Pages

Ads 468x60px

Wednesday, December 16, 2015

MUHIMBILI YAFUNGA CT-SCAN NYINGINE

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH) inafunga mashine nyingine ya CT- Scan ambayo inategemewa kuanza kutoa huduma kesho mchana.

"Hivyo kufikia jumatatu ijayo Hospitali hiyo itakua na mashine mbili za CT-Scan ambazo zitakua zinafanya kazi hatua ambayo itaboresha zaidi utoaji wa huduma kwa wagonjwa ambao wanatakiwa kupimwa kwa kutumia mashine hiyo," amesema Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Watoto na Wazee Ummy Mwalimu.

Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Watoto na Wazee Ummy Mwalimu ameyasema hayo leo wakati alipotembelea mashine za CT-Scan na MRI katika hospitali hiyo.

Pamoja na mambo mengine Waziri huyo ameshauri ripoti za wagonjwa wanapimwa kwa kwa kutumia mashine hizo zitolewe haraka ili kuwapunguzia gharama za kukaa muda mrefu wagonjwa wanaotoka katika mikoa mingine.

Akizungumzia kuhusu mashine ya CT-Scan na MRI ambazo zimeharibika Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MHN Profesa Lawrence Mseru amesema juhudi za kutengeneza mashine hizo zinafanyika na kwamba kifaa cha CT- Scan kilichoharibika kitaingia leo usiku wakati Spea ya MRI imeshawasili na matengenezo yanaendelea.


Mashine ya CT-Scan hupima wastani wa wagonjwa 40 hadi 60 kwa saa 24 wakati MRI hupima wagonjwa 20 kwa siku.

WAZIRI NAPE NNAUYE AKUTANA NA UONGOZI WA CHAMA CHA WAFANYAKAZI WA TBC OFISINI KWAKE LEO


 Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na Viongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) walipimtembelea ofisini kwake.
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiwasikiliza Viongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) walipimtembelea ofisini kwake.

TANZANIA YAPOKEA BILIONI 210 KUTOKA JAPANI

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile na Balozi wa Japani nchini Bw. Masaharu Yoshida wakibadilishana hati ya mkataba wa mkopo wa Shilingi Bilioni 210 kwa ajili ya mradi wa Umeme kati ya Tanzania na Kenya.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt.Servacius Likwelile na Balozi wa Japani nchini Bw.Masaharu Yoshida wakisaini mkataba wa mkopo. Nyuma yao kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eng. Omar Chambo, kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Japani Seiji Kihara wakishuhudia tukio hilo katika ukumbi wa Wizara ya Fedha Jijini Dares Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt.Servacius Likwelile akitoa ufafanuzi wa matumizi ya mkopo wa bilioni 210 baada ya kusaini mkataba wa mkopo huo katika ukumbi wa Wizara ya Fedha jijini Dar es Salaam.

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesaini mkataba na Serikali ya Japani kiasi cha shilingi Bilioni 210 kwa ajili ya maendeleo ya mradi wa njia ya kusafirishia umeme kati ya Tanzania na Kenya ambao utasaidia upatikanaji wa umeme wa kutosha.

Mkataba huo wa masharti nafuu ulisaininiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile na Balozi wa Japani nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kusaini mkataba huo Dkt. Likwelile alisema kuwa fedha hizo zitaelekezwa katika kusambaza nyaya za umeme zenye KV400, na urefu wa kilometa 414.5 kati ya Singida na Namanga kupitia Babati na Arusha.

Alisema kuwa kukamilika kwa mradi huo kutachochea maendeleo ya jamii na uchumi nchini kwa kuleta muungano wa kibiashara katika nchi za Afrika Mashariki.

Naye Balozi wa Japani nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida alisema kuwa mkopo huo utafanikisha kusambaza nyanya za umeme zenye urefu wa takribani kilometa 508 kati ya Tanzania na Kenya ambapo Tanzania itasambaza kilometa 415 wakati Kenya itakuwa na kilometa 93.

Japani imekuwa ikisaidia Tanzania katika miradi ya umeme kwa muda mrefu, miradi ambayo tayari imekamilika ni pamoja na usambazaji umeme Zanzibar, mradi wa usambazaji nyaya za umeme mkoani Kilimanjaro na mradi wa kutengeneza nyaya mpya za umeme jijini Dar es Saalam.

