Naibu Waziri wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi
Kingwangalla akiwasili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipofanya
ziara ya kushtukiza hospitalini hapo, Januari 4, 2016.(Picha zote na
Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Na Rabi Hume, Modewjiblog
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla
amefanya ziara, Januari 4, 2016 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
na kutembelea idara mbalimbali za hospitali hiyo kuona jinsi ya
ufanyaji kazi.
Baadhi ya idara ambazo, Dk. Kingwangalla
alitembelea ni pamoja na Kitengo cha dharura, Chumba cha wagonjwa
Mahututi (ICU), wodi ya Mwaisela, duka la dawa la MSD na kukagua
ufanyaji wa kazi wa mashine ya CT-Scan na MRI.
Akizungumzia ziara hiyo mara baada ya
kutembelea Hospitalini hapo, Dk. Kigwangalla ameeleza kuwa ili kuweza
kuona hali ya utendaji wa kazi iliyopo katika hospitali hiyo ya taifa
tangu ambapo Rais, Dkt. John Pombe Magufuli alipofanya ziara ya
kushtukiza na kutokuridhishwa na utendaji kazi wa hospitali hiyo hali
iliyopelekea kuivunja bodi iliyokuwa ikisimamia hospitali.
Dk. Kingwangalla alisema amefurahishwa na
utoaji wa huduma katika upimaji kwa kutumia mashine ya CT-Scan na MRI
ambazo awali wakati wanaingia madarakani hazikuwa katika hali nzuri ya
ufanyaji wa kazi na kuwataka watumishi wa hospitali hiyo kufanya kazi
kwa bidii na kuifanya hospitali hiyo kuonekana yenye hadhi ya kuwa
hospitali ya taifa.
Alisema limekuwa jambo ambalo
linasikitisha kuona huduma zinazopatikana katika hospitali ya taifa
zinashindwa na huduma zinazotolewa katika hospitali za watu binafsi na
akilinganisha huduma za kulipia vitanda zinazotolewa Muhimbili kuwa
hazina viwango vya juu ambavyo vinaweza kuwashawishi wananchi wenye
uwezo kuacha kwenda hospitali binafsi na kwenda hospitalini hapo.
“Ni jambo la kushangaza hospitali za watu
binafsi zinakuwa na watu wengi kuliko hapa na wakati sisi tuna
madaktari bingwa zaidi ya 500 hapa Muhimbili lakini hizo hospitali zao
hazina hata daktari mmoja bingwa lakini na huduma zinazopatikana katika
madaraja ya juu zinatakiwa kuboreshwa,
“Kama tunaweza kuwa na huduma nzuri
katika first class (daraja la kwanza) tunaweza kuwavuta wananchi wengi
waje hapa na waache kwenda hospitali binafsi, wanatakiwa kutengwa
madaraja ya juu ambayo huduma zake zinakuwa zimeboreshwa sio mtu anakuwa
daraja la kwanza alafu bado anachangia choo na wengine au anaelala nae
hapewi kitanda,” alisema Mhe. Kingwangalla.
Aidha Mhe. Dkt.Kingwangalla aliwatupia
lawama Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa jinsi wanavyopanga
madaraja ya hospitali na kuilinganisha Muhimbili na hospitali zingine za
watu binafsi kuwa jambo hilo siyo sahihi kwa kuiweka hospitali ya taifa
sawa na hospitali za watu binafsi.
“NHIF wanaweka sehemu moja hospitali ya
taifa na hospitali binafsi hili haliwezekani walinganishe huduma
zilizopo hospitali ya taifa na zile zingine, nina mpango wa kuwatembelea
hivi karibuni nitazungumza nao,” alisema Kingwangalla.
Aidha Mhe. Naibu Waziri aliupongeza
uongozi wa hospitali hiyo kwa kuongeza vitanda katika wodi ya wagonjwa
mahututi (ICU) ambayo awali ilikuwa na vitanda sita hali ambayo ilikuwa
ikiwashangaza wananchi wengi kutokana na kuwepo kwa vitanda zaidi ya
1350 katika hospitali hiyo na hivyo kuongezeka kwa vitanda katika wodi
hiyo kutasaidia upatikanaji wa wa huduma bora kwa wagonjwa wanaofika
hospitalini hapo kupata huduma.
Awali akitoa taarifa mbele ya Mhe. Dkt.
Kingwangalla, Mkuu wa Idara ya Mionzi katika hospitali hiyo, Dkt. Flora
Rwakatare alisema tangu kuanza kwa kutumika kwa mashine ya MRI mwishoni
kwa mwezi Novemba mwaka jana jumla ya wagonjwa 560 wamefanyiwa vipimo
katika mashine hiyo na ndani ya siku tatu amabazo wamefunga mashine mpya
ya CT-Scan wameshawapima wagonjwa 26.
