Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifanya
kazi ofisini kwake Ikulu jijini Dar es salaam kwa mmara ya mwisho leo
Novemba 4, 2015 kabla ya kukabidhi madaraka kwa Rais wa awamu ya Tano
anayetarajiwa kuapishwa kesho Dkt John Pombe Joseph Maguful.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitoka ofisini kwake Ikulu jijini Dar es
salaam baada ya kufanya kazi katika siku ya mwisho leo Novemba 4, 2015
kabla ya kukabidhi madaraka kwa Rais wa awamu ya Tano anayetarajiwa
kuapishwa kesho Dkt John Pombe Joseph Maguful.
Wakati tukizisubiria saa chache zijazo
ili kuifikia November 5,2015 kwaajili ya kushuhudia tukio la kitaifa la
kuapishwa kwa rais mteule wa Tanzania kwa awamu ya tano DK. John Pombe
Magufuli,nakusogezea hii stori kutoka kwa aliyekuwa mgombea urais
nchini kupitia chama cha “CHAUMA” Hasheem Rungwe ambaye amepanga
kufungua kesi mahakama kuu ili iweze kutoa tafsiri ya nguvu ya tume ya
uchaguzi kutohojiwa au kupelekwa mahakamani.
‘Mahakama
itupe tafsiri ya sheria, wanamaana gani kwa kutuzuia kuihoji tume.?
Demokrasia haikubaliani na hali hii, watu lazima waende mahali na vyombo
vyenye mamlaka kutoa maamuzi viseme, hatuwezi kukaa kimya’ – Hasheem Rungwe
‘Sisi tunaenda mahakamani, kuomba mahakama iingilie kati ili watu wajue na tupate majibu” ;-Hasheem Rungwe


