Pages

Ads 468x60px

Saturday, November 28, 2015

Maagizo ya Rais Magufuli kuhusu safari za nje za watendaji wa Serikali yaanza kutekelezwa

Kufuatia maagizo ya Mhe. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoyatoa hivi karibuni ya kusitisha safari za nje kwa Wizara, Idara na Taasisi za Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imeanza kutekeleza maagizo hayo kwa kutoa maelekezo mahsusi kwa Balozi zake nje.

Wizara imezielekeza Balozi zote zilizopo maeneo mbalimbali duniani kujipanga ili kushiriki kikamilifu katika kuiwakilisha Serikali kwenye mikutano yote ya kimataifa na kikanda inayofanyika katika maeneo yao ya uwakilishi. Tanzania inazo Balozi 35; Balozi Ndogo tatu; Vituo viwili vya Biashara; na Konseli za Heshima 17 katika nchi mbalimbali. Hizi zote zitahusika katika kuendeleza utekelezaji wa Diplomasia yetu ya Uchumi na uwakilishi wa maslahi ya nchi yetu.

Aidha, hadi sasa Mikutano ambayo tayari imefanyika na Balozi zetu kuwakilisha ni pamoja na Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) unaoendelea nchini Malta na Mkutano wa Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Habari wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika nchini Lesotho.

Aidha, Wizara inatoa wito kwa Wizara, Idara na Taasisi za Serikali kuwasilisha mapema taarifa za mikutano inayohusu sekta zao ili kutoa fursa kwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kuzifanyia kazi kwa wakati ili kuhakikisha ushiriki wa Tanzania unakuwa wenye tija kwa taifa.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inaungana na wadau wengine kumpongeza Mhe. Rais Magufuli kwa hatua anazozichukua za kuleta ufanisi mkubwa wa kazi na kubana matumizi ili kuiwezesha Serikali kuwahudumia wananchi kikamilifu.

Imetolewa na:
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
27 Novemba, 2015

Ni kazi mpaka Jumamosi !! wengine watatu wamesimamishwa kazi leo TRA ..



Jana November 27 2015 Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa aliendelea na majukumu yake kwa kufanya ziara ya ghafla bandarini Dar na kukutana na mambo ambayo yalimkwaza ikiwemo upotevu wa makontena zaidi ya 340 pamoja na ubadhirifu… akaamrisha watu watano wasimamishwe kazi na uchunguzi uendelee juu yao.
Hii ilikuwa jana, Kikao cha waziri Mkuu Majaliwa pamoja na Maafisa wa TRA na TPA
Hii ilikuwa jana, Kikao cha Waziri Mkuu Majaliwa pamoja na Maafisa wa TRA na TPA
Muda mfupi baadaye jana hiyohiyo ikatoka taarifa Ikulu kwamba na Kamishna Mkuu wa TRA, Rished Bade nae amesimamishwa kazi… leo nina taarifa nyingine kuhusu wengine watatu kusimamishwa kutoka hapohapo Mamlaka ya Mapato TRA.
Majina ya waliosimamishwa leo Anangisye Mtafya, Nsajigwa Mwandengele na Robert Nyoni… agizo la kusimamishwa kwao limetoka kwa Waziri Mkuu ambae amenukuliwa na blog ya Issa Michuzi kuhusu uamuzi huo >>> “Kazi ya kuwachunguza ilianza jana ileile na sasa tumeona hawa watu wanapaswa kuwa nje ya utumishi ili kupisha uchunguzi ufanyike kwa uhuru zaidi” >>> Waziri Mkuu Majaliwa.
Hii taarifa nimeitoa kwenye Blog ya Issa Michuzi.
MAJALIWA BOY
Mpaka sasa jumla ya watumishi tisa wamesimamishwa na agizo la Serikali ni kwamba hawatoruhusiwa kusafiri nje ya nchi mpaka uchunguzi juu yao utakapokamilika.

Abiria wamepona kwenye ajali ya ndege na bado wanafungua na kesi ya ajali..



Ikitokea unakuwa sehemu ya watu walionusurika kwenye ajali, jambo kubwa ambalo wengi wanaanza nalo ni kumshukuru MUNGU kwa kutoka salama !!
Kama uko karibu na headlines za stori za kimataifa najua utakumbuka ile ajali ya ndege ya British Airways iliyotokea uwanja wa ndege  Las Vegas Marekani wakati ndege ikijiandaa kupaa.
Taarifa nyingine toka Chicago Marekani inahusu kesi ambayo imefunguliwa kuzishtaki Kampuni mbili, GE Aviation watengenezaji wa engine ya ndege iliyopata ajali, pamoja na Boeing Company ambao ndio watengezaji wa ndege yenyewe.
777 Everett Factory K65682-02
Abiria hao 65 waliofungua kesi hiyo wamesema wanazishtaki Kampuni hizo kwa sababu walipata misukosuko wakati wa ajali hiyo ambayo ndege waliyopanda ililipuka na kushika moto kwenye engine yake moja wakati ikiwa kwenye njia ya kurukia ndege uwanja wa McCarran International Airport, September 8 2015.
 
Blogger Templates