Pages

Ads 468x60px

Wednesday, December 23, 2015

DAWASCO YAONGEZA USAMABAZAJI WA MAJI SAFI KUPAMBANA NA UGONJWA WA KIPINDUPINDU DAR

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Said Meck Sadick akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani ofisini kwake leo alipokutana nao kuelezea utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa kwa DAWASCO kuhusu usambazaji wa maji safi na salama ili kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.
Afisa Mtendaji Mkuu wa  DAWASCO Mhandisi Cyprian Luhemeja akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani Dar es salaam  leo alipokutana nao kuelezea utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na  Serikali kuhusu usambazaji wa maji safi na salama ili kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.Picha zote na Ally Daud-Maelezo.

Shirika la Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASCO) limeongeza uzalishaji na usambazaji wa Maji safi na Salama kwa wakazi wa jiji hilo hadi kufikia mita za ujazo 280,000 kwa siku ili kubabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu  uliolikumba jiji hilo hivi karibuni. 

Hatua hiyo inatokana na utekelezaji wa maagizo ya Serikali yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadiki kuitaka DAWASCO kusambaza maji safi na salama kwa wakazi wa jiji hilo ili kupambana na Ugonjwa wa Kipindupindu.

Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mkuu wa mkoa huo Bw. Sadick amesema kuwa kufuatia maagizo aliyoyatoa kwa shirika hilo ikiwemo kusambaza maji safi na salama kwa wananchi pamoja na kutengeneza mifereji ya kupitsha maji taka ili yasiingiliane na mikondo ya maji safi, DAWASCO wametekeleza kwa kiasi kikubwa maagizo hayo.

“Dawasco imehakikisha inazalisha maji safi na salama kati ya mita za ujazo 270,000 na 280,000 kila siku kwa muda wote tangu mlipuko ulipotokea na imehakikisha inasafisha na kusambaza kwa wananchi yakiwa katika viwango vya ubora unaokubalika kwa ajili ya matumizi kwa binadamu” amesema Bw. Sadick.

Ameongeza kuwa Dawasco imejenga vizimba vya maji  safi na salama kwenye maeneo mbalimbali ambayo hayajakumbwa na yaliyokumbwa na athari za mlipuko wa ugonjwa huo kwa jumla ya vizimba 48 ambavyo maeneo ya Kinondoni vizimba 5, Magomeni vizimba 38 na Ilala vizimba 5.

Aidha, amesema kuwa DAWASCO kwa kushirikiana na Ofisi ya Bonde Wami Ruvu imeanza kazi ya kusajili na kuwatambua watu binafsi wenye visima virefu vilivyopo kisheria ambao wanauza maji kwa wananchi ili kuvitambua na kudhibiti ubora wa maji na bei yake ambapo zoezi hili litaendelea hadi Machi 2016.

“Dawasco imefanya jitihada za kuweka dawa ya kuua wadudu aina ya chrolination kwenye maboza  wakati wa  usajili kabla ya kuruhusiwa kufanya biashara ya kuuza maji kwa wananchi na kuongeza sehemu za kuchota maji kwa kuwapelekea wananchi huduma hiyo wakitumia magari yenye matanki yaliyokuwepo kutoka 12 mpaka kufika 49 kwa sasa” aliongeza Bw.Sadick.Katika hatua nyingine Bw. Sadick alitoa rai kwa wakazi wa jiji hilo kuendelea na tabia ya kufanya usafi mara kwa mara ili kutokomezakabisa ugonjwa wa kipindupindu kwani kuanzia juzi hakuna wagonjwa waliopokelewa katika vituo vyote.

Kwa upande wa Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO Mhandisi Cyprian Luhemeja alisema kuwa wako katika hatua za mwisho kukamilisha ujenzi wa mifereji ya kupitisha maji machafu ili isiingiliane na maji safi kwa wiki mbili zijazo.

“kufikia Februari mwakani tutaweza kutoa maji safi na salama ya kutosha kwa wananchi  wote wa Dar es salaam bila ya matatizo yoyote” alisisitiza Mhandisi Cyprian.   

RAIS MAGUFULI ATOA ZAWADI ZA SIKUKUU YA KRISMASI KWA WATOTO WANAOISHI KWENYE KITUO CHA KUHUDUMIA WATOTO WA KIJIJI CHA MATUMAINI MKOANI DODOMA.

 Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Sekretarieti ya Mkoa wa Dodoma Bi. Ziada Nkinda (Aliyebeba Mtoto) akikabidhi zawadi za siku kuu ya Noeli (Christmas) zilizotolewa na Mhe. Rais John Pombe Magufuli kwa watoto wanaoishi kwenye kituo cha kuhudumia watoto cha kijiji cha matumaini Mkoani Dodoma.
Meneja wa kituo cha kuhudumia watoto cha kijiji cha matumaini kilichopo Dodoma  Padiri Vicent, kwa niaba ya watoto wa kituo hiko, akimshukuru Bi. ziada Nkinda kwa kukabidhi zawadi zilizotolewa na Mhe. Rais John Pombe Magufuli zikijumuisha mchele kilo 121, Mbuzi wawili na mafuta ya kupikia lita 40 vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya laki sita.