Alisema kufungwa kwa mashine ya CT-Scan
kunaonekana kuwepo kwa matumaini mapya kwa watanzania kutokana na kasi
ya ufanyaji kazi kwa mashine hiyo ambayo imetengenezwa na kampuni ya
Siemens ambayo inauwezo wa kupima kifua na tumbo kwa sekunde 6.
“Mashine ya CT-Scan ambayo imefungwa ina
ubora mkubwa na ni ya pili kwa ukubwa Afrika Mashariki na kwasasa
tunategemea kufanya kazi kwa ubora zaidi kutokana na ukubwa iliyonayo na
inaweza kufanya kazi kwa kasi tofauti na ile iliyokuwa ikitumika
awali,” alisema Dkt. Flora.
Nae Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru alisema awali hawakuwa
wakifanya visingizo ili wasifanye kazi lakini ni hali halisi iliyokuwepo
kuwa mashine iliyokuwepo awali ilikuwa na matatizo lakini kufanikisha
kufungwa kwa mashine mpya ambayo imeigharimu serikali Dola za Kimarekani
Milioni 1.7 ambapo ni zaidi ya Milioni 400 za kitanzania kutawapa wao
motisha ya kufanya kazi kwa kutumia kifaa cha kisasa na chenye kufanya
kazi kwa haraka.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi
Kingwangalla akitoka katika ofisi ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
Hospitali hiyo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi
Kingwangalla akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru (kushoto). Katikati ni Mkuu wa Idara ya
Magonjwa ya Dharura na Ajali ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya
dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Juma Mfinanga.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi
Kingwangalla akiongozana na Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru (kushoto) pamoja na Mkuu wa Idara ya
Magonjwa ya Dharura na Ajali ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya
dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Juma Mfinanga
(kulia) kuelekea kwenye chumba cha vipimo vya CT Scan pamoja na MRI
alipofanya ziara ya kushtukiza hospitalini hapo, Januari 4, 2016.
Baadhi ya watumishi katika kitengo cha
vipimo cha MRI wakiandaa kitanda kwa ajili ya kumpokea mgonjwa wa kipimo
cha MRI (hayupo pichani) kama walivyokutwa na mpiga picha wa wetu.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi
Kingwangalla akipata taarifa ya idadi ya wagonjwa waliofanyiwa vipimo
tangu mashine hiyo ipone kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Mionzi katika
hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Flora Rwakatare (kulia).
Mkuu wa Idara ya Mionzi katika
hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Flora Rwakatare akizungumza jambo
na waandishi wa habari katika chumba cha vipimo vya MRI wakati wa ziara
ya kushtukiza iliyofanywa na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla,
Januari 4, 2016.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi
Kingwangalla akiwa ndani ya chumba cha vipimo vya MRI katika hospitali
ya Taifa ya Muhimbili ya jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya
kushtukiza, Januari 4, 2016.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi
Kingwangalla akipata maelezo ya mashine mpya ya CT Scan iliyonunuliwa
hivi karibu na Serikali kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru.
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru (kushoto) akitoa maelezo ya uwezo
mashine mpya ya CT-Scan iliyonunuliwa na Serikali hivi karibuni ambayo
hadi kufikia Januari 4, 2016 ikiwa na muda wa siku tatu tangu kuanza
kutumika hospitalini hapo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi
Kingwangalla akimpongeza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru baada ya kuona mabadiliko makubwa
katika hospitali hiyo tangu alipokaimu kiti hicho wakati wa zaiara ya
kushtukiza katika chumba kilichofungwa mashine mpya ya CT-Scan
iliyonunuliwa na Serikali hivi karibu na inauwezo mkubwa wa kufanya
kipimo kwa sekunde 6 na kutoa majibu. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Mionzi
katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Flora Rwakatare.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi
Kingwangalla akiwa kwenye dirisha la malipo ya matibabu hospitalini hapo
wakati wa ziara ya kushtukiza aliyoifanya, Januari 4, 2016.
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na
Ajali ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya dharura katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Juma Mfinanga akitoa maelezo kwa
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla aliyetembelea kitengo chake,
Januari 4, 2016. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Dk. Hamisi Kingwangalla
akiendelea kupewa maelezo ya namna wananchi wanavyohudumiwa katika
kitengo hicho na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali ambaye
pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya dharura katika Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili, Dkt. Juma Mfinanga.
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na
Ajali ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya dharura katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Juma Mfinangaakitoa maelezo ya
ubao maalum unaowaongoza madaktari na wagonjwa wanaohudumiwa katika
kitengo hicho kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Dk. Hamisi Kingwangalla.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Dk. Hamisi Kingwangalla
akikagua wodi mpya ya wagonjwa mahututi (ICU) ambayo ipo kwenye hatua
za mwisho kukamilika. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru akimtembeza Mh. Naibu Waziri
kwenye wodi hiyo.
0 comments:
Post a Comment