Baadhi
ya vijana wakiwa wanaendelea kufanya usafi maeneo ya Uwanja wa Taifa wa
Ifakara eneo ambapo Tamasha hilo la Msafara lilifanyika.
Katibu
Tawala wa Wilaya ya Kilombero Bw. Yahya Naniya(aliyevaa miwani) akiwa
katika ushiriki wa kufanya usafi kaika uwanja wa Taifa wa Ifakara.
Vijana wengi wa
Ifakara Wilayani Kilombero mkoani Morogoro wamepewa nasaha kutumia vipaji vyao
kwa lengo la kutimiza ndoto zao ili maisha yao yaende sawa na kukuwa kiuchumi.
Mwenyekiti wa
Programu ya Msafara James Isdore akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu ya msafara
wilayani Kilombero kata ya Ifakara alisema asilimia kubwa ya vijana wenye umri
kati ya miaka 14-15 wamekuwa wakijirudisha nyuma kutumia vipaji vyao kutimiza
ndoto zao kwa sababu mbalimbali.
"Tumeamua
kuja Ifakara kwa lengo la kuja kuinua vijana kupitia programu hii ambapo programu hii kwa sasaa ipo
katika majaribio inatarajia kuanza rasmi mwakani 2016 hadi sasa majaribio ya
programu hii yameweza kufanyika katika mikoa miwili Dar es Salaam na Ifakara na
matokeo yake tumeanza kuona ni makubwa mno katika kusaidia jamii ya vijana
kutimiza ndoto zao na sio kukaa vijiweni kudidimiza ndoto zao"alisena
Isdore
Alisema Programu
hiyo inaendeshwa kwa kupitia mashirika matano yanayojishughulisha na masuala ya
vijana yakiratibiwa na Shirika la Oxfam Tanzania.
Veronica Malwata ambaye ni Mkazi wa mji wa Ifakara alisema ndoto ya kipaji haiwezi kuja
hivi hivi bila kujituma hivyo vijana wanapaswa kupambanua wapi walipo na
wanataka kwenda wapi.
Ramadhani Lihapa ni mmoja wa vijana ambaye alifanikiwa kutimiza ndoto zake, alisema
kijana anapaswa kujitambua ananafasi gani katika jamii na kuona ni namna
gani anaweza kufikia ndoto yake aliyekuwa anaiwaza siku nyingi.
Mwenyekiti wa Maandalizi wa Msafara kutoka TYDC James Isdore akielezea maana ya msafara kwa wakazi wa Ifakara
Baadhi ya wakazi wa Ifakara wakiendelea kusikiliza kinacho endelea
Baadhi ya watoto wa shule mbalimbali za Msingi katika mji wa Ifakara wakiwa katika Tamasha la Msafa
Kikundi cha young Feminist forums wakiwa wanatoa somo kwa vijana pamoja na burudani kwa njia ya ngonjera
Mmoja
wa wadau akiwa anatoa neno la kuwajenga vijana juu ya kujitambua lakini
pia kuwajengea uwezo vijana kuwa wafumbuzi na wabunifu ili waweze pata
kujitambua
Bi.
Nusura Salum akitoa ushuhuda wake wa namna alivyo anza maisha yake kwa
kuuza maandazi , kuwa mkulima na sasa mfanyabiashara mkubwa na
alivyopitia katika safari yake ya mafanikio
Mwanamuziki Chipukizi wa Bongo Fleva anayeishi Morogoro One Darin akitoa Burudani wakati wa Tamasha la Msafara
Ramadhani
Lyasa akielezea kwa ufupi jinsi alivyopitia changamoto mbalimbali ikiwa
ni pamoja na kutokusoma na kuwa alianza na kilimo na sasa ni
mfanyabiashara
MC Fadhiri akiendelea kutoa utaratibu wa wazungumzaji katika Tamasha la Msafara
Bi.
Veronica Malwata mkazi wa Ifakara akieleza jinsi alivyotaka kukata
tamaa ya maisha baada ya kushindwa endelea na shule na baadae kujiinua
kwa kuanza kufanya kazi katika moja ya Zahanati kama muhudumu na baadae
alipelekwa shule ya uuguzi na sasa ni muuguzi katika Hospitali ya
Ifakara.
Kijana Narsis nae akitoa ushuhuda wake wa yale aliyopitia mpaka amefanikiwa kaika maisha.
Baadhi ya waandaaji wa Msafara wakiwa wanatoa neno la Shukurani kwa wakazi wa Ifakara.
Baadhi wa wanavyuo wakiendelea kufuatilia Msafara.
0 comments:
Post a Comment