Waziri
Mkuu, Kassim Majliwa akikagua bandari ya Dar es salaam Desemba 3, 2015
ambako alikwenda kupata ukweli kuhusu makontena 2,431 yaliyopitia
kwenye bandari hiyo bila kulipiwa kodi ya serikali.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mfumo wa kukagua makontena bandarini
kwa kutumia scaner huku akipata maelzo kutoka kwa Ofisa wa forodha,
January Shauri wakati alipotembelea bandari ya Dar es salaam Desemba 3,
2015 kutaka kujua ukweli wa tuhuma za makontena 2431 yaliyopita
bandarini hapo bila kulipiwa kodi ya serikali.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu utoaji bili za kulipia
kodi za serikali kwa watumiaji wa bandari ya Dar es salaam kutoka kwa
ofisa mwandamizi wa masuala ya fedha , Bw. Sartho Mbuya wakati
alipotembelea bandari hiyo Desemba 3, 2015 kutaka kujua ukweli wa
tuhuma za makontena 2431 yaliyopita bandarini hapo bila kulipiwa kodi za
serikali.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akimwonyesha Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es
salaam, Bw. Abel Mhanga (kulia) orodha ya makontena 2,431 yaliyopitia
kwenye banda ya Dar es salaam bila kulipiwa kodi wakati alipofanya ziara
kwenye bandari hiyo Desemba ,3, 2015.
Waziri
Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika
la Reli nchini TRL wakati alipotembelea stesheni ya Dar es salaam
kukagua uendeshaji wa Shirika hilo Desemba 3, 2015.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akitembelea steheni ya reli ya Dar es salaam Desemba 3, 2015.
WAZIRI MKUU ATINGA TENA BANDARINI NA TRL
*Akuta makontena 2,431 yametoka bila kulipiwa ushuru
*Ataka majina yaletwe ofisini leo saa 11 jioni
*Atoa wiki wiki moja kwa mfumo wa malipo kubadilishwa
*Akagua mabehewa, awaweka kiporo TRL
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amefanya ziara nyingine ya kushtukiza bandarini na
kukagua mfumo wa upokeaji na utoaji mizigo na utozaji wa malipo baada
ya kupewa taarifa kwamba kuna makontena 2,431 yametolewa bila kulipiwa
ushuru.
Waziri
Mkuu alisema kwa mujibu wa taarifa ya ukaguzi wa bandari ya kuanzia
Machi hadi Septemba 2014, makontena hayo yalipita bila kulipiwa kodi
kupitia bandari kavu nne (ICDs) ambazo ni JEFAG, DICD, PMM na AZAM.
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo, ni watumishi 10 tu ambao wamesimamishwa kazi
kutokana na makosa hayo. “Mmeamua kuwasimamisha kazi watu wadogo na
kuwaacha wakubwa wanaendelea na kazi. Hatuwezi kuendelea kuikosesha
Serikali mapato namna hii,” alisema Waziri Mkuu.
Waziri
Mkuu amemtaka Kaimu Meneja wa Bandari, Bw. Hebel Mhanga amletee ofisini
majina ya watumishi wote waliohusika na ukwepaji kodi huo ifikapo leo
saa 11 jioni. Pia amempa Meneja huyo wiki moja kuhakikisha kuwa mamlaka
hiyo inabadilisha mfumo wa utozaji malipo kutoka kwenye billing system
na badala yake kuweka mfumo wa malipo wa kielektroniki (e-payment).
Ametoa
agizo hilo leo (Alhamisi, Desemba 3, 2015), wakati akikagua idara
mbalimbali za mamlaka ya bandari na kuona ukaguzi wa mizigo
unavyofanyika kwa kutumia scanners. Akiwa kwenye chumba cha scanner
mojawapo, Waziri Mkuu alikuta manifest moja ikisema kontena limejaa
diapers lakini picha ya kwenye kompyuta ya scanner ilionyesha kuwa ndani
ya kontena hilo kuna vitu kama vifaa vya umeme.
Kwa
mujibu wa Kaimu Meneja Bandari upande wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA), Bw. Ben Usaje ambaye pia ni msimamizi wa kitengo cha scanner,
inapobainika taarifa kama hiyo inapaswa itumwe kwa wenye ICDs ili
wafanye ukaguzi kwa kulifungua kontena ili kuhakikisha mali zilizomo
ndizo zilizoandikishwa kwenye manifest.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu Majaliwa amefanya ziara ya kushtukiza
kwenye ofisi za Shirika la Reli (TRL) na kukagua mabehewa yaliyokuwepo
kisha akazungumza na baadhi ya wafanyakazi waliokuwepo kwenye stesheni
hiyo ambako alibaini madudu kwenye malipo ya mishahara na makato ya
michango ya wafanyakazi.
Akizungumza
na Mkurugenzi Mkuu TRL, Mhandisi Elias Mshana, Waziri Mkuu alisema
amefika kwenye shirika hilo ili kujifunza utendaji wao kazi lakini anazo
taarifa za wao kupewa fedha na Serikali kiasi cha sh. bilioni 13.5/-
ili waendeleze miundombinu ya reli lakini hawakufanya hivyo. “Nia ya
kuwapa fedha hizo ilikuwa ni kuboresha miradi ili muweze kujiendesha
kibiashara lakini nyie mkaamua kujilipa wenyewe,” alisema.
“Ninazo
taarifa kuwa baada ya hapo, mlikopa sh. bilioni 3 kutoka benki ya TIB
ili kuendesha miradi ya shirika lakini badala ya kufanya miradi, fedha
hizo mkaamua nazo kujilipa mishahara. Sasa sijui mnarudishaje huo mkopo
wakati hakuna mradi wowote uliofanyika,” alihoji bila kupata majibu.
Alipoulizwa
wafanyakazi wana matatizo gani hapo TRL, Katibu wa TRAWU, Bw. Boaz
Nyakeke alisema wanadai malimbikizo ya makato yao kwenye mifuko ya
pensheni, malimbikizo ya makato kwenye SACCOS na malimbikizo ya kuanzia
Julai – Novemba 2014.
Waziri
Mkuu kwa upande wake alimtaka Mhandisi Mshana asimamie uboreshaji
huduma za usafiri wa treni katika Jiji la Dar es Salaam ili hata mabasi
ya mwendo kasi yatakapoanza wananchi waweze kuwa na uhuru wa kuchagua
aina ya usafiri wautakao.
“Tunataka
kujenga yadi kubwa nje ya mji ili watu wenye magari wawe wanayaacha
huko na kutumia usafiri wa treni au DART kuja mjini kama njia mojawapo
ya kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es Salaam,” alisema.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
ALHAMISI, DESEMBA 3, 2015.
0 comments:
Post a Comment