Jaji Mkuu na Mwanasheria Mkuu Mstaafu, Mark Boman akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
JAJI
Mkuu na Mwanasheria Mkuu Mstaafu, Mark Boman amesema kuwa Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja Zanzibar, Maalim Seif Hamad akubali
uchaguzi urudiwe Zanzibar kwani kama alishinda atashinda tena kutokana
na waliompigia katika uchaguzi ulifutwa watampIgia kura tena.
Boman
ameyasema hayo leo jijini Dar eS Salaam , wakati akizungumza na
waandishi wa habari amesema kuwa Maalim kujitangazia kuwa ameshinda ni
suala ambalo halikufuata utaratibu hivyo kutokana na mazingira hayo
uchaguzi ufanyike ili kupata Rais wa Serikali ya Zanzibar.
“Kurudia uchaguzi Zanzibar ni jambo lisilo epukika lakini wakae na
kuangalia dosari zilizojitokeza na kufuta uchaguzi lazima lishughukiwe
kisheria bila kufanya hivyo kunaweza kuleta matatizo”amesema Jaji
Mstaafu, Boman.
Amesema kuwa uchaguzi uliofanyika Zanzibar walitakiwa kukaa na
kuona wapi walikosea katika kuondoa changamoto hizo ambapo ilikuwa ngumu
kutokana na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salum Jecha
na wajumbe walishindwa kuafikiana.
Hata hivyo Boman ametaka suala la katiba lazima lishughulikiwe
kuacha kwake ni aibu ya nchi kutokana na mabilioni ya fedha yametumika
katika mchakato huo.
Amesema kuwa migogoro inayotokea ya ardhi na wafugaji pamoja
wakulima inatokana na kutokuwa na katiba ambayo ndio ingekuwa suluhu ya
utatuzi wa migogoro hiyo.
0 comments:
Post a Comment