Pages

Ads 468x60px

Friday, December 4, 2015

RAIS MAGUFULI AHUTUBIA VIONGOZI NA WAWAKILISHI WA UMOJA WA SEKTA BINAFSI NCHINI - TPSF IKULU JIJINI DAR ES SALAAM


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Viongozi na Wawakilishi wa Umoja wa Sekta Binafsi nchini (Tanzania Private Sector Foundation - TPSF) katika ukumbi wa mkutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 3, 2015.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Viongozi na Wawakilishi wa Umoja wa Sekta Binafsi nchini (Tanzania Private Sector Foundation - TPSF) katika ukumbi wa mkutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 3, 2015.

NHIF YAJA NA MPANGO WA BIMA YA AFYA KAYA KWA KAYA

 Mwakilishi wa Kaimu Mkuruegenzi Mkuu wa NHIF, Eugen Mikongoti akifungua kikao kilichowashirikisha wenyeviti wa bodi na makatibu wa Vituo Vya Afya, Zahanati na Hospitali wa Manispaa ya Temeke juu ya mpango wa bima ya afya kwa kayo iliyofanyika leo jijni Dar es Salaam.
 Meneja wa Mkoa wa Temeke wa NHIF, Costantino Makala akitoa maada katika kikao hicho leo latika ukumbi wa Temeke jijini Dra es Salaam.wa katikati ni Mwakilishi wa Kaimu Mkuruegenzi Mkuu wa NHIF,Eugen Mikongoti Kushoto ni Mganga Mkuu wa Manispaa Temeke,Silvia Mamkwe.
Sehemu ya Wenyeviti wa Bodi na Makatibu wa Vituo vya Afya ,Zahanati na Hospitali katika kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii)
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umesema mpango wa huduma ya afya katika kaya utasaidia upatikanaji wa huduma bora ya matibabu kwa jamii kutokana na mchango wao wa uanachama.

Akizungumza leo Wenyekiti wa Bodi na Makatibu Afya wa Manispaa ya Temeke, Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Eugen Mikongoti amesema sharia iko tayari kwa ajili ya mpango huo kinachotakiwa ni utekelezaji kwa wananchi katika kupata huduma hiyo.

Mikongoti amesema kuwa kila mtu mmoja katika kaya kwa Manispaa ya Temeke atachangia Sh.50000 ambapo atapata matibabu kwa mwaka mmoja katika Vituovya Afya,Zahanati na Hospitali katika Manispaa hiyo.

Amesema fedha ambazo watachangia zitatumika katika kununua dawa na vifaa tiba katika Manispaa hiyo hivyo kila mwananchi atakayejiunga na mpango huo matibabu kwa kutambua mchango wake na dawa lazima ziwepo pamoja na vifaa tiba.

Mikongoti amesema kuwa fedha zinazochangwa na wanachama katika mpango ho zitatumika kwa malenfo yaliyokusudiwa na serikali itachangia asilimia 50.

Amesema NHIF itahakikisha kila mwananchi anakuwa na bima ya afya ili kuweza kupata matibabu yake wakati akifikwa na magonjwa kwani wakati mtu anaweza kuugua ugonjwa na kuweza kushindwa kupata matibabu kutokana na kutokwepo katika mapango wowote.

“NHIF itakuwa karibu na wananchi kama tunavyofanya nia yetu ni kutaka kila mwananchi anakuwa na bima ya afya ya kumfanya maisha yake yawe  mazuri ya uhakika wa matibabu”amesema Mikongoti.

WAZIRI MKUU AVAMIA TENA BANDARINI NA TRL,AKUTA MAKONTENA 2431 YEMETOKA BILA KULIPIWA KODI.

