Pages

Ads 468x60px

Thursday, December 17, 2015

25 kuibuka washindi katika droo ya tatu ya promosheni ya "Jaza Mafuta na Ushinde" ya GAPCO



Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa kampuni ya GAPCO Tanzania, Jane Mwita (kati) akibonyeza kitufe kwenye kompyuta kuwatafuta washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya "Jaza Mafuta na Ushinde" inayoendeshwa na Kampuni hiyo kwa Wateja wake wa jijini Dar es Salaam,ambapo zaidi ya wateja 20 huibuka kidedea kila wiki. Kulia anaeshuhudia ni Mkaguzi wa michezo ya kubahatisha nchini, Chiku Saleh na Kushoto ni Meneja Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi.

KAMATI YA URATIBU YA SHIRIKISHO LA VYUO ELIMU YA JUU YAANZA VIKAO VYA SIKU MBILI


Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Zainab Abdallah (MNEC) akiongoza kikao cha Kamati ya Uratibu Taifa ya la Vyuo vya Elimu ya juu kilichofanyika kwenye ukumbi wa Sekretarieti, Makao Makuu ya CCM Ofisi Ndogo Lumumba jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Zainab Abdallah (MNEC) akiongoza kikao cha Kamati ya Uratibu Taifa ya la Vyuo vya Elimu ya juu, kulia ni Katibu Mtendaji Ally S. Hapi

Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Zainab Abdallah (MNEC) akijadiliana jambo pamoja na Daniel Zenda (katikati) na Ally S. Hapi wakati wa kikao cha Kamati ya Uratibu Taifa ya la Vyuo vya Elimu ya juu.
Wajumbe wa kikao wakichambua mambo mbali mbali.

Kamati ya Uratibu taifa ya Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu leo imeanza kikao cha siku mbili kinachofanyika makao makuu ya CCM Ofisi Ndogo Lumumba jijini Dar es salaamchini ya Mwenyekiti wake bi Zainab Abdallah(Mnec). Viongozi wengine wanaohudhuria kikao hicho ni Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho Ndg. Hamid Mhina (Mnec), Katibu Mtendaji Ally S. Hapi, Katibu mtendaji Daniel Zenda, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM taifa kutoka Shirikisho Joseph Chitinka,Katibu uchumi na Fedha Richard Luhende, katibu wa siasa na uenezi Fikiri Mzome na katibu wa uhamasishaji Mganwa Nzota.

JAJI MARK BOMANI AMSHAURI MAALIM SEIF AKUBALI UCHAGUZI URUDIWE




Jaji  Mkuu na Mwanasheria Mkuu Mstaafu, Mark Boman akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
JAJI Mkuu na Mwanasheria Mkuu Mstaafu, Mark Boman amesema kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja Zanzibar, Maalim Seif Hamad akubali uchaguzi urudiwe Zanzibar kwani kama alishinda atashinda tena kutokana na waliompigia katika uchaguzi ulifutwa watampIgia kura tena.

Boman ameyasema hayo leo jijini Dar eS Salaam , wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa Maalim kujitangazia kuwa ameshinda ni suala ambalo halikufuata utaratibu hivyo kutokana na mazingira hayo uchaguzi ufanyike ili kupata Rais wa Serikali ya Zanzibar.

“Kurudia uchaguzi Zanzibar ni jambo lisilo epukika lakini wakae na kuangalia dosari zilizojitokeza na kufuta uchaguzi lazima lishughukiwe kisheria bila kufanya hivyo kunaweza kuleta matatizo”amesema Jaji Mstaafu, Boman.

Amesema kuwa uchaguzi uliofanyika Zanzibar walitakiwa kukaa na kuona wapi walikosea katika kuondoa changamoto hizo ambapo ilikuwa ngumu kutokana na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salum Jecha na wajumbe walishindwa kuafikiana.

Hata hivyo Boman ametaka suala la katiba lazima lishughulikiwe kuacha kwake ni aibu ya nchi kutokana na mabilioni ya fedha yametumika katika mchakato huo.


Amesema kuwa migogoro inayotokea ya ardhi na wafugaji pamoja wakulima inatokana na kutokuwa na katiba ambayo ndio ingekuwa suluhu ya utatuzi wa migogoro hiyo.