Benki ya Exim yazindua kituo chake cha huduma kwa wateja

 Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya Exim Tanzania, Bw. Selemani Ponda, (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusiana  na  uzinduzi wa kituo kipya cha  huduma  kwa wateja wa benki hiyo kwa njia ya mawasiliano ya simu ikiwa ni sehemu ya mkakati wa benki hiyo kuboresha huduma zake kupitia teknolojia ya mawasiliano. Pembeni yake ni Mkuu wa Hazina wa Benki hiyo, Bw George Shumbusho (wa pili kushoto), Afisa masoko wa benki hiyo, Bw Abdulrahman Nkondo (kushoto) na Meneja Mwandamizi Huduma kwa wateja Bw. Frank Matoro.
BENKI ya Exim Tanzania imezindua kituo chake kipya cha  huduma  kwa wateja kwa njia ya mawasiliano ya simu ikiwa ni sehemu ya mkakati wa benki hiyo kuboresha huduma zake kupitia benki hiyo teknolojia ya mawasiliano.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Meneja Mwandamizi Huduma kwa wateja  wa Benki hiyo Bw. Frank Matoro alisema pamoja na kusogeza upatikanaji wa huduma kwa wateja wa benki hiyo, vituo hivyo pia vitasaidia kuboresha mahusiano na wateja wa benki hiyo.
“Ni matarajio yetu kwamba wateja wetu watafurahia zaidi huduma bora kutoka kwa wahudumu wenye vigezo na uelewa wa kutosha kuhusiana na masuala ya kibenki kila siku za Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 1:00 jioni na siku za Jumamosi kuanzia saa 2:30 asubuhi hadi saa 7:00 mchana kupitia namba yetu ya 0784 107600,’’ alisema
Kwa mujibu wa Bw Matoro kituo hicho kinatarajiwa kuleta mabadiliko kwenye biashara kupitia huduma za kibenki huku akiongeza: “Ni adhma yetu kuhakikisha kwamba tunapambana siku zote ili tu hali ya kiuchumi kwa wateja wetu iendelee kuwa bora na ni  hicho tu ndio kimekuwa kikitusaidia kuwa na matokeo mazuri,’’.
Alibainisha kuwa huduma hiyo ilibuniwa mahususi ili kuleta tija kwa wateja wa benki hiyo kwa kuwa inaenda sambamba na mahitaji yao, mfumo wao wa maisha pamoja na hadhi yao hatua aliyoilezea kuwa itaiongezea benki hiyo uaminifu miongoni mwa wateja wake.
“Pia tunatarajia kwamba huduma hii itatuongezea ukubwa wa soko kwa kuwa itapanua wigo wa kuwafikia wateja, kujiongezea ukuaji wa fursa  sambamba na kutoa fursa kwa wateja wetu waweze kutupa mrejesho wa huduma mbalimbali tunazowapatia,’’ alisema.
Akizungumzia hati fungani za benki ya hiyo zinazouzwa katika soko la hisa la Dar es Salaam DSE, Mkuu wa Hazina wa benki hiyo Bw. George Shumbusho alisema idadi kubwa ya watu wameendelea kujitokeza kununua hati hizo huku akibainisha kuwa hati hizo zilizoanzwa kuuzwa tarehe 23 Novemba, 2015 huku zikitarajia  kufungwa tarehe 18 Disemba mwaka huu  zinalenga kukusanya takribani bilioni 15.

