Waziri
 wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye(kushoto) akiongea 
na Mchezaji wa Timu ya TP Mazembe Mbwana Samatta(kulia) leo jijini Dar 
es salaam.Mbwana  amemtembelea waziri Nape ofisini kwake na kuomba 
baraka za wizara katika kinyanganyiro cha kugombea uchezaji bora wa 
afrika anayechezea ligi za ndani  na pia kumpa habari njema za yeye 
kutegemea kujiunga na timu ya Ubelgiji ya Genk.
Waziri
 wa Habari,Utamaduni,sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye(katikati)akiongea 
na waandishi wa Habari na kuwaomba watanzania kumwombea Mbwana Samatta 
ili ashinde katika kinyanganyiro cha kugombea uchezaji bora wa afrika 
anayechezea ligi za ndani kwani ni jambo la Taifa zima.Mhe Nape pia 
alimhakikishia kuwa Serikali ipo nyuma yake  na ipo katika mkakati wa 
kuifanya michezo kuwa Shughuli Rasmi kwani itawafaidisha wanamichezo na 
Serikali kwa kupata kodi. 
Mchezaji
 wa TP Mazembe Mbwana Samatta(wa kwanza kushoto)akiongea na waandishi wa
 habari(hawapo pichani) sababu za yeye kumtembelea Waziri wa 
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo katika ofisi ya Wizara hiyo.Mbwana 
alisema kuwa amemtembelea  waziri uyo kwa ajili ya kumfahamisha kuwa 
yumo katika kinyanganyiro cha kugombea uchezaji bora wa afrika 
anayechezea ligi za ndani na hivyo kuomba baraka za Wizara.Pia 
kumpongeza Mhe. Nape kwa kuchaguliwa kuwa waziri wa 
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.Mbwana anategemea kujiunga na klabu ya
 Mpira ya Genk ya Ubelgiji kwa mkataba wa miaka minne.
 
 
 
 
 
 



 
 
0 comments:
Post a Comment