Pages

Ads 468x60px

Wednesday, October 28, 2015

Rais Kikwete apokea hati za Utambulisho kutoka kwa mabalozi wanne

JA1
Balozi mpya wa Misri hapa nchini Mhe.Yasser Ahmed Al Eldin Elshawaf wakiwalisha hati zake za utambulisho kwa Rais Kikwete ikulu jijini Dar Es Salam leo.

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo amepokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi wanne wanaziwakilisha nchi zao hapa Tanzania.Mabalozi waliowasilisha hati zao kwa Rais Kikwete ikulu asubuhi ya leo ni pamoja Mhe.Yasser Ahmed Al Eldin Elshawaf Balozi mpya wa Misri hapa nchini, Mhe.Yahel Vilan Balozi mpya wa Israel nchini Tanzania, Mhe.Bayani Mangibin balozi mpya wa Ufilipino nchini na Mhe. Tan Puay Hiang Balozi mpya wa Singapore nchini Tanzania.Pichani Mabalozi hao wakiwasilisha hati zao za utambulisho.
JA2
-Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea hati za utambusho kutoka kwa Mhe.Yahel Vilan Balozi mpya wa Israel hapa nchini,
JA3
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea hati za utambulisho kutoka kwa mhe.Bayani Mangibin Balozi mpya wa Ufilipino nchini Tanzania.
JA4
-Balozi mpya wa Singapore nchini Tanzania Mhe.Tan Puay Hiang akiwasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es salaam

Matokeo mengine ya kura za Urais 2015, time hii ni kutoka Dar, Mwanza, Manyara, Geita na kwengine



WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAAJIRI WATUMISHI WAPYA 588

1Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Adelhelm Meru akizungumza na waajiriwa wapya katika Ufunguzi wa   Semina Elekezi  iliyofanyika  katika Chuo cha Taifa cha  Utalii Kampasi ya Temeke, jijini  Dar es salaam.  Wengine ni Mkurugenzi  wa Idara Rasilimali watu Bw. Said Msambachi ( wa pili kushoto)    akiwa na   Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali watu Bi. Aurelia Matagi , ( wa kwanza kushoto) , Kwa upande wa kulia  ni Mkurugenzi wa Idara ya Utalii Bw. Zahoro Kimwaga pamoja Mkurugenzi  wa Idara ya Wanyamapori Bw. Herman Keryaro 

      Mkurugenzi  Msaidizi wa Rasilimali watu Bi Aurelia Matagi ( kulia) akiwa na Afisa Utumishi Mwandamizi  Bw. Safari, wakiwa wanatoa maelekezo ya kujaza fomu za kuajiriwa katika  Semina Elekezi  iliyofanyika  katika Chuo cha Taifa cha  Utalii Kampasi ya Temeke, jijini  Dar es salaam.
       Baadhi ya Watumishi wapya  walioajiriwa na Wizara ya Maliasili na Utalii wakiwa  katika  Ufunguzi wa  Semina Elekezi ya Waajiriwa wapya  iliyofanyika  katika Chuo cha Taifa cha  Utalii Kampasi ya Temeke, jijini  Dar es salaam.
       Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru akiwa ameongozana na Mkurugenzi  wa Idara ya Wanyamapori Bw. Herman Keryaro ( kushoto)  akiwa   pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali watu  Bw. Said Msambachi  ( kulia) mara baada ya Katibu Mkuu, Dkt.  Meru   kuwasili katika ufunguzi  wa  Semina Elekezi ya waajiriwa wapya  iliyofanyika  katika Chuo cha Taifa cha  Utalii Kampasi ya Temeke, jijini  Dar es salaam. 

MALALAMIKO YA CCM KUHUSU MATOKEO KWENYE BAADHI YA MAJIMBO.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

CCM inapenda kutoa taarifa ifuatayo kwa wana-CCM na kwa umma:
Chama cha Mapinduzi hakijaridhishwa na utaratibu wa kukusanya na kujumlisha matokeo kwenye baadhi ya majimbo. Katika majimbo manne kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa utaratibu wa uchaguzi, hasa katika kujumlisha matokeo, uliopelekea wabunge wa upinzani kutangazwa washindi. Majimbo hayo ni Iringa Mjini, Mikumi, Ndanda na Kawe.

