Siku moja baada ya Rais wa Tanzania kuweka headlines kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kwa raia wa Kenya, Rais Uhuru Kenyatta ameingia kwenye headlines za aina hiyo baada ya kufanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri la Kenya kwa kuchukuwa maamuzi ya kuwapiga chini Mawaziri wote ambao Wizara zao zinakumbwa na kashfa nzito za ufisadi!
Kama ilikuwa haijakufikia mpaka muda huu basi ikufikie kuwa uamuzi wa Rais Uhuru Kenyatta umekuja siku moja baada ya kutangaza kuwa tatizo la ufisadi Kenya ni tishio kubwa kwa kitaifa hilo na kuahidi kufanya mabadiliko hivi karibuni kama Rais anayeshikilia ofisi.
Vitu vimetendeka, na baadhi ya maamuzi yaliyofanywa na Rais Uhuru Kenyatta siku ya jana ni pamoja na kuongeza idadi ya Wiazara kutoka Wizara 19 hadi Wizara 20
kwa kile alichodai kuwa ni kuzisaidia Wizara kutekeleza majukumu yao
kwa ubora zaidi pamoja na kufanya uchaguzi mdogo ndani ya Wizara hizo.
Mawaziri waliokumbwa na kashfa
za ufisadi walijiondoa kwenye Wizara zao na sasa wanakabiliwa na kesi
za kujibu Mahakamani huku wengine kama Waziri wa Ugatuzi, Anne Waiguru alijiondoa madarakani kutokana na kashfa zilizoweka headlines kubwa Kenya, za kununua kalamu ya moja ya BIC kwa zaidi ya Tzs. 200,000/- za Kitanzania!
Maamuzi haya ya Rais Uhuru Kenyatta yameibua mjadala mkubwa kwa Wakenya na kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, baadhi wakionekana kufuraishwa na kitendo hicho, huku wengine wakihoji maamuzi ya Rais wao.
0 comments:
Post a Comment