Pages

Ads 468x60px

Monday, November 16, 2015

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA VIONGOZI WA DINI WA MKOA WA DODOMA.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Viongozi wa Kamati ya Mahusiano ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dodoma, wakati alipokutana nao kwa mazungumzo kwenye Ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma leo Nov 16, 2015. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa (kulia) ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mahusiano ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dodoma, Sheikh Ahmad Said Ahmed. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akijadiliana jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,  Chiku Galawa, wakati wa mkutano na Viongozi wa Kamati ya Mahusiano ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dodoma, kwenye Ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma leo Nov 16, 2015. Picha na OMR
Baadhi ya Viongozi wa Dini wa Mkoa wa Dodoma,wakimsikiliza Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan, wakati akihutubia alipokuwa akizungumza na Viongozi wa Kamati ya Mahusiano ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dodoma kwenye Ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma, leo Nov 16, 2015. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Viongozi wa Kamati ya Mahusiano ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dodoma, wakati alipokutana nao kwa mazungumzo kwenye Ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma leo Nov 16, 2015. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa.

ZOEZI LA USAJILI WA WABUNGE LAENDELEA MJINI DODOMA


Baadhi ya Wabunge wakibadilishana mawazo katika Viwanja vya Bunge wakati wa zoezi la usajili wa wabunge linaloendelea mjini Dodoma.
Mbunge wa  Jimbo la Makambako Mh Deo Sanga akifanya usajili katika zoezi la usajili wa Wabuge linaloendelea katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.

Baadhi ya Wabunge wakibadilishana mawazo katika Viwanja vya Bunge wakati wa zoezi la usajili wa wabunge linaloendelea mjini Dodoma. 


ECOBANK TANZANIA YAFANYA UKARABATI WA WODI YA WATOTO KATIKA HOSPITALI YA RUFAA

Kaimu mkuu wa mkoa wa Mtwara ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Mtwara Bi. Fatma Ally akikagua wodi ya watoto katika hospitali ya mkoa na rufaa ya Ligula mkoani Mtwara ambayo benki ya Ecobank Tanzania ilijitolea kukikarabati wakati wa hafla ya kuadhimisha siku ya Ecobank ambayo ilifanyika mkoani humo mwishoni mwa juma.
Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank Tanzania Bw. Enoch Osei-Safo akitoa hotuba yake kwa wakazi wa mkoa wa mtwara katika hafla ya kuadhimisha siku ya Ecobank ambayo ilifanyika mkoani Mtwara kitaifa mwishoni mwa juma. Benki ya Eco Tanzania ilisherekea siku hii kwa kukarabati moja ya wodi ya watoto katika hospitali ya Rufaa ya Ligula mkoani Mtwara ambapo walichangia kiasi cha dola za kimarekani elfu kumi na tano.

Kaimu mkuu wa mkoa wa Mtwara ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Mtwara Bi. Fatma Ally (katikati) akiwasili kwenye hafla ya kuadhimisha siku ya Ecobank ambayo ilifanyika mkoani Mtwara kitaifa. Katika kusherekea siku hii, wafanyakazi wa benki hii barani Afrika huhamasishwa kujitolea muda wao kwa ajili ya shughuli za kijamii zenye manufaa kwa jamii husika. Ecobank Tanzania ilisherekea siku hii kwa kukarabati moja ya wodi ya watoto katika hospitali ya Rufaa ya Ligula mkoani Mtwara.

BONDIA MESHACK MWANKEMWA BINGWA MPYA WA KG 66 TPBC



Refarii wa mchezo wa ngumi za kulipwa nchini Kondo Nassoro kulia akimnyoosha mkono juu bondia Meshack Mwankemwa baada ya kumnyuka bondia Hamisi mwakinyo katikati ni Promota wa ngumi za kulipwa Jay Msangi akimvalisha mkanda bingwa huyo mpya wa Kg 66 anaetamuliwa na kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBC kulia ni Shomari Kimbau Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Meshack Mwankemwa kushoto akiwa na bondia Hamisi Mwakinyo na viongozi na kulia ni Shomari Kimbau wa pili kulia ni rais wa kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBC Chaurembo Palasa na Jay Msangi.
Bondia Asha Nzowa 'Asha Ngedere' jkulia akipambana na Joyce Awino wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa CCM Mwijuma mwananyamala Dar es salaam mpambano uho ulimalizika kwa sare.




