Rais
Dkt.John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha wageni muda mfupi baada ya
kuwasili katika makao makuu ya Wizara ya Fedha(HAZINA) kwa ziara ya
kushtukiza leo mchana.Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt.Servacius
Likwelile.Rais Magufuli alitembelea na kukagua ofisi zote wizarani hapo
na kisha kuongea na viongozi waandamizi.
Rais
Dkt.John Pombe Magufuli akiwa na wafanyakazi wawili wa Wizara ya Fedha
ambao ni walemavu Bwana Fundi Maruma na Frank Mkyama wakati Rais
alipofanya ziara ya kushtukiza wizarani hapo leo.
Rais
Dkt.John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi waandamizi wa Wizara ya
Fedha wakati alipofanya ziara ya kushtukiza Wizarani hapo ambapo alitoa
maagizo ya kuziba mianya ya wakwepa kodi.
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa
Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amefanya ziara ya
kushtukiza katika Ofisi za Wizara ya Fedha leo Ijumaa tarehe 6 Novemba,
2015.
Katika ziara hiyo Mhe.Rais
alipata fursa ya kutembelea baadhi ya Ofisi za Wizara na baadae
kuzungumza na Viongozi wa Wizara ili kufahamu changamoto ambazo
zinaikabili Wizara ya Fedha.Wakati akimkaribisha Mhe.Rais
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile
alimueleza kuwa Wizara ya Fedha inakabiliwa na changamoto kubwa
inayotokana na makusanyo ya mapato ya ndani.
Miongoni mwa sababu ni
misamaha ya kodi, wafanyabiashara wengi hasa wakubwa kukwepa kodi,
makusanyo yasiyoridhisha ya maduhuli na kutokulipwa kwa kodi za majengo.
Aidha Dkt. Likwelile alishauri ni bora kuwekwa mifumo mizuri, ikiwemo
matumizi ya Tehama na EFDs.
“Pamoja na ziara yangu kuwa ni ya
kustukiza nimefurahi sana kukuta Viongozi wote wapo ofisini na
wanafanya kazi. Jambo hili limenipa faraja kubwa. Ziara yangu ya kuja
hapa nimejifunza na kujua changamoto zipi zinazowakabili”. Alisema Mhe.
Rais.
Nimesikia
changomoto nyingi na
ninaagiza kuwa muhakikishe walipa kodi wakubwa wanalipa kodi na
kusimamia kikamilifu Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili iweze
kukusanya kodi kikamilifu na si kuwabana wafanya biashara wadogo
wadogo.Mhe.Rais aliwataka Viongozi wa Wizara kufanya kazi kwa bidii ili
kuvuka lengo.
0 comments:
Post a Comment