Mkuu
 wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia 
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues akitoa 
neno la ufunguzi katika mkutano huo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi 
kufungua.
Katibu
 Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Prof. Ole Sante
 Gabriel akisisitiza jambo wakati akifungua rasmi mkutano wa kitaifa wa 
mashauriano kuhusu hali ya usalama wa waandishi wa habari, uzinduzi wa 
kikosi kazi cha usalama wa waandishi wa habari na uandishi unaozingatia 
maadili ambao umeandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na
 Elimu, Sayansi (UNESCO).
Makamu wa Rais wa Chama cha Kijamii cha Wanasheria wa Tanganyika, Bi. Flaviana Charles akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.
Mhadhiri
 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) katika tasnia ya Habari na 
Mawasiliano, Ayub Rioba akiwasilisha mada ya wajibu wa vyombo vya habari
 huku akitolea mfano wa moja ya habari iliyobeba kichwa cha habari 
"Uhuru wa habari watikiswa Zimbabwe" katika moja ya magazeti ya Serikali
 wakati wa mkutano wa kitaifa wa mashauriano kuhusu hali ya usalama wa 
waandishi wa habari, uzinduzi wa kikosi kazi cha usalama wa waandishi wa
 habari na uandishi unaozingatia maadili ulioandaliwa na UNESCO.
Mkurugenzi
 wa Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene akitolea ufafanuzi wa 
swali la Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima, Neville Meena 
(hayupo pichani). 
Ofisa
 Miradi katika kitengo cha Mawasiliano na Tehama UNESCO, Nancy Kaizilege
 akiwasilisha mada ya Uhuru wa vyombo vya Habari katika mkutano huo. 
Mkuu
 wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia 
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues 
(katikati) akisalimiana na Mjumbe wa bodi udhamini ya Mtandao wa Radio 
Jamii Tanzania (COMNETA), Balozi Mstaafu, Christopher Liundi alipowasili
 katika mkutano wa kitaifa wa mashauriano kuhusu hali ya usalama wa 
waandishi wa habari, uzinduzi wa kikosi kazi cha usalama wa waandishi wa
 habari na uandishi unaozingatia maadili ulioandaliwa na UNESCO. Kulia 
ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Prof. 
Ole Sante Gabriel.
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment