Pages

Ads 468x60px

Wednesday, January 6, 2016

tukio la kuzuka moto Wizara ya Mambo ya ndani Dar leo



Huenda umekutana na stori mitandaoni au picha kuhusu tukio la ajali ya moto katika jengo la Wizara ya Mambo ya ndani, posta Dar es Salaam.
Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, SSP Advera Senzo Bulimba amesema ni kweli kulitokea cheche za moto katika jengo hilo katika ghorofa ya nne, taarifa zikatolewa kwa vikosi vya zimamoto ambao walifika na kugundua kuwa chanzo cha moto huo ilikuwa kwenye cyling board.
874f5f29-fcff-48ea-a1c5-5f14ac4a5559Hakuna mfanyakazi yoyote katika jengo hilo aliyedhurika kutokana na tukio hilo na kikosi cha zimamoto waliweka kuuzima kila kitu kikawa sawa.
34dd75ff-dda9-4f1b-a8a4-154b55fae972
Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, SSP Advera Senzo Bulimba
01209479-1925-4f80-90e5-2a790eb33c08
Baadhi ya wafanyakazi wakiwa nje ya Jengo la Wizara hiyo.
e56e04e6-f869-423d-aec9-26f83d541c37
Baadhi ya askari wakitoka nje ya jengo hilo baada ya kutokea tukio hilo.
     f4c76bbe-4024-418e-b86f-bb6f5d03f63e

KATIBU MKUU MPYA WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AJITAMBULISHA KWA WATUMISHI – AWATAKA KUFANYA KAZI KWA BIDII

 Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil ambaye sasa ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, akimkabidhi Katibu Mkuu mpya, Meja Jenerali Projest Rwegasira, moja ya Nyaraka za Ofisi za Wizara hiyo kama ishara ya kumkabidhi ofisi.
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakiwa katika mkutano wa kumuaga aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, ambaye sasa ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, na kuwakaribisha Katibu Mkuu mpya, Meja Jenerali Projest Rwegasira na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Hassan Simba Yahaya.  Hafla hii ilifanyika katika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil ambaye sasa ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, akiwaaga watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (hawapo pichani) katika mkutano uliofanyika katika Makao Makuu ya Wizara hiyo. Katikati ni Katibu Mkuu mpya wa Wzara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira na kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Balozi Hassan Simba Yahaya.

 Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil ambaye sasa ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, akimtambulisha kwa Watumishi wa Wizara hiyo, (hawapo pichani), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira katika mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Wizara, jijini Dar es Salaam.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahaya, akijitambulish kwa Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, katika mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo.  Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara, Meja Jenerali Projest Rwegasira na kushoto ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, ambaye sasa ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahaya, akijitambulish kwa Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, katika mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo.  Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara, Meja Jenerali Projest Rwegasira na kushoto ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, ambaye sasa ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais.

SERIKALI YAWAOMBA WANANCHI KUTII SHERIA ZA ARDHI BILA SHURUTI.

 Mkurugenzi Msaidizi wa usimamizi na udhibiti wa uendelezaji miji Wizara ya Ardhi na maendeleo ya Makazi, George Pangawe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Zoezi la bomoa bomoa linaliendelea katika kingo za mto Msimbazi jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi wa usimamizi na udhibiti wa uendelezaji miji Wizara ya Ardhi na maendeleo ya Makazi, George Pangawe jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii.

Na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
SERIKALI yawaomba wananchi waliojenga makazi kwenye sehemu hatarishi, kingo za mito na maeneo ya wazi kuhama kwa hiyari yao ili kupisha Oparesheni ya bomoa bomoa kuendelea bila kikwazo.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa usimamizi na udhibiti wa uendelezaji miji Wizara ya Ardhi na maendeleo ya Makazi, George Pangawe wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Pangawe amesema kuwa Serikali itahakikisha haki inatendeka kwa wananchi wote pia itahakikisha haki na usawa wa pande zote wakati wa utekelezaji wa zoezi la bomoabomoa linaloendelea tangu lilipoaza tena Januari 5 mwaka huu.

Zoezi la bomoabomoa linaendelea jijini Dar es Salaam katika kingo za mto Msimbazi ili kuepusha wananchi kupatwa na madhara mbalimbali ambayo huwa yanakitokeza wakati wa mvua kubwa na masika.

Pangawe pia amesema kuwa bonde la mto msimbazi liliainishwa kama ni sehemu hatarishi kwa makazi ya binadamu tangu 1979 na wananchi wa maeneo ya mto huo wakaanza kuvamia kutokana uhaba wa maeneo ya makazi na kuanza kujenga katika kingo za mto huo.

PROFESA MUHONGO AKUTANA NA KAMPUNI YA AFRICOMMERCE INTERNATIONAL LTD

WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Africommerce International Limited, Elisante Muro na kuzungumzia fursa mbalimbali za uwekezaji nchini hususan katika sekta ya Nishati.
Muro alimtembelea Waziri Muhongo na kueleza nia ya Kampuni yake kuwekeza kwenye mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirishia mafuta kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza na vilevile uwekezaji kwenye mradi wa ujenzi wa nguzo za umeme za zege. 
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Africommerce International Limited, Elisante Muro wakati wa kikao cha kujadili fursa za uwekezaji.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akizungumza jambo wakati wa kikao chake na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Africommerce International Limited, Elisante Muro (hayupo pichani) ambaye alimtembelea Waziri huyo kuzungumzia fursa za uwekezaji kwenye sekta ya nishati nchini. Wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu- Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo akifuatiwa na Naibu Katibu Mkuu- Madini, Profesa James Mdoe.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akizungumza jambo wakati wa kikao na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Africommerce International Limited, Elisante Muro (hayupo pichani) wakati wa kikao cha kujadili fursa za uwekezaji. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu- Madini, Profesa James Mdoe na wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu- Nishati, Dkt. Mhandisi, Juliana Pallangyo

WAGENI WOTE WANAOISHI NCHINI NA KUFANYA KAZI KINYUME CHA SHERIA KUKAMATWA - MASAUNI

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Hamad Yussuf Masauni akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu hatua zinazochukuliwa na Wizara kudhibiti wageni wanaoishi nchini na kufanya kazi kinyume na sheria. Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam.
Afisa Uhamiaji mkoa wa Dar es Salaam, Naibu Kamishna, Johannes Msumule akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari ambapo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Hamad Yussuf Masauni alizungumzia hatua zinazochukuliwa na Wizara kudhibiti wageni wanaoishi na kufanya kazi nchini kinyume na sheria. Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam.

Sehemu ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Hamad Yussuf Masauni, wakati wa mkutano wa kuzungumzia hatua zinazochukuliwa na Wizara kudhibiti wageni wanaoishi nchini na kufanya kazi kinyume na sheria. Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mazingira na Muungano akutana na Balozi wa Finland na Norway

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, (Mazingira na Muungano) Mh. January Makamba (Kushoto) akifurahia jambo na Balozi wa Norway nchini Bi. Hanne-Marie Kaarstad. Balozi huyo na ujumbe wake walimtembelea Mh. Waziri leo Ofisini kwake Mtaa wa Luthuli kwa lengo la kujadili juu ya kudumisha ushirikiano baina ya Tanzania na Finland katika nyanja za Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira. 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, (Mazingira na Muungano) Mh. January Makamba (Kushoto) akiongea na Balozi wa Finland nchini Bw. Pekke Hukka. Balozi huyo na ujumbe wake walimtembelea Mh. Waziri leo Ofisini kwake Mtaa wa Luthuli kwa lengo la kujadili juu ya kudumisha ushirikiano baina ya Tanzania na Finland katika nyanja za Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, (Mazingira na Muungano) Mh. January Makamba (Kushoto) akiongea na Balozi wa Norway nchini Bi. Hanne-Marie Kaarstad. Balozi huyo na ujumbe wake walimtembelea Mh. Waziri leo Ofisini kwake Mtaa wa Luthuli kwa lengo la kujadili juu ya kudumisha ushirikiano baina ya Tanzania na Finland katika nyanja za Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira.

FASTJET KUZINDUA RASMI SAFARI KATI YA TANZANIA NA KENYA


Shirika la ndege la bei nafuu lapanua wigo wa safari zake barani Afrika na kufungua safari ya kimataifa ya moja kwa moja kutoka Nairobi kwenda Dar es Salaam na Kilimanjaro.


 fastjet imetangaza safari yake mpya ya kimataifa ya kutoka Dar es Salaam kwenda Nairobi, Kenya kuwa itaanza rasmi mnamo tarehe 11 Januari 2016.

Fastjet imepewa ruhusa na serikali ya Kenya kufanya safari zake nchini humo kufuatia makubaliano ya pamoja na mashirika yanayotoa huduma za usafiri wa anga kati ya nchi hizi mbili za Tanzania na Kenya, kama ilivyopitishwa na serikali ya Tanzania.

Vilevile Fastjet imetangaza kuwa inatarajia kuzindua safari zake za anga kati ya Zanzibar na Nairobi na pia kati ya Dar es Salaam na Mombasa ambapo uzinduzi huo utafanyika mapema mwaka huu 2016.

Tiketi za kurudi kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi kwenda uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam na uwanja wa ndege wa Kilimanjaro zitakuwa za kila siku mara tu baada ya uzinduzi huo na wasafiri watasafiri na ndege ya kisasa aina ya  Airbus A319 ambayo hubeba abiria 156.

Kwa mujibu wa Fastjet, safari nyingine za ndege zinatarajia kuzinduliwa kufuatia kuongezaka kwa maombi ya wateja wake na hii ni kwa sababu ya unafuu wa bei zake sambamba na huduma bora.

Tiketi za safari hii mpya zimeanza kuuzwa, na nauli za Nairobi/Dar es Salaam zitatozwa kwa $50 kwa safari moja, na Dar es Salaam/ Nairobi zitatozwa kwa $80 kwa safari moja.

Nauli hizi ni pamoja na kodi ya serikali  ambayo itachajiwa. Kwa mantiki hiyo, Fastjet inawaomba abiria na wateja wake kwa ujumla kufanya booking mapema iwezekanavyo ili kufaidika na bei nafuu ambayo hutozwa kuliko ndege zote ambazo husafirisha abiria kati ya nchi hizi mbili.

“Usafiri wa anga katika uwanda wa Afrika mashariki umekuwa na ushindani mkubwa  kutokana na safari nyingi bado hutoza nauli kubwa jambo linalosababisha abiria wengi kushindwa kumudu safari hizo” alisema John Corse, Meneja Mkuu wa fastjet kanda ya Tanzania.

“Wasafiri wengi wanaosafiri kati ya miji hii miwili mikubwa yenye idadi ya watu wasiopungua milioni 8 hapa Afrika Mashariki wamekuwa wakipatwa na vikazo mbalimbali vinavyowarudisha nyuma kutokana na bei ya safari za ndege kuwa kubwa ambayo tunaamini imewakatisha tamaa wasafiri wengi”, alisema Corse.

Matarajio ya Fastjet kufanya safari zake nchini Kenya zitaleta matumaini mara tu baada ya shirika hilo kuzindua safari hizo ambazo bei zake zimepokelewa na wateja wengi wanaosafiri na ndege zingine hasa pale ambapo nauli za Fastjet zimepungua kwa asilimia 40 hivi.

“Jambo kuu la msingi ni kwamba ushindani ni muhimu kwa wateja, kwa kuwa inampa mteja nafasi ya kuchangua unafuu wa nauli atakayoimudu, na hali hii hufanya watalii na wajasiriamali na wageni wanaotembelea nchi hizi mbili kuwa huru kuamua kwa raha kati ya Tanzania na Kenya” Corse alisema.

“Hali hii baadae italeta maendeleo ya pamoja kati ya nchi hizi mbili ambapo ukuwaji wa biashara zao za ndani na nje, vilevile pia utalii utaimarika kwa kiasi kikubwa na itakayo pelekea kukua kwa uchumi wa nchi hizi mbili”, aliongeza Corse.

Pia alisisitiza kuwa haileti maana halisi kwa mgeni ama mtalii kusafiri kwa zaidi ya masaa 12 kutoka Dar es Salaam kwenda Nairobi Kenya na kumfanya achoke kama ilivyo katika safari zingine. Na kwa kuwa sasa Fastjet imezindua safari mpya kama hii ya nchi na nchi, basi inategemea wasafiri wengi watafaidika na huduma za Fastjet.

Kwa kuunga mkono mategemeo haya hapo baadae, hii ni baada ya Fastjet kufanya utafiti wa kina na kubaini kuwa  abiria wake waliweza kumudu bei zao na kuzikubali moja kwa moja.

Safari za kila siku za fastjet kutoka Dar es Salaam zitaanza saa 3:50 asubuhi na kutua Nairobi-Kenya saa 5:10.

Safari za kurudi kutoka Nairobi kwenda Dar es Salaam zitaanza saa 8:10 na kutua saa 10 :05 kulingana na saa za Afrika mashariki.

Safari za kwenda Kilimanjaro kutoka Nairobi zitaanza saa 5:10 na kutua saa 6:40 na safari ya kurudi kutoka Kilimanjaro kwenda Nairobi zitaanza saa 7:10 na kutua saa 8: 40 kulingana na saa za Afrika mashariki.

Fastjet inatoza nauli iliyo nafuu kadri iwezekanavyo na kwa kutozingatia gharama za ushuru wa mizigo, vinywaji lakini vyote hivi vinapatikana kama msafiri atagharamia kwa hiari yake mwenyewe.

Ukatishaji tiketi mapema unaweza kufanyika kwa njia ya mtandao kwa kupitia tovuti ya festjet ambayo ni www.fastjet.com kupitia kwa mawakala wa shirika hili, ama mteja anaweza kupiga simu Namba 0784 108900. Malipo kwa ajili ya tiketi yanaweza kufanyika taslimu ama kwa kutumia benki ama kwa njia ya mitandao ya simu za mikononi.

Fastjet imepanua wigo wa ofisi zake na kwa sasa wanaendesha shughuli zao kimataifa kati ya Dar es Salaam ambako ndiyo ofisi kuu na kushirikiana na Johannesburg Afrika Kusini, Lusaka-Zambia, Entebbe - Uganda, Harare-Zimbabwe na Lilongwe nchini Malawi. fastjet pia hufanya safari zake kwenda Entebbe.

fastjet pia hufanya safari zake za ndani ya nchi kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza, Mbeya, Kilimanjaro na pia kati ya Kilimanjaro na Mwanza. Safari ya kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar itaanza tarehe 11th Januari 2016.

DK. KIGWANGALLA AFANYA ZIARA MUHIMBILI NA KUKAGUA MASHINE ZA CT-SCAN NA MRI, AFURAHISHWA NA UTENDAJI KAZI

IMG_0833
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akiwasili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipofanya ziara ya kushtukiza hospitalini hapo, Januari 4, 2016.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Na Rabi Hume, Modewjiblog
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla amefanya ziara, Januari 4, 2016 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kutembelea idara mbalimbali za hospitali hiyo kuona jinsi ya ufanyaji kazi.
Baadhi ya idara ambazo, Dk. Kingwangalla alitembelea ni pamoja na Kitengo cha dharura, Chumba cha wagonjwa Mahututi (ICU), wodi ya Mwaisela, duka la dawa la MSD na kukagua ufanyaji wa kazi wa mashine ya CT-Scan na MRI.
Akizungumzia ziara hiyo mara baada ya kutembelea Hospitalini hapo, Dk. Kigwangalla ameeleza kuwa ili kuweza kuona hali ya utendaji wa kazi iliyopo katika hospitali hiyo ya taifa tangu ambapo Rais, Dkt. John Pombe Magufuli alipofanya ziara ya kushtukiza na kutokuridhishwa na utendaji kazi wa hospitali hiyo hali iliyopelekea kuivunja bodi iliyokuwa ikisimamia hospitali.
Dk. Kingwangalla alisema amefurahishwa na utoaji wa huduma katika upimaji kwa kutumia mashine ya CT-Scan na MRI ambazo awali wakati wanaingia madarakani hazikuwa katika hali nzuri ya ufanyaji wa kazi na kuwataka watumishi wa hospitali hiyo kufanya kazi kwa bidii na kuifanya hospitali hiyo kuonekana yenye hadhi ya kuwa hospitali ya taifa.
Alisema limekuwa jambo ambalo linasikitisha kuona huduma zinazopatikana katika hospitali ya taifa zinashindwa na huduma zinazotolewa katika hospitali za watu binafsi na akilinganisha huduma za kulipia vitanda zinazotolewa Muhimbili kuwa hazina viwango vya juu ambavyo vinaweza kuwashawishi wananchi wenye uwezo kuacha kwenda hospitali binafsi na kwenda hospitalini hapo.
“Ni jambo la kushangaza hospitali za watu binafsi zinakuwa na watu wengi kuliko hapa na wakati sisi tuna madaktari bingwa zaidi ya 500 hapa Muhimbili lakini hizo hospitali zao hazina hata daktari mmoja bingwa lakini na huduma zinazopatikana katika madaraja ya juu zinatakiwa kuboreshwa,
“Kama tunaweza kuwa na huduma nzuri katika first class (daraja la kwanza) tunaweza kuwavuta wananchi wengi waje hapa na waache kwenda hospitali binafsi, wanatakiwa kutengwa madaraja ya juu ambayo huduma zake zinakuwa zimeboreshwa sio mtu anakuwa daraja la kwanza alafu bado anachangia choo na wengine au anaelala nae hapewi kitanda,” alisema Mhe. Kingwangalla.
Aidha Mhe. Dkt.Kingwangalla aliwatupia lawama Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa jinsi wanavyopanga madaraja ya hospitali na kuilinganisha Muhimbili na hospitali zingine za watu binafsi kuwa jambo hilo siyo sahihi kwa kuiweka hospitali ya taifa sawa na hospitali za watu binafsi.
“NHIF wanaweka sehemu moja hospitali ya taifa na hospitali binafsi hili haliwezekani walinganishe huduma zilizopo hospitali ya taifa na zile zingine, nina mpango wa kuwatembelea hivi karibuni nitazungumza nao,” alisema Kingwangalla.
Aidha Mhe. Naibu Waziri aliupongeza uongozi wa hospitali hiyo kwa kuongeza vitanda katika wodi ya wagonjwa mahututi (ICU) ambayo awali ilikuwa na vitanda sita hali ambayo ilikuwa ikiwashangaza wananchi wengi kutokana na kuwepo kwa vitanda zaidi ya 1350 katika hospitali hiyo na hivyo kuongezeka kwa vitanda katika wodi hiyo kutasaidia upatikanaji wa wa huduma bora kwa wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kupata huduma.
Awali akitoa taarifa mbele ya Mhe. Dkt. Kingwangalla, Mkuu wa Idara ya Mionzi katika hospitali hiyo, Dkt. Flora Rwakatare alisema tangu kuanza kwa kutumika kwa mashine ya MRI mwishoni kwa mwezi Novemba mwaka jana jumla ya wagonjwa 560 wamefanyiwa vipimo katika mashine hiyo na ndani ya siku tatu amabazo wamefunga mashine mpya ya CT-Scan wameshawapima wagonjwa 26.
Alisema kufungwa kwa mashine ya CT-Scan kunaonekana kuwepo kwa matumaini mapya kwa watanzania kutokana na kasi ya ufanyaji kazi kwa mashine hiyo ambayo imetengenezwa na kampuni ya Siemens ambayo inauwezo wa kupima kifua na tumbo kwa sekunde 6.
“Mashine ya CT-Scan ambayo imefungwa ina ubora mkubwa na ni ya pili kwa ukubwa Afrika Mashariki na kwasasa tunategemea kufanya kazi kwa ubora zaidi kutokana na ukubwa iliyonayo na inaweza kufanya kazi kwa kasi tofauti na ile iliyokuwa ikitumika awali,” alisema Dkt. Flora.
Nae Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru alisema awali hawakuwa wakifanya visingizo ili wasifanye kazi lakini ni hali halisi iliyokuwepo kuwa mashine iliyokuwepo awali ilikuwa na matatizo lakini kufanikisha kufungwa kwa mashine mpya ambayo imeigharimu serikali Dola za Kimarekani Milioni 1.7 ambapo ni zaidi ya Milioni 400 za kitanzania kutawapa wao motisha ya kufanya kazi kwa kutumia kifaa cha kisasa na chenye kufanya kazi kwa haraka.
IMG_0836
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akitoka katika ofisi ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo.
IMG_0857
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru (kushoto). Katikati ni Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Juma Mfinanga.
IMG_0861
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akiongozana na Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru (kushoto) pamoja na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Juma Mfinanga (kulia) kuelekea kwenye chumba cha vipimo vya CT Scan pamoja na MRI alipofanya ziara ya kushtukiza hospitalini hapo, Januari 4, 2016.
IMG_0873
Baadhi ya watumishi katika kitengo cha vipimo cha MRI wakiandaa kitanda kwa ajili ya kumpokea mgonjwa wa kipimo cha MRI (hayupo pichani) kama walivyokutwa na mpiga picha wa wetu.
IMG_0876
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akipata taarifa ya idadi ya wagonjwa waliofanyiwa vipimo tangu mashine hiyo ipone kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Mionzi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Flora Rwakatare (kulia).
IMG_0886
Mkuu wa Idara ya Mionzi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Flora Rwakatare akizungumza jambo na waandishi wa habari katika chumba cha vipimo vya MRI wakati wa ziara ya kushtukiza iliyofanywa na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla, Januari 4, 2016.
IMG_0891
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akiwa ndani ya chumba cha vipimo vya MRI katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ya jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kushtukiza, Januari 4, 2016.
IMG_0900
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akipata maelezo ya mashine mpya ya CT Scan iliyonunuliwa hivi karibu na Serikali kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru.
IMG_0903
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru (kushoto) akitoa maelezo ya uwezo mashine mpya ya CT-Scan iliyonunuliwa na Serikali hivi karibuni ambayo hadi kufikia Januari 4, 2016 ikiwa na muda wa siku tatu tangu kuanza kutumika hospitalini hapo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla.
IMG_0910
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akimpongeza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru baada ya kuona mabadiliko makubwa katika hospitali hiyo tangu alipokaimu kiti hicho wakati wa zaiara ya kushtukiza katika chumba kilichofungwa mashine mpya ya CT-Scan iliyonunuliwa na Serikali hivi karibu na inauwezo mkubwa wa kufanya kipimo kwa sekunde 6 na kutoa majibu. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Mionzi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Flora Rwakatare.
IMG_0924
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akiwa kwenye dirisha la malipo ya matibabu hospitalini hapo wakati wa ziara ya kushtukiza aliyoifanya, Januari 4, 2016.
IMG_0930
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Juma Mfinanga akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla aliyetembelea kitengo chake, Januari 4, 2016. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru.
IMG_0932
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Dk. Hamisi Kingwangalla akiendelea kupewa maelezo ya namna wananchi wanavyohudumiwa katika kitengo hicho na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Juma Mfinanga.
IMG_0935
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Juma Mfinangaakitoa maelezo ya ubao maalum unaowaongoza madaktari na wagonjwa wanaohudumiwa katika kitengo hicho kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Dk. Hamisi Kingwangalla.
IMG_0950
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Dk. Hamisi Kingwangalla akikagua wodi mpya ya wagonjwa mahututi (ICU) ambayo ipo kwenye hatua za mwisho kukamilika. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru akimtembeza Mh. Naibu Waziri kwenye wodi hiyo.
IMG_0951

