HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH) inafunga mashine nyingine ya CT- Scan ambayo inategemewa kuanza kutoa huduma kesho mchana.
"Hivyo
kufikia jumatatu ijayo Hospitali hiyo itakua na mashine mbili za
CT-Scan ambazo zitakua zinafanya kazi hatua ambayo itaboresha zaidi
utoaji wa huduma kwa wagonjwa ambao wanatakiwa kupimwa kwa kutumia
mashine hiyo," amesema Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,
Watoto na Wazee Ummy Mwalimu.
Waziri
wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Watoto na Wazee Ummy Mwalimu
ameyasema hayo leo wakati alipotembelea mashine za CT-Scan na MRI katika
hospitali hiyo.
Pamoja
na mambo mengine Waziri huyo ameshauri ripoti za wagonjwa wanapimwa kwa
kwa kutumia mashine hizo zitolewe haraka ili kuwapunguzia gharama za
kukaa muda mrefu wagonjwa wanaotoka katika mikoa mingine.
Akizungumzia
kuhusu mashine ya CT-Scan na MRI ambazo zimeharibika Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa MHN Profesa Lawrence Mseru amesema juhudi za kutengeneza
mashine hizo zinafanyika na kwamba kifaa cha CT- Scan kilichoharibika
kitaingia leo usiku wakati Spea ya MRI imeshawasili na matengenezo
yanaendelea.
Mashine ya CT-Scan hupima wastani wa wagonjwa 40 hadi 60 kwa saa 24 wakati MRI hupima wagonjwa 20 kwa siku.
0 comments:
Post a Comment