Mwakilishi
wa Kaimu Mkuruegenzi Mkuu wa NHIF, Eugen Mikongoti akifungua kikao
kilichowashirikisha wenyeviti wa bodi na makatibu wa Vituo Vya Afya,
Zahanati na Hospitali wa Manispaa ya Temeke juu ya mpango wa bima ya
afya kwa kayo iliyofanyika leo jijni Dar es Salaam.
Meneja
wa Mkoa wa Temeke wa NHIF, Costantino Makala akitoa maada katika kikao
hicho leo latika ukumbi wa Temeke jijini Dra es Salaam.wa katikati ni
Mwakilishi wa Kaimu Mkuruegenzi Mkuu wa NHIF,Eugen Mikongoti Kushoto ni
Mganga Mkuu wa Manispaa Temeke,Silvia Mamkwe.
Sehemu ya Wenyeviti wa Bodi na Makatibu wa Vituo vya Afya ,Zahanati na Hospitali katika kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii)
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MFUKO
wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umesema mpango wa huduma ya afya katika
kaya utasaidia upatikanaji wa huduma bora ya matibabu kwa jamii kutokana
na mchango wao wa uanachama.
Akizungumza
leo Wenyekiti wa Bodi na Makatibu Afya wa Manispaa ya Temeke,
Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Eugen Mikongoti amesema
sharia iko tayari kwa ajili ya mpango huo kinachotakiwa ni utekelezaji
kwa wananchi katika kupata huduma hiyo.
Mikongoti
amesema kuwa kila mtu mmoja katika kaya kwa Manispaa ya Temeke
atachangia Sh.50000 ambapo atapata matibabu kwa mwaka mmoja katika
Vituovya Afya,Zahanati na Hospitali katika Manispaa hiyo.
Amesema
fedha ambazo watachangia zitatumika katika kununua dawa na vifaa tiba
katika Manispaa hiyo hivyo kila mwananchi atakayejiunga na mpango huo
matibabu kwa kutambua mchango wake na dawa lazima ziwepo pamoja na vifaa
tiba.
Mikongoti
amesema kuwa fedha zinazochangwa na wanachama katika mpango ho
zitatumika kwa malenfo yaliyokusudiwa na serikali itachangia asilimia
50.
Amesema
NHIF itahakikisha kila mwananchi anakuwa na bima ya afya ili kuweza
kupata matibabu yake wakati akifikwa na magonjwa kwani wakati mtu
anaweza kuugua ugonjwa na kuweza kushindwa kupata matibabu kutokana na
kutokwepo katika mapango wowote.
“NHIF
itakuwa karibu na wananchi kama tunavyofanya nia yetu ni kutaka kila
mwananchi anakuwa na bima ya afya ya kumfanya maisha yake yawe mazuri
ya uhakika wa matibabu”amesema Mikongoti.
0 comments:
Post a Comment