwa sasa kundi hilo lipo maeneo ya Oysterbay jijini Dar es
Salaam kikijihusisha na sanaa ya uchoraji.
0 comments:
Post a Comment