Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa (Kulia)
akimkabidhi kombe Meneja masoko wa kampuni ya sukari ya Kilombero
Ephraim Mafuru baada ya kuibuka washindi wa tatu wa Jumla katika tuzo za
muajiri bora wa mwaka zilizo andaliwa na chama cha waajiri Tanzania
(ATE). Hafla hiyo ilifanyika Dar-es-Salaam, mwishoni mwa wiki.
Kampuni
ya Kilombero Sugar Ltd imesema kuwa tuzo za Mwajiri Bora zinazotolewa
na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), zinachangia kwa kiasi kikubwa
kuleta hamasa kwa waajiri na kupelekea kutoa huduma nzuri kwa
wafanyakazi.
Akizungumzia
tuzo hizo zinazotolewa kila mwaka, Meneja Rasilimali watu wa Kilombero
Sugar Beda Marwa Chacha amesema kuwa shindano hilo linasaidia kwa kiasi
kikubwa kuwafanya wajiri kutimiza majukumu yao ili kuweza kujinyakulia
tuzo.
“Napenda
kuwaomba waajiri wenzangu kushirikiana na ATE ili kuwawezesha kuboresha
tuzo hizo. Tutambue kwamba sisi ndio muhimili mkubwa wa kuweza
kuwafanya wao waendelee kuwepo,” alisema Beda ambaye kampuni yake
imekuwa imefanikiwa kuwa mshindi wa tatu wa jumla.Amesema kuwa kadri
wanavyoshiriki wanaendelea kujifunza mambo mengi kwa waajiri wenzao na
hivyo kuendelea kufanya maboresho na kuwaasa ATE kuendelea kupanua wigo
wa mashindano hayo.
Aliwaomba
wanachama wenza kuhakikisha wanaendelea kutoa michango ili kukifanya
chama kiendelee kuwepo na kusaidia kuwapa changamoto waajiri.Alisema
kuwa Kampuni ya Kilombero Sugar imefanikiwa kupata tuzo kwa utoaji
huduma bora kwa wafanyakazi wake, juhudi za kuzuia maambukizi ya virusi
vya UKIMWI, utoaji huduma bora za maendeleo ya jamii na vilevile
ushirikiano bora kwa wafanyazi pindi wawapo kazini.
Tuzo
hizo zilitolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki. Baada ya kukabidhiwa tuzo, Mkurugenzi wa Masoko wa
Kampuni ya Sukari ya Kilombero Ephraim Mafuru alisema: “Tumekuwa karibu
kwenye kila kinyang’anyiro lakini katika sehemu hizi zote tumekuwa bora
sana”.
Katika
kampuni hiyo Serikali inamiliki asilimia 20 ya hisa zote, Kilombero
Sugar inamiliki asilimia 55 ya hisa zote za Kampuni (hisa kubwa kuliko
zote), asilimia 25 inamilikiwa na ED&F Man, kundi ambalo makazi yake
yako jijini London. Kampuni ya Sukari Kilombero inatoa ajira za kudumu
kwa wafanyakazi zaidi ya 4000.
Ikiwa
kama moja ya makampuni yanayotoa huduma bora zaidi za kijamii, kampuni
imejenga hospitali iliyogharimu kiasi cha shilingi milioni 700 ambayo
hutoa huduma zake bure kabisa kwa wakazi wa eneo hilo.Vilevile kampuni
hiyo imejenga shule ya sekondari ambayo inachukua wanafunzi kutoka pande
zote za nchi, ujenzi wa mabweni, miradi ya maji pamoja na vyoo vya
shule.
Moja
ya vitu vinavyounda Kampuni ya Sukari ya Kilombero ni mashamba makubwa
kwa ajili ya kilimo na viwanda cha sukari vya Msolwa na Ruembe vilivyopo
karibu na Mto Ruaha Mkuu ambao umeunganishwa na daraja dogo.
0 comments:
Post a Comment