Pages

Ads 468x60px

Wednesday, December 30, 2015

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR YASAINI MIKATABA MIWILI YA UJENZI NA MAKANDARASI M/S.HUMPHREY CONTRUCTION LIMITED YA ARUSHA NA MINDSET TECHIES (T) YA DAR ES SALAAM.

 Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Khadija Bakari Juma akitoa ufafanuzi kwa Wadau waliohudhuria hafla ya Utiaji Saini wa Mikataba miwili ya Ujenzi baina ya Wizara yake na Makandarasi kutoka M/S. Hamphrey Construction Limited ya Arusha na Mindset Teches (T) ya Dar es Salaam Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Wizara ya Elimu Zanzibar.
 Wadau mbalimbali waliohudhuria katika sherehe za kutiliana saini mikataba hiyo.
  Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Khadija Bakar Juma na Mkandarasi wa Kampuni ya M/s.Humphrey Construction Limited ya Arusha wakitiliana saini Mkataba wa kupanua Taasisi ya Maendeleo ya Utalii iliopo Maruhubi.
 Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Khadija Bakar Juma na Mkurugenzi wa Kampuni ya Ujenzi M/s. Humphrey Construction Limited ya Arusha wakibadilishana Mikataba baada ya kutiliana saini.

SPIKA WA BUNGE, JOB NDUGAI AMEREJEA LEO KUTOKA INDIA


SPIKA WA BUNGE, JOB NDUGAI AMEREJEA LEO KUTOKA INDIA ALIKOKUWA KWA AJILI YA MATIBABU. AWASHUKURU WATANZANIA KWA MAOMBI YAO. AELEZEA HALI YAKE KUWA NI IMARA KABISA.
 Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akilakiwa na Naibu Spika wa Bunge Mhe. Tulia Ackson mara baada ya kuwasili katika uwanja Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Nchini India alikokuwa kwa ajili ya matibabu.
 Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akilakiwa na Naibu Spika wa Bunge Mhe. Tulia Ackson mara baada ya kuwasili katika uwanja Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Nchini India alikokuwa kwa ajili ya matibabu.
  Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akisalimiana na Naibu Waziri wa Nishai na Madini Mhe. Medard Kalemani mara baada ya kuwasili katika uwanja Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Nchini India alikokuwa kwa ajili ya matibabu. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge Mhe. Tulia Ackson na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambula na aliyeko kulia ni Katibu wa

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ampongeza Mbwana Samatta kwa kujiunga na klabu ya Genk ya Ubelgiji

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye(kushoto) akiongea na Mchezaji wa Timu ya TP Mazembe Mbwana Samatta(kulia) leo jijini Dar es salaam.Mbwana amemtembelea waziri Nape ofisini kwake na kuomba baraka za wizara katika kinyanganyiro cha kugombea uchezaji bora wa afrika anayechezea ligi za ndani na pia kumpa habari njema za yeye kutegemea kujiunga na timu ya Ubelgiji ya Genk.
Waziri wa Habari,Utamaduni,sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye(katikati)akiongea na waandishi wa Habari na kuwaomba watanzania kumwombea Mbwana Samatta ili ashinde katika kinyanganyiro cha kugombea uchezaji bora wa afrika anayechezea ligi za ndani kwani ni jambo la Taifa zima.Mhe Nape pia alimhakikishia kuwa Serikali ipo nyuma yake na ipo katika mkakati wa kuifanya michezo kuwa Shughuli Rasmi kwani itawafaidisha wanamichezo na Serikali kwa kupata kodi. 

Mchezaji wa TP Mazembe Mbwana Samatta(wa kwanza kushoto)akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) sababu za yeye kumtembelea Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo katika ofisi ya Wizara hiyo.Mbwana alisema kuwa amemtembelea waziri uyo kwa ajili ya kumfahamisha kuwa yumo katika kinyanganyiro cha kugombea uchezaji bora wa afrika anayechezea ligi za ndani na hivyo kuomba baraka za Wizara.Pia kumpongeza Mhe. Nape kwa kuchaguliwa kuwa waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.Mbwana anategemea kujiunga na klabu ya Mpira ya Genk ya Ubelgiji kwa mkataba wa miaka minne.

Tume ya Mipango waaswa kufanya tafiti ili kuongeza ukusanyaji mapato.


 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akisaini kitabu cha wageni baada ya kufika katika Tume ya Mipango. Kulia ni Kaimu Katibu Mtendaji Bi. Florence Mwanri.

  Baadhi ya wafanyakazi wa Tume ya Mipango wakimpokea Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango alipowatembelea kwa lengo la kuwaaga.
 Mmoja ya watumishi wa Tume ya Mipango Bw. Mohamed Ally akiongea mawili matatu na waziri mara baada ya mkutano kuisha.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Tume ya Mipango wakimpokea Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango alipowatembelea kwa lengo la kuwaaga.
 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiongea na watumishi wa Tume ya Mipango alipowatembelea kwa kusudi la kuwaaga.
 Kaimu Katibu Mtendaji Bi. Florence Mwanri akimsikiliza kwa makini Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango.
 
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango ameiagiza Tume ya Mipango kufanya utafiti kuhusu mapato ya Serikali na namna ya kuongeza wigo wa ukusanyaji mapato.

Amesema Tume ya Mipango kama chombo cha ushauri kwa Serikali kuhusu mipango na uchumi wa nchi, ni lazima ifanye utafiti juu ya ufanisi wa ukusanyaji wa mapato na kuongeza vyanzo wa kukusanya mapato ya Serikali ili kuiwezesha Serikali kuwahudumia wananchi wake.

“Serikali isipokusanya kodi kwa ufanisi haiwezi kuwahudumia wananchi hivyo, ni lazima kodi ikusanywe ipasavyo ili kuiwezesha kujiendesha” alisema.

Dkt Mpango aliyasema hayo alipokutana na wafanyakazi wa Tume ya Mipango kwa lengo la kuwaaga baada ya kuteuliwa na Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kuwa Waziri wa Fedha na Mipango.

Waziri wa Fedha amesema mianya yote ya ukwepaji kodi ni lazima izibwe ili kuiwezesha Serikali kukusanya mapato ya kutosha suala ambalo litairahisishia utoaji wa huduma za msingi kwa wananchi.

Amesema Serikali haiwezi kutegemea kila kitu kutoka kwa wafadhili wakati nchi ina rasilimali za kutosha hivyo.Dkt. Mpango amesema Tume ya Mipango ni lazima iongoze nchi kuelekea katika uchumi wa viwanda ambavyo vitafanya pato la taifa kuongezeka na kutoa ajira kwa wananchi.

“Sisi kama wataalamu tunatakiwa kuiongoza nchi katika kufikia kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 jambo ambalo linawezekana” alisema.Waziri pia amesema ni lazima tujenge uchumi imara na madhubuti utakaowezesha kupunguza umaskini miongoni mwa wananchi.

“Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuboresha ufanisi na utendaji wa Serikali kwa ujumla hivyo ninyi kama wataalamu mna mchango mkubwa katika kutimiza hilo” alisema.

Tume ya Mipango ni chombo mahususi cha fikra rejea na ushauri kwa serikali kuhusu sera na mikakati ya maendeleo, kiuchumi na kijamii ambao unaambatana na ufuatiliaji na utathmini wa mwenendo wa uchumi nchini.

Aliwataka wafanyakazi wa Tume ya Mipango kufanyakazi kwa bidii, maarifa na weledi mkubwa ili kuimarisha utendaji Serikalini.
 
Blogger Templates