WATUMISHI WA KADA ZA AFYA NCHINI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA KUFUATA MAADILI NA VIAPO VYA TAALUMA ZAO

IMG-20160105-WA0026
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akimjulia hali mama aliyejifungua kwenye wodi ya wazazi hospitali teule ya rufaa ya mkoa wa Geita.(Picha Zote na Catherine Sungura WAMJW-GEITA).
IMG-20160105-WA0030
Wauguzi wa wodi ya akinamama katika hospitali teule ya mkoa wa Geita.
IMG-20160105-WA0029
Tabibu wa kituo cha afya Nyankumbu, Abdallah Kiroboto akimsikiliza Waziri Ummy mara alipoingia kwenye chumba cha kutolea huduma, pembeni ni mama aliyefika kituoni hapo na watoto wake kupata matibabu.
IMG-20160105-WA0031
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwlimu akisalimiana na wagonjwa kwenye kituo cha afya Nyankumbu mkoani Geita alipotembelea kituo hicho.
IMG-20160105-WA0028
Wagonjwa waliofika hospitalini hapo wakisubiri huduma kwenye hospitali hiyo.
IMG-20160105-WA0027
Mganga mfawidhi wa hospitali teule ya mkoa wa Geita, Dkt. Adam Sijaona (kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu mara baada ya kutembelea hospitali hiyo.

