Mkuu
 wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Said Meck Sadick akiongea na waandishi wa 
habari hawapo pichani ofisini kwake leo alipokutana nao kuelezea 
utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa kwa DAWASCO kuhusu usambazaji wa maji 
safi na salama ili kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.
Afisa Mtendaji Mkuu wa  DAWASCO Mhandisi Cyprian Luhemeja akiongea
 na waandishi wa habari hawapo pichani Dar es salaam  leo alipokutana 
nao kuelezea utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na  Serikali kuhusu 
usambazaji wa maji safi na salama ili kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa 
wa kipindupindu.Picha zote na Ally Daud-Maelezo.
Shirika
 la Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASCO) limeongeza uzalishaji
 na usambazaji wa Maji safi na Salama kwa wakazi wa jiji hilo hadi 
kufikia mita za ujazo 280,000 kwa siku ili kubabiliana na mlipuko wa 
ugonjwa wa kipindupindu  uliolikumba jiji hilo hivi karibuni. 
Hatua
 hiyo inatokana na utekelezaji wa maagizo ya Serikali yaliyotolewa na 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadiki kuitaka DAWASCO kusambaza
 maji safi na salama kwa wakazi wa jiji hilo ili kupambana na Ugonjwa wa
 Kipindupindu.
Akiongea
 na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mkuu wa mkoa huo Bw. 
Sadick amesema kuwa kufuatia maagizo aliyoyatoa kwa shirika hilo ikiwemo
 kusambaza maji safi na salama kwa wananchi pamoja na kutengeneza 
mifereji ya kupitsha maji taka ili yasiingiliane na mikondo ya maji 
safi, DAWASCO wametekeleza kwa kiasi kikubwa maagizo hayo.
“Dawasco
 imehakikisha inazalisha maji safi na salama kati ya mita za ujazo 
270,000 na 280,000 kila siku kwa muda wote tangu mlipuko ulipotokea na 
imehakikisha inasafisha na kusambaza kwa wananchi yakiwa katika viwango 
vya ubora unaokubalika kwa ajili ya matumizi kwa binadamu” amesema Bw. 
Sadick.
Ameongeza
 kuwa Dawasco imejenga vizimba vya maji  safi na salama kwenye maeneo 
mbalimbali ambayo hayajakumbwa na yaliyokumbwa na athari za mlipuko wa 
ugonjwa huo kwa jumla ya vizimba 48 ambavyo maeneo ya Kinondoni vizimba 
5, Magomeni vizimba 38 na Ilala vizimba 5.
Aidha,
 amesema kuwa DAWASCO kwa kushirikiana na Ofisi ya Bonde Wami Ruvu 
imeanza kazi ya kusajili na kuwatambua watu binafsi wenye visima virefu 
vilivyopo kisheria ambao wanauza maji kwa wananchi ili kuvitambua na 
kudhibiti ubora wa maji na bei yake ambapo zoezi hili litaendelea hadi 
Machi 2016.
“Dawasco
 imefanya jitihada za kuweka dawa ya kuua wadudu aina ya chrolination 
kwenye maboza  wakati wa  usajili kabla ya kuruhusiwa kufanya biashara 
ya kuuza maji kwa wananchi na kuongeza sehemu za kuchota maji kwa 
kuwapelekea wananchi huduma hiyo wakitumia magari yenye matanki 
yaliyokuwepo kutoka 12 mpaka kufika 49 kwa sasa” aliongeza Bw.Sadick.Katika
 hatua nyingine Bw. Sadick alitoa rai kwa wakazi wa jiji hilo kuendelea 
na tabia ya kufanya usafi mara kwa mara ili kutokomezakabisa ugonjwa wa 
kipindupindu kwani kuanzia juzi hakuna wagonjwa waliopokelewa katika 
vituo vyote.
Kwa
 upande wa Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO Mhandisi Cyprian Luhemeja 
alisema kuwa wako katika hatua za mwisho kukamilisha ujenzi wa mifereji 
ya kupitisha maji machafu ili isiingiliane na maji safi kwa wiki mbili 
zijazo.
“kufikia
 Februari mwakani tutaweza kutoa maji safi na salama ya kutosha kwa 
wananchi  wote wa Dar es salaam bila ya matatizo yoyote” alisisitiza 
Mhandisi Cyprian.   
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment