Pages

Ads 468x60px

Wednesday, November 25, 2015

PAPA FRANCIS ALAKIWA NA RAIS UHURU KENYATA JIJINI NAIROBI




Papa Francis akisalimiana na Rais wa Kenya, Mh. Uhuru Kenyatta wakayi alipowasili nchini Kenya leo ambapo atakuwa na ziara ya siku sita katika nchi za Afrika. Kushoto ni Mke wa Rais Kenyatta, Magret Kenyatta. 
Papa Francis  amewasili jana nchini Kenya hapo jana,ambapo anatarajia kuwa na ziara ya siku sita  katia nchi za Afrika kiwemo Uganda.

 Papa Francis akizungumza jambo na Rais wa Kenya, Mh. Uhuru Kenyatta mara baada ya kuwasili nchini Kenya jana ,ambapo leo atakuwa na ziara ya siku sita katika nchi za Afrika. Kushoto ni Mke wa Rais Kenyatta, Magret Kenyatta.
  Papa Francis akisaini kitabu cha wageni Ikulu,huku
Rais wa Kenya, Mh. Uhuru Kenyatta na Mkewe Magret wakishuhudia


 Picha ya Pamoja na Marais Wastafu wa Kenya,Mh Daniel Arap Moi na wa pili kutoka kulia ni Mwai Kibaki

TAARIFA KUHUSU UGONJWA WA MNYAUKO FUSARI WA PAMBA NA MBEGU ZISIZOOTA



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAARIFA KUHUSU UGONJWA WA
MNYAUKO FUSARI WA PAMBA NA MBEGU ZISIZOOTA
Serikali imewataka wachambuaji na wasambazaji  wa mbegu za pamba kuacha kuwasambazia wakulima mbegu zilizozalishwa katika maeneo yaliyobainika kuwa na ugonjwa wa mnyauko fusari (Fusarium Wilt Disease).  Kauli hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Huduma za Usimamizi, Bodi ya Pamba Tanzania, Bwana James Shimbe.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Bwana Shimbe amesema, ugonjwa wa mnyauko fusari unaweza kudhibitiwa ikiwa wakulima wa pamba watatumia mbegu bora kutoka kwa wasambazaji wanaotambulika na Bodi ya Pamba Tanzania.
Akizungumzia tatizo la kuenea kwa ugonjwa huo Bwana Shimbe amesema kwa kiasi fulani limetokana na baadhi ya wachambuaji wasio waaminifu kuendelea kusambaza mbegu za pamba za kupanda ambazo zinaweza kuwa zimetoka katika maeneo yaliyobainika kuwa na  ugonjwa wa mnyauko fusari.
“Tulishatoa maelekezo kwa kuwataka wasambazaji wa mbegu za pamba za kupanda kutosambaza mbegu zilizozalishwa katika maeneo yenye ugonjwa.”
Hivyo tunaendelea kusisitiza kuwa wakulima wawe makini wanapo nunua mbegu kutoka kwa wasambazaji wasiotambulika na watoe taarifa haraka kwa Bodi wanapoona mbegu hizo hazioti ili hatua za haraka zichukuliwe za kupeleka mbegu zingine mbadala ili kuendana na msimu wa kilimo.
Aidha, Bwana Shimbe amewataka wachambuaji wa pamba ambao ndio wasambazaji wa mbegu kuacha mara moja kuwasambazia wakulima mbegu ambazo zimetoka kwenye maeneo yaliyobainika kuwa na ugonjwa na badala yake mbegu za pamba hizo zisindikwe kuzalisha mafuta ya kula kama walivyokuwa wameelekezwa na Bodi hapo awali.

BODI YA CHAKULA,DAWA NA VIPODOZI YAKAMATA VIPODOZI FEKI BANDARI KUU YA MALINDI ZANZIBAR



Baadhi ya Vipozi vyenye Kemikali ambavyo vimepigwa marufuku kutumika duniani vikiwa vimetolewa katika Maboxi ambayo yalitumika kuviihifadhi. Vipodizi hivyo Vinasubiri kuteteketezwa na Maafisa wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Maafisa wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar wakifungua moja ya Boxi lenye Vipozi vyenye Kemikali ambavyo vimepigwa marufuku kutumika duniani baada ya kuvikama Bandarini vikitokea Marekani na Italy.

Na Miza Kona Maelezo Zanzibar .

Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi imekamata vipodozi haramu katika Bandari Kuu ya Malindi Zanzibar ambavyo vimepigwa marufuku kuingizwa nchini.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari huko Ofini Mombasa Unguja Mkaguzi wa Bodi hiyo Nassir Buheti amesema vipodozi hivyo haramu vimepigwa marufuku kuingizwa nchini kutokana na kuwa viatamba vyenye kemikali ambazo zenye kuleta madhara kwa binadamu kwa mwenye kuvitumia ikwemo kansa ulemavu pamoja na uharibifu wa ngozi.

Amevitaja vipodozi vyenyewe ni pamoja na Movet Crèame kutoka Itali na Medical Fade Crème kutoka Marekani vyote hivyo ni vyenye uzito wa tani tatu vilivyokuwa vimehifadhiwa katika Makontena yaliyochanganishwa na vitu vingine yaliyowekwa bandarini hapo.

Aidha amefahamisha kuwa vipodozi vya aina Movet Cream hutumika kwa matibabu ya ngozi lakini mpaka upate ushauri wa daktari ili kuepukana na madhara yaliyomo na kuweza kutumika kisheria.

Mkaguzi huyo ameeleza mawakala wa vipodozi hivyo wamedai kuwa havikukusudiwa kuingizwa nchini jambo ambalo vipodozi vya aina hiyo vimepigwa marufuku dunia nzima.Amesema Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi inafanya juhudi ya kutaka kudhibiti kuingiza bidhaa haramu nchini hivyo inaomba mashiriano makubwa kwa jamii ili iweze kufikia lengo lililokusudiwa.

Aidha Mkaguzi Buheti amesema Sheria inasema si ruhusa kuingiza, kuuza, kusambaza vipodozi haramu na kuwataka wafanyabiasha wa vipodozi, dawa pamoja na Chakula kutofanya udanganyifu wa bidhaa wanazoingiza ili kuepuka madhara yasiongezeke nchini.

MKEMIA MKUU WA SERIKALI AANDAA WARSHA


Beatrice Lyimo,Dar es Salaam.

Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imeandaa warsha ya mafunzo juu ya kujiandaa kukabiliana na dharura ya kemikali hatari na zenye madhara kwa afya na mazingira kwenye maeneo ya bandari.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mkemia mkuu wa serikali Prof. Samweli Manyele amasema kuwa lengo la warsha ya mafunzo hayo ni kuwasilisha na kusambaza matokeo ya utafiti kwa kuhamasisha matumisi salama ya kemikali katika ukanda wa afrika.

“kufundisha nchi za ukanda wa Afrika Mashariki juu ya namna ya kushughulika na kusimamia kemikali hatari na zenye madhara, namna ya kujiandaa na kukabiliana na matukio ya kemikali pamoja na kubadilisha uzoefu wa ushughulikiaji salama wa kemikali hizo kati ya nchi na nchi” aliongeza Prof Manyele.

Pia kujadili mahitaji ya nchi na kikanda pamoja na kutambua hatua za kuelekea njia bora Zaidi ya kujianda na kukabiliana na matukio ya kemikali katika maeneo ya bandari na njia za usafirishaji ni moja ya lengo ya warsha hiyo.

“Ni matumaini yangu warsha ya mafunzo hayo yatakuwa muhimu katika kuongeza uelewa wa washiriki na kujenga uwezo wao wa kushughulikia mizigo ya kemikali hatari kwa usalama na hivyo kulinda afya, mazingira na mali dhidi ya madhara ya kemikali hizo” alifafanua Prof. Manyele.

Warsha hiyo itafanyika kwa muda siku mbili kuanzia tarehe 26 hadi 27 Noverma, 2015 kwenye ukumbi wa Protea Courtyard Hotel iliyopo jijini dar es salaam na kuhusisha nchi mbalimbali.

Matumizi ya TEHAMA yaboresha ufanisi Serikalini.


Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini toka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Florence Temba akiwaeleza waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu utaratibu wa Serikali kutumia TEHAMA katika kufanya mikutano kwa kutumia mfumo wa Mawasiliano ya (Video comference) ambapo kikao kimoja kitawaunganisha pamoja washiriki kutoka Mikoa 8 ambapo mada huwasilishwa na kutoa fursa ya kuwasiliana moja kwa moja (interactivity) kwa maswali na ufafanuzi leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Bi Zamaradi Kawawa.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bi Zamaradi Kawawa akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano kati ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na vyombo vya habari uliofanyika leo jijini Dar es asalam.Kulia kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini toka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Florence Temba na Mkurugenzi wa TEHAMA Serikalini toka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Priscus Kiwango.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi kuhusu utaratibu wa Serikali kutumia TEHAMA katika kufanya mikutano ambapo mfumo wa Mawasiliano ya (Video comference) utatumika ili kupunguza gharama za mikutano kwa Taasisi za Serikali.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini toka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Florence Temba akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari kuhusu faida za kutumia TEHAMA ikiwemo kuokoa fedha zilizokuwa zinatumika awali kuandaa mikutano hiyo ambapo kwa sasa washiriki watashiriki mikutano hiyo wakiwa katika vituo vyao vya kazi leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa TEHAMA Serikalini toka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Priscus Kiwango.

JAJI MKUU WA TANZANIA MHE. OTHMAN CHANDE ATOA SOMO KWA WAANDISHI WA HABARI.

MO1
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande akitoa ufafanuzi kwa wanabari (hawapo pichani) kuhusu uandishi bora wa habari za Mahakama wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa Habari za Mahakama leo jijini Dar es salaam.
MO2
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande (kushoto) na Meneja wa Maadili wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Allan Lawa (kulia) wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari za Mahakama yaliyoandaliwa na Mahakama ya Tanzania leo jijini Dar es salaam.
MO3
Rais wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Jaji Mstaafu Thomas Mihayo akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari namna wanavyoweza kuandika habari za Mahakama kwa kuzingatia weledi wa taaluma zao.
MO4
Washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa Habari za Mahakama wakiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande leo jijini Dar es salaam.

HAKIELIMU YAZINDUA JOPO LA WASHAURI MABINGWA

Timu ya Menejimenti ya HakiElimu ikiwa katika picha na Mwenyekiti wa Bodi ya HakiElimu na Mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa jopo la washauri bingwa
Wafanyakazi wa Shirika la HakiElimu waliohudhuria uzinduzi katika picha ya pamoja na jopo la washauri bingwa
Waliosimama ni Prof. J. Galabawa (kushoto) Prof. Kitila Mkumbo (katikati) na Prof. Elias Jengo (kulia) Waliokaa ni John Kalage (Mkurugenzi wa HakiElimu) Prof. G.Mmari (katikati) na Prof. Prof. Martha Qorro (Kulia).
Mgeni rasmi Prof. Geofrey Mmari,akizungumza jambo katika hafla fupi ya uzinduzi wa jopo la washauri mabingwa akitoa neno la ufunguzi.
Prof. Kitila Mkumbo mmoja wa wajumbe wa ThinkTank akitoa neno kwa niaba ya jopo la washauri bingwa wa HakiElimu.
Mwakilishi wa Kamishna wa Elimu Bi, Joyce Sekimanga kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi akiwasilisha ujumbe kutoka serikali katika uzinduzi wa jopo la washauri wa HakiElimu
Prof. Martha Qorro mmoja wa wajumbe wa jopo la washauri mabingwa akipokea mpango mkakati wa HakiElimu kutoka kwa mgeni Rasmi Prof Geofrey Mmari
Prof. J. Galabawa mmoja wa wajumbe wa jopo la washauri mabingwa akipokea mpango mkakati wa HakiElimu
Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu John Kalage akielezea lengo la kuanzishwa kwa Think Tank
Washiriki katika uzinduzi wa jopo la washauri mabingwa wa HakiElimu


Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
SHIRIKA la HakiElimu  limezindua Jopo la Washauri Mabingwa  linaloundwa na maprofesa 10 waliobobea katika fani ya elimu ili  kuleta mabadiliko katika sekta ya elimu kwa watoto kupata elimu bora.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu , John Kalage amesema kazi ya jopo hilo itakuwa kutoa ushauri wa kitaalam juu ya masuala ya elimu kadri litakavyoombwa na  HakiElimu.
Amesema jopo hilo litatoa ushauri juu ya mikakati ,taratibu na mbinu za kuhakikisha ushiriki madhubuti katika kukuza na kutetea ubora wa elimu nchini.
Kalage aliwataja maprofesa wanaounda jopo hilo kuwa ni Abel Ishumi,Herme Mosha,Justinian Galabawa,Kitila Mkumbo,Suleiman Sumra,Martha  Qorro, Mwajabu Possi,Akundaeli Mbise, Masalukulangwa pamoja na Elias Jengo.
Amesema kuanzishwa kwa jopo hilo litasaidia shirika kupata mawazo mapana zaidi ya kitafiti na uchambuzi wa changamoto za sekta ya elimu.
Kalage amesema kuwa jopo hilo litakwenda sambamba na jitihada za serikali kuwa na mikakati mingi ya kuboresha elimu na azma ya serikali kutekeleza maazimio mbalimbali ya kimataifa kama  Malengo Maendeleo Endelevu (SDGs) na Incheon ya uboreshaji wa elimu.