  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua bandari ya Dar es salaam  Desemba 3, 2015 ambako alikwenda kupata ukweli kuhusu makontena 2,431 yaliyopitia kwenye bandari hiyo bila kulipiwa kodi ya serikali.  
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mfumo wa kukagua makontena bandarini kwa kutumia scaner huku akipata maelzo kutoka kwa Ofisa wa forodha, January Shauri wakati alipotembelea bandari ya Dar es salaam Desemba 3, 2015  kutaka kujua ukweli wa tuhuma za makontena 2431 yaliyopita bandarini hapo bila kulipiwa kodi ya serikali.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu utoaji bili za kulipia kodi za serikali kwa watumiaji wa bandari ya Dar es salaam kutoka kwa ofisa mwandamizi wa masuala ya fedha , Bw. Sartho Mbuya wakati alipotembelea bandari hiyo  Desemba 3, 2015 kutaka kujua ukweli wa tuhuma za makontena 2431 yaliyopita bandarini hapo bila kulipiwa kodi za serikali. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimwonyesha Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es salaam, Bw. Abel Mhanga (kulia) orodha ya makontena 2,431 yaliyopitia kwenye banda ya Dar es salaam bila kulipiwa kodi wakati alipofanya ziara kwenye bandari hiyo Desemba ,3, 2015. 
 Waziri Mkuu,  Kassim Majliwa  akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli nchini TRL wakati alipotembelea stesheni ya Dar es salaam kukagua uendeshaji wa Shirika hilo Desemba 3, 2015. 
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akitembelea steheni ya reli ya Dar es salaam Desemba 3, 2015.
WAZIRI MKUU ATINGA TENA BANDARINI NA TRL
*Akuta makontena 2,431 yametoka bila kulipiwa ushuru
*Ataka majina yaletwe ofisini leo saa 11 jioni
*Atoa wiki wiki moja kwa mfumo wa malipo kubadilishwa
*Akagua mabehewa, awaweka kiporo TRL
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya ziara nyingine ya kushtukiza bandarini na kukagua mfumo wa upokeaji na utoaji mizigo na utozaji wa malipo baada ya kupewa taarifa kwamba kuna makontena 2,431 yametolewa bila kulipiwa ushuru.
Waziri Mkuu alisema kwa mujibu wa taarifa ya ukaguzi wa bandari ya kuanzia Machi hadi Septemba 2014, makontena hayo yalipita bila kulipiwa kodi kupitia bandari kavu nne (ICDs) ambazo ni JEFAG, DICD, PMM na AZAM.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ni watumishi 10 tu ambao wamesimamishwa kazi kutokana na makosa hayo. “Mmeamua kuwasimamisha kazi watu wadogo na kuwaacha wakubwa wanaendelea na kazi. Hatuwezi kuendelea kuikosesha Serikali mapato namna hii,” alisema Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu amemtaka Kaimu Meneja wa Bandari, Bw. Hebel Mhanga amletee ofisini majina ya watumishi wote waliohusika na ukwepaji kodi huo ifikapo leo saa 11 jioni. Pia amempa Meneja huyo wiki moja kuhakikisha kuwa mamlaka hiyo inabadilisha mfumo wa utozaji malipo kutoka kwenye billing system na badala yake kuweka mfumo wa malipo wa kielektroniki (e-payment).
Ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Desemba 3, 2015), wakati akikagua idara mbalimbali za mamlaka ya bandari na kuona ukaguzi wa mizigo unavyofanyika kwa kutumia scanners. Akiwa kwenye chumba cha scanner mojawapo, Waziri Mkuu alikuta manifest moja ikisema kontena limejaa diapers lakini picha ya kwenye kompyuta ya scanner ilionyesha kuwa ndani ya kontena hilo kuna vitu kama vifaa vya umeme.
Kwa mujibu wa Kaimu Meneja Bandari upande wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Ben Usaje ambaye pia ni msimamizi wa kitengo cha scanner, inapobainika taarifa kama hiyo inapaswa itumwe kwa wenye ICDs ili wafanye ukaguzi kwa kulifungua kontena ili kuhakikisha mali zilizomo ndizo zilizoandikishwa kwenye manifest.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Majaliwa amefanya ziara ya kushtukiza kwenye ofisi za Shirika la Reli (TRL) na kukagua mabehewa yaliyokuwepo kisha akazungumza na baadhi ya wafanyakazi waliokuwepo kwenye stesheni hiyo ambako alibaini madudu kwenye malipo ya mishahara na makato ya michango ya wafanyakazi.
Akizungumza na Mkurugenzi Mkuu TRL, Mhandisi Elias Mshana, Waziri Mkuu alisema amefika kwenye shirika hilo ili kujifunza utendaji wao kazi lakini anazo taarifa za wao kupewa fedha na Serikali kiasi cha sh. bilioni 13.5/- ili waendeleze miundombinu ya reli lakini hawakufanya hivyo. “Nia ya kuwapa fedha hizo ilikuwa ni kuboresha miradi ili muweze kujiendesha kibiashara lakini nyie mkaamua kujilipa wenyewe,” alisema.
“Ninazo taarifa kuwa baada ya hapo, mlikopa sh. bilioni 3 kutoka benki ya TIB ili kuendesha miradi ya shirika lakini badala ya kufanya miradi, fedha hizo mkaamua nazo kujilipa mishahara. Sasa sijui mnarudishaje huo mkopo wakati hakuna mradi wowote uliofanyika,” alihoji bila kupata majibu.
Alipoulizwa wafanyakazi wana matatizo gani hapo TRL, Katibu wa TRAWU, Bw. Boaz Nyakeke alisema wanadai malimbikizo ya makato yao kwenye mifuko ya pensheni, malimbikizo ya makato kwenye SACCOS na malimbikizo ya kuanzia Julai – Novemba 2014.
Waziri Mkuu kwa upande wake alimtaka Mhandisi Mshana asimamie uboreshaji huduma za usafiri wa treni katika Jiji la Dar es Salaam ili hata mabasi ya mwendo kasi yatakapoanza wananchi waweze kuwa na uhuru wa kuchagua aina ya usafiri wautakao.
“Tunataka kujenga yadi kubwa nje ya mji ili watu wenye magari wawe wanayaacha huko na kutumia usafiri wa treni au DART kuja mjini kama njia mojawapo ya kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es Salaam,” alisema.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
ALHAMISI, DESEMBA 3, 2015.

