Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (aliyesimama) akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika leo (15.12.2015) Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Donald Mmbando na wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Hamis Kigwangalla.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (aliyesimama) akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika leo (15.12.2015) Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Donald Mmbando na kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Hamis Kigwangalla.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika leo (15.12.2015) Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wa nne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii mara baada ya kulifungua Baraza hilo leo (15.12.2015) Jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Hamis Kigwangalla (wa tano kutoka kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Donald Mmbando.
PICHA NA ISMAIL NGAYONGA- MAELEZO
Na Ismail
Ngayonga
MAELEZO
Dar Es
Salaam
15.12.2015
SERIKALI imewataka watumishi
wa sekta ya afya nchini kutofanya kazi kwa mazoea na badala yake kufanya kazi
kwa bidii na uadilifu ili kufikia malengo yaliyowekwa.
Hatua
hiyo inaelezwa itasiaidia kurahisisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa
wananchi kwa kutoa huduma bora na zinazofikiwa kwa wakati.
Akifungua
mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy
Mwalimu alisema kila mtumishi wa umma anapaswa kutekeleza kwa bidii ilani ya
Chama Tawala ya mwaka 2015.
“Sekta
ya Afya imeingizwa kwenye mpango wa Tekeleza kwa Matokeo makubwa sasa, ili
tuyakifia matokeo makubwa sasa pamoja na mambo mengine tunahitaji kubadilika
sana katika utendaji wetu wa kazi” alisema Mwalimu.
Aidha Waziri huyo alisema alisema pamoja na
mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa katika sekta ya afya, Wizara hiyo hiyo hiyo
haina budi kuakabiliana na chyangamoto mbalimbali zinazojitokeza ikiwemo vifo
vya akina mama wajawazito wakati wa kujifungua.
Kwa
mujibu wa Waziri Mwalimu aliwataka watumishi wa Wizara hiyo kutekeleza kwa
vitendo maagizo yaliyotolewa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika hotuba
yake ya kuzindua Bunge la 11, kwani hotuba yake ni dira ya maelekezo rasmi ya
masuala muhimu yanayopaswa kutekelezwa na kusimamiwa katika kipindi cha miaka
mitano.
Kwa
upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Donald Mmbando alisema katika
kutekeleza mpango wa tekeleza kwa matokeo makubwa sasa, Serikali imeanisha
maeneo 4 ya utekelezaji ili kuboresha huduma bora za afya kwa wanachi.
Dkt.
Mmbando alianisha maeneo hayo kuwa ni pamoja mgawanyo wa watumishi wa kada ya
afya, upatikanaji wa dawa, vifaa, vifaa
tiba na vitendanishi, ubora wa huduma pamoja na kupunguza vifo vya akina mama
wajawazito na watoto.
“Katika
kutekeleza haya, wiki ijayo tutazindua mpango mkakati wa miaka 5 wa sekta ya
afya (2016-20), ambapo tutahakikisha kuwa yote yaliyoanishwa katika Ilani ya
Chama Tawala tunaweza kuyafikia na kuyatekeleza” alisema Dkt. Mmbando
0 comments:
Post a Comment