MAJALIWA AKABIDHI MSAADA WA PIKIPIKI NA PAMPU ZA MAJI


pu3
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi  Bw.Bakari Amir pampu  mbili za kusukuma maji na mipira yake, Mwenyekiti wa kikundi cha kufyatua matofali ya kuchoma cha Jitumecha kilichopo eneo la Gogovivu wilayani Ruangwa  Desemba 23, 2015.  Pampu hizo zitawapunguzia wnakikundi mzigo wa kubeba maji toka mtoni. 
pu4
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi funguo na kadi ya pikipiki Mwenyekiti wa kikundi cha Bodaboda Mkowe cha kijiji cha Nandagara, Yahya Chitanda ambayo ameikipatia kikundi hicho  Desemba 23, 2015 ili kiweze kukuza mtaji wake.
pu1
Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na  maofisa wa jeshi la Polisi wakati alipotembelea kituo kikuu cha polisi zcha wilaya ya Ruangwa kusalimana na Askari Desemaba 23, 2015. Wapili kushoto ni mkewe Mary na watatu kushoto ni Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Lindi, Renata  Mzinga.

RAIS MAGUFULI AONANA NA MJUMBE MAALUMU WA RAIS PAUL KAGAME WA RWANDA NA MABALOZI WA USWISI NA KUWAIT



Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na balozi wa Kuwait hapa nchini Mhe. Jasem Al Najem Ikulu jijini Dar es salaam leo Disemba 23, 2015.
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na Mjumbe Maalum wa Rais Paul Kagame wa Rwanda ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Louise Mushikwabo Ikulu jijini Dar es salaam leo Disemba 23, 2015.
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na balozi wa Uswisi hapa nchini Mhe. Florence Tinguely Ikulu jijini Dar es salaam leo Disemba 23, 2015.

TTCL Yazindua Teknolojia ya 4G LTE




Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) na Ofisa Ufundi (IT) wa kampuni hiyo, Rehema Maswanya (kulia) kwa pamoja wakifungua pazia kuashiria uzinduzi wa teknolojia ya 4G LTE iliyozinduliwa leo jijini Dar es Salaam.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya uzinduzi wa teknolojia ya 4G LTE inayotolewa na kampuni hiyo. Kushoto ni Ofisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya TTCL, Peter Ngota akiwa katika mkutano huo.

Ofisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya TTCL, Peter Ngota (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hafla ya TTCL kuzinduwa teknolojia ya 4G LTE iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) na Ofisa Ufundi (IT) wa kampuni hiyo, Rehema Maswanya (kulia) kwa pamoja wakifungua pazia kuashiria uzinduzi wa teknolojia ya 4G LTE iliyozinduliwa leo jijini Dar es Salaam.


Uzinduzi wa mtandao unaotumia teknolojia ya 4G LTE toka TTCL leo.

Kulia ni wataalamu wa huduma ya teknolojia ya 4G LTE kutoka TTCL wakitoa ufafanuzi kwa baadhi ya wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya uzinduzi wa mtandao unaotumia teknolojia ya 4G LTE.

Kulia ni wataalamu wa huduma ya teknolojia ya 4G LTE kutoka TTCL wakitoa ufafanuzi kwa baadhi ya wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya uzinduzi wa mtandao unaotumia teknolojia ya 4G LTE.

Kushoto ni wataalamu wa huduma ya teknolojia ya 4G LTE kutoka TTCL na maofisa waandamizi wakitoa ufafanuzi kwa baadhi ya wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya uzinduzi wa mtandao unaotumia teknolojia ya 4G LTE


KAMPUNI ya Simu nchini Tanzania (TTCL) leo imezinduwa mtandao unaotumia teknolojia ya 4G LTE unaoanza kutoa huduma jijini Dar es Salaam. Mtandao huo wenye teknolojia mpya na ya kisasa wenye kasi kubwa utatoa huduma katika maeneo 11 ambayo ni pamoja na Uwanja wa Ndege wa Mwalimu J.K. Nyerere, Pugu Road, Posta Mpya, Upanga, Kinondoni, Ubungo, Oysterbay, Mwenge, Mbezi Tangibovu, Mbezi Exchange, Kunduchi Salasala, na Wazi Tegeta.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati akizinduwa rasmi teknolojia hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura alisema licha ya kuzinduwa huduma hiyo katika maeneo 11 kwa sasa mafundi wa kampuni hiyo wapo kazini wakiendelea na awamu ya pili ya kufunga mitambo ili huduma hiyo itolewe pia katika maeneo mengine 14 ya jiji la Dar es Salaam.

