Pages

Ads 468x60px

Sunday, November 8, 2015

MAGUFULI AFUTA SAFARI ZA NJE KWA WATUMISHI WA UMA,AANZA MIKAKATI YA KUJENGA NCHI

     Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli leo asubuhi katika Ikulu ya Dar es Salaam  amefanya kikao na Makatibu wakuu, Manaibu Makatibu wakuu, Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)  ili kutoa uelekeo wa Serikali anayoitaka  mara baada ya  kuapishwa.

     “Nataka Serikali iendelee kwa nguvu zote na katika kutekeleza dhana ya ‘HAPA KAZI TU’ na viongozi kuzingatia na kukumbuka ahadi nilizotoa ili zianze kuonekana na kufanyiwa kazi mara moja” Rais Magufuli amesema.

     Katika Kikao chake, Rais ametoa mwongozo na kusisitizia kuwa ni lazima kila mtendaji Serikalini kuuzingatia, kufuata sheria na taratibu ili taifa lisonge mbele kwa ufanisi zaidi. Katika kikao hicho Rais ameelekeza mambo kadhaa ambayo watendaji hao wanapaswa kuyasimamia, kuyawekea mikakati na kuyapanga vizuri ili atakapo teua Baraza lake la Mawaziri mambo hayo yawe tayari ili Mawaziri watakaoteuliwa waweze kuyasimamia bila kukosa.
    
 Mambo hayo muhimu ni kama ifuatavyo:
Kuanzia mwezi  Januari mwaka 2016, wanafunzi wote wanaoanza shule watasoma bure bila kulipa ada, Katika jambo hili, Rais amewataka watendaji kuanza kuliwekea mikakati tayari kwa utekelezaji Suala la mikopo ya wanafunzi nalo lifanyiwe kazi na mipango yake ikamilike kwa ajili ya utekelezaji mzuri zaidi Amefuta safari zote za nje ya nchi kuanzia leo hadi hapo atakapolitolea suala hilo maamuzi mengine na kueleza kuwa shughuli zote zinazotakiwa kufanywa nje ya nchi zifanywe na kusimamiwa  na mabalozi wa Tanzania  wanaowakilisha nchi  huko nje.

Pengine patokee jambo la dharura sana na hata hilo lazima kibali kitolewe na Rais au Katibu Mkuu Kiongozi. Badala yake Rais amewataka watendaji hao kufanya zaidi ziara za kwenda vijijini ili kuzijua na kutatua kero za wananchi wa Tanzania.

     Katika Kikao hicho, Rais amemtaka Kamishna wa TRA, Ndugu Rished Bade kusimamia kwa makini zoezi la ukusanyaji wa mapato nchini na kuhakikisha kero ndogo ndogo kwa wananchi lianze kutekelezwa kama alivyo ahidi kwa  kufanyiwa  kazi mapema  zaidi.

     Rais ameitaka TRA kukusanya mapato hayo kutoka kwa wafanya biashara wakubwa zaidi na wale wanaokwepa kodi bila kuogopa mtu wala taasisi yoyote hapa Tanzania na kusisitiza kuwa katika Serikali hii wa kutoa maamuzi vinginevyo zaidi ya haya ni yeye Rais  ama Makamu wake.

     Rais Magufuli pia ameagiza usimamizi katika suala la manunuzi ambalo limekuwa likitumika vibaya na kuwa mwanya wa kuibia Serikali  kwa watu kuongeza bei ya vitu hata kama ni vya bei ndogo kabisa katika jamii.

     “Ikitokea suala hilo likagundulika kwa watu kuongeza bei ya vitu, watendaji watawajibishwa mara moja”. Rais amesema, na kuwataka watendaji hao kufanya kazi zao kwa kuzingatia Sheria na taratibu zilizopo na kuzingatia maadili mema ya kazi.

RAIS DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI AKUTANA NA MAKATIBU WAKUU, MANAIBU MAKATIBU WAKUU NA WATENDAJI WAKUU WA SERIKALI LEO IKULU

 
 Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.
  Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono  Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na  kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.
 Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono  Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na  kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.
 Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bwana Rished Bade na  Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na  kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.
 Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono na Katibu Mkuu Utumishi Mhe HAB Mkwizu  na  Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na  kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.
 Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono  Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na  kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.
 Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono  Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na  kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.
 Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono  Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na  kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.
 Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono  Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na  kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.
 Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Mcheche Masaju na  Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na  kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.Kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.
Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli  katika picha ya pamoja Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na  kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.