MKUU WA MKOA AZINDUA MTAMBO ULIONUNULIWA NA MANISPAA YA KINONDONI

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadick akipanda kwenye mtambo maalum wa kuchimbia mitalo (Scaveter), wakati wa uzinduzi uliofanyika leo jijini Dar,Mtambo huo umenunuliwa na Manispaa ya Kinondoni  kwa  thamani zaidi ya Sh. Milioni 600.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni ,Mussa Natty akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadick baada ya kuzindua scaveter iliyonunuliwa na Manispaa hiyo leo  katika viwanja vya Manispaa , jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii

BENKI YA DCB YATOA DAWA ZA MAJI KATIKA KUPAMBANA NA UGONJWA WA KIPINDUPINDU

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya DCB, Balozi Paul Rupia akimkabidhi  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki sehemu ya katoni 58 za dawa za maji (Water Guard) kuajili ya kupambana na ugonjwa wa Kipindupindu  leo katika  katika a Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, SaidMeck Sadiki akizungumza na watendaji wa Manispaa ya Kinondoni (hawapo pichani) juu ya kusimamia usafi wakati makadhibiano ya dawa za maji katoni 58 ilifanyika leo Katika viwanja vya Manispaa hiyo jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya DCB, Balozi Paul Rupia akimukabidhi  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki sehemu ya katoni 58 za dawa za maji (Water Guard) kuajili ya kupambana na ugonjwa wa Kipindupindu  leo katika  katika a Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.


Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
MKUU wa Mkoa wa Dar es  Salaam,Said Meck Sadiki amewataka watendaji wa Manispaa ya Kinondoni kusimamia kikamilifu usafi katika kupambana na ugonjwa wa kipindupindu.
Meck Sadiki ameyasema hayo  wakati akikabidhiwa dawa za maji katoni 58 zenye thamani ya Sh. Milioni Tano (5) zilizotolewa na Baenki ya DCB ,amesema umefika wakati wa kutofumbia macho watu ambao hawatimizi wajibu wao katika suala la kufanya usafi.
Amesema watendaji wote ni lazima wawajibike katika kusimamia suala la usafi kwani kinondoni ndio ilikuwa ya kwanza kuwa na mgonjwa wa kipindupindu hivyo ni lazima kuwa ya kwanza ya kutokuwa na ugonjwa huo katika Manispaa ya Kinondoni.
Aidha amewataka watu kufuata ushauri wa watendaji  katika masualanya afya kutokana na kuwepo kwa magonjwa ya milipuko nambayo yanatokana na uchafu katika mitaa mbalimbali katika manispaa hiyo.Meck Sadiki amesema Benki ya DCB imetoa dawa ya maji kutokana na kutambua watu wanaogua wanamchango katika taifa pamoja na benki .
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya DCB, Balozi Paul Rupia amesema kuwa kutoa dawa hizo ni kutokana na kutambua wanaougua ni watu ambao wanazalisha hivyo wanawajibu kutoa msaada huo kadri ya uwezo wao.
Rupia amesema benki itaendelea kushirikiana na serikali katika masuala mbalimbali yanayohusu jamii kuweza kwenda sambasamba na serikali katika kutatua changamoto kwa namna moja au nyingine.

WWF YAIJENGEA UWEZO HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI


Mganga Mkuu wa Jiji la Arusha, Dk Bakari Salum akifungua mkutano wa Wasaa wa Mazingira (Earth Hour City Challenges) kwa watumishi wa halmashauri ya Jiji la Arusha unaowajengea uwezo kuweka mipango inayoendana na mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika kwenye hotel ya Palace jijni Arusha kushoto ni Mratibu wa mradi wa nishati wa shirika la Utunzaji wa mazingira duniani(WWF- Tanzania)Dk Teresia Olemako.
Mratibu wa mradi wa nishati wa shirika la Utunzaji wa mazingira duniani(WWF- Tanzania)Dk Teresia Olemako akizungumza kwenye mkutano wa Wasaa wa Mazingira(Earth Hour City Challenges).
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Jiji la Arusha, Nteghenjwa Hoseah akiwasilisha mada ya namna Jiji hilo lilijipanga kuhakikisha linakua safi kwa kushirikiana na wadau na kulifanya kuwa kivutio cha watalii na wegeni wengine. 
Watumishi wa halmashauri ya Jiji la Arusha wakifatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa zenye lengo la kulifanya Jiji kuwa la mfano barani Afrika. 
 
Blogger Templates