WATANZANIA WANNE WAPATA TUZO ZA UANDISHI WA FASIHI YA KISWAHILI AFRIKA

Afisa Masoko wa Alaf, Theresia Mmasy akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani)jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mwandishi wa kitabu cha Kolonia Santita, Enock Maregesi na Mwandishi wa Ushairi la Kifaurongo, Christopher Budebah.
Mkuu wa Idara ya Fasihi ya Mawasiliano na Uchapishaji (TATAKI) WA wa chuo kikuu cha Dar es Salaam akiwa na baadhi ya viongozi ya ALAF Limited. 
Mshiriki wa Taaluma ya Kiswahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa, Adrian Mtembei  akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Mwandishi wa kitabu cha Kolonia Santita, Enock Maregesi akipokea ua kutoka kwa Meneja Huduma na Masooko Alaf ,Piyush Kanti Nath leo wakati wa kuwapongeza washindi wa uanishi wa fasihi za kiswahili Afrika.
Mwandishi wa kitabu cha Kolonia Santita, Enock Maregesi akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na tuzo aliyoipata katika uandishi wa wa kitabu cha Kolonia ya Santita.
Mwandishi wa Ushairi la Kifaurongo, Christopher Budebah akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waandishi.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

KWA mara ya kwanza Lugha ya Kiswahili imeingia katika rekodi ya dunia kwa watanzania wanne kuchomoza katika tuzo ya waandishi ya Fasihi Afrika. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mshiriki wa Taaluma ya Kiswahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa, Adrian Mtembei amesema lugha ya Kiswahili ya kujivunia kutokana na watanzania wenye lugha yao kuwa washindi.

Washindi wa tuzo hizo ni Enock Maregesi ambaye aliandika Kolonia Santita,Chiristophee Bubebah, Anna Manyaza aliandika Penzi la Damu, Mohamed Ghassani aliandika N’na Kwetu.

Walioshiriki katika tuzo hiyo walikuwa 65 na kuweza kuibuka watu wanne ambao ni washindi wakitokea nchini na sherehe hizo zilifanyika Nchini Kenya.

Amesema kwa lugha ya kifaransa na Kiingereza zimekuwa zikijitokeza kila mwaka kwa watu kuandika riwaya na mashairi lakini Kiswahili imekuwa ikisahaulika hivyo na kufanya Chuo Cornell Nchini Marekani iliamua kufanya hivyo kuwa watu kuandika Riwaya na Mashairi.

Katika tuzo hizo Kampuni ya watengenezaji wa Mabati ya Alaf ilizamini tuzo hizo na kutaka watu wajitokeze katika kuinua lugha ya Kiswahili duniani.



Afisa Masoko wa Alaf, Theresia Mmasy amesema kazi wataendelea kushirikiana na watanzania katika kukuza Kiswahili katika kudhamini tuzo hizo.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto yatangaza Mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele


Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Donan Mmbando  akieleza kuhusu Mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele mbele ya Waandishi wa Habari leo 17 Desemba, 2015.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Donan Mmbando akionyesha aina ya dawa zinazotakiwa kugawiwa kwa umma wakati alipotangaza Mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele mbele ya Waandishi wa Habari leo 17 Desemba, 2015.




Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa ya kutangazwa kwa Mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele iliyotolewa leo 17 Desemba, 2015 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
(Picha zote na Benedict Liwenga)


Na Shamimu Nyaki.
 
Serikali  kupitia Mpango wa  wa Taifa wa kudhibiti Magonjwa yasiyopewa kipaumbele leo   imetangaza tarehe 19 hadi 23 mwezi huu kuwa itaanza zoezi la kugawa dawa kwa makundi yanayopaswa kupata dawa za magojwa hayo. 

 Tamko  hilo  limetolewa  na Katibu mkuu wa Wizara Ya Afya na Ustawi wa Jamii,Wazee,na Watoto  Bw. Donald  Mmbando   alipokuwa anazungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam na kusema kuwa Magonjwa  ambayo hayapewi kipaumbele  ni Usubi,Vikope (Trakoma), Matende, Mabusha,Ngiri maji, na Minyoo ya tumbo  hivyo dawa hizo zitasaidia kupunguza tatizo.

Ameongeza kuwa zoezi hilo la ugawaji wa dawa litatekelezwa katika vituo vyote vya Afya, Zahanati,Hospitali, shule za msingi na sekondari,sokoni,vituo vya usafiri,pamoja na Ofisi za Serikali na Mashirika ya Umma na hivyo wananchi wanaombwa kujitokeza kwa wingi  kupata huduma hiyo ambayo haina malipo yoyote.