Boko Beach Veterans wamkabidhi zawadi Mchezaji bora wa Mwezi Oktoba 2015


Mwenyekiti wa Timu ya Boko Beach Veterans (BBV), Danny Ole a.k.a Aguero (wa nne toka kushoto) akimkabidhi zawadi ya mpira Mchezaji bora wa Mwezi Oktoba, Henry Horombe (wa nne toka kulia), baada ya kuonyesha kiwango kizuri kwa kipindi chote cha mwezi mwezi huo 2015. Zawadi hizo hutolewa na mdau mkubwa wa soka nchini na mmiliki wa maduka ya Zizzou Fashion, Othman Tippo Shaaban ambaye nae ni mwanachama wa timu hiyo.
Sehemu ya wachezaji wa Timu ya Boko Beach Veterans (BBV) wakimpongeza mchezaji mwanzao aliebuka kidedea na kutwaa taji la Mchezaji bora wa Mwezi Oktoba, Henry Horombe (katikati) mara baada ya mtangango uliopigwa mapema leo asubuhu katika uwanja wa Boko.
 Timu ya Boko Beach Veterans (BBV) ikiwa imegawanyika katika mchezo wa mazoezi mapema

TNRF WAMTAKA MAGUFULI ADHIBITI UPOTEVU WA MALIASILI NCHINI


 Mwenyekiti wa Jumuiko la Maliasili nchini (TNRF) ,Dr.Suma Kaare akizungumza katika mkutano wa 7 wa jumuiko hilo uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel
  Mkurugenzi wa Shirika la Haki kazi Catalyst Alais Moridant akifafanua jambo  katika mkutano wa 7 wa jumuiko hilo uliofanyika jijini
Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka
wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel
  Mkurugenzi wa Shirika la AWF ,John Salehe
akifafanua jambo  katika mkutano wa 7 wa jumuiko hilo uliofanyika jijini
Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka
wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel
  Washiriki wa  mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini
Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka
wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel
  Viongozi mbalimbali wa jumuiko la maliasili wakiwa katika mkutano wa 7 wa jumuiko hilo uliofanyika jijiniArusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel
Washiriki wa  mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini
Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka
wizara ya maliasili.Picha na Gadiola Emmanuel 
Washiriki wa  mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini
Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka
wizara ya maliasili.

Rais Magufuli akutana na Makamu Mwenyekiti wa Chama Tawala Cha China


po2
Rais Dkt.John Pombe Magufuli akimkaribisha na kufanya mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa Chama Tawala Cha China Mhe.Zhang Ping ikulu jijini Dar es Salaam leo.Bwana Zhang alimwakilisha Rais wa China katika sherehe za kuapishwa Rais wa Awamu ya Tano(picha na Freddy Maro). 
po3
Rais Dkt.John Pombe Magufuli akipiga picha  na kufanya mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa Chama Tawala Cha China Mhe.Zhang Ping ikulu jijini Dar es Salaam leo.Bwana Zhang alimwakilisha Rais wa China katika sherehe za kuapishwa Rais wa Awamu ya Tano kulia ni Balozi wa China nchini Tanzania Mh.  Lu Youqing  na kushoto ni  Mh.Balozi  Abdulrahman Shimbo Balozi wa Tanzania nchini China
po4
Rais Dkt.John Pombe Magufuli akifanya mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa Chama Tawala Cha China Mhe.Zhang Ping ikulu jijini Dar es Salaam

Rais Magufuli akutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria Ramtane La mamra






Rais Dkt. John Pombe Magufuli akutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria Mhe. Ramantane Lamamra Ikulu jijini Dar es Salaam leo.

ENEO LA LEBANON KATIKA SOKO LA KIMATAIFA LA SAMAKI LA FERI JIJINI DAR NI HATARI KWA UCHUMI.


Mwenyekiti wa Kamati ya Soko la Samaki la Kimataifa la Feri, Ali Kibwana, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi wanaotembelea masoko mbalimbali ya Manispaa ya Ilala kuona jinsi gani vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia umepungua katika soko hilo baada ya Shirika la Equality for Growth (EfG) kutoa mafunzo ya kupinga ukatili katika masoko hayo. Kushoto ni Mwezeshaji wa Sheria katika soko hilo, Bakari Said.
Mwonekano wa sehemu ya soko la Samaki la Feri.

Na Dotto Mwaibale
ENEO la Lebanon katika Soko la Kimataifa la Samaki la Feri ambalo lipo jirani na Ikulu jijini Dar es Salaam limedaiwa kuwa ni hatari kwa wafanyabiashara wa soko hilo na kuwa linadhohofisha uchumi kutokana na kukithiri kwa watu wasio rasmi.

Hayo yamebainishwa na Mwezeshaji wa Sheria wa soko hilo, Asha Malenda wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi wanaotembelea masoko mbalimbali ya Manispaa ya Ilala kuona jinsi gani vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia umepungua katika soko hilo baada ya Shirika la Equality for Growth (EfG) kutoa mafunzo ya kupinga ukatili katika masoko hayo.

"Tunachangamoto kubwa sana katika soko letu la Feri tunayoipata kutoka eneo la Lebanon lenye mwingiliano wa watu wasio rasmi kutoka nje ya soko ambao ni kama wamejianzishia soko lao na wamekuwa na maamuzi yao lakini viongozi wa soko la Feri wanashindwa kuwachukulia hatua hali ambayo inatudhalilisha sisi wafanyabiashara hasa mama lishe na kuharibu uchumi wa soko letu" alisema Malenda.

