Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu
Benjamin Wiliam Mkapa Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza na Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu Benjamin William Mkapa Ikulu
jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akimkaribisha Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu jijini Dar es
Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza na Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu jijini Dar
es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiagana na Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu jijini Dar es
Salaam. PICHA NA IKULU
JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu:
255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425
|
|
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA
BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 07
Januari, 2016 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu
Mheshimiwa Benjamin William Mkapa na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde
Warioba Ikulu Jijini Dar es salaam.
Akizungumza
mara baada ya Mazungumzo hayo Rais Mstaafu Mkapa amesema lengo la kukutana na
Rais Magufuli ni kumpongeza kwa dhamana aliyopewa na watanzania kuiongoza nchi,
kuunda serikali na kumtakia heri ya Mwaka Mpya.Rais
Mstaafu Mkapa pia amemhakikishia Rais Magufuli kuwa yupo tayari kutoa
ushirikiano wakati wote ama kufanya kazi yoyote endapo atahitajika kufanya
hivyo.
Kwa
upande wake Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba pamoja na kumtakia
heri ya Mwaka Mpya, amempongeza Rais Magufuli kwa jinsi alivyoanza kazi vizuri
hususani katika kusimamia ukusanyaji wa mapato, kubana matumizi na kuelekeza
matumizi kwenye maeneo muhimu ambayo yanawahusu wananchi yakiwemo afya na maji.Jaji
Warioba ameongeza kuwa Watanzania wote wanapaswa kumuunga mkono Rais Magufuli
kwa kazi kubwa anazofanya, ambazo ni kukomesha rushwa, ufisadi, matumizi mabaya
ya madaraka na wizi wa mali ya umma.
"Lazima
kila mmoja amuunge mkono Rais, tusije tukamuachie, pale ulipo kama ni mambo ya
rushwa uanzie hapo hapo, kama ni mambo ya matumizi mabaya ya madaraka anzia
hapohapo, tusije tukamuachia Rais pekee yake, yeye awe kiongozi wetu, lakini
watanzania wote tushughulike na matatizo hayo" alisisitiza Jaji Warioba.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
07
Januari, 2016