 Wasimamizi wa uchaguzi katika majimbo haya wamevuruga uchaguzi. Kutokana na utata uliokuwa umejitokeza wakati wa zoezi la kujumlisha kura, CCM iliomba kura zihesabiwe upya lakini ikanyimwa haki hiyo ya msingi ambayo iko kwenye sheria. Kwenye baadhi ya majimbo, ikiwemo Nyamagana, wapinzani walipewa haki ya kura kuhesabiwa upya. 

Kwa msingi huo, CCM imeamua kwenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi katika majimbo haya. Tunataka sote tujiridhishe kwamba utashi wa wananchi umeheshimiwa. Bado tunaendelea kukusanya taarifa za maeneo mengine kama kulikuwa na ukiukwaji mkubwa uliobadilisha matakwa ya wapiga kura. 

Hata hivyo, tunakiri kwamba kwenye maeneo mengi tulikopoteza viti vya Ubunge, tumepoteza kihalali, hatuna malalamiko, tunaheshimu maamuzi ya wananchi, na tutafanya tathmini baada ya uchaguzi ili tubaini makosa na kuyarekebisha.

MAONI YA WAANGALIZI WA UCHAGUZI

CCM imepokea maoni ya awali ya waangalizi wa uchaguzi. Tumefarijika kwamba karibu wote wametoa kauli ya pamoja kwamba uchaguzi huu ulikuwa wa haki na huru, uliofanyika kwa uwazi na kwa amani – na kwamba changamoto zilizojitokeza ni ndogo na zimetokea katika maeneo machache kiasi zisingeweza kubadilisha matokeo ya uchaguzi yanayotangazwa sasa. 

Tumepokea mapendekezo waliyoyatoa kwa wadau mbalimbali kuhusu namna ya kuboresha mchakato wa uchaguzi kwa miaka ijayo, na hivyo kuimarisha demokrasia nchini mwetu. Kwa kauli za waangalizi hawa, kwamba, kwa jinsi uchaguzi ulivyoendeshwa, matokeo yanayotangazwa sasa ni kielelezo sahihi cha utashi wa Watanzania kuhusu viongozi wanaowataka.

MALALAMIKO YA UKAWA.

Tumesikia malalamiko ya viongozi wa UKAWA kupitia mkutano wao na waandishi wa habari jana. Tumeshangazwa na kauli kwamba hawakubali matokeo ya Urais yanayotangazwa na Tume. Hata hivyo, matokeo ya Ubunge wanayakubali na, kule wanakoshinda, wanayasheherekea. Tunashangazwa kwasababu Tume iliyoandaa uchaguzi wa Rais ni hiyo hiyo iliyoandaa uchaguzi wa Wabunge, wasimamizi ni walewale, vituo ni vilevile, na sheria na taratibu zilizotumika ni zilezile. 

Hata fomu ya matokeo walizosaini wakala wao kwenye vituo vya kupiga kura, zimegawanywa katika sehemu (columns) tatu: Urais, Ubunge na Udiwani. Mawakala wao walisaini fomu hizo kwenye vituo vya kupiga kura.  Wameanza kuwa na matatizo na matokeo haya baada ya kuona mwelekeo wa kushindwa. Kama mwelekeo ungekuwa tofauti, wangekuwa na imani na Tume, wasimamizi na taratibu zote. 

Tunaomba ifike pahala sasa kwamba, katika kuijenga demokrasia yetu na kuliimarisha taifa letu, tuanze utamaduni mpya wa anayeshindwa kunyanyua simu kumpigia anayeshinda na kumpongeza. Nafasi ya mwisho aliyonayo Mgombea wa UKAWA kuendelea kujijengea heshima katika jamii yetu, na kuwa mwanademokrasia, ni kwa kufanya hivyo siku Dkt. Magufuli atakapotangazwa mshindi.  

BREAKING NEWS : MATOKEO YA AWAMU YA SABA(7) KWA MAJIMBO 51 YA UCHAGUZI KWA NGAZI YA URAIS

























 
Blogger Templates