Katibu Mkuu huyo  amesema  kuwa wahusika wakuu katika kupatiwa dawa hizo ni Watu wote kuanzia miaka mitano na kuendelea,isipokuwa watoto chini ya miaka mitano,wajawazito, mama    anaenyonyesha mtoto chini ya siku saba na Wagonjwa Mahututi.

“Tunataka kulinda afya zao na Uhai wao hivyo tunaomba wafuate maelekezo vizuri”.Alisema Bw Mmbando.

Aidha zoezi hilo litatekelezwa  katika mikoa ya Katavi, Rukwa, Singida, Dodoma,Mtwara, Lindi na Pwani kwa ajili ya kujikinga  na kutibu  magonjwa hayo na Mikoa mingine iliyobaki  itafanya zoezi hilo  katika  ngazi ya  jamii na shuleni mwishoni mwa mwezi Januari kuendelea hadi Februari 2016.

Naye Mratibu wa Mpango  huo Dkt  Edward kirumbi ameeleza kuwa takwimu zainaonyesha kuwa magonjwa yasiyopewa kipaumbele hapa nchini ni kubwa ambapo ugonjwa wa Usubi umeenea zaidi katika mikoa sita ikiongozwa na Dodoma, Ugonjwa wa Minyoo ya tumbo wagonjwa million 13, kichocho ,Matende na Mabusha tathmini za awali zinaonyesha mikoa 18  imeathirika kwa kuwa na wagonjwa million 12.

 Vile vile Dkt  Kirumbi ameeleza kuwa Magonjwa haya yamekuwa na athari kubwa hasa kwa kuathiri nguvu kazi ya Taifa hivyo wananchi wanapaswa kupata dawa hizo ambazo zitakuwa zinatelewa kwa mwaka mara moja  ili kukinga upungufu wa Damu, kuuwa vimelea vya ugonjwa huo, kupungua kwa magonjwa ya ngozi, na kuongeza virutubisho bora mwilini.

Hata hivyo jamii inapaswa kupewa elimu zaidi kuhusu Magonjwa haya kwa vile bado haijaelewa athari za magonjwa haya kwa  kiasi kikubwa hasa kwa maeneo ya vijijini ambayo ndio waathirika wakubwa.

MHAGAMA; alitaka SHIVYAWATA kuondoa tofauti zao


 




44
Mkalimani wa lugha ya alama akifafanua mazungumzo kwa alama kwa baadhi ya wajumbe wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) wakati wa  mkutano wa shirikisho hilo na Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Dk. Abdalla Possi (hayupo pichani), jana jioni (Jumatano, Desemba 16, 2015), katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Jijini Dar es Salaam.
43
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Bibi Jenista Mhagama (Mb), (katikati) akimsikiliza  Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Amon Mpanju wakati shirikisho hilo  lilipo kutana na Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Dk. Abdalla Possi (wa kwanza kushoto), jana jioni (Jumatano, Desemba 16, 2015), katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Jijini Dar es Salaam, (wa tatu kulia), Naibu Katibu Mkuu Ofisi  ya Waziri Mkuu, Bibi. Regina Kikuli.
46
Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Dk. Abdalla Possi, akiteta  jambo na mmoja wa wajumbe wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) mara baada ya kukutana na wajumbe wa shirikisho hilo  jana jioni (Jumatano, Desemba 16, 2015), katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Jijini Dar es Salaam.
45
Baadhi ya wajumbe wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) wakifuatilia mazungumzo ya mkutano huo, wakati wa  mkutano wa shirikisho hilo na Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Dk. Abdalla Possi, jana jioni (Jumatano, Desemba 16, 2015), katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Jijini Dar es Salaam.
…………………………………………………………………………………. WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia, (Sera,Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Bibi Jenista Mhagama (Mb), amelitaka Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) kuondoa tofauti zao ili kuweza kushirikiana na serikali ya awamu ya tano ambayo imedhamiria kuimarisha na kulinda haki za watu wenye ulemavu.
  “Mnapaswa kuhakikisha kuwa wale wote wanaoleta tofauti zenu kuwashughulikieni mapema katika vikao vyenu ili muweze kushirikiana na sisi katika kuhakikisha mnapata haki ya kulindwa , kuheshimiwa na usalama. Tunataka nchi yetu baada ya miaka mitano iwe katika historia nzuri kwa kuwajali watu wenye ulemavu”. Amesema.
  Ametoa wito huo wakati akizungumza na Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) jana jioni (Jumatano, Desemba 16, 2015), katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Jijini Dar es Salaam.
  Bibi Mhagama alisema: “Tunapaswa tusimuangushe Rais Magufuli kwa imani aliyoionesha kwenu na kuteua Naibu waziri anayeshughulikia masuala yanayowahusu ambayo yanaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu,” alisema.Awali akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa shirikisho hilo, Amon Mpanju pamoja na kumshukuru Waziri na Naibu Waziri anayeshughulikia (Watu wenye ulemavu) kwa kuitisha mkutano uliolenga kujadili vipaumbele vya watu wenye ulemavu nchini pamoja na nchi zinazowakabili ili kuzipatia ufumbuzi alimuomba waziri huyo kuhairisha ili waweze kukamilisha uaiinishaji changamoto zao vizuri.
  “Tunaomba mheshimiwa waziri utupatie muda zaidi tuweze ili tuweze kuainisha vizuri zaidi changamoto zetu ambazo naamini Naibu waziri mwenye dhamana ya kushughulikia watu wenye ulemavu amabye pia tunaimani naye sana ataweza kubaini masuala yanayotuhusu na kuweza kuyatekeleza katika majukumu yake” alisema.
  Mkutano huo uliandaliwa na Naibu Waziri anayeshughulikia watu wenye Ulemavu Dk. Abdalla Possi, pia ulihudhuliwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu aliye wakilishwa na Naibu wake, Bibi. Regina Kikuli na Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu, Obey Assery.