TAMKO LA JUKWAA HURU LA WAZALENDO KUUNGA MKONO HOTUBA YA MAGUFULI



Mwenyekiti wa Jukwaa Huru la Wazalendo Ndugu Salum Ally Hapi akizungumza na waandishi wa habari kwenye hotel ya Travetine ,Magomeni jijini Dar es Salaam, kulia ni Katibu wa Jukwaa hilo Ndugu Mtela Mwampamba.

Ndugu wanahabari,
Mbele yenu sisi tuliowaita hapa ni Jukwaa Huru la Wazalendo ambalo limeitisha mkutano huu ili kufikisha yale tuliyoyakusudia kuwaeleza umma wa watanzania.

Sote tunatambua kuwa nchi yetu imetoka katika uchaguzi mkuu ambao umetupatia viongozi wapya wa awamu ya tano ya uongozi wa taifa letu chini ya Dr. John Pombe Joseph Magufuli. Tunapenda kuwapongeza watanzania wote kwa uchaguzi wa amani na utulivu. Aidha kwakua ndio mara yetu ya kwanza kuzungumza nanyi tunapenda kuwapongeza wanahabari wote kwa kazi nzuri ambayo mmekua mkiifanya kabla, wakati na baada ya uchaguzi mkuu nchini. Tunawashukuru sana.

Mkutano wetu huu umebeba madhumuni makubwa mawili.
Kwanza ni kumpongeza Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hotuba yake aliyoitoa Bungeni siku ya ufunguzi wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo tarehe 19/11/2015.

Tunaiunga mkono Hotuba yake ambayo kwa kweli ilikuwa imebeba Uzalendo, Ujasiri, dira ya kweli ya maendeleo ya taifa letu na muuelekeo mpya wa Serikali ya awamu ya tano. Mambo yote aliyozungumzia Mh. Rais yamebeba maslahi mapana ya nchi yetu na yanalenga kuijenga Tanzania mpya ambayo waasisi wa Taifa letu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Abeid Amani Karume walikusudia kuijenga.

Pili, pamoja na mambo mengi yaliyogusiwa na hotuba ya Mh. Rais, eneo la kubana matumizi na kupunguza matumizi yasiyo ya lazima kwa Serikali ni moja katika mambo ambayo Jukwaa hili limeamua kuyaunga mkono kwa vitendo. Mh. Rais alitoa mchanganuo wa eneo moja tu la safari za nje na jinsi lilivyo ligharimu Taifa mabilioni ya shilingi na kuahidi kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wake itajikita katika kupunguza matumizi yasiyo ya lazima.

Airtel yazindua 'Airtel Care' programu kwa wateja

Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando pamoja na Afisa Masoko Intaneti wa Airtel , Eric Daniel wakionyesha huduma mpya ya Airtel Care itakayowawezesha wateja wa Airtel kudownload application na kupata huduma zote kwa urahisi kupitia simu zao .
Afisa Masoko Intaneti wa Airtel , Eric Daniel (kushoto) akionyesha kwenye simu huduma mpya ya Airtel Care itakayowawezesha wateja wa Airtel kupata kudownload application ijulikanayo kamaAirtel Care na kupata huduma zote kwa urahisi. Akishuhudia ni Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando.