WATANZANIA MSIKUBALI KUTOZWA RUSHWA KWA AJILI YA DAMU, TOA TAARIFA KWA NESI, DAKTARI ATAKAYETOZA DAMU!- DK. KIGANGWALLA

IMG_0681
Afisa Uendeshaji wa Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Bw. Abdu Juma akitoa maelezo ya namna wanavyoendesha shughuli zao kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla aliyefanya ziara ya kushtukiza katika ofisi hizo, Januari 4, 2016.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameagiza watanzania wote wasikubali kutozwa rushwa kwa ajili ya damu salama na baadala yake kwa mtu atakayefanya hivyo watamchukulia hatua kali.
Kauli hiyo imetolewa mapema Januari 4 (jana) na Naibu huyo wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Kingwangalla alipofanya ziara katika Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dares Salaam.
Dk. Kigwangalla amefafanua kuwa, kwa watu wote ikiwemo Nesi, Daktari ama mtaalamu wa afya, atakayemtoza mtu damu, atachukuliwa hatua kali ikiwemo kufukuzwa kazi.
“Kwa watanzania wote, msikubali kutoa rushwa kwa ajili ya damu. Na kama itatokea Nesi ama Daktari ama nani, anakuambia ulipie ili upate damu!. Kwa sababu kuna uhaba wa damu kwa sasa.. Ripoti kwa Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa ama Daktari Mkuu husika ama fika Wizara ya afya moja kwa moja na kuna namba tutaitoa kwa watanzania wote mtupatie ripoti.
Mtu atakayekutoza damu, wewe tuambie, huyo tutamfukuza kazi moja kwa moja, hatuwezi kuendekeza watu wa namna hii... Serikali inaingia gharama kubwa kukusanya damu kwa watu, Kuna watu wanajitolea damu zao bure. Leo wewe nesi ama mganga ukauze damu, hilo jambo hatutakubali hata kidogo kwa hiyo natoa rai kwa watanzaia hiyo damu ni bure na haiuzwi na usikubali kuuziwa damu hata kidogo.” Ameeleza hilo Dk. Kigwangalla.
Awali katika ziara hiyo, Dk. Kigwangalla ameipongeza Ofisi ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama kwa kazi wanayofanya na ubunifu waliofikia wa kuhusisha Halmshauri katika ukusanyaji wa damu huku wao wakisimamia kudhibiti viwango vya damu ya matumizi kwa watanzania huku akitumia wasaha huo kutoa maelekezo ya kuboresha mfumo wa motisha kwa wanaochangia damu salama ambapo kwa wachangiaji damu kuingizwa kwenye mfumo wa kieletroniki wa kuwatambua watu wanaochangia damu, kutoa taarifa jinsi damu zao zilivyookoa miasha ya wagonjwa na kuwapa motisha ili waweze kuwa wachangiaji endelevu.
“Motisha sio soda na maji kwa wanaochangia damu. Motisha ni hata kupewa taarifa kwamba damu yake imesaidia kuokoa maisha ya mwanadamu mwenzake aliyekuwa anaumwa ugonjwa fulani, hii ni motisha kubwa sana kuliko hata pesa, ama soda ama maji yanayotolewa anapochangia damu..
Lakini kama imeshajitokeza mtu kuwa na tabia ya kuchangia damu, huyu sio wa kumpoteza, maana yake kuna uwezekano mkubwa wa akarudi tena kuchangia damu, mtu huyu ni lazima kuwe na mfumo wa kielekrioniki wa komputa wa kumtakia salamu, taarifa na anakuwa kwenye database yenu.
“Mnatakiwa muwe na mfumo wa kumpa taarifa pindi damu yake imetumika, ikiwemo kumueleza kuwa damu yako imemsaidia Mama mjamzito aliyejifungua na kutokwa damu nyingi, na mtu huyo akipata taarifa hiyo ni motisha tosha hivyo ni lazima muwe na huo mfumo kutoa motisha zaidi.
IMG_0689
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla na msafara wake wakishuka ngazi kuelekea kukagua idara mbalimbali katika ofisi hizo, Januari 4, 2016
Awali akielezwa na Meneja wa kanda ya Mashariki katika Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Eveline Mgassa kwamba changamoto zilizopo katika upatikanaji wa damu nchini ni halimshauri kutenga bajeti za kutosha kwa ajili ya huduma hiyo, Kwa hatua hiyo, Dk. Kigwangalla ameziagiza Halmshauri zote nchini kuhakikisha zinatenga bajeti za kutosha ilikusapoti mpango wa damu salama.
Katika hilo Dk. Kigwangalla ameapa kuwashughulikia wale wote watakaozembea na kuwachukulia hatua kali Ma DMO, Wakurugenzi na kushtakiwa kwa mamlaka zilizopo na kufukuzwa kazi.
“Naziagiza Halmashauri zote kuhakikisha zinatenga bajeti za kusapoti mpango wa ukusanyaji damu salama. Na Halmashauri zitakazoshindwa, DMO na Mkurugenzi wake tutahakikisha tunawashtaki kwa mamlaka zilizowateua ili uteuzi wao ukome mara moja. Maana hatuwezi kuacha akinamama wajawazito wapoteze damu wakati wa kujifungua, watu wanaopata ajali wapoteze maisha kwa sababu ya watu hawataki kutimiza wajibu wao.
Hilo haliwezi kukubalika, Mfumo wa hali ya damu kwa Tanzania kwa sasa unatisha. Kwa sasa nchi inakiwango cha chini mno, tokea wafadhili wajiondoe katika hili. Ni lazima tuwe makini sana maana leo mzima kesho umepata ajali, umepasuka mfupa wa kwenye paja damu nyingi zimemwagika unahitaji damu!!
Kwa upande wa watu wote wanaopata damu salama nchini, huduma hiyo wanazipata bure kwani damu hizo ni za Serikali, Hata hivyo mifuko na vitu vinavyotumika kuhifadhia damu hiyo vina gharama kubwa.
“Damu inatolewa bure na serikali. Mtambue kuwa, vifaa vya kutunzia damu hii ni gharama kubwa. Hivyo mifuko mashirika ya Bima, na mashirika mengine kuanzia leo kutazama namna ya kulipa gharama za vifaa vya utunziaji damu hizo. Damu ni bure, lakini mfuko ule wa kutunzia ile damu ni gharama kubwa sana na hata vifaa vya kupimia damu ile nayo ni gharama kubwa hivyo walipie kwa kila damu watakayochukua.” Alieleza Dk. Kigwangalla.
IMG_0703
Meneja wa kanda ya Mashariki Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Eveline Mgassa (mwenye miwani) akielezea utaratibu wa ukusanyaji wa damu unavyofanyika kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla aliyefanya ziara ya kushtukiza katika ofisi hizo, Januari 4, 2016 jijini Dar.
IMG_0690
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla (aliyeipa mgongo kamera) akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Uendeshaji wa Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Bw. Abdu Juma ya namna wanavyopokea watu wanaofikia kuchangia damu kwa hiari na kuhifadhiwa kwenye benki hiyo yaTaifa ya Damu Salama, alipofanya ziara ya kushtukiza, Januari 4, 2016 katika ofisi hizo.
IMG_0725
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla akitoa mkono wa pongezi kwa wananchi walioonyesha uzalendo kwa kufika katika ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Januari 4, 2016 na kuchangia damu kwa hiari yao ambapo mmoja kati yao alisema hii ni mara yake ya nne na ni utararibu aliojiwekea.
IMG_0729
IMG_0743
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla akisalimiana na kumpongeza mmoja wa wananchi (jina lake halikuweza kupatikana) aliyefika kuchangia damu kwa hiari, Januari 4, 2016 katika makao makuu ya ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama.
IMG_0764
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla akiwa ndani ya maabara ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye ofisi hizo, Januari 4, 2015 jijini Dar es Salaam.
IMG_0770
Afisa Uendeshaji wa Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Bw. Abdu Juma akimwonyesha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla moja ya damu ambayo ni maalum kwa wamama wajawazito wakati wa kujifungua zilizohifadhiwa kwenye jokofu katika mabara hiyo.
IMG_0760
Mmoja wa watumishi katika maabara ya ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama (ambaye jina lake halipatikana) akiendelea kutekeleza majukumu yake kama alivyokutwa na mpiga picha wetu.
IMG_0774
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla akisaini vitabu vya wageni nje ya ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Januari 4, 2016 wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika ofisi hizo.
IMG_0826
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufanya ziara ya kushtukiza na kuzungikia vitengo mbalimbali katika ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama jijini Dar es Salaam.
 
Blogger Templates