Timu
 ya Menejimenti ya HakiElimu ikiwa katika picha na Mwenyekiti wa Bodi ya
 HakiElimu na Mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa jopo la washauri 
bingwa
Wafanyakazi wa Shirika la HakiElimu waliohudhuria uzinduzi katika picha ya pamoja na jopo la washauri bingwa
Waliosimama
 ni Prof. J. Galabawa (kushoto) Prof. Kitila Mkumbo (katikati) na Prof. 
Elias Jengo (kulia) Waliokaa ni John Kalage (Mkurugenzi wa HakiElimu) 
Prof. G.Mmari (katikati) na Prof. Prof. Martha Qorro (Kulia).
Mgeni
 rasmi Prof. Geofrey Mmari,akizungumza jambo katika hafla fupi ya 
uzinduzi wa jopo la washauri mabingwa akitoa neno la ufunguzi. 
Prof. Kitila Mkumbo mmoja wa wajumbe wa ThinkTank akitoa neno kwa niaba ya jopo la washauri bingwa wa HakiElimu.
Mwakilishi
 wa Kamishna wa Elimu Bi, Joyce Sekimanga kutoka Wizara ya Elimu na 
Mafunzo ya Ufundi akiwasilisha ujumbe kutoka serikali katika uzinduzi wa
 jopo la washauri wa HakiElimu
 Prof. Martha Qorro mmoja wa wajumbe wa jopo la washauri 
mabingwa akipokea mpango mkakati wa HakiElimu kutoka kwa mgeni Rasmi 
Prof Geofrey Mmari
Prof. J. Galabawa mmoja wa wajumbe wa jopo la washauri mabingwa akipokea mpango mkakati wa HakiElimu
Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu John Kalage akielezea lengo la kuanzishwa kwa Think Tank
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
SHIRIKA la HakiElimu 
limezindua Jopo la Washauri Mabingwa 
linaloundwa na maprofesa 10 waliobobea katika fani ya elimu ili  kuleta mabadiliko katika sekta ya elimu kwa
watoto kupata elimu bora.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es
Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu , John Kalage amesema kazi ya jopo
hilo itakuwa kutoa ushauri wa kitaalam juu ya masuala ya elimu kadri
litakavyoombwa na  HakiElimu.
Amesema jopo hilo litatoa ushauri juu ya mikakati
,taratibu na mbinu za kuhakikisha ushiriki madhubuti katika kukuza na kutetea
ubora wa elimu nchini.
Kalage aliwataja maprofesa wanaounda jopo hilo kuwa ni
Abel Ishumi,Herme Mosha,Justinian Galabawa,Kitila Mkumbo,Suleiman
Sumra,Martha  Qorro, Mwajabu
Possi,Akundaeli Mbise, Masalukulangwa pamoja na Elias Jengo.
Amesema kuanzishwa kwa jopo hilo litasaidia shirika
kupata mawazo mapana zaidi ya kitafiti na uchambuzi wa changamoto za sekta ya
elimu.
Kalage amesema kuwa jopo hilo litakwenda sambamba na
jitihada za serikali kuwa na mikakati mingi ya kuboresha elimu na azma ya
serikali kutekeleza maazimio mbalimbali ya kimataifa kama  Malengo Maendeleo Endelevu (SDGs) na Incheon ya
uboreshaji wa elimu. 
 
 
 
 
 
 











 
 
0 comments:
Post a Comment