IKULU YAKANUSHA KUTOA TAARIFA YA RATIBA SIKU YA UHURU 9 DISEMBA


WANAHARAKATI WA TANZANIA WANATOA WITO KWA JAMII KUCHUKUA HATUA ILI KUMLINDA MTOTO APATE ELIMU BORA NA SALAMA

  Eda Malick kutoka Tanzania Women and Children Welfare center akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia
 Afande Christina Onyango, Afisa wa Polisi, mkoa wa kipolisi Ilala akielezea namna ambavyo dawati la jinsia wamejipanga kufikisha ujumbe wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
  Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini Tanzania wakihudhuria mkutano na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
 Bahati Mandago kutoka shirika la Tanzania Human Rights fountain akielezea mikakati ya shirika lake katika kufikisha ujumbe wa Funguka. Chukua Hatua Mlinde Mtoto apate elimu.

MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI MWAKA 2015 KUFANYIKA KITAIFA DESEMBA MOSI MKOANI SINGIDA


 Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk.Fatma Mrisho (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana, kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani mwaka 2015 yatakayofanyika kitaifa Desemba Mosi mkoani Singida. Kulia ni Mkurugenzi wa Habari na Uraghibishi.
 National Programe Officer wa UNAIDS, Fredrick Macha (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
 Mkurugenzi wa Uendeshaji Programu wa Taasisi ya Tunajali, Dk.Mussa Ndile akizungumza katika mkutano huo.
 Ofisa Uhusiano wa Tacaids (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
 Wapiga picha wa TV wakichukua tukio hilo.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Wadau wa masuala ya Ukimwi wakiwa katika mkutano huo wakisubiri kujibu maswali ya wanahabari.

Muhimbili yapatiwa msaada wa vifaa vya kuokoa maisha ya watoto

ST5
Baadhi ya vifaa vilivyokabidhiwa.
ST6
Mwakilishi wa UNICEF Tanzania, Dk Juma Gulaid akimkabidhi hati ya vifaa vya kuwahudumia watoto kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donan Mmbando.
ST7
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Mseru akipokea hati ya vifaa kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Donan Mmbando. Vifaa hivyo vimetolewa  na UNICEF.
ST1
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) Tanzania, Dk Juma Gulaid akisoma taarifa kabla ya kukabidhi vifaa vya kuhudumia watoto katika hafla fupi iliyofanyika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH). Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Donan Mmbando

SERIKALI YAAHIDI KUSHIRIKIANA NA MASHIRIKA NA WADAU WA HABARI KUTOKOMEZA VITENDO VYA UKATILI KWA WAANDISHI WA HABARI

IMG_2843
Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues akitoa neno la ufunguzi katika mkutano huo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua.
IMG_2914
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Prof. Ole Sante Gabriel akisisitiza jambo wakati akifungua rasmi mkutano wa kitaifa wa mashauriano kuhusu hali ya usalama wa waandishi wa habari, uzinduzi wa kikosi kazi cha usalama wa waandishi wa habari na uandishi unaozingatia maadili ambao umeandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Elimu, Sayansi (UNESCO).
IMG_3149
Makamu wa Rais wa Chama cha Kijamii cha Wanasheria wa Tanganyika, Bi. Flaviana Charles akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.
IMG_3178
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) katika tasnia ya Habari na Mawasiliano, Ayub Rioba akiwasilisha mada ya wajibu wa vyombo vya habari huku akitolea mfano wa moja ya habari iliyobeba kichwa cha habari "Uhuru wa habari watikiswa Zimbabwe" katika moja ya magazeti ya Serikali wakati wa mkutano wa kitaifa wa mashauriano kuhusu hali ya usalama wa waandishi wa habari, uzinduzi wa kikosi kazi cha usalama wa waandishi wa habari na uandishi unaozingatia maadili ulioandaliwa na UNESCO.
IMG_3212
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene akitolea ufafanuzi wa swali la Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima, Neville Meena (hayupo pichani).
IMG_3115
Ofisa Miradi katika kitengo cha Mawasiliano na Tehama UNESCO, Nancy Kaizilege akiwasilisha mada ya Uhuru wa vyombo vya Habari katika mkutano huo.
IMG_2832
Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues (katikati) akisalimiana na Mjumbe wa bodi udhamini ya Mtandao wa Radio Jamii Tanzania (COMNETA), Balozi Mstaafu, Christopher Liundi alipowasili katika mkutano wa kitaifa wa mashauriano kuhusu hali ya usalama wa waandishi wa habari, uzinduzi wa kikosi kazi cha usalama wa waandishi wa habari na uandishi unaozingatia maadili ulioandaliwa na UNESCO. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Prof. Ole Sante Gabriel.
 
Blogger Templates