Refarii Kondo Nassoro katikati akiwainuwa mikono juu mabondia Asha Nzowa kushoto na Joyce Awino baada ya kutoka droo.

WAFANYAKAZI WA BENKI YA CRDB WAKISHIRIKI MICHEZO MBALIMBALI KATIKA SIKU YA FAMILIA YA CRDB


 Wafanyakazi wa  Benki ya CRDB mkoa wa Arusha  wakishindana kuvuta kamba katika viwanja vya Olasiti Garden leo katika sherehe za siku ya familia ya CRDB ambazo  hufanyika kila mwaka na kuhudhuriwa na familia za wafnayakazi wa benki pamoja na familia za wateja.
Meneja wa Benki ya  CDRB  tawi la Usa River  lilipo mkoani Arusha  Jenipher  Tond akikabidhi zawadi ya tisheti kwa mtoto aliyeshinda kucheza mziki leo sherehe za siku ya familia ya CRDB ambazo  hufanyika kila mwaka na kuhudhuriwa na familia za wafnayakazi wa benki pamoja na familia za wateja.
 Watoto wakimkimbiza kuku katika mashindano yaliyofanyika kwenye sherehe za  siku ya familia ya CRDB ambazo  hufanyika kila mwaka na kuhudhuriwa na familia za wafanyakazi wa benki pamoja na familia za wateja
 Malindi band ya mkoani kilimanjaro ikitumbuiza sherehe za siku ya familia ya CRDB ambazo  hufanyika kila mwaka na kuhudhuriwa na familia za wafanyakazi wa benki pamoja na familia za wateja
Mfanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la USA akikabidhi zawadi kwa mtoto

WABUNGE WA CCM WAAMUA KWA PAMOJA NAFASI YA USPIKA NI JOB NDUGAI


 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiongea na waandishi wa habari mara baada ya Wabunge wa CCM kupitisha jisha la Spika.

Katibu wa NEC (CCM) Itikadi na Uenezi ambaye pia ni mbunge wa Mtama, Nape Nnauye alisema “Kamati ya Wabunge wote wa CCM imekamilisha kazi yake ya kwanza kuchambua na kupitisha moja kati ya majina matatu yaliyoteuliwa na Kamati Kuu.
 
“Kama tulivyoona wagombea wawili walijitoa, hivyo Job Ndugai amepitishwa kwa kauli moja kugombea nafasi ya uspika. Tunamuombea kura kwa sababu sifa zote anazo, bila shaka hakutatokea mgombea wa upinzani atakayezidi sifa zake,” alisema Nape.
Mbunge wa Jimbo la Kongwa Ndugu Job Ndugai akiongea na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa NEC baada ya jina lake kupitishwa na wabunge wa CCM.

Katibu Mkuu wa CCM akihutubia kwenye kikao maalum cha wabunge wa CCM kwenye ukumbi wa NEC mjini Dodoma.
Katibu Mkuu wa CCM akipokea pongezi alizopewa na wabunge wa CCM kwa kazi nzuri iliyowapa CCM ushindi mkubwa katika uchaguzi uliofanyika oktoba 2015.
Sehemu ya wabunge wa CCM walioshiriki kwenye kikao maalum cha uchaguzi wa Spika kutoka Chama Cha Mapinduzi.
Mbunge Mteule wa Nzega mjini Hussein Bashe akizungumza na Mbunge mteule wa jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye pamoja na Jerry Slaa (katikati) kabla ya zoezi la upigaji kura kwenye ukumbi wa NEC.
 
Blogger Templates