SHIRIKA
la ndege la Etihad, ndege rasmi ya taifa za Falme za kiarabu na
Cognizant (NSADAQ: CTSH), shirika linaloongoza kwa huduma za teknolojia
ya habari, ushauri na biashara, leo wametangaza makubaliano ya kimkakati
yatakayoendesha mabadiliko ya kidijitali pande zote za shirika hilo
pamoja na washirika wake.
Chini
ya mpango wao wa miaka mitatu wenye thamani ya mamilioni ya madola,
Cognizant watawasaidia Etihad kufafanua mkakati wao wakidigitali na
kutengeza dhana mpya ambayo itatumika katika kutoa huduma bora kwa
wageni wao watakaosafiri popote na ndege za Etihad.
Kwa kuleta pamoja mikakati ya kidijitali, teknolojia, sekta na
uzoefu wa ubunifu, Cognizant watafanya utafiti wa hali ya sasa ya
biashara na teknolojia ya shirika la ndege la Etihad na kutumia utafiti
huo kutengeneza mazingira ya kidijitali ya kiwango cha hali ya juu,
itakachowezesha usambazaji kupitia idhaa nyingi, ugawaji wa wateja kwa
kina zaidi na kubinafsisha ujuzi katika masoko.
Kwa kutumia taarifa mbalimbali na ufahamu wa mteja, Cognizant
italiwezesha shirika la ndege la Etihad na washirika wake, kuelewa zaidi
mahitaji ya wageni wake.
Kwa kuunganisha tafiti hizi na mazoea bora, michakato na
teknolojia, shirika hilo litawapa wageni wake suluhisho, ofa
zitakazoendana na kila mteja kwa mapenzi yake na itaboresha huduma
zinazotolewa katika safari nzima kutokana na hali ya uaminifu wao na
upendeleo wa mteja kama vile bidhaa na huduma, kuchagua wapendapo kukaa
wakati wa safari, chaguo la mlo, safari kipindi cha sikukuu na
kadhalika. Kwa shirika hili, hii inamaanisha kufungua mitiririko mipya
ya mapato, kuongeza chapa na kutengeneza fursa nyingine za kibiashara.
Afisa Mkuu wa Biashara wa shirika la Etihad Peter Baumgartner,
alisema, “Wageni wetu wamezidi kugeukia idhaa za kidijitali zaidi
kujiunga nasi na hivyo tunatambua umuhimu wa kuwafikishia ubora wa
kipekee na usio wa dosari katika sehemu zote tunazofikia. Ushirikiano
wetu na Cognizant utatusaidia kufikia kiwango bora katika safari za
kidijitali ambayo itawaburudisha wateja kuanzia kupanga safari hadi
kununua tiketi, kwenye uwanja wa ndege na kwenye ndege, na itaboresha
uaminifu wa wageni kwa kuwavutia na kuwashirikisha wageni katika njia
mpya na za kisasa.”
Robert Webb ambae ni Afisa Mkuu Habari na Teknolojia wa shirika la
Ndege la Etihad, alisema “Ushirikiano huu ni muhimu kwa mikakati yetu
teknolojia na uvumbuzi ambayo hutuimarisha na washirika wetu katika
kujipanga upya kuwapatia wageni wetu huduma bora katika safari zao
ambayo inaendana wakati wa safari na tamati yake. Tumechagua Cognizant
kwa sababu wanaongoza katika programu za kidijitali, uzoefu wa
kidigitali kwenye huduma za usafiri, ukarimu na ushirikiano wa muda
mrefu na shirika na pia ni viongozi katika dunia ya teknolojia.”
Afisa Mtendaji Mkuu wa Cognizant, Francisco D’Souza, alisema:
“Tumefurahia kushirikiana na Etihad kutengeneza shirika la ndege lenye
kuwapa kilicho bora wateja wake wakati wa safari zao kwa kutumia nguvu
ya teknolojia ya kisasa. Kwa Cognizant, mfumo wa kidijitali’ inamaanisha
kuwa na uwezo wa kuunganisha teknolojia, takwimu za kisayansi, vifaa,
ubunifu na mikakati ya kibiashara kubadili mifumo na uzoefu.
Ushiriki huu unaweka alama ya kuungana kwa mashirika mawili yenye
kasi ya uongozi ambayo mikakati yao ya ukuaji inabebwa na uvumbuzi wa
kidijitali. Timu ya kazi za kidijitali ya Cognizant inafurahia na
kutegemea mengi kwa kusaidiana na shirika la ndege la Etihad pamoja na
washirika wake ikiwemo kuleta udhibiti, urahisi na uwazi kwa msafiri wa
kisasa.
Muamko wa kidijitali utazidi kuimarisha shirika la Etihad katika
kuwa na chapa yenye kiwango cha hali ya juu kwa kutoa huduma bora kwa
wateja.
Kama sehemu ya ushirikiano huu, Cognizant itasimamia program za
Etihad na kuziunganisha katika jukwaa jipya la kidijitali. Kituo cha
ubora wa kidijitali itaanzishwa kuendesha uvumbuzi pamoja na washirika
wakuu wa kiteknolojia wa Etihad.
0 comments:
Post a Comment