Kilombero Sugar: Tuzo za ATE ni hamasa kwa waajiri

 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa (Kulia) akimkabidhi kombe Meneja masoko wa kampuni ya sukari ya Kilombero Ephraim Mafuru baada ya kuibuka washindi wa tatu wa Jumla katika tuzo za muajiri bora wa mwaka zilizo andaliwa na chama cha waajiri Tanzania (ATE). Hafla hiyo ilifanyika Dar-es-Salaam, mwishoni mwa wiki. 
Kampuni ya Kilombero Sugar Ltd imesema kuwa tuzo za Mwajiri Bora zinazotolewa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), zinachangia kwa kiasi kikubwa kuleta hamasa kwa waajiri na kupelekea kutoa huduma nzuri kwa wafanyakazi. 
Akizungumzia tuzo hizo zinazotolewa kila mwaka, Meneja Rasilimali watu wa Kilombero Sugar Beda Marwa Chacha amesema kuwa shindano hilo linasaidia kwa kiasi kikubwa kuwafanya wajiri kutimiza majukumu yao ili kuweza kujinyakulia tuzo.
“Napenda kuwaomba waajiri wenzangu kushirikiana na ATE ili kuwawezesha kuboresha tuzo hizo. Tutambue kwamba sisi ndio muhimili mkubwa wa kuweza kuwafanya wao waendelee kuwepo,” alisema Beda ambaye kampuni yake imekuwa imefanikiwa kuwa mshindi wa tatu wa jumla.Amesema kuwa kadri wanavyoshiriki wanaendelea kujifunza mambo mengi kwa waajiri wenzao na hivyo kuendelea kufanya maboresho na kuwaasa ATE kuendelea kupanua wigo wa mashindano hayo.
Aliwaomba wanachama wenza kuhakikisha wanaendelea kutoa michango ili kukifanya chama kiendelee kuwepo  na kusaidia kuwapa changamoto waajiri.Alisema kuwa Kampuni ya Kilombero Sugar imefanikiwa kupata tuzo kwa utoaji huduma bora kwa  wafanyakazi wake, juhudi za kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI, utoaji huduma bora za maendeleo ya jamii na vilevile ushirikiano bora kwa wafanyazi pindi wawapo kazini.
Tuzo hizo zilitolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Baada ya kukabidhiwa tuzo, Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Sukari ya Kilombero Ephraim Mafuru alisema:  “Tumekuwa karibu kwenye kila kinyang’anyiro lakini katika sehemu hizi zote tumekuwa bora sana”.
Katika kampuni hiyo Serikali inamiliki asilimia 20 ya hisa zote, Kilombero Sugar inamiliki asilimia 55 ya hisa zote za Kampuni (hisa kubwa kuliko zote), asilimia 25 inamilikiwa na ED&F Man, kundi ambalo makazi yake yako jijini London. Kampuni ya Sukari Kilombero inatoa ajira za kudumu kwa wafanyakazi  zaidi ya 4000. 
Ikiwa kama moja ya makampuni yanayotoa huduma bora zaidi za kijamii, kampuni imejenga hospitali iliyogharimu kiasi cha shilingi milioni 700 ambayo hutoa huduma zake bure kabisa kwa wakazi wa eneo hilo.Vilevile kampuni hiyo imejenga shule ya sekondari ambayo inachukua wanafunzi kutoka pande zote za nchi, ujenzi wa mabweni, miradi ya maji pamoja na vyoo vya shule.
Moja ya vitu vinavyounda Kampuni ya Sukari ya Kilombero ni mashamba makubwa kwa ajili ya kilimo na viwanda cha sukari vya Msolwa na Ruembe vilivyopo karibu na Mto Ruaha Mkuu ambao umeunganishwa na daraja dogo.

Waatalam Wajadili mbinu za kupambana na magonjwa ya mlipuko Arusha



Dokta Mwele Malecela wa Kituo cha Utafiti wa Madawa (NIMR) Tanzania akifanya mahojiano jana na baadhi ya vyombo vya habari vilivyoshiriki katika warsha ya siku mbili inayofanyika mkoani Arusha kujadili njia bora za kupambana na magonjwa ya mlipuko kwa binadamu na wanyama ukiwemo ugonjwa wa Ebola na mengineyo katika bara la Afrika na kwingineko duniani.Warsha hiyoimeandaliwa kwa pamoja na taasisi za afya za SACIDS na EAIDSNet na kufadhiliwa na taasisi ya afya ya CORDS ya nchini Ufaransa.
Wadau mbalimbali wa Sekta ya Afya kutoka katika mashirika na taasisi mbalimbali za barani Afrika na Ulaya wakiwa katika picha ya pamoja walipokutana katika warsha ya siku mbili inayofanyika mkoani Arusha kujadili njia bora za kupambana na magonjwa ya mlipuko kwa binadamu na wanyama kama Ebola na mengineyo katika bara la Afrika na kwingineko duniani. Warsha hiyo imeandaliwa kwa pamoja na taasisi za afya za SACIDS na EAIDSNet na kufadhiliwa na taasisi ya afya ya CORDS ya nchini Ufaransa.

Ripoti kutoka Zanzibar kuhusu ajali ya moto kwenye meli December 15



Hii stori imenifikia baada ya kuenea kwenye mitandao pamoja na picha zikionesha tukio la meli kuwaka moto
Nimeipata ripoti pia kwenye habari ya ITV kwamba meli hiyo ya MV Royal imepata ajali ya kuwaka moto ikiwa katikati ya safari kutoka Unguja kwenda Pemba, moto huo umeunguza injini za meli hiyo lakini kwa bahati nzuri ikatokea meli nyingine ya MV Serengeti, ambapo ikafanyika kazi ya kuokoa abiria waliokuwa kwenye meli hiyo pamoja na kuuzima moto huo.
MELI
Kamanda wa Polisi Pemba, Shehan Mohamed Shehan amesema meli ilikuwa na abiria zaidi ya 300 pamoja na watoto 70.. wote wametoka salama na meli imefanikiwa kuvutwa mpaka bandarini Pemba.
 
Blogger Templates