MREFA YAANDAA KOZI YA LESENI C

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kwa kushirikiana na Chama cha Soka Mkoa wa Mbeya (MREFA) wameandaa kozi ya makocha wa mpira wa miguu Leseni C, itakayofanyika jijini Mbeya kuanzia Disemba 21- 04 Januari, 2016.


Jumla ya makocha 46 kutoka katika kanda ya Nyanda za Juu Kusini wanatazamiwa kushiriki kozi hiyo ya wiki mbili, ambayo itaendeshwa na wakufunzi Kidao Wilfred na Salum Madadi.

Washiriki wa kozi hiyo ni Mussa Kasalika, Steven Viera, Golya, Mlekwa, Matokeo Sigalla, Ernest Nkandi, Felix A. Sosteness, Michael Mwamaja, Daniel Mwaisabila, Deus Nsheka, Albert Gama, Joseph Abiero, Simon Mwapili, Bahati Mwaipopo, Willy Ngailo, Charles Makwaza, Paul Msyahila, Osward Morris, Jacob Ndago, Castor Mahona, Ambilikile Albion, Jumanne Nsunye, Gowdin Mulenga.


Wengine ni Abel Shizya, Matatizo Abdallah, Michael Kasekenya, Thomas Kasombwe, James Wanyato, Rose Njobelo, Amos Chiwaya, Baraka Kibanga, Mohamed Dondo, Josephat Digna, Shabani Mwaibara, Lucas Kibaja, Yusuph Mlekwa, Joel Makitta, Josiah Steven, Rashid Kasiga, Charles Njango, Alex Lusekelo, Shabani Kazumba, Ismail Suleiman, Ibrahim Kasegese, Simon Bernard, Anthony Mwamlima, Christian Simkoko.

BOMOA BOMOA YATIKISA TENA WAKAZI WA BONDE LA MTO MSIMBAZI JIJINI DAR LEO.


Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Manispaa za jiji la Dar es salaam zitafanya zoezi la kuondoa wavamizi maeneo yote ya Mabondeni, kingo za mito  na za Bahari, maeneo ya wazi, maeneo ya miundombinu na maeneo yote hatarishi zaidi ya 150 katika  jiji la Dar es salaam. Bomoa bomoa ya leo inaendelea katika Bonde la mto msimbazi.Mkuu wa Kitengo cha Sheria Balaza la Taifa la usimamizi wa mazingira Tanzania (NEMC), Manchale Heche akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam juu ya zoezi la Bomoabomoa maeneo ya miundombinu na maeneo yote hatarishi nakuwataka wananchi waliojenga katika fukwe za bahari Kingo za mito na mikondo ya bahari kuhamisha mali zao mapema.
Wananchi wakitoa samani pamoja na vitu mbalimbali ndani ya nyumba zao ili kupisha ubomoaji wa nyumba zilizo maeneo hatarishi. 