Alisema wengi wa watu waliopo katika eneo hilo lisilo rasmi wamekuwa wakifanya biashara kiholela huku wakipika vyakula katika maeneo yanayoweza kuhatarisha afya ya mlaji wakati katika soko hilo kuna eneo maalumu la mama lishe na wengi wa watu hao wakienda kula eneo hilo rasmi wamekuwa hawalipi fedha na wakibanwa kulipa wanadiliki kutoa visu na silaha za jadi kuwatishia wanaodai.

"Eneo hilo la Lebanon ni hatari na kinachoshangaza linatizamana na Ikulu lakini hakuna hatua yoyote ya makusudi inayochukuliwa na viongozi wetu na linapopelekwa kwa viongozi wa kisiasa wanadai waachwe kwani ndio wapiga kura wao" alisema Mwezeshaji wa Sheria katika soko hilo, Bakari Said.

Said alisema katika soko hilo kuna changoto nyingi za udhalilishaji wanawake kwa kushikwa katika maungo yao lakini kupitia EfG wamejitahidi kupunguza changamoto hizo kwani wasaidizi wa sheria waliopatiwa mafunzo na shirika hilo wanajitahidi kuupenyeza ujuzi waliopata kuifikishia jamii ambayo imeanza kuelewa kuhusu vitendo hivyo.

Aliongeza kuwa uvaaji wa nguo za kubana na kuacha vifua wazi kwa upande wa wanawake pia ulikuwa ukichochea kukithiri kwa vitendo vya udhalilishaji uliokuwa ukifanywa na vijana wasio rasmi katika eneo hilo la Feri ambao hawana makazi na maisha yao yapo Feri lakini baada ya kufikiwa na mafunzo ya EfG hali hiyo imepungua kwa asilimia 80.

Rais Magufuli afanya Ziara ya Kushtukiza Hazina.

 Rais Dkt.John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha wageni muda mfupi baada ya kuwasili katika makao makuu ya Wizara ya Fedha(HAZINA) kwa ziara ya kushtukiza leo mchana.Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt.Servacius Likwelile.Rais Magufuli alitembelea na kukagua ofisi zote wizarani hapo na kisha kuongea na viongozi waandamizi.
 Rais Dkt.John Pombe Magufuli akiwa na wafanyakazi wawili wa Wizara ya Fedha ambao ni walemavu Bwana Fundi Maruma na Frank Mkyama wakati Rais alipofanya ziara ya kushtukiza wizarani hapo leo.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi waandamizi wa Wizara ya Fedha wakati alipofanya ziara ya kushtukiza Wizarani hapo ambapo alitoa maagizo ya kuziba mianya ya wakwepa kodi.


Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza katika Ofisi za Wizara ya Fedha leo Ijumaa tarehe 6 Novemba, 2015.
Katika ziara hiyo Mhe.Rais alipata fursa ya kutembelea baadhi ya Ofisi za Wizara na baadae  kuzungumza na Viongozi wa Wizara ili kufahamu changamoto ambazo zinaikabili Wizara ya Fedha.Wakati akimkaribisha Mhe.Rais Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha        Dkt. Servacius Likwelile alimueleza kuwa Wizara ya Fedha inakabiliwa na changamoto kubwa inayotokana na makusanyo ya mapato ya ndani. 
 Miongoni mwa sababu ni misamaha ya kodi, wafanyabiashara wengi hasa wakubwa kukwepa kodi, makusanyo yasiyoridhisha ya maduhuli na kutokulipwa kwa kodi za majengo. Aidha Dkt. Likwelile alishauri ni bora kuwekwa mifumo mizuri, ikiwemo matumizi ya Tehama na EFDs.
“Pamoja na ziara yangu kuwa ni ya kustukiza nimefurahi sana kukuta Viongozi wote wapo ofisini na wanafanya kazi. Jambo hili limenipa faraja kubwa. Ziara yangu ya kuja hapa nimejifunza na kujua changamoto zipi zinazowakabili”. Alisema Mhe. Rais.
Nimesikia changomoto nyingi na ninaagiza kuwa muhakikishe walipa kodi wakubwa wanalipa kodi na kusimamia kikamilifu Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili iweze kukusanya kodi kikamilifu na si kuwabana wafanya biashara wadogo wadogo.Mhe.Rais aliwataka Viongozi wa Wizara kufanya kazi kwa bidii ili kuvuka lengo.

BALOZI MULAMULA AWASINDIKIZA MRAIS WA DRC NA MSUMBJIA


Rais wa Jamuhuri ya Demokrasia ya Kongo, Mhe. Joseph Kabila (wa kwanza kushoto) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula wakitizama Kikundi cha Ngoma kilichokuwa kikitoa Burudani kwenye Uwanja wa Ndege, Rais Kabila alikuja nchini kuhudhuria Sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli iliyofanyika hapo jana katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Rais Kabila (katikati) akielekea kwenye ndege, kulia ni Balozi Mulamula na kushoto ni Balozi wa Kongo nchini Mhe. Khalifani Mpango
Mhe. Rais Kabila akipita kwenye gwaride la heshima lililoandaliwa na Jeshi la wananchi Tanzania.
Katibu Mkuu Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kulia) akiagana na Rais Joseph Kabila tayari kwa kuanza safari ya kuelekea nchini kwake.
 
Blogger Templates