Aliyataja maeneo mengine ambayo mitambo inaendelea kufungwa kwa sasa kuwa ni pamoja na Kigamboni, Masaki, Temeke, Kimara, Jangwani, Kariakoo, Chuo Kikuu, Kurasini, Mbezi Chini Gongo la Mboto, Tabata, Kibamba, Kongowe na Bunju.

"...Awamu ya pili ya mradi huu itakuwa imekamilisha maeneo yaliyobaki ya mkoa wa Dar es Salaam na pia kupeleka mawasiliano hayo katika mikoa mingine ikiwa ni pamoja na Arusha, Mwanza, Mbeya, Dodoma na kwingineko," alisema Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kazaura.

Alisema uzinduzi wa teknolojia ya 4G LTE unakuwa umekamilisha nia ya siku nyingi ya kampuni ya TTCL ya kuwahudumia wateja katika nyanja zote za mawasiliano (Fixed-mobile convergence) kwa kutumia teknolojia ya simu za mezani na simu za mkononi.

Akifafanua zaidi Dk. Kazaura alisema uzinduzi wa teknolojia ya 4G LTE utakuwa na mchango mkubwa katika kukuza na kuongeza kasi ya shughuli za maendeleo ya kijamii na kiuchumi, kuchangia katika kukuza teknolojia ya habari na mawasiliano na pia kuongeza uzalishaji kwenye sekta mbalimbali za maendeleo.

Aidha aliongeza kuwa TTCL inaamini mtandao wa 4G LTE utafungua fursa pekee katika kukuza sekta ya elimu nchini kwa njia ya mtandao (E education). Na pia ubora wa huduma hiyo ya intaneti utatoa fursa kwa wanafunzi, wakufunzi, wataalam, wanazuoni na walimu kutumia teknolojia katika kujifunza mambo mbalimbali ya kitaaluma na nje ya taaluma.

Kwa upande wake Ofisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya TTCL, Peter Ngota akifafanua zaidi kwa wanahabari alisema mtandao wa 4G LTE utaongeza fursa katika sekta ya afya ambapo hospitali, vituo vya afya, vyuo vya afya na wadau mbalimbali wataweza kutumia mtandao huo katika kuongeza ufanisi wa kutoa huduma bora za afya kwa wananchi tena kwa haraka zaidi.

Alisema mtandao huo pia utazinufaisha sekta nyingine za kiuchumi kama vile sekta ya biashara, viwanda, kilimo na nyinginezo. "...Wafanyabiashara na wazalishaji wa bidhaa wanahitaji mawasiliano ya uhakika katika shughuli zao. Mtandao huu wa 4G LTE utakuwa mkombozi wao na utaleta mageuzi katika kuongeza uzalishaji, kupanua wigo wa masoko ya bidhaa kwa wakulima, masoko kwa wajasiliamali, masoko kwa makampuni ndani na nje ya mipaka ya Tanzania," alisema Peter Ngota.

Hata hivyo, Ngota aliongeza kuwa uzinduzi huo unaenda sambamba na uboreshaji vifurushi rafiki vya intaneti kwa wananchi hivyo kuwaomba wananchi kuiunga mkono kampuni ya kizalendo ya TTCL katika kuboresha huduma za mawasiliano nchini.

WAZIRI KITWANGA ATANGAZA OPERESHENI YA KUKAMATA WAHAMIAJI HARAMU NCHINI



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (aliyevaa tai) akiwasalimia wananchi  wanaosubiri kupata huduma ya Hati za Kusafiria katika Ofisi za Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam. Waziri Kitwanga alifanya ziara ya kikazi katika ofisi hizo kwa lengo la kujifunza kazi mbalimbali zinazofanywa na Uhamiaji. Katika hotuba yake, licha ya maelekezo mengine aliyoyatoa kwa viongozi wakuu, pia aliitaka Idara hiyo ya Uhamiaji kuanza rasmi kwa operesheni ya kuwakamata Wahamiaji Haramu nchini. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Afisa Uhamiaji anayeshughulika na uchapaji wa Hati za Kusafiria, Amir Hassan (kushoto), akitoa maelezo ya jinsi wanavyozichapisha Hati za Kusafiria, kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) ambaye alifanya ziara ya kikazi katika ofisi za Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile (kushoto) akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, wakati Waziri huyo alipokuwa anafanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Uhamiaji. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akiwaeleza jambo Watendaji Wakuu wa Idara ya Uhamiaji wakati alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya idara hiyo, Kurasini, jijini Dar es Salaam leo. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (wasita kulia), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil (watano kushoto), Naibu Katibu Mkuu, John Mngodo (wanne kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Wakuu wa Idara ya Uhamiaji wakati Waziri huyo alipotembelea Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam. Wasita kushoto ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akimsalimia Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile wakati alipowasili Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya ziara ya kikazi. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, John Mngodo. Katika ziara hiyo, Waziri Kitwanga aliitaka Idara hiyo ya Uhamiaji kuanz rasmi kwa operesheni ya kuwakamata Wahamiaji Haramu nchini. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
 
Blogger Templates