Ubomoaji ukiendelea maeneo ya Mto msimbazi jijini Dar es Salaam. 
Wananchi pamoja na polisi (Wazee wa kazi) wakiangalia ubomoaji unavyoendelea bila vurugu.
Vijana wakiokota vitu mbalimbali katika maeneo yaliyobomolewa leo jijini Dar es Salaam. 
Wananchi wakiwa maeneo hatarishi ambayo yanasubiri kubomorewa. 
Uondoaji wa vyuma katika nyumba inayongoja kubomolewa. 
 Wazee wa kazi wakihakikisha usalama wa eneo ya ubomoaji. 
 Vitu mbalimbali vikiwa vimetolewa nje ili kupisha ubomoaji wa nyumba.

BANKI YA BARCLAYS WAZINDUA OFISI MPYA JIJINI DAR ES SALAAM

Mwenyekiti wa bodi wa Benki ya Barclays hapa nchini, Ramadhani Dau akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ofisi mpya kwenye ghorofa ya pili ya jengo la benki hiyo lililopo jengo la Makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Mkurugenzi mkuu mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina akiwa na baadhi ya wadau wa benki hiyo wakati wa kuzindua ofisi ya benki hiyo ghorofa ya pili ya benki hiyo.
Mwenyekiti wa bodi wa Benki ya Barclays hapa nchini, Ramadhani Dau  akifungua kitambaa kuashiria uzinduzi wa ofisi ya benki hiyo  katika jengo la benki ya Barclays ghorofa ya pili leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi mkuu mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina akishuhudia wakati akifungua kitambaa hicho.
Mkurugenzi mkuu mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina akizungumza na wafanyakazi wa benki ya Barclays hapa nchini (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam.

 Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Barclays hapa nchini wakimsikiliza Mkurugenzi mkuu mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina.

Baadhi ya wanabodi ya benki ya Barclays wakimsikiliza Mkurugenzi mkuu mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina mara baada ya kuzindua ofisi mpya leo jijini Dar es Salaam. 

Uongozi wa StarTimes waishukuru Serikali kwa ushirikiano mzuri inaowapa


 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akimkaribisha ofisini kwake Makamu wa Rais wa Kampuni ya Star Times Tanzania Bi. Zuhura Hanif leo jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akielezea jambo wakati wa mazungumzo baina yake na uongozi wa Star Times waliomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. LEO Liofang na Makamu wa Rais wa StarTimes Africa Bw. Eric Xue
 Makamu wa Rais wa StarTimes Africa Bw. Eric Xue afafanua jambo wakati wa mazungumzo baina ya wawakilishi wa  StarTimes na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel (kulia) leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. LEO Liofang.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. LEO Liofang akielezea jambo wakati wa mazungumzo baina ya wawakilishi wa StarTimes na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel leo jijini Dar es Salaam.Katikati ni Makamu wa Rais wa StarTimes Africa Bw. Eric Xue

 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akipokea zawadi ya Kadi ya Krismasi aliyokabidhiwa kwa niaba ya uongozi wa StarTimes Tanzania na Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. LEO Liofang. Katikati ni Makamu wa Rais wa StarTimes Africa Bw. Eric Xue
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akishukuru mara baada ya kupokea zawadi ya Kadi ya Krismasi aliyokabidhiwa kwa niaba ya uongozi wa StarTimes Tanzania na Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. LEO Liofang (kushoto). Katikati ni Makamu wa Rais wa StarTimes Africa Bw. Eric Xue
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel(mwenye tai) akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa StarTimes kwa kumtembelea ofisini kwake na kuipongeza Serikali kwa ushirikiano inaowapa katika kutekeleza wajibu wao kama wabia wa habari hapa nchini.Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO Bw. Assah Mwambene,Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. LEO Liofang,Makamu wa Rais wa StarTimes Africa Bw. Eric Xue na Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania Bi. Zuhura Hanif
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel(katikati)akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa StarTimes Tanzania walipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO Bw. Assah Mwambene, Makamu wa Rais wa StarTimes Africa Bw. Eric Xue, Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. LEO Liofang na Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania Bi. Zuhura Hanif
 
Blogger Templates